1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Inashangaza sana , anataka credit za ushiriki hataki kuwa sehemu ya ushiriki. Weird

Miaka iliyopita Mohamed alisema '' A. Sykes alimuungiza Nyerere katika siasa''.

Tulimtembeza Mo katika maandiko yake mwenye na ku-prove Nyerere alianza siasa Makerere. Akiwa Tabora alikuwa katibu wa tawi la TAA na mwaka 1948 alihudhuria mkutano Dar es Salaam. Kwamba, eti Abdul alimjua Mwl miaka ya 50! Hivi zama za 40 na 50 msomi kama Nyerere na katibu wa Tawi muhimu kama Tabora hakujulikana na HQ ya Sykes.

Ndio maana tukimuuliza atuoenyeshe sehemu moja tu, I mean moja nje ya Gerezani Abdul alipofanya mkutano wa siasa, Mohamed hana jibu. Kama atakaribia jibu atakueleza mikutano ya siri na Jomo Kenyatta huko Kenya. Mkutano wa faragha Kenya si Tanganyika ni nchi tofauti Mo!

Mohamed asiyetueleza wapi Abdul aliwashirikisha Watanganyika ndiye anataka umma uamini harakati za Familia zake ni harakati za Tanganyika. Tuna Video za Nyerere akiwa Lindi na kwingine akihutubia mikutano ya siasa, hatuna picha ya Abdulwahid Sykes

Mohamed anatuhumu wasomi wa misheni, asichokumbuka kuanzia 1929 Kleist akiwa Katibu mkuu wa AA hadi Abdul anashindwa uchaguzi wa Arnatouglo hakukuwepo katiba ya chama.

Aliyeandika katiba ya chama ni Nyerere katika transformation ya chama kutoka Familia kuwa mali ya nchi. Kwa nia ya kufifisha mchango huo Mohamed atakuambia Nyerere ali-copy katiba ya Nkrumah, well, hilo mbona halikufanyika miaka 20 ya utawala wa Familia ya Sykes?

Fundi hicho kitabu cha Mwakingile nilikisoma kitambo, nilikipoteza ahsante kwa kukileta nakirejea
Nguruvi3 wewe ni hasidi na mwenzio bwana mdogo Fundi Mchundo, hoja zenu misingi yake ni kuonyesha chuki tu kwa Mohamed Said hamna la zaidi, na huo si usomi madhali mmepata jukwaa basi mnakiuka hata miiko, matusi, kebehi, uongo na mizaha

Haya madai kwamba unafanya mijadala na Moh tangu 2010 yananifikirisha nadhani kichwa chako ni kizito kuelewa na chuki yako hasadi imetopea, hata hoja zako huzianishi kwa ueledi unajikanyagakanyaga tu mathalan ulimtetea mdogo wako Mchundo aliposema Tanganyika halikuwa Koloni la muingereza nilipokubainisha ukaruka viunzi ukakimbilia kwingine

Mwl Nyerere alikuwa ni msomi hakuna atakae kataa ukweli huo, lakini kuna madoa yanatilia shaka usomi wake mathalan kuificha historia kwa makusudi, kupambana na wenzie alikuwa nao kabla ya Uhuru kisha baadae kuwapa uadui n. K
 
Onyesha hizo chuki. Onyesha miiko , matusi, kebehi, uongo na mizaha.
Nitafafanua ukionyesha

Rejea nyuzi za nyuma, si mimi ni JF iliyojadili kila mmoja kwa upande wake.

Mbona haya tumeyasema miaka mingi sana. Historia ya Kivukoni haikuwa sahihi. Je, hiyo inafanya nyingine ziwe sahihi? Je, tunarekebisha kosa kwa kosa?
 
Hasidi ni pale unapombagaza Moh kwamba kana kwamba anafanya khiyana kutokueleza umahiri wa mwl Julius Nyerere, yaani picha za mwalimu lindi Moh kazificha kwasababu sykes hayumo kwenye video?
Kwamba katiba iliandikwa na mwalimu lakini Moh anadanganya kwamba ilihaririwa na mengineyo mfano kuna mahala unamtandika Moh juu ya usuhuba, nasaba na udugu wake familia ya sykes kwamba huoni la maana zaidi ni kama anajaribu kuiinua familia hiyo.
pia kuna mahala huonyeshi kuthamini juhudi alizofanya moh za kutafiti na hata lugha utumiayo si ya kiungwana(huko ndiko kukiuka miiko, kuleta mizaha, uongo, chuki na hasidi)
 
