1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Mimi sidhani kama kuna watu wanakukasirikia kwa sababu umeandika historia ya ndugu zako na uhusiano wao na TANU. Ni pale unapoigeuza kuwa ni historia ya jinsi waislamu hawakutendewa haki na wakristu kwa sababu ya uislamu wao ndio tunakushambulia. Historia yako inahojiwa kwa sababu mara nyingi unatumia ukaribu wako na ndugu zako kuwanyamazisha wote wasiokubaliana na wewe. Historia mara nyingi inaandikwa na wengi na hakuna mwenye hati miliki juu yake. Ni katika kuunganisha hizo historia tofauti ndio historia yenye uhalisia itakapopatikana. Kutegemea kuwa kila mtu atakubali kila unachoandika kwa sababu tu hao ni wazee wako na umepiga picha nao ni kujidanganya. Mara nyingi wanaoandika historia za watu waliokuwa karibu nao wanakuwa na upofu fulani kuhusu historia wanazoandika.

Amandla...
Fundi...
Vipi mimi ninaweza kuwa na uwezo wa kumnyamazisha mtu?
Wala sijasema mimi nina haki miliki ya historia ya Tanganyika.

Hizi picha zangu zinakuchoma sana ndugu yangu.
 
Hakuna, na ana haki ya kuandika 'memoir' na Mohamed hatakuwa wa kwanza

Na pia kuifanya historia ya ukoo wa Sykes kuwa historia ya Tanganyika.
Hakuna ushahidi wowote wa Sykes kufanya siasa nje ya Gerezani na kama upo Mohamed atueleze mkutano mmoja tu. Lakini pia hautuwezi kusahau kuwa ukoo wa Sykes ni mamluki waliokuja kuwapinga Wazalendo. Hivyo, walikuwa Wahalifu kabla ya kukumbatia Uzalendo

Ndio maana akiulizwa kwanini Wapelekwe Wamakonde wa Kipumbwi hana jibu
Ni kwasababu katika kutengeneza 'narrative' kuna gap na kama ujuavyo historia hujidhihiri haiandikwi kwa utashi.

Ni historia inayoandikwa kwa prejudice, kwamba, Wanamapinduzi habari zao haziandikwi kwasababu wapo hai. Mawaziri wa Sultan ambao ni beneficiaries wa utawala wa kiarabu ndio wanafanyiwa quotations kana kwamba tulitegemea Muhsin aseme mapinduzi ni halali

Mohamed kachukua hati miliki pale anaposema ''Historia ya Kweli ya Tanganyika'' badala ya historia ya kweli ya wazee wake wa kidongo chekundu.

Ndio maana tunasoma vitabu na machapisho mbali mbali. Hili la kujimilikisha historia Mohamed kafaulu sana. Kawa hypnotize watu kiasi cha kwamba wanalipuka tu kwasababu Mohamed kaandika. Hili ni jambo la hatari sana, yaani hajengi watu kuwa na critical thinking, yeye ana pump incendiary remarks na hawa vijana wanabeba tu. Ukiwauliza maswali wanakwama kwasababu ya kujazwa hasira badala ya fikra

Hili analitumia sana kukwepa hoja. Ukimuuliza kitu kidogo utapata kurasa 4 kati ya hizo 3 ni picha na moja haielezi majibu ya hoja.

Yes, Mohamed Said yupo biased. Hivi tunategemea Mohamed aeleze kwa uyakinifu kisa cha Nyerere kukosana na Abdul Sykes! Mohamed hawezi kwasababu kufanya hivyo ataiudhi familia ya Sykes na wale waliokaribu. Ni obvious kulikuwa na tiff kati ya Abdul na Nyerere kitu ambacho Mohamed hataki kukisogelea. Anajua wazi nini Abdul alikuwa nyuma yake kiasi Mwl alimweka pembeni.
Nguruvi3,
Tuanze na hili la Sykes kufanya harakati nje ya Dar es Salaam.
Abdul Sykes alichukua uongozi wa TAA mwaka wa 1950.

Hupendi taarifa ndefu lakini hapa tunamzungumza mtu muhimu sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika:

''Mimi niliogopa nilipokabidhiwa Nyaraza za Sykes.
Nilikuwa nasoma hadi usiku wa manane na hii ni katika 1980s.

Najiuliza.
Hii ni kweli au naangalia Blockbuster ya Hollywood?

