1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Kwa hiyo unaangalia unaona afadhali ya watu waliowaswaga ndugu zetu kama ng'ombe ( na kubonda vichwa vya watoto walioshindwa kutembea) mpaka Bagamoyo, wengine wakatubebesha hizo pembe za ndovu,halafu wakatuvusha kama dagaa na kutupiga mnada kama vile wanauza maharage. Baada ya hapo wengine tukapelekwa kulima, wengine kazi za nyumbani na wengine walipelekwa uarabuni, Mauritius ( kufanya kazi kwenye mashamba ya miwa), wengine walihasiwa ili waweze kuwahudumia wake na vimada wao bila kuingia tamaa, kuliko mtu aliyemkata kichwa mtu mmoja ( kwa maelezo yako)? Wazungu wa magharibi hawakuwa malaika, nao walitufanyia uovu mwingi sana lakini katika eneo letu uovu waliotufanyia haufikii ambao walitufanyia waarabu na uzao wao. Kufungia macho uovu huo kwa sababu za kidini sio sawa.

Amandla...
Kwani fuvu la kichwa cha Ali songea mbano liko wapi? Amandla mbona umeghadhibika na kuelezwa ukweli juu ya ukatili waliofanyiwa babu zetu na Hawa watu? Pole sana kama nimekukwaza, lakini hakika inasikitisha kuilipua kilwa na mabomu kwasababu ya husda za kinyang'au ' huenda hilo jukumu la Nyerere kwenda UNO lisingekuwa tija Leo endapo dola adhwim ya kilwa ingekuwepo hadi hii Leo
 
Screenshot_20211226-121940_Google.jpg
 
Huyo bwana mdogo ni kumsamehe tu , hajui historia ya Zbar maswali ya mapinduzi ni kumuonea

Moyes , swali hilo nimewauliza akina Mohamed Said, Ghassani , Jusa , Ahmed Rajabu n.k. hakuna jibu. Ahmed Rajabu alizunguka zunguka kupitia gazeti la Raia Mwema lakini hakutoa jibu

Mtu aliyewahi kusimama na kusema bila kumung'unya maneno ni Mansour Himid. Huyu bwana namheshimu kwa misimamo yake. Alipokuwa CCM alikosana nao kwa misimamo yake thabiti.
Alipohamia CUF alibaki na misimamo yake lakini aliwaambia wazi ' Mapinduzi Daima'

Inaweza kuwa ni kutokana na historia ya mzazi wake hata hivyo misimamo yake ni thabiti kwa kile anachoona ni sahihi kwake na hili la mpainduzi yeye analisema bila kumeza maneno

Watu kama VP O. Masoud wana wakati mgumu sana wa kuamua iwapo mapinduzi ni Halali au ni Haramu.
Nguruvi3,
Ndiyo kwanza naiona hii post na nimesoma kuwa mimi ni mmoja wa watu uliowauliza swali la uhalali na uharamu wa mapinduzi.

Sijui kwa nini swali hili linaulizwa leo.
Iwe itakavyokuwa itasaidia nini kuwa na jibu la swali hili?

Nimebahatika kukutana na viongozi wa serikali ya Zanzibar iliyopinduliwa kama Sheikh Ali Muhsin Barwani na Dr. Baalawy Muscat na Dubai na tukawa na mazungumzo.

Nmesoma kumbukumbu za Sheikh Ali Muhsin na kumsikiliza uso kwa macho na kumsikiliza katika audio na video.

Nimebahatika pia kukutana na mmoja wa viongozi wa Hizbu Aman Thani na tukazungumza mengi uso kwa macho nimesikiliza kumbukumbu zake katika video akiyaeleza mapinduzi na nimesoma kitabu alichoandika, ''Ukweli ni Huu,'' nakala ambayo ninayo kanipa kwa mkono wake na ina sahihi yake.

Nimemsoma pia Maulid Mshangama mmoja wa mawaziri wa serikali ya Zanzibar iliopinduliwa.

Nina mengi kutoka kwa huu upande wa pili ambao si wengi wanayajua kwa kuwa ilikuwa kwa muda mrefu historia isiyofahamika.

Lakini kubwa kwangu ni kuwa nilikuwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti kitabu chake maarufu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Katika utafiti huu ndipo nilipojua historia ya kweli ya mapinduzi nani kahusika nani katoa fedha, mchango wa askari mamluki kutoka kambi ya Kipumbwi Tanga, mchango wa Algeria, Wayahudi, Waingereza, serikali ya Tanganyika nk. nk.