Hasidi ni pale unapombagaza Moh kwamba kana kwamba anafanya khiyana kutokueleza umahiri wa mwl Julius Nyerere, yaani picha za mwalimu lindi Moh kazificha kwasababu sykes hayumo kwenye video?
Hapana hukuelewa hoja. Nilichosema ni kuwa Abdul Sykes hakuwahi kuhutubia mikutano nje ya Gerezani. Nilimaanisha eneo jingine la Tanganyika. Nikamuomba Mohamed kama ana ushahidi wa hilo aweke. Hakuna ushahidi. Nikaenda mbali kueleza kuwa kuna video za mikutano wakati wa Uhuru. Ipo ya Nyerere akihutubia Lindi iliyopigwa na mu-Australia. Zipo picha za mikoani.
Maana yangu ni kuwa kama kuna evidence za Abdul katika hilo ziwekewe.
Kuna kosa gani hapo?
Kwamba katiba iliandikwa na mwalimu lakini Moh anadanganya kwamba ilihaririwa na mengineyo
Maneno hayo kayasema Mohamed ndiyo maana nilikurudisha miaka nyuma. Yupo hapa muulize kama si kweli.
mfano kuna mahala unamtandika Moh juu ya usuhuba, nasaba na udugu wake familia ya sykes kwamba huoni la maana zaidi ni kama anajaribu kuiinua familia hiyo.
Mohamed anawaita wazee wake na kuna habari anazoandika za uswahiba na undugu wa Familia zao. Kuna kosa gani kulieleza hilo? Kwamba sioni la zaidi kwa Familia ya Sykes hayo sijasema hata kidogo. Nilichosema ni kuwa Historia ya Familia ya Sykes siyo ya nchi nzima ni sehemu ya Historia ya Tanganyika kinyume na mtazamo wa Moh
pia kuna mahala huonyeshi kuthamini juhudi alizofanya moh za kutafiti na hata lugha utumiayo si ya kiungwana(huko ndiko kukiuka miiko, kuleta mizaha, uongo, chuki na hasidi)
Mbona huonyeshi lugha mbaya ni ipi?

Mfano, kuuliza 'wadhifa wa Babu TRAU' ni lugha mbaya?
Kusema KK na Tambwe ni special branch officers au Fitna ni lugha mbaya ? Kazi ya special branch ni fitna, sasa hapo nini kosa?

Ningeomba ulete vipande vya ushahidi wa tuhuma usifanye dhania yako kuwa tuhuma

Mimi nathamini wazee wote waliopigania uhuru popote walipo.

Kitu kimoja tu ninachotofautiana na watu kwama wewe, huwa simezi kila kinachorushwa, natafuna au kule Windsor Castle wanasema 'digest'

Huwezi kuniambia eti Nyerere alianza siasa 1951 na Sykes wakati alikuwa katibu mkuu wa Tawi 1948 ana alishakuwa exposed na siasa za kimataifa halafu utegemee nitaidhulumu akili yangu kwa kukubali tu ili niwe na busara na nidhamu ! nope!
 
Mimi mahali nililoamini hakika kuwa J.K Nyerere ni kichwa na Mzalendo ni kwenye ile interview ya ''Prospects of Mankind'' na Anna Roosevelt
😜
😜😜😜😜😜😜😜😜😜
 
Hapana hukuelewa hoja. Nilichosema ni kuwa Abdul Sykes hakuwahi kuhutubia mikutano nje ya Gerezani. Nilimaanisha eneo jingine la Tanganyika. Nikamuomba Mohamed kama ana ushahidi wa hilo aweke. Hakuna ushahidi. Nikaenda mbali kueleza kuwa kuna video za mikutano wakati wa Uhuru. Ipo ya Nyerere akihutubia Lindi iliyopigwa na mu-Australia. Zipo picha za mikoani.
Maana yangu ni kuwa kama kuna evidence za Abdul katika hilo ziwekewe.
Kuna kosa gani hapo?

Maneno hayo kayasema Mohamed ndiyo maana nilikurudisha miaka nyuma. Yupo hapa muulize kama si kweli.

Mohamed anawaita wazee wake na kuna habari anazoandika za uswahiba na undugu wa Familia zao. Kuna kosa gani kulieleza hilo? Kwamba sioni la zaidi kwa Familia ya Sykes hayo sijasema hata kidogo. Nilichosema ni kuwa Historia ya Familia ya Sykes siyo ya nchi nzima ni sehemu ya Historia ya Tanganyika kinyume na mtazamo wa Moh

Mbona huonyeshi lugha mbaya ni ipi?

Mfano, kuuliza 'wadhifa wa Babu TRAU' ni lugha mbaya?
Kusema KK na Tambwe ni special branch officers au Fitna ni lugha mbaya ? Kazi ya special branch ni fitna, sasa hapo nini kosa?

Ningeomba ulete vipande vya ushahidi wa tuhuma usifanye dhania yako kuwa tuhuma

Mimi nathamini wazee wote waliopigania uhuru popote walipo.

Kitu kimoja tu ninachotofautiana na watu kwama wewe, huwa simezi kila kinachorushwa, natafuna au kule Windsor Castle wanasema 'digest'

Huwezi kuniambia eti Nyerere alianza siasa 1951 na Sykes wakati alikuwa katibu mkuu wa Tawi 1948 ana alishakuwa exposed na siasa za kimataifa halafu utegemee nitaidhulumu akili yangu kwa kukubali tu ili niwe na busara na nidhamu ! nope!
Ukosoaji kama huo wa para ya mwisho ndio muhimu, kwamba Mohamed Said kaandika 1951 kinyume na uhalisia
Lakini pili mbona hukuhoji kina kimambo na vitabu vyao vya 1969 ambavyo haviwataji waasisi wa TAA?
 
