Hivi huyu Chifu Erasto A.M Mang'enya yupo kweli au aliishatangulia mbele za haki?
Maisha ni fumbo.
Naomba uweke tena hiyo picha boss
Matatizo yalianza baada ya athari za sera ya Ujamaa. Watu walihamishwa pasi kuwa na maandalizi ya kutosha. Vijiji vingi havikuwa na maji, umeme wala barabara za kueleweka. Pia dhana ya kufanya kazi kwa pamoja ilizalisha goigoi wengi.Tuseme nchi ingeenda alivyotaka mwalimu Nyerere ni nini kingetokea ?
Hakuwa na tamaa ie mzee Kenyatta aliyejigawiya karibia ardhi ya nchi nzima.
Madini huku akijua kabisa chini kuna madini ila akasema ngojeni
Nidhamu ya kazi ilikuwepo.
All things changed sasa
Sema sera ya vijiji vya ujamaa ingeundwa vizuri tungekuwa mbali.Matatizo yalianza baada ya athari za sera ya Ujamaa. Watu wakihamishwa pasi kuwa na maandalizi ya kutosha. Vijiji vingi havikuwa na maji, umeme wala barabara za kueleweka. Pia dhana ya kufanya kazi kwa pamoja ilizalisha goigoi wengi.
Uchumi uliharibika sana baada ya vita ya Kagera. Hata mwenyewe alitangaza miezi 18 ya kufunga mikanda.
Collectiveness au Ujamaa unahitaji nidhamu ya hali ya juu. Kuwaamini wachache watunze pesa za wengi inahitaji kuweka kanuni madhubuti za adhabu itakayowapata wabadhirifu. Bila hivyo yanatokea yaliyotokea Urusi na hata hapa kwetu.Sema sera ya vijiji vya ujamaa ingeundwa vizuri tungekuwa mbali.
Nahisi watu wa mikoa hii ya arusha Kilimanjaro hasa ndo waliingilia kupinga ujamaa.
Vile walijua vihamba vyao vitagawiwa.
Kufanya kazi pamoja kwa manufaa yenu wote ni nzuri.
Ni kama wasomi waliokuwepo hawakumsaidia mwalimu kuunda hivi vitu.
Mngezaliwa mjikute hivyo ni kuwa yangekuwa ndo maisha yetu.
Vita kweli vilipukuta uchumi wetu.
Akiba yote ikaishia vitani.
Ni kama tokea pale nchi haijakaa sawa tena.
Anyway nilimpenda sana Mwalimu Nyerere.
Tuseme nchi ingeenda alivyotaka mwalimu Nyerere ni nini kingetokea ?
Hakuwa na tamaa ie mzee Kenyatta aliyejigawiya karibia ardhi ya nchi nzima.
Madini huku akijua kabisa chini kuna madini ila akasema ngojeni
Nidhamu ya kazi ilikuwepo.
All things changed sasa
Historia ya Mang'enya na Muheza inasisimua sana. Inataka nafasi kuilezea
Baba wa Taifa, Mzalendo wa kweli kabisaPichani ni Julai 16, 1963, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Julius Nyerere akiweka katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant pini yenye alama ya mwenge wa taifa.
Kulia kabisa ni mwakilishi wa kudumu wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa wakati huo Chifu Erasto A.M Mang'enya na kushoto kabisa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanganyika Oscar Kambona.
Mwenge wa taifa ulipandishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro pindi Tanganyika ilipopata uhuru wake, mnamo tarehe 9, Desemba, mwaka 1961.
View attachment 2050781
📸: UN Photo
Wakati Mang’enya akiwa balozi wa kudumu wa Tanzania UN na JF Kennedy akiwa Rais, Mwalimu allionekana katika picha nyingi kipindi hiki. Kuna moja alikaribishwa na Kennedy kwenye presidential retreat.U-Thant mwanadamu aliyezuia vita ya kinyuklia baina ya Marekani na Umoja wa Kisovieti.
Dunia haimkumbuki sana bali wanaokumbukwa ni J.F Kennedy na N.S Khrushchev.
Historia ya Mang'enya na Muheza inasisimua sana. Inataka nafasi kuilezea
Luka Kitandula alikuja kua Mbunge wa Muheza baadae. Naona na mwanae Dan Luka Kitandula anaendelea kua Mbunge wa Jimbo la Mkinga kwa kipindi cha tatu mfululizo sasa
Kwenye kupigania Uhuru hutosikia majina ya machifu...hawa walikuwa beneti na wakoloni
Ajabu Nyerere alivyopewa nchi Tu..
Akaleta hawa machifu kwenye serikali..
Mang'enya
Fundikira na wengineo
Ccm figisu walianza zamani sana..nadhani kwa kiasi fulani Machifu walipewa jina baya ili kuhalalisha maamuzi ya serikali ya Tanu kufuta uchifu.
..mfano mzuri ni propaganda dhidi ya Mangi Marealle kwamba alikwenda UN na kupinga petition ya Tanganyika kupata uhuru.
..USHAHIDI wa maelezo na maoni ya Mangi Marealle UN upo na alieleza mambo tofauti kabisa na ambavyo Watanganyika tumedanganywa kwa muda mrefu.
..Mangi Marealle alitetea Watanganyika kupewa uhuru na alisisitiza suala la Watanganyika kupatiwa nafasi nyingi zaidi za masomo kama maandalizi ya kujitawala.
..Mangi Marealle pia aliulizwa kuhusu nafasi ya Machifu ktk Tanganyika huru na jibu lake lilikuwa anapendekeza tuige mfumo wa Machifu wa Ghana.
..Hata Nyerere alipokuwa UN ali acknowledge mchango wa Mangi Marealle kabla yake kuwa unashabihiana na msimamo wake na wa Tanu.
..Hili suala anayetaka kujiridhisha aende kwenye ARCHIVE za UN atakuta mahojiano ya Mangi Marealle, na Mwalimu Nyerere, mbele ya kamati ya udhamini ya UN.
..Ukiacha hilo, kuna ushahidi wa Machifu wa Usukumani kuunga mkono Tanu. Kazi ya kuwashawishi Machifu wa Kisukuma ilifanywa na Paul Bomani.
..Nyerere alimheshimu Paul Bomani kutokana na ushawishi wake na kazi kubwa alivyofanya kuipenyeza Tanu kanda ya Ziwa.
..Jambo lingine ni mchango wa FEDHA toka Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuendesha Tanu. Nimewahi kusoma kwamba kuna wakati kanda ya Ziwa ilikuwa inachangia 2/3 ya fedha za kuendesha chama. Kama sijakosea habari hii iko ktk kitabu cha John Illife kuhusu historia ya Tanganyika.
Cc Nguruvi3, Mamndenyi, Pascal Mayalla, Fundi Mchundo, MALCOM LUMUMBA
Ccm figisu walianza zamani sana