Huu utangulizi mrefu nimeuleta kutandika jamvi la mazungumzo.

Mkadama huo hapo juu na hayo maneno hapo chini niliyoandika hapa JF miaka michache iliyopita yatamsaidia msomaji katika kuelewa uhalali au uharamu wa mapinduzi:

''Sheikh Ali Muhsin Barwani wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar alikuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) vilevile chama hiki kikijulikana kama Hizbu.

Kwa mapenzi makubwa wanachama wa Zanzibar walikuwa wanamwita, “Zaim” yaani Kiongozi.

Ilikuwa nia ya Sheikh Ali Muhsin Zanzibar ipiganie uhuru wake chini ya chama kimoja cha kizalendo chenye nguvu chama cha kitaifa badala ya vyama vilivyojijenga katika misingi ya rangi.

Ilikuwa pigo kubwa sana kwake Abeid Amani Karume alipoasisi Afro Shirazi Party, chama kilichosimama kwa maslahi ya Waafrika na Washirazi. Sheikh Ali Muhsin alipigania uhuru wa Zanzibar mpaka ukapatikana tarehe 10 December 1963.

Sheikh Ali Muhsin alishiriki katika mkutano wa katiba Lancaster House.

Baada ya mapinduzi yaliyotokea Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 Sheikh Ali Muhsin alikamatwa na kusafirishwa Tanganyika ambako alifungwa Ukonga na jela nyingine kwa kipindi cha miaka 10 na miezi michache.

Katika kipindi alichokuwa kifungoni Sheikh Ali Muhsin aliandika miswada kadhaa ambayo alikuja kuichapa kama vitabu baada ya kutoka kifungoni.

Kabla hajafa mwaka 2006 Sheikh Ali Muhsin aliandika kitabu cha maisha yake, ‘’Conflict and Harmony in Zanzibar,’’ ambacho kilikuja kufasiriwa kama ‘’Kujenga na Kubomolewa Zanzibar.‘’

Katika kitabu hiki cha maisha yake Sheikh Ali Muhsin anaeleza yaliyopitika Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi.

Baada ya kushindwa kupata pasi ya kusafiria, Sheikh Ali Muhsin alitoroka nchini mwaka 1974.

Hadi anafariki siku zote Sheikh Ali Muhsin alikuwa akisema yale hayakuwa mapinduzi bali mavamizi.''

1640520003865.png

Niko na Sheikh Ali Muhsin Barwani nyumbani kwake Muscat December, 1999.

Nilijua kimbilio lako ni mdini mwenzako Mohammed Said. Utamuamini vipi mtu anayedai kuwa waarabu hawakuua waafrika wala kuwatesa!

Ili upate balance, nakushauri usome kitabu cha Ali Sultan Issa, kinachoitwa Walk on Two Legs, aliyezaliwa Wete, Pemba mwaka 1932, mwanachama wa ZNP ambae alihamia chama cha Umma. Anazungumzia waafrika waliojiita washirazi ili kujitofautisha na wale walioletwa kama watumwa au wafanyakazi. Anazungumzia watumwa walioletwa kutoka Congo. Anazungumzia mjomba wake aliyerithi mtumwa kutoka kwa babu yake. Aliwajua watu waliokuwa watumwa. Anazungumzia jinsi waarabu wa Pemba walivyozaa na waafrika. Yeye mwenyewe upande wa mama yake asili yao ilikuwa Yemen, upande wa baba Oman. Hata hivyo mama wa bibi yake mzaa mama, ( aliitwa Bibi Ruzuna Binti Tamim, aliyewahi kuwa mke wa Sultan Ali bin Hamoud) alikuwa mzaramo na bibi huyo huyo alikuwa na damu ya wanandi kutoka Kenya. Huyu bwana alikuwa rafiki mkubwa wa Babu na anaelezea kuhusu ushirikiano kati ya chama cha Umma na ASP kuandaa mapinduzi ya Zanzibar. Anaelezea jinsi wao wakommunisti waliwaachia shughuli nzima ASP Youth League kwa sababu wao hawakuwa wengi na serikali iliwahofia zaidi UMMA kuliko ASP. Anaelezea jinsi Yusuf Himidi, Said wa Shoto, Abdullah Said Natepe, Khamis Darweshi, Ramadhan Haji, Pili Khamis, Seif Bakari na Saidi Iddi walivyoongoza uvamizi wa armoury iliyokuwa Ziwani. Hawa walivamia pia Police Barracks zilizokuwa Mtoni. Ukitaka kujua zaidi kuhusu Mapinduzi soma dissertation ya Ph. D ya Ann Lee Grimstad aliyoitetea mwaka 2018 katika Chuo Kikuu cha Florida. Kama nilivyokuambia hapo awali, udini unakupa ujinga. Usiwasikilize wakina Mohammed Said peke yao. Fanya utafiti wako mwenyewe ndio utajua ukweli.