Hasidi ni pale unapombagaza Moh kwamba kana kwamba anafanya khiyana kutokueleza umahiri wa mwl Julius Nyerere, yaani picha za mwalimu lindi Moh kazificha kwasababu sykes hayumo kwenye video?
Kwamba katiba iliandikwa na mwalimu lakini Moh anadanganya kwamba ilihaririwa na mengineyo mfano kuna mahala unamtandika Moh juu ya usuhuba, nasaba na udugu wake familia ya sykes kwamba huoni la maana zaidi ni kama anajaribu kuiinua familia hiyo.
pia kuna mahala huonyeshi kuthamini juhudi alizofanya moh za kutafiti na hata lugha utumiayo si ya kiungwana(huko ndiko kukiuka miiko, kuleta mizaha, uongo, chuki na hasidi)
Makala...
Marehemu mama yangu akinionya sana kuhusu hasad.
Alikuwa akiniambia na siku hizo mimi mtoto mdogo shule ya msingi.

Akisema hasid jicho lake akiangalia mgomba uliomea vizuri basi unaweza ukanyauka.
Akinambia, "Mwanangu Allah kakupa vitu viwili sudi na maji ya nguo."

Sudi maana yake kupendwa na watu na maji ya nguo ni kuwa nikivaa nguo napendeza kwa kunikaa vyema.

Akimalizia kwa kusema, "Baba uchukue tahadhari kwa akina mama."
Mimi naijua hasad katika maisha yangu.

Picha zangu zinachoma nyoyo.
Akili zao zinakataa kuamini wanachokiona.

Hawataki.
Picha hizi ni makala tosha za kusisimua na mtu kuuliza maswali ya kujenga.

Uko na Prof. Ali Mazrui. ..mlifahamiana vipi nk. nk.
Miaka hii ya udogo upo London ulikwenda shule nk.

Naiona hapa chuki katika maneno na ghadhabu kila nikiwaonyesha kuwa nina vitu navijua kutoka kwa wengi na hizo picha ni ushahidi.

Kwao ati nakunywa chai.
Nikanywe chai New York?

Pamoja na picha nina shajara ndani wako mabwana wakubwa wa siasa za Tanzania.

Mtu namkwepa kujitafutia salama yangu na shari yake.
Hakubali wananiandama na kejeli na kebehi.

Hushangai ukumbi mzima watu wanaongezeka kusikiliza mnakasha?
Jiulize wanakuja kusoma kejeli, ghadhabu na kebehi?

Hapana.
Wanakuja kunisikiliza.

1959 Abdul Sykes alinunua Mercedes Benz 220 SE.
Uhuru bado.

Walitamani ipigwe radi na yeye afe ndani ya hilo Benz.

Husda.
Kaka kaa mbali na hawa watu.

Soma vichwa vya nyuzi wanazofungua kuhusu mimi utawajua.
Nyerere kahutubia mikutano ya hadhara baada ya kuundwa TANU 1954.

Mikutano yote hiyo ikipangwa nyumbani kwa Abdul Sykes siku moja kabla na akitokea nyumbani kwa Abdul Sykes kwenda mkutanoni Mnazi Mmoja au Jangwani baadae.

Lunch zote zikiliwa hapo kwa usalama wa Nyerere.
Wazungumzaji walikuwa yeye Mwalimu, Sheikh Suleiman Takadir na Bi. Titi Mohamed.

Nyerere alipata kuhutubia mkutano wowote kabla ya TANU?
Hapakuandikwa katiba.

Earle Seaton ndiye aliyempa Abdul ujanja wa "adoption," ya katiba ya Nkrumah iliyopitishwa na Waingereza Ghana ili washindwe kuikataa kwa TANU hapa Tanganyika.

Wakati huo wala Abdul hajakutana na Nyerere.
Yapo mengi.

Haya nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

1640947544615.png

Columbia University, New York
 
[emoji12]
[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
Umefurahi sana kijana, kulikoni?

Umepata kumsikiliza Nyerere katika interview hiyo?
 
Pichani ni Julai 16, 1963, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Julius Nyerere akiweka katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant pini yenye alama ya mwenge wa taifa.

Kulia kabisa ni mwakilishi wa kudumu wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa wakati huo Chifu Erasto A.M Mang'enya na kushoto kabisa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanganyika Oscar Kambona.

Mwenge wa taifa ulipandishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro pindi Tanganyika ilipopata uhuru wake, mnamo tarehe 9, Desemba, mwaka 1961.

View attachment 2050781

[emoji991]: UN Photo
Subiri Matusi, Vijembe na Chuki kutoka kwa Waislam [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nianze na suala la ukoloni. Tanganyika haijawahi kuwa koloni la Uingereza. Hiyo ni fact. Wazungu walipogawana Afrika mwaka 1884, sehemu iliyokuja kuwa Tanganyika, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ujerumani kama moja ya koloni zake. Koloni nyingine za Ujerumani zilikuwa Togo na Afrika ya Kusini Magharibi.Kwa hatua eneo la nchi hizi lilitambuliwa na mataifa ya ulaya kuwa mali ya ujerumani na watu wake wakawa sehemu ya himaya hiyo. Jirani zetu Kenya ikagaiwa kwa Uingereza. Hakuna kiongozi wa Afrika mweusi aliyeshirikishwa katika gawio hilo. Sehemu ikitangazwa kuwa koloni ina maana imekuwa mali ya taifa lingine in perpetuity, yaani hamna ukomo wa milki ya mtawala. Kwa sababu waafrika na watawala wa jadi hawakushiriki kwenye mgao huo, baadhi yao walileta ubishi. Watu kama Abushiri bin Salim bin Harith na Mkwawa walikataa kutawaliwa na Mjerumani. Baba yake Kleist Sykes, Sykes Mbuwane na wazulu wenzake kutoka kijiji cha Kwa Likunyi Msumbiji wakaletwa kuwashikisha adabu wakina Mkwawa na Abushiri ili wakubali utawala wa Mjerumani na kuwa nchi yao ni milki ya Kaizari wa Ujerumani. Abushiri alinyongwa mwaka 1889 na Mkwawa alijiua mwaka 1894. Sykes Mbuwane alifariki katika mto Ruaha wakati wanarudi kutoka kupambana na Mkwawa. Mwanae, Kleist Sykes, aliyemzaa na Mnyaturu nae alijiunga na jeshi la Mjerumani.

