Msaada, anayefahamu Salum Abdallah (pichani mwenye mshale ) alikuwa na wadhifa gani TRAU atusaidie tafadhaliView attachment 2062111
Viongozi wa TRAU Salum Abdallah ni huyo kwenye mshale na anaefuatia ni Kassanga Tumbo
Makala...
Kuna kitu kinanifurahisha hapa.
Kuna juhudi kubwa sana inafanyika ya kuokoteza historia hapa na hapa na bahati nzuri ni kuwa wanatumia vyanzo vyangu ambavyo mimi nimeweka kutia nguvu niliyopata kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Lakini nadhani wao hili hawalijui na kama nisemavyo siku zote kutokujua ni katika silka ya ubinadamu hakuna anaejua kila kitu ila Allah mwenyewe.
Tuanze juu kichwani.
Kabla mimi sijamleta Abdul Sykes hakuna yeyote katika hao wanaonishambuia mimi alikuwa anamjua.
Historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha Kivukoni ndiyo ilikuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Mimi nikifanya rejea ya kitabu cha Judith Listowel na Nyaraka za Sykes ndiye niliyemrejesha kwa mfano Denis Phombeah kuwa kadi yake ya TANU ni No. 5.
Sikuhishia hapa sasa nikifanya rejea za Nyaraka za Sykes nikaeleza safari ya Phombeah na Ally Sykes kwenda Southern Rhodesia mwaka wa 1953.
Naweka link hapo chini.
Ilinichukua karibu miaka 20 kuipata picha ya Phombeah na aliyenipatia ni Ahmed Rajab kutoka kwa mwanae Gray Phombeah.
Mikutano ya siri ikifanyika baada ya TANU kuundwa na kabla ile 1953/54 ilikuwa kwa Abdul Sykes na kamati hii ni mbali na TAA Political Subcommitee ya 1950 ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Hapa tumuongeze Earle Seaton.
hakuna aliyekuwa anajua historia ya Seaton na Abdul Sykes na mchango wake katika hii kamati na mapendekezo ya katiba hadi mimi niipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii nimepata katika Nyaraza za Sykes.
Leo hawa ndiyo wa kunifundisha mimi historia ya Earle Seaton?
Hii historia yote haukuwapo kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
Nakuongezea kitu hapa.
Huo urafiki wa Seaton, Marealle wamuongeze na Abdul Sykes.
David Marealle alikuwa jirani yangu iko siku nimemsika anasema.
''Walionipokea mimi mara ya kwanza nakuja Dar es Salaam ni hawa akina Sykes,'' anamnyoshea kidole Abbbas Sykes aliyenipeleka kwake.
Nimesoma barua za Marealle kwa akina Sykes lakini sikuzitumia katika kitabu kwa kuwa zilikuwa na faragha baina yao.
Hizi barua zina mambo kaka.
Kamati hii TAA Political Subcommitte baada ya kutoka mapendekezo ya katiba Twining akaisambaratisha kwa kuwa uhamisho Dr. Kyaruzi na Hamza Mwapachu.
Mikutano ya Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu wamesoma kutoka kwangu nani nimepata kutoka kwa Judith Listowel na pia nimekazia kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Phombeah asingeweza kufanya mkutano Arnautoglo hapakuwa na faragha hii kwanza halafu hakuwa mtu wa kamati ya ndani.
Amir Jamal kaja TANU 1958 mkutano gani utafanyika kwa Muhindi na sku zile za mwanzo ninazozizungumza ulikuwa wakati wa Afrika kwa Waafrika?
Erica Fiah.
Kleist Sykes kamweleza kwa kirefu katika mswada wake alioandika kabla ya kifo chake 1949.
Wamsoma Daisy Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' wakipenda wanisome mimi: ''Kleist Sykes Man of Ideas,'' katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mercedes Benz iliwachoma wale wa 1959 kama inavyowachoma haw wa leo ati nini.
Mercedes zilikuwa mbili ya Abdul na ya Abbad Abdulwahab kijana wa Kiarabu ambae alikuwa na biashara kubwa ya kuuza maziwa.
Katiba ya TANU ni ya Labour Party wanasema na ya CPP.
Kaka mimi naandika kwa ajili yako.
Hawa wanajifunza historia hii leo mimi nimeishi na watu hawa na wamenifungulia nyaraka zao na mioyo yao.
Kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile mimi nisingeyajua haya yote.
Na kama nisingenyanyua kalamu kuandika hawa wangebakia na historia ya Kimambo na Temu.
Kaka Amandla naomba tafsiri na utuwekee tofauti ya 1. U koloni 2. Koloni 3. Utawala wa kikoloni kisha utuhusianishie na mada hii ya dada Sky Eclat
Ahsante sana, angalia hapo kati ya Thomas na David. Hajui tofauti ya hawa wawili na hataki kujifunzaMimi nimesema Earle E Seaton, mwanasheria mzaliwa wa Bermuda, alumni wa Howard University alialikwa na Thomas Marealle kuja Tanganyika baada ya kukutana nae London, Uingereza. Walikutana wakati Seaton anasomea sheria London University na Thomas Marealle akiwa anasoma London School of Economics. Wewe unaleta ya DAVID Marealle na kuwa alipokewa na Abbas Sykes Dar es Salaam? David na Thomas wapi na wapi?
Tena alitumia neno ''yote'' hakuacha nafasiSasa kama unajua kuwa kuna mikutano ilifanyika Welfare kwa Hamza Mwapachu kwa nini ulitaka kutuaminisha kuwa mikutano yote ilifanyika kwa Abdul Sykes peke yake? Unajichanganya mwenyewe.
Hataki kukubali kuwa Nyerere ali tranform chama kutoka Familia kuwa wanachamaUnasema Katiba ya TANU ni ya Labour Party wakati awali ulituambia kuwa Seaton alimshauri mwandishi wa katiba hiyo, Abdul Sykes a copy ya Nkrumah ili ikubaliwe na wazungu! Nkrumah alikuwa Labour Party? Chama cha CPP ni cha Gold Coast, na katiba yake na ya Labour Party ya Uingereza ilitumiwa na Nyerere kutayarisha draft ya Katiba ya TANU. Na hili nimelisema.
Sijui ana uhakika gani kama hakukuwa na 'underground'' yeye anaamini zilikuwepo kwa Sykes tuUnasema wasingeweza kufanya mikutano kwa Amir Jamal kwa sababu alijiunga na TANU 1958. Unajuaje kama hakuwa shabiki wa TANU wa chinichini kabla ya kujiunga rasmi? Unataka kutuambia kuwa wakati unaozungumzia waafrika walikuwa wanazuiwa kwenda kwa wahindi? Na mikutano ilipamba moto baada ya TANU kuzaliwa na haikuishia Anatouglou na Jangwani.
Kambona hakutendewa haki!Mmojawapo wa watu waliochangia sana kuimarika kwa TANU ni Oscar Kambona ambae alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU aliambiwa kuwa mshahara wake utatokana na wanachama atakaowaingiza kwenye chama. Leo nani anamtaja? Nani hata anajua mke wake Flora aliishia wapi? Wakina Sykes wana mtaa, lakini Kambona hata kichochoro hana. Na ingekuwa ni kwa sababu ya kesi ya uhaini basi hata Bibi Titi asingekuwa na mtaa!
Mohamed hakubali kukosolewa na hapa inatia shaka sana. Moja ya kazi za academician ni kukubali kukosolewa, kukubali mitazamo tofauti na kukubali kukutokubaliana kwa heshima na adabuIshara kubwa ya mtu aliye elimika ni kukubali kukosolewa, kurekebisha alichokiandika kama taarifa nyingine zitatokeza nakutambua kuwa anachojua yeye ni sehemu tu ya ukweli uliopo.
Dive,uliaFather of the nation legacy Yake inapotea hivi hivi View attachment 2064310View attachment 2064311View attachment 2064312
Acha Umbea.Makala...
Kuna kitu kinanifurahisha hapa.
Kuna juhudi kubwa sana inafanyika ya kuokoteza historia hapa na pale na bahati nzuri ni kuwa wanatumia vyanzo vyangu ambavyo mimi nimeweka kutia nguvu niliyopata kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Lakini nadhani wao hili hawalijui na kama nisemavyo siku zote kutokujua ni katika silka ya ubinadamu hakuna anaejua kila kitu ila Allah mwenyewe.
Tuanze juu kichwani.
Kabla mimi sijamleta Abdul Sykes hakuna yeyote katika hao wanaonishambuia mimi alikuwa anamjua.