Kwangu mimi sina zaidi ya kuchangia kuliko haya. Una uhuru wa kuamini utakacho.

Amandla....
Fundi Mchundo,
Unasema kuwa mimi nisisikilizwe na unamtaja Ann lee Grimstad na utafiti wake.

Labda hujui nafasi yangu kwa hawa watafiti katika historia iwe ya Tanganyika au ya Zanzibar.

Ann alikuwa mgeni wangu na nimemweleza mengi na kumpitisha kwingi katika yale yeye alikuwa anataka kuyajua.

Kama si utafiti wa Dr. Harith Ghassani dunia isingejua kuwa lilitoka jeshi la Wamakonde kutoka Kipumbwi, Tanga, Tanganyika kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi.

Waliohusika katika kuweka kambi hii na mafunzo ya hawa Wamakonde na kuwavisha kwa majahazi kuingia Zanzibar walikuwa Mohamed Mkwawa na Victor Mkello.

Nilikuwako katika mazungumzo yote aliyofanya na wahusika wakuu katika utafiti wake.
Angalia picha:

1640527583185.png

Ann Lee Grimstad akimhoji mke wa marehemu Victor Mkello nyumbani kwake Nguvumali Tanga

1640527759805.png

Ann Lee Grimstad akimhoji Mohamed Omari Mkwawa nyumbani kwake Sahare Tanga picha zote hizi mbili nimepiga mimi.
 
View attachment 2058485
Ann Lee Grimstad akimhoji mke wa marehemu Victor Mkello nyumbani kwake Nguvumali Tanga

View attachment 2058486
Ann Lee Grimstad akimhoji Mohamed Omari Mkwawa nyumbani kwake Sahare Tanga picha zote hizi mbili nimepiga mimi.
Mohamed Said, mtafiti yeyote makini anahoji watu wengi na sio kila mtu anayehojiwa ni authority katika atakachokiandika. Ili thesis yake ikubalike alitakiwa a validate alichokiandika kwa kile ambacho wasomi wenzake wanaita triangulation. Kupiga nae picha sebuleni kwako, kumhoji Mohamed Omari Mkwawa sio uthibitisho kuwa wanachokisema ni kweli. Au kwa sababu Ghassani alifanya utafiti hakuhakikishi kuwa hapakuwa na bias katika utafiti wake.

Mimi nilimwambia kijana wako kuwa wewe sio authority wa Mapinduzi ya Zanzibar kama vile usivyo authority wa mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika. Wewe ni authority wa historia ya wakina Sykes na ndugu zako wengine lakini sio wa picha kamili ya mapambano yale. Unakosa validity kwa sababu unajaribu kupindisha kila kitu ili ki fit narrative yako ya udini, hususan udini wa kiislamu. Ungekuwa na mchango mkubwa sana kama ungeondoa hiyo bias yako.

Fundi...
Nimependa sana hii kuwa mimi siyo ''authority,'' historia ya uhuru wa Tanganyika bali ni ''authority,'' wa akina Sykes.

Umenikosha sana hapa.

Ulikuwa unajua mchango wa akina Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika kabla mimi sijawaandika?

Historia ya TANU ya Kivukoni ilikuwepo toka 1981 na iliwafuta akina Sykes na wapigania uhuru wengi mbona hukusema kitu ulikuwa kimya?

Unajua kuwa umuhimu wa akina Sykes katika historia ya uhuru wa Tanganyika ni kuwa ni wao katika wale waasisi wa African Association ndiyo walioandika historia ya AA na kuacha nyaraka ambazo ndizo hizi nimezitumia kuandika historia yao na historia ya kuamka kwa Waafrika kudai haki zao katika nchi yao.

