1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Ajabu sana wewe Fundi Mchundo kuleta upupu kwamba "Madai ya Uhuru hayakuwa ya watu weusi peke yao" hii hoja mbona iko wazi sana haipaswi kuandikwa kwa kujitutumua kama ulivyofanya hapa, hivi ni nani asiefahamu kwamba Tanganyika lilikuwa koloni la muingereza likiandaliwa kuja kujitawala lenyewe yaani kwa maana nyingine hata Hao waingereza walishiriki kuiandaa Tanganyika kuwa huru baada ya kumtwanga mjerumani
 
Mohamed Said angekuwa nchi nyingine wangemuenzi sio hapa kwetu ambako wajuaji ni wengi na mabwana wadogo, humu Moh anapicha hadi za 1970s akiwa kwenye 20s kijana mdogo mtafiti badala yake vijana wadogo kina Fundi Mchundo ambao nao wanapita njia hizo hizo wanakuja kumnanga kana kwamba hana jema, kweli? Iko wapi Nidhamu ya kitaaluma?
 

Hauwezi kuhitimisha mjadala kwa sababu huna la kuongeza. Wenye ya kuongeza wataendelea kuongeza tu.

Ulichokifanya kwa kitabu cha Alfred Tandau ni sawa na sisi tunavyokukatalia kuwa historia unayoijua/unayoisimulia wewe haiko kamili kwa sababu kuna wengi zaidi ya hao unaowataja wewe walipaswa kuenziwa katika historia ya TANU. Aidha, unarudia tena kosa lako la kuona historia yeyote ni lazima iwape kipaumbele ndugu zako ndio iwe imekamilika. Alfred Tandau pamoja na wakina Rashid Kawawa, Michael Kamaliza, Kassanga Tumbo, Joseph Rwegasira, M.M. Mpangala na wengine walianzisha Tanzania Federation of Labour mwaka 1955 baada ya kuungana trade union 17 kwa hiyo ni wazi kuwa alitoa upendeleo kwa trade unions nyingine.

Aidha, vyama hivi havikuanzia Dar es Salaam kama ambavyo wengi wanaweza kudhani. Chama cha kwanza kilianzishwa mwaka 1927 mjini Moshi na madereva na mafundi magari wa kiafrika na kiliitwa Motor Drivers Union. Kama nilivyosema awali, chama cha Tanganyika African Civil Service Association kilianzishwa Tanga mwaka 1922 na Martin Kayamba lakini kilionekana sio chama cha wafanyakazi wa kawaida ingawa TAA ilichipuka kutoka chama hiki. Ilipofika 1947, serikali iliviandikisha vyama kama Stevedores and Dockers Union, African cooks, washermen and houseboys Association, African Tailors Association, Dar es Salaam African Motor Drivers Union. Hii ilisababishwa kwa kiasi kikubwa na migomo iliyofanyika 1937 katika bandari ya Tanga ambako wafanyakazi 250 waligoma, 1939 katika bandari ya Dar es Salaam, 1943 katika bandari za Mwanza na Lindi na 1947 tena katika bandari ya Dar es Salaam. katika bandari za Tanga na Dar es Salaam. Ilipofika mwaka 1950 tayari palikuwa na vyama vya wafanyakazi kwa uchache vifuatavyo 1) Transport Workers Union 2) Agricultural and Plantation Workers Union 3) Dar es Salaam Dockworkers Union 4) Tanga Dock Workers Union 5) Custom Workers Union 6) Railway Workers Union 7) Dar es Salaam Hotel Workers Union 8) Public Employees Union 9) Local Government Workers Union 10) Mine Workers Union 11) Postal Workers Union 12) Teachers Union na vingine. Kutokana na haya sio kweli kuwa wakati makuli wanafanya migomo miaka ya 1940 hapakuwa na vyama vingine vya wafanyakazi.