Sasa nikawa nachanganya na yale niliyokuwa nayaona udogoni nikajiambia mimi nina bahati kubwa kuzaliwa nyakati zile na watu wale.

Siku moja Ahmed Rashad Ali huyu alikuwa rafiki yake mkubwa Abdul Sykea ananieleza kuwa 1950 alimsindikiza Abdul Sykes kuonana na Jomo Kenyatta kwenye mkutano wa siri Nairobi.

Ilikuwa wakati wa Kombe la Gossage na yeye alikuwa Captain wa timu ya Zanzibar na mashindano yalikuwa Nairobi.

Nimekaa mwili umekufa ganzi.
Abdul Sykes anakwenda kuonana na Kenyatta na kasindikizwa na Ahmed Rashad.

Abdul ana miaka 24.

Hii kweli au Mzee Rashad sasa anatunga stori?
Ahmed Rashad akiwa mwanafunzi India 1945 WWII imemalizika.

Abdul Sykes yuko Kalieni Camp nje kidogo ya Bombay, sasa Mumbai.
Askari wa Burma Infantry wanangoje ''repatriation,'' kurudishwa makwao.

Amekwenda kumtembelea rafiki yake Abdul Kambini.
Hapo Kalieni ndipo Abdul na wenzake walipoamua kuunda TANU.

Nilikuwa nimeingia katika dunia ambayo sikujua kama ipo.
Nikasema lazima nikamilishe hiki kitabu hii historia ije kusomwa.

Waliokataa kuiweka historia hii katika kitabu cha Histria ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni walijua wanachokifanya.

Huyu ndiye mimi na baba yangu Abdulwahid Sykes:

Sijui kama umepatapo kusoma habari hizi hapo chini:
Mohamed Said: TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952

"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":

"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."

“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended
by leading members of the Mwanza Branch...”

(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda).''

1622613485739.png

Wewe hupendi taarifa ndefu kwa hiyo tusimame hapa tukimaliza nifahamishe tuzungumze kuhusu unachosema, ''ugomvi baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere na hili la historia ya Abdul Sykes kufutwa chembelecho kuwekwa, ''pembeni.''

Nachelea hapa tusiwe na makala ndefu sana.
Wala ndugu yangu sintokuhesabu kuwa ni muongo, nikukejeli na kukukebehi.

Mimi najua fika kuwa huwajui wazee wangu.
Siwezi kukulaumu kwa kutojua wala kutojua kitu si ujinga.

Hujui unajifunza.

Hivi ndivyo nilivyowachukulia Chuo Cha CCM Kivukoni walipokataa kumtia Abdul Sykes katika kitabu chao.

Ukweli unapodhihiri uongo ni wenye kutoweka.
 
Sema sera ya vijiji vya ujamaa ingeundwa vizuri tungekuwa mbali.

Nahisi watu wa mikoa hii ya arusha Kilimanjaro hasa ndo waliingilia kupinga ujamaa.

Vile walijua vihamba vyao vitagawiwa.

Kufanya kazi pamoja kwa manufaa yenu wote ni nzuri.

Ni kama wasomi waliokuwepo hawakumsaidia mwalimu kuunda hivi vitu.

Mngezaliwa mjikute hivyo ni kuwa yangekuwa ndo maisha yetu.

Vita kweli vilipukuta uchumi wetu.

Akiba yote ikaishia vitani.

Ni kama tokea pale nchi haijakaa sawa tena.

Anyway nilimpenda sana Mwalimu Nyerere.
Tanzania Hatuwezi kufanya kazi pamoja, kuna familia za watu wavivu na watu wachapakazi haiwezekani kuwaunganisha lazima ufeli.
 
Mohamed Said
Hapo ndipo tunapotofautiana sana.
Rejea bandiko#224 ukijibu hoja ya '' Wapi na lini Abdul Sykes alifanya mkutano wa hadhara nje ya Gerezani''

#224 inaeleza Abdul kwenda kuonana na Kenyatta kwa Siri kupitia Ahmed Rashad
1. Kumbuka Nairobi si Tanganyika na wala hoja haikuhusu mkutano nje ya nchi
2. Maelezo ya Rashad na wewe ni ya 'kusadikika' chochote kinaweza kuwa kilitokea
3. Mzee Mkwawa hakukueleza kwanini Kipumbwi walipelekwa Wamakonde Unguja, hilo linabaki kuwa tamthlia, na kwavile ni mzee Mkwawa peke yake hilo ni vema ukabaki nalo
4. Mzee Kitwana ni special branch, Tambwe ni 'mole'' na ni Waislam !!Unasemaje kwa hili?