Huyu ni baba yao Kleist Sykes mwaka wa 1929.

Sasa njoo kwa watoto Abdul na Ally hawa wanaanza harakati 1942 wakiwa Burma.

Nimetumia nyaraka za Sykes kuandika historia ya TANU na historia ya Julius Nyerere.

Kuna yeyote mwenye ushahidi wa picha na nyaraka wa historia ya Nyerere katika TAA kuanzia alipokutana na Abdul Sykes 1952 na kutiwa katika uongozi wa juu 1953?

Umepata kuona au kusoma popote pale historia ya Nyerere kama nilivyoieleza katika kitabu cha Abdul Sykes?

Sikujua kama kurudisha historia ya zaidi ya miaka 50 iliyofutwa ni udini.

Vipi wale walioifuta historia hii na kuweka ya kwao nini kiliwasukuma kufanya hivyo?

Haikuwa uoga wa kuona kuwa Waislam watakuwa kila mahali katika historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika?

Kaa kitako jitulize na fikiri iweje Nyerere afikie mahali asahau hata kama alimkuta Abdul Sykes Secretary na Act. President wa TAA pale alipompokea Dar es Salaam 1952?

Asahau pia aligombea na yeye nafasi ya urais wa TAA.

Inawezekana vipi Nyerere atoe medali 3, 979 wakati anaacha uongozi na Abdul na Dossa hawamo katika orodha ile?

Unajua nini alisema alipoulizwa na watu wake wa karibu kuhusu hili?

Mimi nimewarejesha katika historia Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Sulemaiman Takadir, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Tatu bint Mzee. Mama bint Maalim, Amina Kinabo, Nyange bint Chande, Zarula bint Abdulrahman kwa kukutajia wachache katika wanawake waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Si akina Sykes peke yao.

Naijua historia kubwa ya Tanganyika kutoka kila pembe.

Sikuwapiga Mama Mkello na Mohamed Mkwawa picha sebuleni kwangu.

Picha hizo nimezipiga majumbani kwao Tanga nikiwa na Ann Lee.

Mimi haya mambo kaka nayajua na si kwa kuwa mimi nina akili kuwapita watu wengine.

Hii historia imekuwapo nyumbani kwetu mimi mdogo wala sikuwa najua nashuhudia jambo kubwa katika historia ya Tanganyika na Zanzibar.

Hivi hujajiuliza kwa nini akina Sykes walinifungulia mimi ile hazina ya nyaraka zao na si mtu yeyote yule.

Hivi unajua baada ya historia ya kweli kuwa hadhir kila mtafiti akienda kuwahoji akina Sykes na kutaka kuona nyaraka zao jibu lao ni, ''Mohamed Said keshaandika someni kitabu chake.''

Unajua kwa nini wanasema maneno haya?

Leo tunaisoma upya historia ya Nyerere na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hivi hujajiuliza kwa nini Dr. Ghassany alinichukua mimi kama msaidizi wake katika utafiti wa kitabu chake na si mtu mwingine yeyote yule?

Jiuilize maswali haya yote na jaribu kupata majibu.

Hivi unajua kuwa ni Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo waliompeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume?

Baba yangu alikuwa rafiki mkubwa wa Abdulaziz Twala na Jaha Ubwa wote hawa ASP na wanamapinduzi na waliuliwa baada ya mapinduzi.

Inawezekana kweli mimi si ''authority,'' lakini wengi wakitaka kujua mambo wanakuja kwangu hata jopo la Prof. Shivji walioandika Biography of Julius Nyerere walikuja kunihoji na nikawapa picha na baadhi ya Nyaraka za Sykes.

Hii ndiyo nafasi yangu katika historia ya Tanganyika na Zanzibar.

1640537301073.png

Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wazi Kamatha wakinihoji nyumbani kwangu kuhusu Julius Nyerere wakati wanatafiti maisha yake kwa ajili ya kitabu chake.
 
Si Zanzibar Tu Nyoka Nyerere aliyafanya Yale yale ya Zanzibar kwa Seychelles

TUFUNUWE KITABU (SILSILA 16):

SEYCHELLES GLOBAL CITIZEN cha Sir James Mancham - YouTube

Sir James Mancham alikuwa Rais wa kwanza wakati Seychelles inapata Uhuru wake mwaka 1976, lakini akapinduliwa mwaka mmoja tu baada ya kuingia madarakani katika mapinduzi ambayo mwenyewe anaituhumu Tanzania kuhusika. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za kitabu alichokiandika mwanadiplomasia huyo wa kimataifa kuelezea maisha yake: Seychelles Global Citizen.
 