Baada ya TFL kuanzishwa palikuwa na migomo ya wafanyakazi katika mashamba ya katani, wafanyakazi katika machimbo ya almasi Mwadui, ya wafanyakazi wa reli, wafanyakazi wa posta. Kwa sababu TFL, chini ya uongozi wa Rashidi Kawawa ilikuwa iko upande wa TANU, haiku unga mkono migomo ile. Hii ni kwa sababu serikali ya mwisho wa 1950s ilikuwa tayari ya TANU na waliwaona hawa wanaogoma kama wanaowaletea vurugu tu na wanaweza kuharibu transition ya kwenda kwenye serikali kamili huru ya Tanganyika. Msimamo huu unaeleweka ukizingatia kuwa mwaka 1960 palikuwa na migogoro 203 ya kikazi, na mwaka 1962 ilikuwepo migogoro 152. Ndio maana mara baada ya uhuru serikali ikaamua kutunga sheria ya kutaka mazungumzo yafanyike kabla ya mgomo wowote na mwaka 1962 wakaingiza mfumo wa vyama vya wafanyakazi serikalini. Kwa mifano hii utatambua kuwa sio Mzee Salum Abdallah peke yake ndie aliongoza migomo dhidi ya wakoloni. Kwa mifano hii ni wazi kuwa babu yako peke yake hakuongoza migomo yote Tanganyika.

Umefanya kosa lingine, kwa kutaka kutuaminisha kuwa ni Tandau peke yake ndie aliyeandika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika. Wakina Frieland na Chachage nao wameandika kuhusu vyama hivyo. Hivi karibuni, David Hyde ameandika kwa kirefu akiunganisha juhudi za chama cha wafanyakazi wa reli Tanganyika na zile za Kenya ( zikiongozwa na Tom Mboya) na za Uganda kwa maana shirika la reli la wakati ule lilikuwa East African Railways and Harbour. Kulingana na Hyde, Katibu Mkuu wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) alikuwa ni E.N.N. Kanyama na huyu ndie aliyeongoza mipango yote ya migomo. Mwaka 1959, Katibu Mkuu alikuwa C.S.K. Tumbo na hawa ndio walioongoza migomo yote, mara nyingi (sio mara zote) kwa kushirikiana na wenzao wa Kenya na Uganda. Itakuwa vizuri kama tukijua Mzee Salum Abdallah alikuwa na nafasi gani ya uongozi katika TRAU na mchango wake katika hiyo migomo ili historia iwekwe vizuri.

Kitu kingine ni tabia yako ya kuona watu kama Eccles wanakukosoa kwa sababu ya dini yako na sio mapungufu katika uandishi wako au pengine wao kutokuwa na taarifa ulizokuwa nazo. Inawezekana unaamini hata Fundi Mchundo na Nguruvi3 wanafanya hivyo kwa sababu tu ni wagalatia wasiowatakia mema waislamu. Kama ni hivyo, utakuwa hauwatendei haki. Wanachojaribu kuonyesha ni kuwa historia ni complex na sio rahisi kwa mtu mmoja kuimiliki.

Amandla...

cc: Nguruvi3
 

Kama haujui kuwa Tanganyika haijawahi kuwa koloni la Uingereza, tutajadiliana nini?

Amandla....
 

Nchi nyingine ipi hiyo ambayo ingemuenzi kwa sababu ana picha za 1970s?

Amandla.....
 

Aliyesema kuwa Mohamed Said sio authority kwenye historia ya TANU na Tanganyika ni kijana Fundi Mchundo. Na bado anaamini hivyo.

Amandla...
 
We bwana nguruvi ipi hasa hoja yako? Nikweli huwezi kuanisha 1,23.. Huyu kijana Fundi Mchundo anakuacha mbali sana
Fundi tupo naye miaka mingi, huyu si kijana hayo anayoandika mengine kayaona. Mpe heshima yake tafadhali. Tena uliwahi kuuliza kuhusu elimu yangu, hakika si kubwa nilishindwa kufanya mtihani wa Territorial std VIII matriculation kwasababu ya nazi. Wakati wa mtihani nilikuwa nafanya kazi ya Urabai nikiteremsha majanguo na kupeleka Ngamiani. Nikitoka Ngamiani napeleka ndaza Pongwe nikitokea mjasani. Ndaza ya Mtindiro ikipendwa sana

Kuhusu Fundi, tafadhali bwana! hebu rejea bandiko#257 la Fundi Mchundo .
Kuna vitu vitatu vinapatikana pale, kwanza, contents zenyewe, pili, mtiririko wa hizo contents zikiunganishwa na kujenga hoja maridhiwa.
Kubwa ni kuwa maudhui yake hayaachi swali wala shaka