Pengine la Abdul Sykes tuliache, hakuwahi kufanya mkutano wowote nje ya Kariakoo sasa kumvisha kilemba cha Historia ya Tanganyika si uungwana, ni kama kumsimanga na hilo hatupendi. Hao ni wazee wako

Hadi sasa tunajua, kwa mujibu wa Mohamed, Mapinduzi ni haramu, pili Mohamed hajafanya mahojiano na wanamapinduzi wa Zanzibar akisubiri wafariki ili atuletee habari, tatu Mohamed amehoji wanaufaika wa Sultan kama Mawaziri akitegemea majibu anayotaka, nne, Mohamed hajui kwanini walichukuliwa Wamakonde kwenda kufanya mapinduzi na si askari, na tano, Abdul hakuwahi kufanya mkutano nje ya kidongo chekundu.

Nayaweka haya ili vijana wako wanaomeza wajifunze critical thinking

Kitendo cha kukutaja katika bandiko ni baada ya vijana wako kukunukuu tu kwasababu umesema na hawaelewi chochote kingine zaidi ya matusi. Mohamed hiki unachokifanya cha kujaza vijana jazba na kuviza uelewa wao si uungwana! Huwasidii unawadumaza kifikra
 
Mohamed Said
Hapo ndipo tunapotfautiana sana. Rejea bandiko#224 ukijibu hoja ya '' Wapi na lini Abdul Sykes alifanya mkutano wa hadhara nje ya Gerezani''

Maelezo ya #224 yanaeleza Abdul kwenda kuonana na Kenyatta kwa Siri kupitia Ahmed Rashad
1. Kumbuka Nairobi si Tanganyika na wala hoja haikuhusu mkutano nje ya nchi
2. Maelezo ya Rashad na wewe ni ya 'kusadikika' kwasababu chochote kinaweza kuwa kilitokea
3. Kwavile Mzee Mkwawa hakukueleza kwanini Kipumbwi walipelekwa Wamakonde Unguja, hilo linabaki kuwa tamthlia. Tunajua laiti ingalikuwa askari tungepata maelezo lakini kwa vile ni mzee Mkwawa peke yake hilo ni vema ukabaki nalo
4. Mzee Kitwana alikuwa special branach, na Tambwe alikuwa 'mole'' na hawa ni Waislam !!Unasemaje kwa hili?
Nguruvi,
Mimi sina tatizo.

Mimi naeleza yale ambayo hamkuwa mnayajua na hapa nazungumza na dunia nzima naandika wasome historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wala silazimishi watu kuniamini.
Usipate tabu.

Siko katika ubishani.
Wewe hukumjua Ali Mwinyi Tambwe.

Mimi ndiye nimekuletea historia yake.
Huu Uislam katika historia ya TANU unataabisha sana.

Lakini mimi nina khiyari gani?
Ndiyo niliowakuta katika historia hii na ndiyo walionizaa mimi.
 
Mo tafadhali sheikh usighadhabike. Ukiwaleta akina Ali Mwinyi Tambwe, sisi tunaotumia akili hatubebi tu na kukimbia nalo. Na hapa hoja kubwa kuhusu Tambwe na Kitwana ni hii;

Marhum Kitwana Kondo alikuwa special branch ya Wazungu na ndani ya TANU alikuwepo pandikizi la special branch uliloita 'mole' ambalo ni Marhum Ali Mwinyi Tambwe

Swali, hawa si wazee wako kwa maana Waislam? Hivi walichokuwa wanafanya ilikuwa kupigania Uhuru au kupigana dhidi ya Uhuru?
Hawa si ndio unatuambia walivuja jasho na damu!

Ndio maana nimekuuliza, unasemaje?
 
Again, Mohamed Said alaumiwe kwa kulisha watu habari zinazoviza akili zao.

Tumemuuliza Mohamed Said kwanini wachukuliwe Wamakonde wa Kipumbwi Tanga na siyo askari waliofunzwa! Mapinduzi hayakuwa jambo rahisi hivyo palihitajika wataalamu.
Mohamed Said hajajibu, katupia picha na maelezo mareeefu.