Fundi...
Nimependa sana hii kuwa mimi siyo ''authority,'' historia ya uhuru wa Tanganyika bali ni ''authority,'' wa akina Sykes.

Umenikosha sana hapa.

Ulikuwa unajua mchango wa akina Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika kabla mimi sijawaandika?

Historia ya TANU ya Kivukoni ilikuwepo toka 1981 na iliwafuta akina Sykes na wapigania uhuru wengi mbona hukusema kitu ulikuwa kimya?

Unajua kuwa umuhimu wa akina Sykes katika historia ya uhuru wa Tanganyika ni kuwa ni wao katika wale waasisi wa African Association ndiyo walioandika historia ya AA na kuacha nyaraka ambazo ndizo hizi nimezitumia kuandika historia yao na historia ya kuamka kwa Waafrika kudai haki zao katika nchi yao.

Huyu ni baba yao Kleist Sykes mwaka wa 1929.

Sasa njoo kwa watoto Abdul na Ally hawa wanaanza harakati 1942 wakiwa Burma.

Nimetumia nyaraka za Sykes kuandika historia ya TANU na historia ya Julius Nyerere.

Kuna yeyote mwenye ushahidi wa picha na nyaraka wa historia ya Nyerere katika TAA kuanzia alipokutana na Abdul Sykes 1952 na kutiwa katika uongozi wa juu 1953?

Umepata kuona au kusoma popote pale historia ya Nyerere kama nilivyoieleza katika kitabu cha Abdul Sykes?

Sikujua kama kurudisha historia ya zaidi ya miaka 50 iliyofutwa ni udini.

Vipi wale walioifuta historia hii na kuweka ya kwao nini kiliwasukuma kufanya hivyo?

Haikuwa uoga wa kuona kuwa Waislam watakuwa kila mahali katika historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika?

Kaa kitako jitulize na fikiri iweje Nyerere afikie mahali asahau hata kama alimkuta Abdul Sykes Secretary na Act. President wa TAA pale alipompokea Dar es Salaam 1952?

Asahau pia aligombea na yeye nafasi ya urais wa TAA.

Inawezekana vipi Nyerere atoe medali 3, 979 wakati anaacha uongozi na Abdul na Dossa hawamo katika orodha ile?

Unajua nini alisema alipoulizwa na watu wake wa karibu kuhusu hili?

Mimi nimewarejesha katika historia Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Sulemaiman Takadir, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Halima Selengia, Tatu bint Mzee. Mama bint Maalim, Amina Kinabo, Nyange bint Chande, Zarula bint Abdulrahman kwa kukutajia wachache katika wanawake waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Si akina Sykes peke yao.

Naijua historia kubwa ya Tanganyika kutoka kila pembe.

Sikuwapiga Mama Mkello na Mohamed Mkwawa picha sebuleni kwangu.

Picha hizo nimezipiga majumbani kwao Tanga nikiwa na Ann Lee.

Mimi haya mambo kaka nayajua na si kwa kuwa mimi nina akili kuwapita watu wengine.

Hii historia imekuwapo nyumbani kwetu mimi mdogo wala sikuwa najua nashuhudia jambo kubwa katika historia ya Tanganyika na Zanzibar.

Hivi hujajiuliza kwa nini akina Sykes walinifungulia mimi ile hazina ya nyaraka zao na si mtu yeyote yule.

Hivi unajua baada ya historia ya kweli kuwa hadhir kila mtafiti akienda kuwahoji akina Sykes na kutaka kuona nyaraka zao jibu lao ni, ''Mohamed Said keshaandika someni kitabu chake.''

Unajua kwa nini wanasema maneno haya?

Leo tunaisoma upya historia ya Nyerere na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hivi hujajiuliza kwa nini Dr. Ghassany alinichukua mimi kama msaidizi wake katika utafiti wa kitabu chake na si mtu mwingine yeyote yule?

Jiuilize maswali haya yote na jaribu kupata majibu.

Hivi unajua kuwa ni Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo waliompeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume?

Baba yangu alikuwa rafiki mkubwa wa Abdulaziz Twala na Jaha Ubwa wote hawa ASP na wanamapinduzi na waliuliwa baada ya mapinduzi.