Baada ya vita ya kwanza ya dunia, nchi zilizokuwa makoloni ya ujerumani yakawekwa chini ya uangalizi wa League of Nations. League of Nations ikazikabidhi nchi hizo kwa nchi zilizoshinda Vita ili wazisimamie lakini sio kuzimiliki. German East Africa ikagawanywa na sehemu moja ikakabidhiwa kwa Uingereza ambao wakaibadilisha jina na kuiita Tanganyika. Kwa mntika hii, Muingereza hajawahi kukaribishwa na muafrika aliyeishi Tanganyika ili aje kuwatawala. Aidha, hajawahi kupigana vita ili aitawale Tanganyika. Vita yake na Von Lettow ilikuwa ni kati yake na Ujerumani, sio waafrika waliokuwa chini ya himaya ya Ujerumani. Ni kwa sababu hiyo Tanganyika iliitwa Mandate Territory (baadae ikawa a United Nations Trust Territory baada ya vita kuu ya pili). Mwaka 1961, Trust Territory ya Tanganyika ikawa nchi huru kamili lakini Malkia Elizabeth akageuka kuwa Malkia wa Tanganyika ( mfumo kama wa Australia na Canada). Mwaka 1962, Tanganyika ilipitisha Katiba ya Jamhuri, Tanganyika ikawa Jamhuri ndani ya Jumuia ya Madola. Uthibitisho wa kuwa Uingereza ilikuwa mlezi tuu na sio mkoloni kwa Tanganyika ni barua za TANU na safari za Nyerere kwenda New York kudai uhuru wao. Ratiba ya Uhuru wa Tanganyika ilitayarishwa na Umoja wa Mataifa na sio Uingereza.

Nimeulizwa pia kwa nini tunazungumzia serikali ya "kikoloni" kama nchi haikuwa koloni. Uingereza iliisimamia nchi zote zilizokuwa chini yake ( Dominions, Crown colonies, Protectorates na Trust Territory) chini ya mfumo mmoja wa utawala wa kikoloni (colonial administration). Kuwa chini ya mfumo huu haukubadilisha status ya eneo husika. Afrika ya Kusini (dominion), India na Kenya (colonies), Zanzibar, Nyasaland na Uganda (Protectorates) na Tanganyika( United Nations Trust territory) zote zilitawaliwa ( administered sio ruled) katika mfumo wa kikoloni. Ndio maana tupozungumzia utawala uliokuwepo Tanganyika tunauita utawala wa kikoloni ingawa Tanganyika haikuwa koloni.

Amandla...

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

cc. Nguruvi3
 
Kijana nianze kwa kukupongeza, uko tofauti sana na wafanya mizaha kama Nguruvi3 au bingwa wa matusi na udini Azarel nadhani kwasababu ya elimu na silka, kwa maana nyingine wangekuwa wanakuachia nafasi ya kunakasha badala ya wao kuja kueleza chuki, ghadhabu na uadui wao kwasababu haiwasaidii, nadhani tuwapuuze japo umetengeneza mafungamo kiasi unam Cc Nguruvi3 katika mjadala ambao yeye anauita wa wazi lakini kishachagua upande nikomee hapo.

Umeeleza vyema sana kitu ulichojifunza shuleni si vibaya, lakini napenda kukuuliza je huko shuleni walitoa tafsiri ya "koloni"?, ukoloni na utawala wa kikoloni? Ili hoja yako isimame, kisha hapa Chini nakuwekea picha ya Kitabu ulichopendekeza na kukisifia
 
Ni vigumu kuamini kuwa mikutano yote ya TAA na TANU ilikuwa ikifanyiwa nyumbani kwa Abdul Sykes peke yake. Kuna mahali imesemwa watu walikuwa wanakutana kwenye ofisi za Welfare ambako Hamza Mwapachu alikuwa anafanya kazi, Anatouglo (ambako Dennis Phombeah alikuwa akifanya kazi na baadae hata nyumbani kwa Amir Jamal. Aidha, si mikutano yote ilifanyika Mnazi Mmoja na Jangwani. Nyerere alizunguka nchi nzima kwa kutumia gari lililokuwa la Dossa Aziz na kote alifanya mikutano ya hadhara. Mikutano yote hii haikupangwa kwa Abdul Sykes. Sasa Abdul Sykes kuwa na Benzi mwaka 1959 kunasaidia nini katika mjadala huu? Hakuwa peke yake mwenye Benz wakati ule maana hata watoto wa John Rupia walikuwa wanapelekwa shule kwa Benzi.