Kuhusu hoja yangu ni ipi, nadhani wewe ni mgeni. Tumechambua vitabu vya Mohamed mwaka 2010 kwa miezi 6 mfululizo hapa JF. Kinachofanyika sasa ni kujadili habari mpya zinazojitokeza lakini si vitabu tena. Tulimuonyesha Mohamed matundu na wakati huo mjadala ukiitwa 'Ngano'
K. Kondo na A.M. Tabwe walikuwa special branch a.k.a Fitna.
Sasa Nyerere anakuwaje kibaraka wa Waingereza kabla ya hawa Fitna
Mohamed kaniita Hasidi, choyo na wewe ukishadidia Samaki, mpumbavu. Kwa ka-umri namshkuru MwnyaziMungu nimeshaitwa majina sana, ninasubiri tusi jipya katika dictionary litangazwe ha ha ha .
Sina indhara au tashatiti na yeyote awaye. Muhimu kwangu ni watu kunielewa

Namshukuru sana Mwenyezi maana wanaonielewa ni wengi kuliko wasionielewa.
Nyuzi za Mo watu wana ni tag sana, njoo huku bwana lipo jambo, kuna neno!
 

Makala...
Narejea hapa kwa heshima yako na nakuwekea haya aliyoniandikia Juma Mwapachu baada ya Pius Msekwa kuandika historia siyo ya kuundwa kwa TANU.

Mimi nilimjibu kwa adabu sana nikizingatia umri wake na nafasi yake katika taifa hili.

Nyuma ya ubongo wangu nikijiambia kuwa huyu hawajui wazee wangu kwa hiyo siwezi kumwita muongo ni hajui tu.

Mimi nina wajibu wa kumfunza historia ya hawa wazee wangu aijue.

Juma Mwapachu baada ya kunisoma mimi na kumsoma Pius Msekwa alithibitisha niliyosema.

Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nansio, Ukerewe wakati Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda Nansio mwaka wa 1953 kumuona baba yake, Hamza Kibwana Mwapachu kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka huo uliokuwa ufanyike miezi michache mbele.

Abdul Sykes alikuwa anataka kauli ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu Nyerere kuwa ndiyo Hamza hajabadili fikra yake na anamtaka Abdul ampishe Nyerere katika nafasi ya urais wa TAA?

Hamza Mwapachu alirejea katika fikra yake na akamueleza Abdul kuwa Nyerere achukue nafasi ya urais na mwaka ujao, 1954 iundwe TANU.

Juma Mwapachu kashuhudia haya kwa macho yake hakuhadithiwa.

Juma Mwapachu baada ya kusoma niliyoandika kuhusu historia ya TANU na hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoniandikia:

''Mohamed naafiki kabisa na maelezo yako.

Ndugu Msekwa hajaandika historia ya ukweli kuhusu vuguvugu la siasa za kugombea uhuru kuelekea uundwaji wa TANU.

Historia haifutiki wala kupinduliwa.
Hivi tatizo ni nini hasa kutoa maelezo ya ukweli?

Dr. Kyeruzi alinipa nakala ya makala ya kitabu chake ' The Muhaya Doctor' baada ya kunitumia salaams kupitia kwa kaka yangu Harith Bakari kuniita niende kumuona nyumbani kwake Bukoba.

Nilikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo akitaka nimsaidie kuchapisha kitabu chake.

Nisiseme zaidi.

Muhimu ni sura moja ya kitabu hicho ikifafanua historia ya kukuzwa kwa uongozi wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mapambano yalishika moto kuanzia 1949 mjini Dar-es-Salaam. Dr. Kyeruzi ameandika kwa makini historia hiyo.

Wewe Mohamed ni mkweli katika kunukuu historia sahihi.

Ajabu kwangu Mwalimu Nyerere naye hakutaka kuandika kuhusu historia hii, kwa mfano, Nyerere baada tu ya harusi yake Butiama alipitia Mwanza na kuonana na rafiki yake, Hamza Mwapachu ambaye alisafiri toka Ukerewe kuonana na Kambarage kwa mara ya kwanza baada ya kurejea kutoka Scotland masomoni.

Chief Abdallah Fundikira pia alikutana na Nyerere wakati huo.
Mazungumzo yao yalikuwa kumshawishi Nyerere kuongoza vita ya uhuru.

Wakati huo Edward Twinning alikuwa bado hajapiga marufuku watumishi wa serikali kujihusisha na siasa.