Madhara ya kauli zake ndiyo haya, mtu anasema 'Wakata mkonge' kwasababu amemsoam Mohamed, nikikuuliza kwanini wakata mkonge na si askari utajibu nini?

Mohamed angali madhara ya kauli zako yanavyo hypnotize society.
Hivi nyinyi vijana hata tukiwaomba mfanye majadiliano ya wazi na moh mtaweza? Hivi kwanini mnajadili zaidi moh na si alichokiandika? Hizi kasumba zitawatafuna
 
Mo tafadhali sheikh usighadhabike. Ukiwaleta akina Ali Mwinyi Tambwe, sisi tunaotumia akili hatubebi tu na kukimbia nalo. Na hapa hoja kubwa kuhusu Tambwe na Kitwana ni hii;

Marhum Kitwana Kondo alikuwa special branch ya Wazungu na ndani ya TANU alikuwepo pandikizi la special branch uliloita 'mole' ambalo ni Marhum Ali Mwinyi Tambwe

Swali, hawa si wazee wako kwa maana Waislam? Hivi walichokuwa wanafanya ilikuwa kupigania Uhuru au kupigana dhidi ya Uhuru?
Hawa si ndio unatuambia walivuja jasho na damu!

Ndio maana nimekuuliza, unasemaje?
Swala lako zuri lakini mbaya umejikita kwenye kuattack subject, hii itakuondoa kwenye maono ang'avu huwezi kuwa mwenye kufikiri vyema kama tayari umechagua upande (yaani umechagua kuwa hakuna muislam utakae mkubali katika historia)
 
Hivi nyinyi vijana hata tukiwaomba mfanye majadiliano ya wazi na moh mtaweza? Hivi kwanini mnajadili zaidi moh na si alichokiandika? Hizi kasumba zitawatafuna
Kwa taabu sana ninalazimika kukujibu
Majadiliano haya yapo wazi si siri yanasomeka na mtu aliye popote dunia anayeingia JF ,sijui unataka ya wazi yapi tena.

Kwamba , tunaweza kufanya mahojiano naye hilo si tatizo kwetu pengine ni tatizo kwako na wala usilifanye tatizo la umma.

Kumtaja Mohamed ni kumu adress. Huwezi kumtenga Mohamed na contents za maandishi yake
 
Hamna anaepinga kuwa kuna wengi waliochangia historia ya TANU lakini hawatajwi katika historia. Shida yangu na wewe ni pale unapojenga conspiracy theory kwenye kutengwa huko. Kwa mfano, kwenye picha hiyo kuna wanawake watano, wanne wamevaa baibui na mmoja hajavaa lakini wewe umewaona waliovaa baibui peke yake. Na kuweko picha yao pamoja na Nyerere hakuna maana kuwa wao walikuwa wanawake pekee waliomsindikiza Nyerere airport. Hauwezi kutumia picha kama hii kujenga hoja kuwa ni wanawake wakiislamu peke yao ndio waliomuunga mkono Nyerere. Na kutokuwepo picha hii Lumumba hakumaanishi kuwa ni ushahidi wa nia mbaya dhidi yao. Nyerere alipiga picha nyingi na watu tofauti na itakuwa vigumu kuwatendea wote haki sawa. Unapofanya kuwa absence ya picha kama hizi ni ushahidi wa hujma za Nyerere na TANU dhidi ya uislamu ni distortion ya makusudi ya historia.

Amandla...

Screenshot_20211214-191725_WhatsAppBusiness.jpg
 
Kwa taabu sana ninalazimika kukujibu
Majadiliano haya yapo wazi si siri yanasomeka na mtu aliye popote dunia anayeingia JF ,sijui unataka ya wazi yapi tena.

Kwamba , tunaweza kufanya mahojiano naye hilo si tatizo kwetu pengine ni tatizo kwako na wala usilifanye tatizo la umma.

Kumtaja Mohamed ni kumu adress. Huwezi kumtenga Mohamed na contents za maandishi yake
Lakini humtaji vyema, Laiti kama huna chembe za unafiki ni wazi mbali na kumtoa kasoro (jambo ambalo si baya hata yeye mwenyewe yu Radhi) basi walau ungetoa credit kwake, unajua mtu kama Paschal Mayalla Ana haiba tofauti kidogo na wagalatia wengi mfano wewe, sijui kwasababu paschal amapata kuishi na waislam, wewe samaki umekuwa ni mtu wakuchukizwa tu siku zote na Moh kiasi hana jema alilofanya
 
Tanzania Hatuwezi kufanya kazi pamoja, kuna familia za watu wavivu na watu wachapakazi haiwezekani kuwaunganisha lazima ufeli.

