Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Fundi ...Hamna anaepinga kuwa kuna wengi waliochangia historia ya TANU lakini hawatajwi katika historia. Shida yangu na wewe ni pale unapojenga conspiracy theory kwenye kutengwa huko. Kwa mfano, kwenye picha hiyo kuna wanawake watano, wanne wamevaa baibui na mmoja hajavaa lakini wewe umewaona waliovaa baibui peke yake. Na kuweko picha yao pamoja na Nyerere hakuna maana kuwa wao walikuwa wanawake pekee waliomsindikiza Nyerere airport. Hauwezi kutumia picha kama hii kujenga hoja kuwa ni wanawake wakiislamu peke yao ndio waliomuunga mkono Nyerere. Na kutokuwepo picha hii Lumumba hakumaanishi kuwa ni ushahidi wa nia mbaya dhidi yao. Nyerere alipiga picha nyingi na watu tofauti na itakuwa vigumu kuwatendea wote haki sawa. Unapofanya kuwa absence ya picha kama hizi ni ushahidi wa hujma za Nyerere na TANU dhidi ya uislamu ni distortion ya makusudi ya historia.
Amandla...
Sikulaumu kwa kuwa hujui historia za hao akina mama.
Huyo wa kwanza kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa mke wa Shariff Abdallah Omar Attas.
Shariff Attas alikuwa Collector wa nafaka Soko la Kariakoo Market Master akiwa Abdul Sykes.
Nyerere alipoacha kazi ya ualimu mwaka wa 1955 alikuja kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu si mbali na sokoni.
Ikawa Nyerere anapomaliza kunywa chai anakwenda pale sokoni ofisini kwa Abdul Sykes kusoma magazeti nk.
Mchana wakati wa chakula cha mchana Shariff Attas anakuja na Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes kula chakula.
Wanapumzika kidogo kisha pamoja wanarudi sokoni.
Hapa ndipo katika kipindi hiki Nyerere alijuana na watu wengi sana maarufu wa Dar es Salaam mmoja wapo akiwa Mshume Kiyate ambae yeye alikuwa dalali wa samaki hapo sokoni.
Hapa ndipo Mwalimu alipofahamiana na Shariff Attas mmoja wa watu maarufu Dar es Salaam ile ya miaka 1950s.
Mkewe Shariff Attas Bi Chiku akajuana na Mama Maria Nyerere pamoja na wanae Mwalimu Sakina na Mwalimu Fatna wakisomesha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School na Mama Maria alikuwa na duka dogo karibu na nyumba ya hawa akina mama Mtaa wa Mchikichi na Livingstone akiuza mafuta ya taa.
Sasa mikutano ya hadhara ya TANU ilipoanza ikawa jioni kama kesho kuna mkutano wa TANU Mnazi Mmoja hawa akina mama akina Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed, Bi. Hawa bint Maftah na wanawake wengine wanakutana na viongozi wa TANU nyumbani kwa Abdul Sykes na Nyerere akiwemo kupanga jinsi ya kuwaleta wanawake mkutanoni kujaza uwanja na kutia shamrashamra kwa nyimbo zao za lelemama.
Hawa akina mama ndiyo katika wanawake wa mwanzo wanachama wa TANU.
Si kama hawa akina mama katika picha hiyo walifika hapo kwa bahati mbaya.
Dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya kwanza kwenda UNO ilifanyika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika New Street na Livingstone na hili jengo lipo hadi leo.
Hili jengo lilijengwa na uongozi wa Kleist Sykes na Mzee bin Sudi wakati wakiwa na nafasi hizo hizo katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na katika African Association.
Hii kwangu mimi ni historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika sasa ikiwa kuna wengine na wao wanazo historia kama hizi na picha hakuna aliyewakataza kuandika.
Nakuwekea picha nyingine ya Uwanja wa Ndege siku ya kumsindikiza Mwalimu:
Huyo alie mkono wa kulia wa Nyerere anaitwa Iddi Faiz Mafungo alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya na TANU na ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Nyerere UNO. Pembeni yake ni Zuberi Mtemvu, Robert Makange na aliyeshika kikapu cha ukili ni Rashid Sisso kushoto kwa Mwalimu ni John Rupia na Bi. Titi Mohamed.