Hakuna, na ana haki ya kuandika 'memoir' na Mohamed hatakuwa wa kwanza
Na pia kuifanya historia ya ukoo wa Sykes kuwa historia ya Tanganyika.
Hakuna ushahidi wowote wa Sykes kufanya siasa nje ya Gerezani na kama upo Mohamed atueleze mkutano mmoja tu. Lakini pia hautuwezi kusahau kuwa ukoo wa Sykes ni mamluki waliokuja kuwapinga Wazalendo. Hivyo, walikuwa Wahalifu kabla ya kukumbatia Uzalendo
Ndio maana akiulizwa kwanini Wapelekwe Wamakonde wa Kipumbwi hana jibu
Ni kwasababu katika kutengeneza 'narrative' kuna gap na kama ujuavyo historia hujidhihiri haiandikwi kwa utashi.
Ni historia inayoandikwa kwa prejudice, kwamba, Wanamapinduzi habari zao haziandikwi kwasababu wapo hai. Mawaziri wa Sultan ambao ni beneficiaries wa utawala wa kiarabu ndio wanafanyiwa quotations kana kwamba tulitegemea Muhsin aseme mapinduzi ni halali
Mohamed kachukua hati miliki pale anaposema ''Historia ya Kweli ya Tanganyika'' badala ya historia ya kweli ya wazee wake wa kidongo chekundu.
Ndio maana tunasoma vitabu na machapisho mbali mbali. Hili la kujimilikisha historia Mohamed kafaulu sana. Kawa hypnotize watu kiasi cha kwamba wanalipuka tu kwasababu Mohamed kaandika. Hili ni jambo la hatari sana, yaani hajengi watu kuwa na critical thinking, yeye ana pump incendiary remarks na hawa vijana wanabeba tu. Ukiwauliza maswali wanakwama kwasababu ya kujazwa hasira badala ya fikra
Hili analitumia sana kukwepa hoja. Ukimuuliza kitu kidogo utapata kurasa 4 kati ya hizo 3 ni picha na moja haielezi majibu ya hoja.
Yes, Mohamed Said yupo biased. Hivi tunategemea Mohamed aeleze kwa uyakinifu kisa cha Nyerere kukosana na Abdul Sykes! Mohamed hawezi kwasababu kufanya hivyo ataiudhi familia ya Sykes na wale waliokaribu. Ni obvious kulikuwa na tiff kati ya Abdul na Nyerere kitu ambacho Mohamed hataki kukisogelea. Anajua wazi nini Abdul alikuwa nyuma yake kiasi Mwl alimweka pembeni.
Nguruvi3,
Tuanze na hili la Sykes kufanya harakati nje ya Dar es Salaam.
Abdul Sykes alichukua uongozi wa TAA mwaka wa 1950.
Hupendi taarifa ndefu lakini hapa tunamzungumza mtu muhimu sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika:
''Mimi niliogopa nilipokabidhiwa Nyaraza za Sykes.
Nilikuwa nasoma hadi usiku wa manane na hii ni katika 1980s.
Najiuliza.
Hii ni kweli au naangalia Blockbuster ya Hollywood?
Sasa nikawa nachanganya na yale niliyokuwa nayaona udogoni nikajiambia mimi nina bahati kubwa kuzaliwa nyakati zile na watu wale.
Siku moja Ahmed Rashad Ali huyu alikuwa rafiki yake mkubwa Abdul Sykea ananieleza kuwa 1950 alimsindikiza Abdul Sykes kuonana na Jomo Kenyatta kwenye mkutano wa siri Nairobi.
Ilikuwa wakati wa Kombe la Gossage na yeye alikuwa Captain wa timu ya Zanzibar na mashindano yalikuwa Nairobi.
Nimekaa mwili umekufa ganzi.
Abdul Sykes anakwenda kuonana na Kenyatta na kasindikizwa na Ahmed Rashad.
Abdul ana miaka 24.
Hii kweli au Mzee Rashad sasa anatunga stori?
Ahmed Rashad akiwa mwanafunzi India 1945 WWII imemalizika.
Abdul Sykes yuko Kalieni Camp nje kidogo ya Bombay, sasa Mumbai.
Askari wa Burma Infantry wanangoje ''repatriation,'' kurudishwa makwao.
Amekwenda kumtembelea rafiki yake Abdul Kambini.
Hapo Kalieni ndipo Abdul na wenzake walipoamua kuunda TANU.
Nilikuwa nimeingia katika dunia ambayo sikujua kama ipo.
Nikasema lazima nikamilishe hiki kitabu hii historia ije kusomwa.
Waliokataa kuiweka historia hii katika kitabu cha Histria ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni walijua wanachokifanya.
Huyu ndiye mimi na baba yangu Abdulwahid Sykes:
Sijui kama umepatapo kusoma habari hizi hapo chini:
Mohamed Said: TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952
"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":
"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."
“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended
by leading members of the Mwanza Branch...”
(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda).''
Wewe hupendi taarifa ndefu kwa hiyo tusimame hapa tukimaliza nifahamishe tuzungumze kuhusu unachosema, ''ugomvi baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere na hili la historia ya Abdul Sykes kufutwa chembelecho kuwekwa, ''pembeni.''
Nachelea hapa tusiwe na makala ndefu sana.
Wala ndugu yangu sintokuhesabu kuwa ni muongo, nikukejeli na kukukebehi.
Mimi najua fika kuwa huwajui wazee wangu.
Siwezi kukulaumu kwa kutojua wala kutojua kitu si ujinga.
Hujui unajifunza.
Hivi ndivyo nilivyowachukulia Chuo Cha CCM Kivukoni walipokataa kumtia Abdul Sykes katika kitabu chao.
Ukweli unapodhihiri uongo ni wenye kutoweka.