Wala hawakuwa wanajua ilikuwaje Nyerere akawa maarufu Dar es Salaam ilhali yeye ni mgeni mtu kutoka bara tena bara ya mbali sana.
Historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha Kivukoni ndiyo ilikuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nyerere anazuka.
Mimi nikifanya rejea ya kitabu cha Judith Listowel na Nyaraka za Sykes ndiye niliyemrejesha kwa mfano Denis Phombeah kuwa kadi yake ya TANU ni No. 5.
Wengi walishangaa walikuwa hawajapata kusikia jina hili.
Sikuiishia hapa sasa nikifanya rejea za Nyaraka za Sykes nikaeleza safari ya Phombeah na Ally Sykes kwenda Southern Rhodesia (Zambia) mwaka wa 1953.
Naweka link hapo chini.
Ilinichukua karibu miaka 20 kuipata picha ya Phombeah na aliyenipatia ni Ahmed Rajab kutoka kwa mwanae Gray Phombeah.
Mikutano ya siri ikifanyika baada ya TANU kuundwa na kabla ile 1953/54 ilikuwa kwa Abdul Sykes na kamati hii ni mbali na TAA Political Subcommitee ya 1950 ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Hapa tumuongeze Earle Seaton katika hii kamati.
Hakuna aliyekuwa anajua historia ya Seaton na Abdul Sykes na mchango wa Seaton katika hii kamati na mapendekezo ya katiba hadi mimi niipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii nimepata katika Nyaraza za Sykes.
Leo hawa ndiyo wa kunifundisha mimi historia ya Earle Seaton?
Hii historia yote haikuwapo kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
Walikuwa wapi?
Nakuongezea kitu hapa.
Huo urafiki wa Seaton, Marealle wamuongeze na Abdul Sykes.
David Marealle alikuwa jirani yangu iko siku nimemsikia anasema.
''Walionipokea mimi mara ya kwanza nakuja Dar es Salaam ni hawa akina Sykes,'' anamnyoshea kidole Abbbas Sykes aliyenipeleka kwake.
Nimesoma barua za Marealle kwa akina Sykes lakini sikuzitumia katika kitabu kwa kuwa zilikuwa na faragha baina yao.
Hizi barua zina mambo kaka.
Kamati hii TAA Political Subcommitte baada ya kutoka mapendekezo ya katiba Twining akaisambaratisha kwa kuwapa uhamisho Dr. Kyaruzi na Hamza Mwapachu.
Kyaruzi akapelekwa Kingolwira kisha Nzega na Mwapachu kisiwani Nansio.
Hii 1951.
Mikutano ya Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu wamesoma kutoka kwangu nami nimepata kutoka kwa Judith Listowel na Judith Listowel huwezi kuamini katoka katika mswada wa Dr. Kyaruzi, The Muhaya Doctor,'' na kaweka katika kwenye kitabu chake ''word to word,'' ndani ya kitabu hicho.
Ninao huu mswada katika Maktaba yangu.
Turejee kwa Phombeah.
Phombeah asingeweza kufanya mkutano Arnautoglo hapakuwa na faragha hii kwanza halafu hakuwa mtu wa kamati ya ndani.
Amir Jamal kaja TANU 1958 mkutano gani utafanyika kwa Muhindi na siku zile za mwanzo ninazozizungumza ulikuwa wakati wa Afrika kwa Waafrika?
Erica Fiah.
Kleist Sykes kamweleza kwa kirefu katika mswada wake alioandika kabla ya kifo chake 1949.
Wamsome Daisy Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' wakipenda wasome: ''Kleist Sykes Man of Ideas,'' katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mercedes Benz iliwachoma wale wa 1959 kama inavyowachoma hawa wa leo.
Wakahitimisha kwa kufuta historia yote.
Ati nini kununua Mercedes Benz.
Niliweka makusudi kuwasikiliza.
Hasad, wivu na choyo zimewajaa.
Mercedes kwa vijana hawa wa Karikaoo zilikuwa mbili ya Abdul na ya Abbas Abdulwahab na walikuwa majirani.
Abdulwahab alikuwa kijana wa Kiarabu ambae alikuwa na biashara kubwa ya kuuza maziwa.
Katiba ya TANU ni ya Labour Party wanasema na ya CPP.
