Ukosoaji kama huo wa para ya mwisho ndio muhimu, kwamba
Mohamed Said kaandika 1951 kinyume na uhalisia
Lakini pili mbona hukuhoji kina kimambo na vitabu vyao vya 1969 ambavyo haviwataji waasisi wa TAA?
Makala...
Kuna kitu kinanifurahisha hapa.
Kuna juhudi kubwa sana inafanyika ya kuokoteza historia hapa na pale na bahati nzuri ni kuwa wanatumia vyanzo vyangu ambavyo mimi nimeweka kutia nguvu niliyopata kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Lakini nadhani wao hili hawalijui na kama nisemavyo siku zote kutokujua ni katika silka ya ubinadamu hakuna anaejua kila kitu ila Allah mwenyewe.
Tuanze juu kichwani.
Kabla mimi sijamleta Abdul Sykes hakuna yeyote katika hao wanaonishambuia mimi alikuwa anamjua.
Wala hawakuwa wanajua ilikuwaje Nyerere akawa maarufu Dar es Salaam ilhali yeye ni mgeni mtu kutoka bara tena bara ya mbali sana.
Historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha Kivukoni ndiyo ilikuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nyerere anazuka.
Mimi nikifanya rejea ya kitabu cha Judith Listowel na Nyaraka za Sykes ndiye niliyemrejesha kwa mfano Denis Phombeah kuwa kadi yake ya TANU ni No. 5.
Wengi walishangaa walikuwa hawajapata kusikia jina hili.
Sikuiishia hapa sasa nikifanya rejea za Nyaraka za Sykes nikaeleza safari ya Phombeah na Ally Sykes kwenda Southern Rhodesia (Zambia) mwaka wa 1953.
Naweka link hapo chini.
Ilinichukua karibu miaka 20 kuipata picha ya Phombeah na aliyenipatia ni Ahmed Rajab kutoka kwa mwanae Gray Phombeah.
Mikutano ya siri ikifanyika baada ya TANU kuundwa na kabla ile 1953/54 ilikuwa kwa Abdul Sykes na kamati hii ni mbali na TAA Political Subcommitee ya 1950 ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Hapa tumuongeze Earle Seaton katika hii kamati.
Hakuna aliyekuwa anajua historia ya Seaton na Abdul Sykes na mchango wa Seaton katika hii kamati na mapendekezo ya katiba hadi mimi niipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii nimepata katika Nyaraza za Sykes.
Leo hawa ndiyo wa kunifundisha mimi historia ya Earle Seaton?
Hii historia yote haikuwapo kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
Walikuwa wapi?
Nakuongezea kitu hapa.
Huo urafiki wa Seaton, Marealle wamuongeze na Abdul Sykes.
David Marealle alikuwa jirani yangu iko siku nimemsikia anasema.
''Walionipokea mimi mara ya kwanza nakuja Dar es Salaam ni hawa akina Sykes,'' anamnyoshea kidole Abbbas Sykes aliyenipeleka kwake.
Nimesoma barua za Marealle kwa akina Sykes lakini sikuzitumia katika kitabu kwa kuwa zilikuwa na faragha baina yao.
Hizi barua zina mambo kaka.
Kamati hii TAA Political Subcommitte baada ya kutoka mapendekezo ya katiba Twining akaisambaratisha kwa kuwapa uhamisho Dr. Kyaruzi na Hamza Mwapachu.
Kyaruzi akapelekwa Kingolwira kisha Nzega na Mwapachu kisiwani Nansio.
Hii 1951.
Mikutano ya Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu wamesoma kutoka kwangu nami nimepata kutoka kwa Judith Listowel na Judith Listowel huwezi kuamini katoka katika mswada wa Dr. Kyaruzi, The Muhaya Doctor,'' na kaweka katika kwenye kitabu chake ''word to word,'' ndani ya kitabu hicho.
Ninao huu mswada katika Maktaba yangu.
Turejee kwa Phombeah.
Phombeah asingeweza kufanya mkutano Arnautoglo hapakuwa na faragha hii kwanza halafu hakuwa mtu wa kamati ya ndani.
Amir Jamal kaja TANU 1958 mkutano gani utafanyika kwa Muhindi na siku zile za mwanzo ninazozizungumza ulikuwa wakati wa Afrika kwa Waafrika?
Erica Fiah.
Kleist Sykes kamweleza kwa kirefu katika mswada wake alioandika kabla ya kifo chake 1949.
Wamsome Daisy Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' wakipenda wasome: ''Kleist Sykes Man of Ideas,'' katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mercedes Benz iliwachoma wale wa 1959 kama inavyowachoma hawa wa leo.
Wakahitimisha kwa kufuta historia yote.
Ati nini kununua Mercedes Benz.
Niliweka makusudi kuwasikiliza.
Hasad, wivu na choyo zimewajaa.
Mercedes kwa vijana hawa wa Karikaoo zilikuwa mbili ya Abdul na ya Abbas Abdulwahab na walikuwa majirani.
Abdulwahab alikuwa kijana wa Kiarabu ambae alikuwa na biashara kubwa ya kuuza maziwa.
Katiba ya TANU ni ya Labour Party wanasema na ya CPP.
Kaka mimi naandika kwa ajili yako.
Hawa wanajifunza historia hii leo mimi nimeishi na watu hawa na wamenifungulia nyaraka zao na mioyo yao na nimeandika papers na makala wala sijui hesabu yake.
Kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile mimi nisingeyajua haya yote.
Na kama nisingenyanyua kalamu kuandika hawa wangebakia na historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha CCM Kivukoni.
Ndipo nakuambia wakati mwingine nawaonea huruma.
Wananukuu yale niliyoandika mimi bila ya kujua.
Hakika mtaka nyingi nasaba humkuta mwingi msiba.
Denis Phombeah
KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953 SEHEMU YA KWANZA Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa African National Congress (ANC) na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini...