Kuna juhudi kubwa sana inafanyika ya kuokoteza historia hapa na hapa na bahati nzuri ni kuwa wanatumia vyanzo vyangu ambavyo mimi nimeweka kutia nguvu niliyopata kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Lakini nadhani wao hili hawalijui na kama nisemavyo siku zote kutokujua ni katika silka ya ubinadamu hakuna anaejua kila kitu ila Allah mwenyewe.
Tuanze juu kichwani.
Kabla mimi sijamleta Abdul Sykes hakuna yeyote katika hao wanaonishambuia mimi alikuwa anamjua.
Historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha Kivukoni ndiyo ilikuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Mimi nikifanya rejea ya kitabu cha Judith Listowel na Nyaraka za Sykes ndiye niliyemrejesha kwa mfano Denis Phombeah kuwa kadi yake ya TANU ni No. 5.
Sikuhishia hapa sasa nikifanya rejea za Nyaraka za Sykes nikaeleza safari ya Phombeah na Ally Sykes kwenda Southern Rhodesia mwaka wa 1953.
Naweka link hapo chini.
Ilinichukua karibu miaka 20 kuipata picha ya Phombeah na aliyenipatia ni Ahmed Rajab kutoka kwa mwanae Gray Phombeah.
Mikutano ya siri ikifanyika baada ya TANU kuundwa na kabla ile 1953/54 ilikuwa kwa Abdul Sykes na kamati hii ni mbali na TAA Political Subcommitee ya 1950 ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Hapa tumuongeze Earle Seaton.
hakuna aliyekuwa anajua historia ya Seaton na Abdul Sykes na mchango wake katika hii kamati na mapendekezo ya katiba hadi mimi niipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii nimepata katika Nyaraza za Sykes.
Leo hawa ndiyo wa kunifundisha mimi historia ya Earle Seaton?
Hii historia yote haukuwapo kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
Nakuongezea kitu hapa.
Huo urafiki wa Seaton, Marealle wamuongeze na Abdul Sykes.
David Marealle alikuwa jirani yangu iko siku nimemsika anasema.
''Walionipokea mimi mara ya kwanza nakuja Dar es Salaam ni hawa akina Sykes,'' anamnyoshea kidole Abbbas Sykes aliyenipeleka kwake.
Nimesoma barua za Marealle kwa akina Sykes lakini sikuzitumia katika kitabu kwa kuwa zilikuwa na faragha baina yao.
Hizi barua zina mambo kaka.
Kamati hii TAA Political Subcommitte baada ya kutoka mapendekezo ya katiba Twining akaisambaratisha kwa kuwa uhamisho Dr. Kyaruzi na Hamza Mwapachu.
Mikutano ya Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu wamesoma kutoka kwangu nani nimepata kutoka kwa Judith Listowel na pia nimekazia kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Phombeah asingeweza kufanya mkutano Arnautoglo hapakuwa na faragha hii kwanza halafu hakuwa mtu wa kamati ya ndani.
Amir Jamal kaja TANU 1958 mkutano gani utafanyika kwa Muhindi na sku zile za mwanzo ninazozizungumza ulikuwa wakati wa Afrika kwa Waafrika?
Erica Fiah.
Kleist Sykes kamweleza kwa kirefu katika mswada wake alioandika kabla ya kifo chake 1949.
Wamsoma Daisy Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' wakipenda wanisome mimi: ''Kleist Sykes Man of Ideas,'' katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mercedes Benz iliwachoma wale wa 1959 kama inavyowachoma haw wa leo ati nini.
Mercedes zilikuwa mbili ya Abdul na ya Abbad Abdulwahab kijana wa Kiarabu ambae alikuwa na biashara kubwa ya kuuza maziwa.
Katiba ya TANU ni ya Labour Party wanasema na ya CPP.
Kaka mimi naandika kwa ajili yako.
Hawa wanajifunza historia hii leo mimi nimeishi na watu hawa na wamenifungulia nyaraka zao na mioyo yao.
Kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile mimi nisingeyajua haya yote.
Na kama nisingenyanyua kalamu kuandika hawa wangebakia na historia ya Kimambo na Temu.
Unasogeza tu magoli Mohammed. Hii unataka kutuaminisha kuwa Dar es Salaam nzima uliyejua habari za Abdul Sykes ni wewe tu?
Mimi nimesema Earle E Seaton, mwanasheria mzaliwa wa Bermuda, alumni wa Howard University alialikwa na Thomas Marealle kuja Tanganyika baada ya kukutana nae London, Uingereza. Walikutana wakati Seaton anasomea sheria London University na Thomas Marealle akiwa anasoma London School of Economics. Wewe unaleta ya DAVID Marealle na kuwa alipokewa na Abbas Sykes Dar es Salaam? David na Thomas wapi na wapi?
Kama vile wewe unavyozungumzia benz ya Sykes, mimi naweza kukuambia kuwa nilikuwa napanda benz ya mzee John Rupia.
Sasa kama unajua kuwa kuna mikutano ilifanyika Welfare kwa Hamza Mwapachu kwa nini ulitaka kutuaminisha kuwa mikutano yote ilifanyika kwa Abdul Sykes peke yake? Unajichanganya mwenyewe.
Unasema Katiba ya TANU ni ya Labour Party wakati awali ulituambia kuwa Seaton alimshauri mwandishi wa katiba hiyo, Abdul Sykes a copy ya Nkrumah ili ikubaliwe na wazungu! Nkrumah alikuwa Labour Party? Chama cha CPP ni cha Gold Coast, na katiba yake na ya Labour Party ya Uingereza ilitumiwa na Nyerere kutayarisha draft ya Katiba ya TANU. Na hili nimelisema.
Unasema wasingeweza kufanya mikutano kwa Amir Jamal kwa sababu alijiunga na TANU 1958. Unajuaje kama hakuwa shabiki wa TANU wa chinichini kabla ya kujiunga rasmi? Unataka kutuambia kuwa wakati unaozungumzia waafrika walikuwa wanazuiwa kwenda kwa wahindi? Na mikutano ilipamba moto baada ya TANU kuzaliwa na haikuishia Anatouglou na Jangwani.
Wakina Kimambo waliandika Historia ya nchi yetu wakati tunaimba " zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wetu" kwa hiyo si ajabu wao kumkuza sana Nyerere na kuwapuuza watu kama Abdul Sykes na wengine. Mmojawapo wa watu waliochangia sana kuimarika kwa TANU ni Oscar Kambona ambae alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU aliambiwa kuwa mshahara wake utatokana na wanachama atakaowaingiza kwenye chama. Leo nani anamtaja? Nani hata anajua mke wake Flora aliishia wapi? Wakina Sykes wana mtaa, lakini Kambona hata kichochoro hana. Na ingekuwa ni kwa sababu ya kesi ya uhaini basi hata Bibi Titi asingekuwa na mtaa!
Ishara kubwa ya mtu aliye elimika ni kukubali kukosolewa, kurekebisha alichokiandika kama taarifa nyingine zitatokeza nakutambua kuwa anachojua yeye ni sehemu tu ya ukweli uliopo. Hata Stephen Hawkins hakuwahi kusema hakuna mtu wa kumfundisha lolote kuhusu physics. Alikuwa anajifunza kila siku kutoka kwa walimwengu wenzake.
Kuna article imeandikwa na N.J. Westcott inayoitwa " An East African Radical : The Life of Erica Fiah" katika Journal of African History ya mwaka 1981. Sijui Westcott alipewa na nani habari za Fiah?
Makala...
Hii makala niliweka wakati wa majuma yale tukifanya kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.
Nimeunganisha hapa kukuambia kuwa yapo mengi ya kuzingatia hii leo kutoka historia kama hizi:
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA: KISA KILICHOWALIZA WANAWAKE WANNE PEMBENI YA JULIUS NYERERE WAKATI WA KUPIGANIA UHURU
''Kwa kuwa umependa kumbukumbu hizi za nyumbani kwetu Gerezani basi nataka nikupe kisa kilicholeta taharuki kubwa ambayo naelezwa haijapata kutokea katika historia ya TANU na Nyerere labda hadi Baba wa Taifa anaaga dunia.
Siku za mwanzo za TANU viongozi wake walikuwa wakiwa na jambo zito la kujadili walikuwa wakikutana nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Walikuwa wakimaliza shughuli basi inakuwa chakula na vinywaji kujipongeza.
Siku hiyo baada ya kikao wakala chakula cha mchana.
Baada ya kula ghafla Nyerere akaanza kulalamika kuwa tumbo linamkata.
Nyerere akawa anajipindua huku na huku kwa maumivu.
Siku zote TANU walikuwa wakiishi chini ya hofu ya Nyerere kudhuriwa na maadui wa TANU lakini katika chakula kile cha nyumbani kwake hapakuwa na hofu kwani chakula chake kilikuwa kinatoka Kariakoo na kwa watu maalum ambao Market Master, Abdul Sykes akiwafahamu na Mzee Mshume na ndiye akikinunua, mpelekaji wa chakula hicho kwa Mama Maria alikuwa dereva wa TANU, Said Kamtawa maarufu kwa jina Said TANU.
Nyerere kalala kwenye kochi anaugulia na taharuki ikazuka na minong'ono haikuweza kukwepeka.
Nyerere kalishwa sumu!
Sumu Nyerere alishwe nyumbani kwa Abdul Sykes?
Uani jikoni walikuwa mama yake Nyerere Bi. Mgaya, Mama Maria, mama yake Abdul Sykes Bi. Mruguru bint Mussa, mkewe Abdul Sykes, Mama Daisy.
Aliposikia kuwa Nyerere anaumwa baada ya kula chakula kitu cha kwanza kilichomjia ni kuwa mwanae kalishwa sumu akawa sasa mikono kichwani analia na kutembea ua mzima.
Bi. Mgaya anasema Kizanaki na anachanganya na Kiswahili.
Ikawa patashika nguo kuchanika kumtuliza.
Wote waliokula chakula kile walikuwa salama na hawa ni watu waliokuwa wakijuana vizuri na wakiaminiana mwisho wa imani.
Nani anaweza kupenya nyumbani kwa Abdul akampa sumu Nyerere?
Nani?
Mama Daisy ndiye alikua akinihadithia alipomaliza aliinamisha kichwa akasema, ''Mwanangu Mohamed, Abdul na Nyerere wametoka mbali sana na walikuwa zaidi ya ndugu.''
Iko siku nitakileta hapa kisa cha sanduku la fedha la Abdul Sykes kama nilivyokipokea kutoka kwa Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.
Picha ya kwanza ni mama yake Julius Nyerere Bi. Mugaya Nyag'ombe, Bi. Mruguru bint Mussa Mohamed mama yake Abdul Sykes, Ally na Abbas, Mama Maria Nyerere na Bi. Mwamvua bint Mrisho.''
Hivi ndiyo dunia ilivyo.
Mtu anaweza leo akawakejeli hawa wazee wetu apendavyo.
Hakuna wa kumzuia.
Leo ni zaidi ya miaka 70 imepita toka haya yatokee na aliye hai katika hawa ni Mama Maria Nyerere peke yake.
Namshuru Allah kuwa nimeihifadhi historia hii kwa sauti yangu nikihadithia yote na kwa kalamu yangu.
Mimi nimesema Earle E Seaton, mwanasheria mzaliwa wa Bermuda, alumni wa Howard University alialikwa na Thomas Marealle kuja Tanganyika baada ya kukutana nae London, Uingereza. Walikutana wakati Seaton anasomea sheria London University na Thomas Marealle akiwa anasoma London School of Economics. Wewe unaleta ya DAVID Marealle na kuwa alipokewa na Abbas Sykes Dar es Salaam? David na Thomas wapi na wapi?
Sasa kama unajua kuwa kuna mikutano ilifanyika Welfare kwa Hamza Mwapachu kwa nini ulitaka kutuaminisha kuwa mikutano yote ilifanyika kwa Abdul Sykes peke yake? Unajichanganya mwenyewe.
Unasema Katiba ya TANU ni ya Labour Party wakati awali ulituambia kuwa Seaton alimshauri mwandishi wa katiba hiyo, Abdul Sykes a copy ya Nkrumah ili ikubaliwe na wazungu! Nkrumah alikuwa Labour Party? Chama cha CPP ni cha Gold Coast, na katiba yake na ya Labour Party ya Uingereza ilitumiwa na Nyerere kutayarisha draft ya Katiba ya TANU. Na hili nimelisema.
Unasema wasingeweza kufanya mikutano kwa Amir Jamal kwa sababu alijiunga na TANU 1958. Unajuaje kama hakuwa shabiki wa TANU wa chinichini kabla ya kujiunga rasmi? Unataka kutuambia kuwa wakati unaozungumzia waafrika walikuwa wanazuiwa kwenda kwa wahindi? Na mikutano ilipamba moto baada ya TANU kuzaliwa na haikuishia Anatouglou na Jangwani.
Mmojawapo wa watu waliochangia sana kuimarika kwa TANU ni Oscar Kambona ambae alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU aliambiwa kuwa mshahara wake utatokana na wanachama atakaowaingiza kwenye chama. Leo nani anamtaja? Nani hata anajua mke wake Flora aliishia wapi? Wakina Sykes wana mtaa, lakini Kambona hata kichochoro hana. Na ingekuwa ni kwa sababu ya kesi ya uhaini basi hata Bibi Titi asingekuwa na mtaa!
Ishara kubwa ya mtu aliye elimika ni kukubali kukosolewa, kurekebisha alichokiandika kama taarifa nyingine zitatokeza nakutambua kuwa anachojua yeye ni sehemu tu ya ukweli uliopo.
Mohamed hakubali kukosolewa na hapa inatia shaka sana. Moja ya kazi za academician ni kukubali kukosolewa, kukubali mitazamo tofauti na kukubali kukutokubaliana kwa heshima na adabu
Hizi habari za ''hawa wanifundishe, mimi nina.. ' ni grandiose zisizo na haiba ya 'academics'
Bado tunauliza, Salum Abdallah babu yake Mohamed Said alikuwa na cheo gani TRAU?
Dive,
Nakuwekea picha za Mwalimu ambazo nimeweza kuzikusanya katika utafiti wangu na kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nikienda nyuma sana miaka ya mwanzoni wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika.
Kuna yeyote anaejua historia za wazalendo hawa wake kwa waume atupe historia zao?:
Kulia Ali Msham na aliyekaa kwenye meza ni Mwalimu Julius Nyerere.
Kulia Julius Nyerere, John Rupia na Sheikh Suleiman Takadir na hao waliosimama nyuma ni Bantu Group wahamaishaji na walinzi wa viongozi wakiwa na silaha za jadi
Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere,
Sheikh Mohamed Ramia na Idd Faiz Mafungo
Kulia Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed kushoto Bi. Titi bin Mzee na katikati Julius Nyerere wakimsindikiza safari ya kwanza UNO
TANZANIA THE STORY OF JULIUS NYERERE From the pages of Drum Picha ya kushoto ni mswada alionipa Jim Bailey mmiliki wa jarida la Drum kuhariri na kutafuta mchapaji yaani "publisher. " Tulifanikiwa na kitabu kikachapwa na ndiyo hiyo picha ya pili. Ni katika kazi hii ndipo nilipopata picha...
Kuna juhudi kubwa sana inafanyika ya kuokoteza historia hapa na pale na bahati nzuri ni kuwa wanatumia vyanzo vyangu ambavyo mimi nimeweka kutia nguvu niliyopata kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
Lakini nadhani wao hili hawalijui na kama nisemavyo siku zote kutokujua ni katika silka ya ubinadamu hakuna anaejua kila kitu ila Allah mwenyewe.
Tuanze juu kichwani.
Kabla mimi sijamleta Abdul Sykes hakuna yeyote katika hao wanaonishambuia mimi alikuwa anamjua.
Wala hawakuwa wanajua ilikuwaje Nyerere akawa maarufu Dar es Salaam ilhali yeye ni mgeni mtu kutoka bara tena bara ya mbali sana.
Historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha Kivukoni ndiyo ilikuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nyerere anazuka.
Mimi nikifanya rejea ya kitabu cha Judith Listowel na Nyaraka za Sykes ndiye niliyemrejesha kwa mfano Denis Phombeah kuwa kadi yake ya TANU ni No. 5.
Wengi walishangaa walikuwa hawajapata kusikia jina hili.
Sikuiishia hapa sasa nikifanya rejea za Nyaraka za Sykes nikaeleza safari ya Phombeah na Ally Sykes kwenda Southern Rhodesia (Zambia) mwaka wa 1953.
Naweka link hapo chini.
Ilinichukua karibu miaka 20 kuipata picha ya Phombeah na aliyenipatia ni Ahmed Rajab kutoka kwa mwanae Gray Phombeah.
Mikutano ya siri ikifanyika baada ya TANU kuundwa na kabla ile 1953/54 ilikuwa kwa Abdul Sykes na kamati hii ni mbali na TAA Political Subcommitee ya 1950 ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Hapa tumuongeze Earle Seaton katika hii kamati.
Hakuna aliyekuwa anajua historia ya Seaton na Abdul Sykes na mchango wa Seaton katika hii kamati na mapendekezo ya katiba hadi mimi niipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii nimepata katika Nyaraza za Sykes.
Leo hawa ndiyo wa kunifundisha mimi historia ya Earle Seaton?
Hii historia yote haikuwapo kabla ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
Walikuwa wapi?
Nakuongezea kitu hapa.
Huo urafiki wa Seaton, Marealle wamuongeze na Abdul Sykes.
David Marealle alikuwa jirani yangu iko siku nimemsikia anasema.
''Walionipokea mimi mara ya kwanza nakuja Dar es Salaam ni hawa akina Sykes,'' anamnyoshea kidole Abbbas Sykes aliyenipeleka kwake.
Nimesoma barua za Marealle kwa akina Sykes lakini sikuzitumia katika kitabu kwa kuwa zilikuwa na faragha baina yao.
Hizi barua zina mambo kaka.
Kamati hii TAA Political Subcommitte baada ya kutoka mapendekezo ya katiba Twining akaisambaratisha kwa kuwapa uhamisho Dr. Kyaruzi na Hamza Mwapachu.
Kyaruzi akapelekwa Kingolwira kisha Nzega na Mwapachu kisiwani Nansio.
Hii 1951.
Mikutano ya Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu wamesoma kutoka kwangu nami nimepata kutoka kwa Judith Listowel na Judith Listowel huwezi kuamini katoka katika mswada wa Dr. Kyaruzi, The Muhaya Doctor,'' na kaweka katika kwenye kitabu chake ''word to word,'' ndani ya kitabu hicho.
Ninao huu mswada katika Maktaba yangu.
Turejee kwa Phombeah.
Phombeah asingeweza kufanya mkutano Arnautoglo hapakuwa na faragha hii kwanza halafu hakuwa mtu wa kamati ya ndani.
Amir Jamal kaja TANU 1958 mkutano gani utafanyika kwa Muhindi na siku zile za mwanzo ninazozizungumza ulikuwa wakati wa Afrika kwa Waafrika?
Erica Fiah.
Kleist Sykes kamweleza kwa kirefu katika mswada wake alioandika kabla ya kifo chake 1949.
Wamsome Daisy Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' wakipenda wasome: ''Kleist Sykes Man of Ideas,'' katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mercedes Benz iliwachoma wale wa 1959 kama inavyowachoma hawa wa leo.
Wakahitimisha kwa kufuta historia yote.
Ati nini kununua Mercedes Benz.
Niliweka makusudi kuwasikiliza.
Hasad, wivu na choyo zimewajaa.
Mercedes kwa vijana hawa wa Karikaoo zilikuwa mbili ya Abdul na ya Abbas Abdulwahab na walikuwa majirani.
Abdulwahab alikuwa kijana wa Kiarabu ambae alikuwa na biashara kubwa ya kuuza maziwa.
Katiba ya TANU ni ya Labour Party wanasema na ya CPP.
Kaka mimi naandika kwa ajili yako.
Hawa wanajifunza historia hii leo mimi nimeishi na watu hawa na wamenifungulia nyaraka zao na mioyo yao na nimeandika papers na makala wala sijui hesabu yake.
Kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile mimi nisingeyajua haya yote.
Na kama nisingenyanyua kalamu kuandika hawa wangebakia na historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha CCM Kivukoni.
Ndipo nakuambia wakati mwingine nawaonea huruma.
Wananukuu yale niliyoandika mimi bila ya kujua.
KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953 SEHEMU YA KWANZA Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa African National Congress (ANC) na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini...
Dive,
Nakuwekea picha za Mwalimu ambazo nimeweza kuzikusanya katika utafiti wangu na kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nikienda nyuma sana miaka ya mwanzoni wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika:
View attachment 2064384
Kulia Julius Nyerere, John Rupia na Sheikh Suleiman Takadir na hao waliosimama nyuma ni Bantu Group wahamaishaji na walinzi wa viongozi wakiwa na silaha za jadi
View attachment 2064392
Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere,
Sheikh Mohamed Ramia na Idd Faiz Mafungo View attachment 2064387
Kulia Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed kushoto Bi. Titi bin Mzee na katikati Julius Nyerere wakimsindikiza safari ya kwanza UNO
Mumepatikana Na Nyerere wenu , vitabu vyenu vya kanisa vikimsifu Tu baada ya kumtumia Kama kibaraka wao. Mzee kawatolea ukweli mnakwenda mbio . Si mtunge vyengine vya kumsuta Mzee Mohammed mnalia Lia nini
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.