Inawezekana kweli mimi si ''authority,'' lakini wengi wakitaka kujua mambo wanakuja kwangu hata jopo la Prof. Shivji walioandika Biography of Julius Nyerere walikuja kunihoji na nikawapa picha na baadhi ya Nyaraka za Sykes.

Hii ndiyo nafasi yangu katika historia ya Tanganyika na Zanzibar.

View attachment 2058609
Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng'wazi Kamatha wakinihoji nyumbani kwangu kuhusu Julius Nyerere wakati wanatafiti maisha yake kwa ajili ya kitabu chake.
Unathibitisha tena kuwa wewe ni authority wa historia ya wakina Sykes. Na kuhusu wakina Sykes, nilijua kuhusu mchango wao kabla ya wewe kuandika. Tofauti na wewe unavyotaka kutuaminisha mapambano ya uhuru hayakuwa ya watu wa Gerezani peke yao. Hao wakina Sykes na wengine uliowataja wasingekubalika kwa wanyakyusa bila wakina Mwakangale, Kanda ya ziwa bila wakina Bomani, Kilimanjaro bila wakina Mbowe, mission quarter bila wakina Phombeah na sehemu nyingine ni watu kama wakina Kasanga Tumbi, Rupia wazee wako wasingeona ndani. Bila wakina Robert Makange na gazeti lake kazi ingekuwa ngumu. Mimi sikatai mchango wa wakina Sykes, Mwapachu na wengine.

Ninachopinga ni wewe kuwavisha joho la udini wakati wengi wao walikuwa Nationalists kuliko wadini ndio maana waliwakubali watu kama Dr. Kyaruzi, Julius Nyerere, Oscar Kambona na wagalatia wengine tu katika mpambano wa kudai uhuru. Hao wakina Sykes walikuwa wapiga muziki, watu wa Klabu, leo unataka kuwageuza wapigania ukombozi wa waislamu na sio watanzania wote?

Kupiga picha na kuhojiwa na watu kama Issa Shivji hakukufanyi authority wa historia ya Tanganyika, bali authority wa sehemu ya historia ya Tanganyika. Badala ya kutuwekea mapicha ukinywa chai nao weka mahali walipo ku "cite" kama source ya maandiko yao! Wewe unatoa anecdotal evidence ambazo zinafurahisha lakini sio scientific. Kutuambia kuwa ulimjua mtu aliyekuwa anampakiza baiskeli Nyerere kutoka Pugu hakukufanyi authority wa maisha yake. Hivi kusema kuwa wakina Sykes na Aziz ndio waliomtambulisha Nyerere kwa Karume kunasaidia nini? Kwa lugha za wagalatia, " so what?". Na hiyo tukikubana utasema tukuamini kwa sababu Abdul Sykes alikusimulia! Kama vile unataka tuamini hiyo tamthilia ya wamakonde kwa sababu wazee fulani wa Tanga walikusimulia! Historia haiandikwi hivyo.

Wewe tusimulie kuhusu mchango wa wakina Sykes na ndugu zako wengine lakini usitake kutulazimisha kuwa hii nchi ni waislamu peke yao ndio waliopata machungu ya kugombea uhuru.

Ndipo ninaposema kuwa mimi nayajua haya si kwa kusoma bali ni sehemu ya maisha yangu kwani hawa ni wazee wangu.

Unazungumza kuhusu muziki wao 1950s.
Basi huzijui nyakati hizo.

Mimi nimeona na parties zao na lifestyle ya hao wote kwa jicho langu ingawa nilikuwa mdogo.

Nimeziona na suti zao na mengi sana.

Kama unadhani unaweza kuwadhalilisha wazee wangu kwa hayo basi huwajui wala hujui maisha yao.

Mimi nimezisikia nyimbo za Septet Habanero, Alma Cogan, Nat King Cole, Bing Crosby, Harry Belafonte, Louis Armstrong kutoka kwa hawa wazee.

Nilipokuwa mdogo nilitamani nikiwa mkubwa niwe kama wao.
Ninajua kupiga piano na guitar na naweza kuimba.

Nimewashangaza wengi katika safari zangu ninapowatembelea rafiki zangu huko nje.

Nilimshangaza Dr. Harith Ghasany na mkewe nilipofungua Grand Piano nyumbani kwake Muscat na kuanza kupiga.

Nimemshangaza Abdilatif Abdallah niliposhka guitar la mwanae aliyekuwa anajifunza nikawa mwalimu wake kwa kipindi nilipokuwa kwake Humburg.

Miaka ikapita akaniletea video ya mwanae sasa bingwa yuko kwenye show anapiga, ''Dark Side of the Street.''

Nilimshangaza zaidi nilipompa historia ya hiyo nyimbo na mabingwa wangapi wa jazz wameipiga.

Yote haya mimi nimepitia nyumbani kwa baba yangu na siku hizo sijafika hata miaka 16 nina guitar langu la umeme Hoffner chumbani kwangu pamoja na viatu vya Adidas na ubao nikisomea Shakespeare.

Nina record player Dansette made in Sussex.
Nasikilikizia nyimbo zangu za Elvis Presley, Cliff Richard, Beatles, Rolling Stones nk.

Nilikuwa na ''ambition'' nivae jezi ya Sunderland na timu ya taifa.

Tulivishwa suti na sisi na tukawa na blazer za blue na vifungo vya shaba tukivaa kwenye ''occassions,'' maalum.

Si vitu vya kueleza lakini nakueleza kwa kuwa umenitukania baba zangu sasa nataka utujue.

Tafuta mengine ya kunitukana mimi na wazee wangu siyo hayo.
Mwakangale mbona humtaji Dr. Wilbard Mwanjisi na nduguye Roland.

Mzee Roland baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes alikuja kwa Ally Sykes na notes za kaka yake akamwambia Bwana Ally, ''Mpe Mohamed Said hizi notes za Dr. Mwanjisi.''

Ungependa nikueleze Dr. Mwanjisi anasema nini?
Notes hizi niliwapa jopo la uandishi wa kitabu cha Nyerere.

Niliwaonyesha pia mswada wa Dr. Vedasto Kyaruzi.

Soma ''acknowledgements,'' za kitabu cha Nyerere uone wamesema nini kuhusu Mohamed Said na Maktaba yake.

Nimekuwa ndani ya Library of Congress toka 1980s wakati huo mkusanyaji wao akiwa Joseph Kimalando kisha Ahmed Rashad Ali.

Niko ndani ya Cambridge Journal of African History (1998).
Niko katika Dictionary of African Biography (2011)

Siwezi kutaja kila kitu.

Unaumia ninapoandika kadi no. 1 ya TANU Julius Kambarage Nyerere, kadi no. 2 Ally Kleist Sykes, kadi no. 3 Abdulwahid Kleist Sykes, kadi no. 4 Waziri Dossa Aziz, kadi. no. 5 Denis Phombeah, kadi no. 6 Dome Okochi Budohi na kadi ya Nyerere kaandikiwa na Ally Sykes na kadi 1000 za kwanza kanunua yeye kutoka mfukoni kwake.

Hasad, choyo na wivu.
Kwa nini hatukuwa sisi.

Misheni Kota unamtaja Denis Phombeah huyu kaja baadae sana.
Kwa nini hukumtaja Erika Fiah au Plantan brothers?

Unamtaja Mbowe mbona umemsahau Yusuf Olotu na timu yake ya akina mama akina Mama bint Maalim mke wa Jumbe Mohamed, Amina Kinabo na Halima Selengia?

Unazungumza Sauti ya TANU mbona hukutaja gazeti la Erika Fiah Kwetu au la Ramadhani Mashado Plantan Zuhra tena linachapwa Misheni Kota?

Hiyo picha hapo chini niko Nairobi na Dome Okochi Budohi mwaka wa 1972 kadi yake ya TANU no. 6.

Mimi hapo nina umri wa miaka 20.

Budohi licheza film na Rashid Kawawa, ''Mgeni Mwema,'' na akipiga drums katika ''The Skylarks,'' kisha ''Black Birds'' bendi ya vijana wa Dar es Salaam miaka hiyo baba yangu akiwamo na Sykes brothers wote.

Sisi watu wa ''club'' kaka wakati ule hadi baadae.
Mengine nimeona niyakalie kimya.