Lakini Twinning alitambua kwa haraka kwamba sera yake ya kuwapeleka uhamishoni mbali na Dar es Salaam wakina Hamza Mwapachu na Dr. Kyeruzi na hata Ally Sykes ilikuwa inashindwa kuzima uongozi wa siasa.

Hivi Msekwa hajui historia hii?
Na kwanini Nyerere hakutaka kuandika historia hii?

Katika mahojiano ambayo Nyerere kaweza kuongelea kuingia kwake katika siasa nasikitika kusema kwamba maelezo yake huwa mepesi au kijuujuu.

Nyerere alinipenda kama mwanawe hivyo siwezi kumlaumu.
Lakini hawa wengine kama Msekwa lazima tuwakosoe.

Wasipinde historia ya vita vya uhuru.

Nasikitika sana kwamba Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walifariki mapema mno baada ya uhuru.

Hawa marafiki kama ndugu walikuwa hazina ya jinsi Tanganyika ilivyojiandaa na kujenga misingi ya vita vya huru.''

Kulia Mohamed Said, William ''Billy" Mfuko, Juma Hamza Mwapachu.
Waliokaa kulia Andrew Gordon, Edward ''Ted'' Makwaia (sasa Chief Edward Makwaia wa Siha), Mama Mary Mackeja (mama yake Ted sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa Ted) nyuma yake ni Wendo Mwapachu 1967.
 
Makala...
Nakupa historia ya babu yangu kwa ufupi.

Ndani ya gazeti la Raia Mwema (Januari 3-9, 2018) kulikuwa na makala ya maisha ya Mzee Fredrick Mchauru.

Kama kawaida yangu kupenda kusoma maisha ya Watanzania maarufu niliitupia jicho.

Haikunipitikia kabisa kama Mzee Mchauru niliyemtaja katika kitabu changu cha historia ya uhuru wa Tanganyika mwaka wa 1998 bado atakuwa hai.

Jina hili likawa linajirudia akilini kwangu. Naam Mzee Mchauru yu hai akiwa sasa na umri wa miaka 97.

Huyu Mchauru ndiye yule aliyekabiliana na babu yangu Salum Abdallah katika uwanja wa mpira wa Town School Tabora chini ya miembe wakati wa kupambana na wakoloni, babu yangu akisimama na wananchi wa Tanganyika wakati Mchauru akiwa mtumishi wa serikali ya Waingereza?

Naam ndiye yeye.

Makala ile ilikuwa tamu haikuisha imekuja kuhitimishwa na toleo la juma hili la Raia Mwema (10 – 16 Januari 2018).

Katika toleo hili mwandishi Ezekiel Kamwaga kanitaja kwa jina kuwa nimemwandika Mzee Mchauru katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kamwaga akaeleza kuwa nimepata kusema kuwa Mzee Mchauru alipata shida kuelewana na wale waliokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Dhulma ilikuwa imezidi sana na wafanyakazi wa bandarini Dar es Salaam wakiongozwa kwa siri na Abdul Sykes wakati ile kijana mdogo wa miaka 23 waliamua kufanya mgomo kudai haki zao.

Mgomo wa Makuli kama ulivyokujafahamika ulienea Tanganyika nzima.

Lakini ili kuuelewa mgomo huu ni muhimu sana msomaji akasoma historia nzima ya mgomo huu chanzo chake na vipi wananchi waliweza kujiunga pamoja hadi kufikia kuwa na uwezo wa kuitingisha serikali kwa mgomo kuenea Tanganyika nzima.

Haiwezekani kwa hapa kueleza historia yenyewe nitakachofanya kukunyambulieni ilikuwaje hadi babu yangu akapambana uso kwa macho na Fredrick Mchauru katika mgomo wa wafanyakazi wa mwaka wa 1947.

Tabora, Western Province 11 Septemba, 1947
β€˜β€™β€¦mgomo huo ulioenea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu.

Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana.

Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na Salum Abdallah waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba.

Chama cha African Association mjini Tabora kilimteua Mwalimu Pinda, aliyekuwa akifundisha shule ya St Mary, kuwa 'mshauri' wa wafanyakazi waliogoma.

Asubuhi ya siku ya mgomo wafanyakazi wa Tanganyika Railways walikusanyika kwenye kiwanja cha mpira chaTown School, wakakaa chini ya miembe kujikinga jua.

Tabora ni maarufu kwa miti hiyo.
Tangu siku hiyo kiwanja hiki kikawa ndicho uwanja maalum kwa mikutano yote ya siasa.