Kuhusu Katiba ya TANU. Mohammed anasema Earle Seaton wakili mwenye asili ya Bermuda, aliyewatetea wakina Japhet Kirilo kwenye kesi ya ardhi ya wameru, ndie alimshauri Abdul Sykes atumie Katiba ya Ghana ili iwe rahisi kupitishwa na wakoloni. Labda ndivyo Abdul Sykes alivyomsimulia.

Kinachojulikana ni kuwa Earle Seaton alihamia Tanganyika mwaka 1948 baada ya kukaribishwa na Thomas Marealle aliyekutana nae London. Seaton ofisi yake ya uwakili ilikuwa Moshi na aliisimamia kesi ya ardhi ya wameru mwaka 1952. Alihamia Houston Texas mwaka 1953 na hakurudi tena Tanganyika mpaka mwaka 1962. Kwa hiyo, Seaton hakuwepo Tanganyika wakati TANU inazaliwa mwaka 1954.

Kinachojulikana ni kuwa Japhet Kirilo, James Mkande, Abdulwahid Sykes walifanya kazi ya kukamilisha Katiba ya TANU ambayo draft yake ilitayarishwa na Julius Nyerere ambae ali i base kwenye Katiba ya chama cha Labour cha Uingereza na ya chama cha Ghana Convention People's Party. Hii ilikuwa mwaka 1954. Katiba hii ilipitishwa na kikao kilichofanyika Julai 1954 na baadhi ya waliohudhuria ni Julius Nyerere, John Rupia, Abdul wahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, Saidi Tewa, C.O. Millinga, Patrick Kunambi, Joseph Kasella Bantu, Germano Pacha, Joseph Kimalando, Kirilo Japhet, Lameck Bogohe, Selemani Kitwana, Kandoro, Kisung'uta Gabora na Abubakari Irangi. Hawa walitoka sehemu zote za Tanganyika, sio Gerezani peke yake.

Ni huku kutaka kumfanya Abdul Sykes kuwa steling wa kila kitu kilichotokea katika kuzaliwa kwa TANU ndiko tunakokupinga. Sisi tunaamini kuwa ingawa Julius Nyerere alikuwa ndio sura ya TANU, asingefika kokote bila kupata ushirikiano wa wakina Sykes, Aziz, Chaurembo, Kyaruzi, Kirilo, Phombeah na wengine wengi. Tunapinga hata yeye kufanywa ndio alpha na omega ya juhudi za kutafuta uhuru. Tunaamini kuwa juhudi zile zilifanikishwa na watu wengi bila kujali tofauti zao za dini kabila, elimu, utaifa na hata rangi. Wanyasa kama Dennis Phombeah na waganda Erica Fiah ambae mwaka 1934 alianzisha the African Commercial Association mwaka 1936 ikabadilisha jina na kuwa the Tanganyika African Welfare and Commercial Association. Ni aibu kuwa watu kama Erica Fiah hawajapewa heshima wanayostahili.

Amandla...

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

cc. Nguruvi3
 
Kuna nini cha ajabu hapo? Kwani kila kitu alichoandika ni lazima kikubaliwe? Wengi walikuwa hawatofautishi kati ya rule na administration. Huyu ni mmojawapo.

Nguruvi3 ni mtu ninaemheshimu sana kwa umakini wake, ujengaji wake wa hoja na anajua mambo mengi kuliko mimi. Kwenye huu mjadala ninakubaliana na maandiko yake kwa kiasi kikubwa.

Kwangu mimi wenye matatizo ni nyinyi ambao hamtaki Mohammed Said akosolewe kwa sababu mnazozielewa wenyewe.

Amandla...

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

cc. Nguruvi3
 
Baba yake Kleist Sykes, Sykes Mbuwane na wazulu wenzake kutoka kijiji cha Kwa Likunyi Msumbiji wakaletwa kuwashikisha adabu wakina Mkwawa na Abushir
Kwahio pamoja na kukumbuka Ukoo huu kwa kupigania Uhuru pia wasisahau sana kuukumbuka ukoo huu huu kwa kutuletea ukoloni kwa kupingana na wapigania uhuru wa hapo Mwanzo ? Yaani tukumbuke historia bila kuwa na selective amnesia...
 