1640552479133.png

Ally Sykes na Mohamed Said Muthaiga Club, Nairobi 1989

1640550551460.png
 
Nguruvi3,
Nimesoma kuwa mimi ni mmoja wa watu uliowauliza swali la uhalali na uharamu wa mapinduzi.
Sijui kwa nini swali hili linaulizwa leo.
Iwe itakavyokuwa itasaidia nini kuwa na jibu la swali hili?
Mohamed, swali hili si mara ya kwanza kukuuliza. Ukinisoma nyuzi nilizokutaja nilieleza matarajio ya jibu lako, kwamba hutajibu bali utaleta maelezo mengi katika kuvuruga wasomaji.
Kati ya mapungufu yako ya kibinadamu ni kutokuwa ''concise'

Swali ni muhimu pale ambapo Mapinduzi yananasibishwa na Mwl Nyerere. Iwe Mwl alishiriki au la hilo si tatizo, Mwl ameshiriki mambo mengi sana kuanzia Biafra, Palestine, na SADC yote ambayo leo mmoja wa mashahidi wake Askofu D. Tutu ametutoka. Hivyo Mwl kushiriki si tatizi kabisa

Tatizo ni pale anapotuhumiwa kwa dhania tu na hisia za watu. Ikiwa Mwl alifanya ''Uvamizi' kama ulivyodai , mapinduzi yale hayana Uhalali na ni Haramu. Kwa uharamu wake ni haramu kwa Wazanzibar kushiriki kila mwaka Jan 12 kusherehekea Haramu ya Nyerere. Fair enough
Hii ni kwa mujibu wako Mohamed Said

Tuwaulize Wazanzibar , hivi huu 'wendwazimu wa kusherehekea Mapinduzi ya uvamizi wa Nyerere wameupata wapi? Ni lini wataacha uhayawani huo kama anavyobainisha Mwanahistoria Mohamed Said ambaye ameshirikiana na watu kama Harith Ghassany katika kuutafuta ''ukweli'' !

Someni hapa chini enyi Wazanzibar wa ''Mapinduzi Daima'' kisha mtafakari ikiwa mnayoyafanya kila Jan 12 yana maana yoyote.
Nimebahatika kukutana na viongozi wa serikali ya Zanzibar iliyopinduliwa kama Sheikh Ali Muhsin Barwani na Dr. Baalawy Muscat na Dubai na tukawa na mazungumzo.
Nmesoma kumbukumbu za Sheikh Ali Muhsin na kumsikiliza uso kwa macho na kumsikiliza katika audio na video.
Umewahi kukutana na viongozi walioongoza Mapinduzi kwa maongezi au video?
Nimebahatika pia kukutana na mmoja wa viongozi wa Hizbu Aman Thani na tukazungumza mengi uso kwa macho nimesikiliza kumbukumbu zake katika video akiyaeleza mapinduzi na nimesoma kitabu alichoandika, ''Ukweli ni Huu,'' nakala ambayo ninayo kanipa kwa mkono wake na ina sahihi yake.
Umewahi kuwasikiliza 'Wana Mapinduzi' nao wanasemaje?
Nimemsoma pia Maulid Mshangama mmoja wa mawaziri wa serikali ya Zanzibar iliopinduliwa.
Umewahi kuzungumza na Mwanapinduzi yoyote katika serikali ya kwanza ya Mapinduzi?
Nina mengi kutoka kwa huu upande wa pili ambao si wengi wanayajua kwa kuwa ilikuwa kwa muda mrefu historia isiyofahamika.
Ya upande wa kwanza yako wapi?
Katika utafiti huu ndipo nilipojua historia ya kweli ya mapinduzi nani kahusika nani katoa fedha, mchango wa askari mamluki kutoka kambi ya Kipumbwi Tanga, mchango wa Algeria, Wayahudi, Waingereza, serikali ya Tanganyika nk. nk.
Historia ya Kweli ya Mapinduzi? Mo , You're entitled to your own opinion...

Hadi anafariki siku zote Sheikh Ali Muhsin alikuwa akisema yale hayakuwa mapinduzi bali mavamizi.''
Mohamed anatoa conclusion ya Ali Muhsin ili asionekane kasema yeye, lakini between the lines hicho ndicho anamaanisha

Mohamed, je, ulizungumza na akina Thabiti Kombo Jecha, Aboud Jumbe, Abdurahman Babu, Abdalla Natepe, Hassan Nassor Moyo, Ali Hassan Mwinyi kwa uchache ili kupata upande wa pili wa maongezi yao? Je, wao wanasemaje kuhusu Mapinduzi?
 
Back
Top Bottom