Serikali ilimtuma kijana mmoja kutoka Masasi aliyesoma katika shule za misheni, Frederick Mchauru kuwahutubia wafanyakazi na kuwaomba wasimamishe mgomo na warudi kazini.

Mchauru alikuwa Mmakonde kutoka Newala.

Alielimishwa St. Joseph's College, Chidya na St. AndrewΓ­s College, Minaki.

Mwaka 1946, Mchauru alikuwa amerudi kutoka LondonUniversity akiwa amehitimu masomo yake na kuanza kazi mjini Tabora kama Assistant Social Development Officer.

Wafanyakazi waliokuwa kwenye mgomo walimpigia kelele wakimtaka anyamaze huku wakimwita msaliti.

Inashangaza namna shule za misheni zilivyowatengeneza watumishi wa serikalini walio wasomi wawe watiifu na waaminifu kwa dola.

Wasomi hawa mara nyingi walijikuta wanasigana na wale waliokuwa wakipinga ukoloni na udhalimu.

Mchauru alishindwa kutambua hali halisi iliyokuwapo pale siku ile.

Mchauru alipuuza zile kelele akaendelea kuzungumza akijaribu kuwasihi wafanyakazi warudi kazini kwao.

Ghafla hali iligeuka.

Watu walipandwa na hasira na kusikia wakisema ashikishwe adabu.

Watu waliokuwa wamehamaki wakaanza kumsogelea.

Salum Abdallah, akiwa kiongozi wa watu wale, alihisi kuwa endapo hatachukua hatua ya kumnusuru Mchauru huenda watu wakamuadhibu.

Alienda pale aliposimama Mchauru.

Aliinua mikono yake juu akawataka watu watulie.

Salum Abdallah alikuwa mtu wa miraba minne na alikuwa na sauti kubwa.

Wanachama wengi wa TRAU wanamkumbuka kwa sauti yake, hasira zake na kwa umbo lake kubwa.

Salum Abdallah alikuja kuunda chama cha TRAU mwaka wa 1955 akiwa Rais muasisi na Kassanga Tumbo Katibu muasisi wakaiegemeza TRAU kwa TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wafanyakazi walipomuona Salum Abdallah walitulia na Mchauru akaondoka pale kimya kimya kupeleka taarifa kwa hao waliomtuma kuwa watu wamegoma, hawasikii la muadhini wala la mnadi sala…’’

(Rafiki zangu kwa muda mrefu wanatia shinikizo niandike kitabu cha historia ya babu yangu).



Viongozi wa TRAU Salum Abdallah ni huyo kwenye mshale na anaefuatia ni Kassanga Tumbo
 
Muhimu kuandika lakini ukipatwa uvivu andika Tawasifu yako kisha umueleze kwa mapana, kwasababu Tawasifu yako ni muhimu sana ukizingatia kumekuwepo na hila na fedhuli za hawa jamaa zetu kukubehua na kukutweza kana kwamba ni mtu usie na mbele wala nyuma umetunga ngano ukazichapa, somo yako mwana wa kiqureish Muhammad Ibn Abdallah( Swalla na salaam zimuendee) yeye katika kuwasilisha kwake Amana (Qur-aan na Dini kwa ujumla) amekuwa akitweza kila Leo, baadhi wakimtuhumu alichanganyikiwa
 
Aliyesema kuwa Mohamed Said sio authority kwenye historia ya TANU na Tanganyika ni kijana Fundi Mchundo. Na bado anaamini hivyo.

Amandla...
Endelea kuamini hivyo, lakini Moh si size yako utaendelea kumshuhudia katika jukwaa mbalimbali akihabarisha
 


kiasi wakutage kwani wameshakuona pimbi , hebu soma ulichoandika hapa

Alfred Tandau pamoja na wakina Rashid Kawawa, Michael Kamaliza, Kassanga Tumbo, Joseph Rwegasira, M.M. Mpangala na wengine walianzisha Tanzania Federation of Labour mwaka 1955

Kazi ipo
 
Hivi una uhakika nimeandika hayo?
Hebu jiridhishe kwanza, halafu urejee tujadiliane. Nadhani ghadhabu zinachukua nafasi ya busara
 
Huu uzi una watu wenye akili tu mimi sichangii chochote. Ila nasoma kila herufi
 
Sasa nimeelewa kwa nini Mohamed Said anasema babu yake hakupata utambuzi aliostahili kama muasisi wa TRAU. Lakini tuanze kwanza na historia.

