..nadhani kwa kiasi fulani Machifu walipewa jina baya ili kuhalalisha maamuzi ya serikali ya Tanu kufuta uchifu.
..mfano mzuri ni propaganda dhidi ya Mangi Marealle kwamba alikwenda UN na kupinga petition ya Tanganyika kupata uhuru.
..USHAHIDI wa maelezo na maoni ya Mangi Marealle UN upo na alieleza mambo tofauti kabisa na ambavyo Watanganyika tumedanganywa kwa muda mrefu.
..Mangi Marealle alitetea Watanganyika kupewa uhuru na alisisitiza suala la Watanganyika kupatiwa nafasi nyingi zaidi za masomo kama maandalizi ya kujitawala.
..Mangi Marealle pia aliulizwa kuhusu nafasi ya Machifu ktk Tanganyika huru na jibu lake lilikuwa anapendekeza tuige mfumo wa Machifu wa Ghana.
..Hata Nyerere alipokuwa UN ali acknowledge mchango wa Mangi Marealle kabla yake kuwa unashabihiana na msimamo wake na wa Tanu.
..Hili suala anayetaka kujiridhisha aende kwenye ARCHIVE za UN atakuta mahojiano ya Mangi Marealle, na ya Mwalimu Nyerere, mbele ya kamati ya udhamini ya UN.
..Ukiacha hilo, kuna ushahidi wa Machifu wa Usukumani kuunga mkono Tanu. Kazi ya kuwashawishi Machifu wa Kisukuma ilifanywa na Paul Bomani.
..Nyerere alimheshimu Paul Bomani kutokana na ushawishi wake na kazi kubwa alivyofanya kuipenyeza Tanu kanda ya Ziwa.
..Jambo lingine ni mchango wa FEDHA toka Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuendesha Tanu. Nimewahi kusoma kwamba kuna wakati kanda ya Ziwa ilikuwa inachangia 2/3 ya fedha za kuendesha chama. Kama sijakosea habari hii iko ktk kitabu cha John Illife kuhusu historia ya Tanganyika.
Cc
Nguruvi3,
Mamndenyi,
Pascal Mayalla,
Fundi Mchundo,
MALCOM LUMUMBA