Ni vigumu kuamini kuwa mikutano yote ya TAA na TANU ilikuwa ikifanyiwa nyumbani kwa Abdul Sykes peke yake. Kuna mahali imesemwa watu walikuwa wanakutana kwenye ofisi za Welfare ambako Hamza Mwapachu alikuwa anafanya kazi, Anatouglo (ambako Dennis Phombeah alikuwa akifanya kazi na baadae hata nyumbani kwa Amir Jamal. Aidha, si mikutano yote ilifanyika Mnazi Mmoja na Jangwani.
Tunakungumiziwa tu kuwa ni nyumbani kwa Abdul Sykes
Nyerere alizunguka nchi nzima kwa kutumia gari lililokuwa la Dossa Aziz na kote alifanya mikutano ya hadhara. Mikutano yote hii haikupangwa kwa Abdul Sykes.
Kwa gari ya Dossa Aziz. Hakuna ubishi kwasababu ushahidi usio na shaka upo
Sasa Abdul Sykes kuwa na Benzi mwaka 1959 kunasaidia nini katika mjadala huu?
Inashangaza sana, just to make him relevant kwasababu hakuna mahali nje ya Gerezani ambako Abdul Sykes amehutubia mkutano.
Hakuwa peke yake mwenye Benz wakati ule maana hata watoto wa John Rupia walikuwa wanapelekwa shule kwa Benzi.
Hana hoja anatafuta la kuandika tu na hii kupoteza hoja kwamba hatujui Babu yake alikuwa na cheo gani TRAU, hajazungumzia na hata zungumzia kwasababu inaelekea alikuwa na 'miraba' minne tu !
Kuhusu Katiba ya TANU. Mohammed anasema Earle Seaton wakili mwenye asili ya Bermuda, aliyewatetea wakina Japhet Kirilo kwenye kesi ya ardhi ya wameru, ndie alimshauri Abdul Sykes atumie Katiba ya Ghana ili iwe rahisi kupitishwa na wakoloni. Labda ndivyo Abdul Sykes alivyomsimulia.
Abdukl aliiangalia tu kama ni hivyo, aliyeifanyia kazi ni Nyerere. Abdul Sykes hakuwa na uwezo wa kielimu wa kuifanyia kazi katiba.
Kinachojulikana ni kuwa Earle Seaton alihamia Tanganyika mwaka 1948 baada ya kukaribishwa na Thomas Marealle aliyekutana nae London. Seaton ofisi yake ya uwakili ilikuwa Moshi na aliisimamia kesi ya ardhi ya wameru mwaka 1952. Alihamia Houston Texas mwaka 1953 na hakurudi tena Tanganyika mpaka mwaka 1962. Kwa hiyo, Seaton hakuwepo Tanganyika wakati TANU inazaliwa mwaka 1954.
Ataweka picha kuua hoja
Kinachojulikana ni kuwa Japhet Kirilo, James Mkande, Abdulwahid Sykes walifanya kazi ya kukamilisha Katiba ya TANU ambayo draft yake ilitayarishwa na Julius Nyerere ambae ali i base kwenye Katiba ya chama cha Labour cha Uingereza na ya chama cha Ghana Convention People's Party. Hii ilikuwa mwaka 1954. Katiba hii ilipitishwa na kikao kilichofanyika Julai 1954 na baadhi ya waliohudhuria ni Julius Nyerere, John Rupia, Abdul wahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, Saidi Tewa, C.O. Millinga, Patrick Kunambi, Joseph Kasella Bantu, Germano Pacha, Joseph Kimalando, Kirilo Japhet, Lameck Bogohe, Selemani Kitwana, Kandoro, Kisung'uta Gabora na Abubakari Irangi. Hawa walitoka sehemu zote za Tanganyika, sio Gerezani peke yake.
Ahsante na harudi hapa , ataongelea uhasidi na alivyoelezwa nguo za maji. Hajibu hoja
Ni huku kutaka kumfanya Abdul Sykes kuwa steling wa kila kitu kilichotokea katika kuzaliwa kwa TANU ndiko tunakokupinga.
Ni hivi katika mkutano wa Arnatouglo ambao Mohamed anasema Abdul alimwachia Mwalimu si kweli. Abdul alishindwa la kama angemwachia basi angejitoa. Kuanzia hapo funda likambana na ndio ukawa mwanzo wa mwisho na Abdulwahid Sykes hakuwahi kuwa hata DC.
Mohamed anachokifanya ni kumkuza Abdul kwa gharama ya Nyerere, kumtweza tu Nyerere
Sisi tunaamini kuwa ingawa Julius Nyerere alikuwa ndio sura ya TANU, asingefika kokote bila kupata ushirikiano wa wakina Sykes, Aziz, Chaurembo, Kyaruzi, Kirilo, Phombeah na wengine wengi. Tunapinga hata yeye kufanywa ndio alpha na omega ya juhudi za kutafuta uhuru.
Ndio maana tunaikataa historia ya Kivukoni kwasababu ina uchechefu. Mtu kama John Rupia alishiriki sana Mzee wa watu leo hatuwezi kusema alikuwa Nyerere.
Tunaamini kuwa juhudi zile zilifanikishwa na watu wengi bila kujali tofauti zao za dini kabila, elimu, utaifa na hata rangi. Wanyasa kama Dennis Phombeah na waganda Erica Fiah ambae mwaka 1934 alianzisha the African Commercial Association mwaka 1936 ikabadilisha jina na kuwa the Tanganyika African Welfare and Commercial Association. Ni aibu kuwa watu kama Erica Fiah hawajapewa heshima
Ni aibu sana hata watu kama Dossa kukosa kutambuliwa kwa ukubwa wao. Ni aibu sana akina Japhet Kirilo hawatwaji wala kuwa na alama zao. Watu kama akina Kasanga Tumbo .

Wapo waliomenyeka hawatambuliwi. Hili ni moja ya mapungufu kwamba hakukufanyika jitihada za lazima za kuwatambua washirika baada ya uhuru.
 
Kuna nini cha ajabu hapo? Kwani kila kitu alichoandika ni lazima kikubaliwe? Wengi walikuwa hawatofautishi kati ya rule na administration. Huyu ni mmojawapo.

Nguruvi3 ni mtu ninaemheshimu sana kwa umakini wake, ujengaji wake wa hoja na anajua mambo mengi kuliko mimi. Kwenye huu mjadala ninakubaliana na maandiko yake kwa kiasi kikubwa.