Chama cha wafanyakazi wa reli ( Railway African Association) kiliundwa mwaka 1945 ( sio 1955) na tarehe 10 Septemba 1947 wanachama wake 2000 waliunga mkono mgomo mkubwa uliokuwa unaendelea nchini mwao. Wafanyakazi wa shirika la reli la East African Railways and Harbour( EARH) wa Morogoro, Kilosa, Dodoma na Tabora waliunga mkono juhudi hizo. Tawi la RAA Tabora lilitaka wafanyakazi wa kiafrika walipwe sawa na wahindi.

Mwaka 1957 TRAU, ikiongozwa na Katibu Mkuu wake E.N.N Kanyama kilipunguza madai ya nyongeza ya mshahara kutoka 35% hadi 15% ili kulingana na madai ya R.A.U (K). General Manager wa EARH , Bw. J.R. Farquharson,aliyakataa madai hayo akisema kuwa shirika lake halina uwezo wa kulipa kiwango hicho.

CHRISTOPHER Kasanga Tumbo alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TRAU mwaka 1959 na akaiondoa TRAU katika chombo cha arbitration na serikali kilichoitwa ALJSAC. Katika kikao cha Agosti 1959, wafanyakazi wa TRAU walikubaliana kugoma. Kabla ya mgomo kikao cha pamoja cha vyama vya wafanyakazi wa reli Tanganyika, Uganda na Kenya kilifanyika mjini Mwanza ambapo walikubaliana kuanzisha the National Confederation of Railwaymen (East Africa). Serikali ya mkoloni ilikataa kutambua muungano huo lakini ari ya ushirikiano kati ya vyama hivi ilizidi kukua.

Mwezi Oktoba 1959, TRAU walianzisha mgomo ambao ulisababishwa na shirika kukataa viongozi wao wapya likidai kuwa hawakuchaguliwa.
Mwezi Novemba 1959, mgomo ulitokea Nairobi baada ya mnyapara wa kizungu kuwatukana wafanyakazi wa kiafrika. Ilipofika tarehe 14 Novemba wafanyakazi 26000 walikuwa kwenye mgomo. Mgomo ulitulizwa na wafanyakazi walirudi kazinini tarehe 30 Novemba. Hofu kubwa ya serikali ya kikoloni ilikuwa mgomo huo kuenea mpaka Tanganyika na Uganda.

Hata hivyo TRAU, wakiongozwa na Christopher Kasanga Tumbo walipanga kuanza mgomo tarehe 18 Desemba lakini waliusiticha baada ya kuanza mazungumzo na serikali ya kikoloni ambayo ilikuwa inakabiliwa na mgomo wa wafanyakazi 1200 wa Posta ulioanza tarehe 24 Desemba. Kwa vile wafanyakazi wa posta waliahidiwa kulipwa mshahara wa shilingi 150 kwa mwezi kama kima cha chini, TRAU walipata matumaini kuwa nao madai yao yatakubaliwa kwa sababu hayakupishana sana na ya wafanyakazi wa Posta.

Tarehe 4 Desemba EARH walipendekeza nyongeza ya sh 4 kwa mwezi. Vyama vya wafanyakazi wa reli wa Afrika Mashirika walikutana Nairobi tarehe 30 desemba na tarehe 2 Januari 1960 TRAU walikataa pendekezo la EARH. Tarehe 5 Januari EARH wakaongeza dau kwa shilingi tatu kwa wafanyakazi wa daraja la chini kabisa. TRAU wakakataa.

Tarehe 9 Februari 1960 mgomo wa wafanyakazi wa reli ulianza rasmi. Siku ya pili wafanyakazi 12,000 walikuwa katika mgomo. Mgomo huo uliendelea kwa wiki 11 na nusu ingawa tarehe 15 Februari TAGWU walikubali malipo ya sh. 107 kwa kima cha chini. TFL, chini ya Kawawa hawakupendezwa na mgomo huo kwa sabau waliona kuwa utaathiri matayarisho ya makabidhiano ya nchi na hivyo walikataa kuunga mkono na walimtaka Gavana Reginald Turnbull aingilie kati.