Kaka mimi naandika kwa ajili yako.
Hawa wanajifunza historia hii leo mimi nimeishi na watu hawa na wamenifungulia nyaraka zao na mioyo yao na nimeandika papers na makala wala sijui hesabu yake.
Kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile mimi nisingeyajua haya yote.
Na kama nisingenyanyua kalamu kuandika hawa wangebakia na historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha CCM Kivukoni.
Ndipo nakuambia wakati mwingine nawaonea huruma.
Wananukuu yale niliyoandika mimi bila ya kujua.
Hakika mtaka nyingi nasaba humkuta mwingi msiba.
View attachment 2064207
Denis Phombeah
Kisa cha Ally Sykes, Denis Phombeah na Kenneth Kaunda Tanganyika na mkutano wa wapigania uhuru kusini ya sahara 1953
KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953 SEHEMU YA KWANZA Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa African National Congress (ANC) na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini...www.jamiiforums.com
KAMWE...!!!Father of the nation legacy Yake inapotea hivi hivi View attachment 2064310View attachment 2064311View attachment 2064312
So what, nawewe umeokoteza picha eehDive,
Nakuwekea picha za Mwalimu ambazo nimeweza kuzikusanya katika utafiti wangu na kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nikienda nyuma sana miaka ya mwanzoni wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika:
View attachment 2064382
Kulia Ali Msham na aliyekaa kwenye meza ni Mwalimu Julius Nyerere.
View attachment 2064384
Kulia Julius Nyerere, John Rupia na Sheikh Suleiman Takadir na hao waliosimama nyuma ni Bantu Group wahamaishaji na walinzi wa viongozi wakiwa na silaha za jadi
View attachment 2064392
Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere,
Sheikh Mohamed Ramia na Idd Faiz Mafungo
View attachment 2064387
Kulia Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed kushoto Bi. Titi bin Mzee na katikati Julius Nyerere wakimsindikiza safari ya kwanza UNO
View attachment 2064390
We we wee....!Msaada wanaJF, kuna picha ya Salum Abdallah. Nani anajua huyu Mzee alikuwa na wadhifa gani TRAU?
πππππUmefurahi sana kijana, kulikoni?
Umepata kumsikiliza Nyerere katika interview hiyo?
Mimi nilishamfahamu siku nyingi, kuna vitu anavikwepa sana na ndio maana hawezi kuquote maneno yangu KABISA na hadhubutu.Katika picha anazoleta Mohamed Said hapo juu hakuna mpya hata moja
Kila uzi anaweka picha hizo hizo, sasa mtu atajiuliza ni kwanini?
Jibu ni rahisi anatumia picha ni ''bamboozle'' yaani kama kiini macho pale hoja inapomfika pabaya
Kwa mfano, hutamuona akirudisha picha ya Babu yake Salum Abdallah kwavile tayari amebaini hana jibu ni upi wadhifa wa Mzee wake?
Pili anataka kufifisha hoja ya Fundi Mchundo kuhusu Thomas na David
Na mwisho amebaini Benz si deal wapo waliotumia nyakati hizo
Someni between the lines wanaJF, si kumeza tu! chambua mchele na mashudu
We we wee....!
Kuna jamaa alishamuuliza huyu Mzee hilo swali, Mzee atalikwepa mpaka mwisho, hebu atuwekee picha ya Baba yake na hasa akiwa hapo Ofisini TRAU.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Katika picha anazoleta Mohamed Said hapo juu hakuna mpya hata moja
Kila uzi anaweka picha hizo hizo, sasa mtu atajiuliza ni kwanini?
Jibu ni rahisi anatumia picha ni ''bamboozle'' yaani kama kiini macho pale hoja inapomfika pabaya
Kwa mfano, hutamuona akirudisha picha ya Babu yake Salum Abdallah kwavile tayari amebaini hana jibu ni upi wadhifa wa Mzee wake?
Pili anataka kufifisha hoja ya Fundi Mchundo kuhusu Thomas na David
Na mwisho amebaini Benz si deal wapo waliotumia nyakati hizo
Someni between the lines wanaJF, si kumeza tu! chambua mchele na mashudu
KAMWE...!!!
This man was an Icon and he still is
The whole World knows and appreciate him
Ni waswahili wachache tu wakishalewa wali wa manjano wanakuja kuwehuka huku