Kwangu mimi wenye matatizo ni nyinyi ambao hamtaki Mohammed Said akosolewe kwa sababu mnazozielewa wenyewe.

Amandla...

Bwana Mdogo Fundi Mchundo

cc. Nguruvi3
Kaka Amandla naomba tafsiri na utuwekee tofauti ya 1. U koloni 2. Koloni 3. Utawala wa kikoloni kisha utuhusianishie na mada hii ya dada Sky Eclat
 
Ukosoaji kama huo wa para ya mwisho ndio muhimu, kwamba Mohamed Said kaandika 1951 kinyume na uhalisia
Lakini pili mbona hukuhoji kina kimambo na vitabu vyao vya 1969 ambavyo haviwataji waasisi wa TAA?
Makala...
Kuna kitu kinanifurahisha hapa.

Kuna juhudi kubwa sana inafanyika ya kuokoteza historia hapa na pale na bahati nzuri ni kuwa wanatumia vyanzo vyangu ambavyo mimi nimeweka kutia nguvu niliyopata kutoka kwa Nyaraka za Sykes.

Lakini nadhani wao hili hawalijui na kama nisemavyo siku zote kutokujua ni katika silka ya ubinadamu hakuna anaejua kila kitu ila Allah mwenyewe.

Tuanze juu kichwani.

Kabla mimi sijamleta Abdul Sykes hakuna yeyote katika hao wanaonishambuia mimi alikuwa anamjua.

Wala hawakuwa wanajua ilikuwaje Nyerere akawa maarufu Dar es Salaam ilhali yeye ni mgeni mtu kutoka bara tena bara ya mbali sana.

Historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha Kivukoni ndiyo ilikuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nyerere anazuka.

Mimi nikifanya rejea ya kitabu cha Judith Listowel na Nyaraka za Sykes ndiye niliyemrejesha kwa mfano Denis Phombeah kuwa kadi yake ya TANU ni No. 5.

Wengi walishangaa walikuwa hawajapata kusikia jina hili.

Sikuiishia hapa sasa nikifanya rejea za Nyaraka za Sykes nikaeleza safari ya Phombeah na Ally Sykes kwenda Southern Rhodesia (Zambia) mwaka wa 1953.

Naweka link hapo chini.

Ilinichukua karibu miaka 20 kuipata picha ya Phombeah na aliyenipatia ni Ahmed Rajab kutoka kwa mwanae Gray Phombeah.

Mikutano ya siri ikifanyika baada ya TANU kuundwa na kabla ile 1953/54 ilikuwa kwa Abdul Sykes na kamati hii ni mbali na TAA Political Subcommitee ya 1950 ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hapa tumuongeze Earle Seaton katika hii kamati.

Hakuna aliyekuwa anajua historia ya Seaton na Abdul Sykes na mchango wa Seaton katika hii kamati na mapendekezo ya katiba hadi mimi niipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii nimepata katika Nyaraza za Sykes.

Leo hawa ndiyo wa kunifundisha mimi historia ya Earle Seaton?
Hii historia yote haikuwapo kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Walikuwa wapi?
Nakuongezea kitu hapa.

Huo urafiki wa Seaton, Marealle wamuongeze na Abdul Sykes.
David Marealle alikuwa jirani yangu iko siku nimemsikia anasema.

''Walionipokea mimi mara ya kwanza nakuja Dar es Salaam ni hawa akina Sykes,'' anamnyoshea kidole Abbbas Sykes aliyenipeleka kwake.

Nimesoma barua za Marealle kwa akina Sykes lakini sikuzitumia katika kitabu kwa kuwa zilikuwa na faragha baina yao.

Hizi barua zina mambo kaka.

Kamati hii TAA Political Subcommitte baada ya kutoka mapendekezo ya katiba Twining akaisambaratisha kwa kuwapa uhamisho Dr. Kyaruzi na Hamza Mwapachu.

Kyaruzi akapelekwa Kingolwira kisha Nzega na Mwapachu kisiwani Nansio.
Hii 1951.

Mikutano ya Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu wamesoma kutoka kwangu nami nimepata kutoka kwa Judith Listowel na Judith Listowel huwezi kuamini katoka katika mswada wa Dr. Kyaruzi, The Muhaya Doctor,'' na kaweka katika kwenye kitabu chake ''word to word,'' ndani ya kitabu hicho.

Ninao huu mswada katika Maktaba yangu.

Turejee kwa Phombeah.

Phombeah asingeweza kufanya mkutano Arnautoglo hapakuwa na faragha hii kwanza halafu hakuwa mtu wa kamati ya ndani.

Amir Jamal kaja TANU 1958 mkutano gani utafanyika kwa Muhindi na siku zile za mwanzo ninazozizungumza ulikuwa wakati wa Afrika kwa Waafrika?

Erica Fiah.

Kleist Sykes kamweleza kwa kirefu katika mswada wake alioandika kabla ya kifo chake 1949.

Wamsome Daisy Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' wakipenda wasome: ''Kleist Sykes Man of Ideas,'' katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mercedes Benz iliwachoma wale wa 1959 kama inavyowachoma hawa wa leo.
Wakahitimisha kwa kufuta historia yote.

Ati nini kununua Mercedes Benz.
Niliweka makusudi kuwasikiliza.

Hasad, wivu na choyo zimewajaa.