Christopher Kasanga Tumbo alikaribishwa Brussels kukutana na uongozi wa ICFTU ( International Confederation of Free Trade Unions). Alikuwa huko kati ya tarehe 29 Machi na 4 Aprili. Aliporudi, Charles Millard wa ICFTU na Pieter De Vries wa ITWF waliongoza majadiliano na EARH.

Christopher Kasanga Tumbo alipendwa sana na wanachama wa TRAU kwa sababu msimamo wake ulikuwa nafasi zote zinazoshikiliwa na wazungu zishikiliwe na waafrika weusi. Nyerere aliupinga msimamo huo kwa sababu alijua kuwa hapakuweko waatanganyika weusi wa kutosha kujaza nafasi zilizokuwa zinashikiliwa na wazungu. Ndio maana TANU ilihakikisha nafasi ya Christopher Kasanga Tumbo inachukuliwa na Michael Kamaliza ambae alipokuwa waziri wa kazi alishauri serkali kuwa TFL iwekwe chini ya wizara yake.

Tofauti na Mohamed Said alivyosema, Mchauru hakuwa mtumishi wa serikali ya wakoloni kwa sababu waliokuwa wanapambana na TRAU walikuwa viongozi wa EARH. Bila shaka mgalatia mmisheni Mchauru aliajiriwa na EARH. Serikali ya "kikoloni" ilikaa pembeni mpaka TANU ilipomuomba Gavana aingilie suala hilo.

Sehemu kubwa ya historia hii nimeitoa kwenye kitabu kinachoitwa " Building A Peaceful Nation" kilichoandikwa na Paul Bjerk ili kuthibitisha sio Tandau peke yake ndie aliyeandika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika.

Ukiisoma, utaona kuwa tofauti na Mohamed Said anavyotaka kutuaminisha, wamisheni walikuwa msitari wa kutetea haki za wafanyakazi wenzao. Kinachomuuma sio kutotambuliwa mchango wa TRAU bali ni kwa nini sifa zote anapewa mgalatia Christopher Kasnga Tumbo na sio babu yake Salum Abdallah. Anachoshindwa kukubali ni kuwa wasomi wa misheni walihitajika sana kuweza kukaa meza moja kupambana na wazungu katika msingi wa usawa. Ni hasira zile zile anazoonyesha kwa mgalatia Julius Kambarage Nyerere kuenziwa kuliko Abdul Sykes. Kitu kibaya anachofanya ni kuvika vyote hivi joho la udini la wagalatia kutowatendea haki waislamu akisahau conveniently kuwa Mwalimu Nyerere aliwaweka kizuizini wagalatia wenzake wengi tu ikiwa pamoja na Christopher Kasanga Tumbo aliyediriki kuanzisha chama cha Peoples' Democratic party kupinga uanzishwaji wa mfumo wa chama kimoja. Upofu huu ndio unaotufanya tuendelee kupingana nae.

Amandla...

cc. Nguruvi3
 
Nakubali kosa. Nilimaanisha Tanganyika Federation of Labour, sio Tanzania Federation of Labour.

Amandla...
 
Endelea kuamini hivyo, lakini Moh si size yako utaendelea kumshuhudia katika jukwaa mbalimbali akihabarisha
Makala...
Hapana haja ya kuvutana.
Ngoja nikueleze jambo.

Paul Bjerk tunafahamiana.
Hafiki nchini mtafiti yeyote ila atanitafuta kunihoji.

Inazungumzwa Railway African Association (RAA) 1945.
Mimi nazungumza Tanganyika Railways African Union (TRAU) 1955.

Hamaki ziko juu sana.
Inatakikana pawepo kwanza utulivu ili kejeli na kebehi ziondoke.

Nakushauri subiri kidogo patulie In Shaa Allah akili zirejee mahali pake.



Kulia Kassanga Tumbo anaefuatia ni Salum Abdallah amevishwa mgolole kama ishara ya deraya ya vita katika kipindi kile TRAU iko katika migomo dhidi ya Waingereza.

Picha inazungumza maneno 1000 huwa najiambia ingekuwaje ingekuwa sina picha hizi za babu yangu na Kassanga Tumbo niwe na maneno matupu.

Katika hali kama hii nani angeniamini?

Wakati wa mgomo wa 1960 nyumbani kwa babu yangu ilikuwa mfano wa Command Post wakikutana pale wakifuatilia taarifa vipi magazeti yalivyokuwa yanauandika mgomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…