Mercedes kwa vijana hawa wa Karikaoo zilikuwa mbili ya Abdul na ya Abbas Abdulwahab na walikuwa majirani.

Abdulwahab alikuwa kijana wa Kiarabu ambae alikuwa na biashara kubwa ya kuuza maziwa.

Katiba ya TANU ni ya Labour Party wanasema na ya CPP.
Kaka mimi naandika kwa ajili yako.

Hawa wanajifunza historia hii leo mimi nimeishi na watu hawa na wamenifungulia nyaraka zao na mioyo yao na nimeandika papers na makala wala sijui hesabu yake.

Kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile mimi nisingeyajua haya yote.

Na kama nisingenyanyua kalamu kuandika hawa wangebakia na historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Ndipo nakuambia wakati mwingine nawaonea huruma.
Wananukuu yale niliyoandika mimi bila ya kujua.

Hakika mtaka nyingi nasaba humkuta mwingi msiba.

1640966676001.png

Denis Phombeah

Picha zangu zinachoma nyoyo.
Picha zinachoma moyo wa nani? Hivi ukinywa chai London inahusu nini.

Kinachokera ni matumizi ya picha kuficha mapungufu yako kwa hila.
Mfano, tumeona picha ya Babu. Tunakuuliza alikuwa na cheo gani TRAU wewe hujibu unahamia kwenye maongezi na mama yako, yanatuhusu nini sisi. Eleza, Babu alikuwa na cheo gani TRAU
Hushangai ukumbi mzima watu wanaongezeka kusikiliza mnakasha?
Jiulize wanakuja kusoma kejeli, ghadhabu na kebehi?
Hapana wanakuja kusoma hoja. Hakuna kipya katika vitabu vyako! nothing
Watu wanakuja kufunguka pale vitabu vyako vinapotobolewa matundu
Msome Fundi Mchundo , anakutembeza katika vyama vya wafanyakazi na leo kateremsha hoja ya E. Seaton! hujibu , kimyaa . Watu wanafuatilia matundu ya historia si vitabu vyako vipo 22 yrs hakuna jipya.
1959 Abdul Sykes alinunua Mercedes Benz 220 SE.
Uhuru bado.
Dah ndicho watu wanakuja kusikiliza hiki. Inahusu nini hata kama alikuwa na Benz 100
Nyerere kahutubia mikutano ya hadhara baada ya kuundwa TANU 1954.
OK, tuonyeshe mahali ambapo Abdulwahi Sykes alihutubia mkutano hata mmoja tokea akiwa na TAA hadi TANU. Mkutano mmoja tu nje ya Gerezani.

Hoja hapa si Nyerere kwasababu alifanya mikutano nchi nzima na wenzake wakipigania Uhuru
Ushahidi upo.
Hoja hapa ni, je, Abdulwahid Sykes aliwahi kuwa na mkutano kwingine Tanganyika nje ya Gerezani?
Nyerere alipata kuhutubia mkutano wowote kabla ya TANU?
Sina kumbukumbu kwamba aliwahi kuhutubia popote. Je hiyo inajibu hoja kwamba Abdul Sykes hakuwahi kuhutubia mkutano akiwa na TAA au TANU toka azaliwe hadi afariki nje ya Gerezani.

Hapa ndipo wanaotumia akili wanabaini jambo. Mtu anaulizwa hivi Abdul Sykes alikuwahi kuhutubia mkutano wowote nje ya Gerezani kwa maana kwingine Tanganyika?
Kinachotakiwa ni jibu na kama kuna swali la Nyerere lifuate.

Wasomaji Mohamed anakwepa hoja, Abdul Sykes hakuwahi kufanya mkutano hata mmoja nje ya Gerezani.

Hapakuandikwa katiba.

Earle Seaton ndiye aliyempa Abdul ujanja wa "adoption," ya katiba ya Nkrumah iliyopitishwa na Waingereza Ghana ili washindwe kuikataa kwa TANU hapa Tanganyika.
Abdul aliandika? Abdul hakufanya chochote kile kama ilitokea hivyo
Nyerere ndiye aliandika katiba si Abdul wala Kleist.

Fundi Mchundo kaeleza jambo kuhusu Seaton na ujio wake. Umeisoma hoja ile?
Naiona kama kitu kizito !
Wakati huo wala Abdul hajakutana na Nyerere.
Yapo mengi.
Abdul alikutana na Nyerere 1948 siyo miaka ya 50!
Nyerere alikuja mkutano mkuu akiwa katibu wa tawi la Tabora na Msomi ambaye haikuwa rahisi kuwa ignored. Elimu yake ilitosha kumfanya yoyote ajiulize huyu ni nani. Abdul hakumuona?
 
...badala ya wao kuja kueleza chuki, ghadhabu na uadui wao kwasababu haiwasaidii, nadhani tuwapuuze japo umetengeneza mafungamo kiasi unam Cc Nguruvi3 katika mjadala ambao yeye anauita wa wazi lakini kishachagua upande nikomee hapo.
Onyesha wapi chuki na ghadhabu?
Unaweza ku ignore au kupuuza kabisa , kuna button! njia ya pili usijibu

Kitu kimoja nakuhakikishia, mimi si type ya kukaa chini na kusema hewala akili ikinajisiwa

Masalam
 
Back
Top Bottom