Ni kweli wachapa kazi tunaolazimishwa tuwajuwe ni hawa wanaotembelea V 8, tunawaona huku wakipiga domo jiiiingi.
 
Ni kweli wachapa kazi tunaolazimishwa tuwajuwe ni hawa wanaotembelea V 8, tunawaona huku wakipiga domo jiiiingi.
Hao ni wanasiasa si wachapakazi. chukua akili ya bakhresa umwambie afanye kazi sawa na mume wa amber rutty.
 
Tanzania Hatuwezi kufanya kazi pamoja, kuna familia za watu wavivu na watu wachapakazi haiwezekani kuwaunganisha lazima ufeli.
Naweza kukubaliana na wewe nusu kwa nusu.

Tungefanya pamoja uvivu haungewepo si ni kila mtu au familia na kipande chake?
 
Mo tafadhali sheikh usighadhabike. Ukiwaleta akina Ali Mwinyi Tambwe, sisi tunaotumia akili hatubebi tu na kukimbia nalo. Na hapa hoja kubwa kuhusu Tambwe na Kitwana ni hii;

Marhum Kitwana Kondo alikuwa special branch ya Wazungu na ndani ya TANU alikuwepo pandikizi la special branch uliloita 'mole' ambalo ni Marhum Ali Mwinyi Tambwe

Swali, hawa si wazee wako kwa maana Waislam? Hivi walichokuwa wanafanya ilikuwa kupigania Uhuru au kupigana dhidi ya Uhuru?
Hawa si ndio unatuambia walivuja jasho na damu!

Ndio maana nimekuuliza, unasemaje?
Nguruvi,
Wewe unajua kama mimi natukanwa sighadhibiki.
Vipi nikuhamakie kwa kuniuliza swali?

Kuwa Kitwana Kondo alikuwa Special Branch yeye mwenyewe akinieleza na watu wote wanajua.

Mimi siku zote naandika lile ninalolijua na simlazimishi mtu kuniamini.

Naam Kitwana Kondo alikuwa Special Branch wala hili halina shaka kama unavyoona hapa nalizungumza kwa wote kusoma na kujua.

Hii ndiyo historia ya TANU.

Nimekueleza kuwa mmoja wa wazee wangu alikuwa rafiki mkubwa wa Kimche ningekaa kimya usingejua lakini ningekuwa nimeifanyia khiyana historia ya mapinduzi.

Nimekueleza pia mkutano wa Nansio kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes Ali Mwinyi akiwapo kumjadili Nyerere kumtia kwenye uongozi wa TAA 1953.

Nimekueleza Abdul na Dossa kumpeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume hii 1954.

Kuisaidia ASP aliyeaminiwa kupeleka mifuko ya fedha kwa Karume alikuwa Abbas Sykes.
Hili sikulisema alipokuwa hai.

Nimeishi maisha yangu yote ya ukubwani pembeni ya Bwana Abbas na hakupenda kabisa yale yaliyotokea Zanzibar.

Nilistahi sana hisia zake.

Uandishi huu wa ukweli ndiyo kwa hakika uliojenga historia hii ya wazee wangu ipendeze na kuvutia wengi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Vyombo vya habari vinapopishana mlangoni pangu haya ndiyo wanayotafuta kutoka kwangu.

Mimi naijua historia hii kwa kuwa ni historia ya baba zangu.
Ndiyo maana na wewe hubanduki kwangu.

Nimekuteka na elimu yangu.
Hauko peke yako.

Mtaani kwangu wajukuu zangu vitoto vya mtaani kwangu wakimuona Mzungu haraka wanamuonyesha nyumba yangu.

Wanajua watu wa sampuli hii huja kwa babu.

Hawa wanafunzi Ph. D. kutoka kwingi akina Ann Lee Grimstad, James Brennan, James ''Sheikh Ahmed'' Brendon kwa kuwataja wachache.

Niliwajua wakiwa watoto wadogo wamenifata Tanga na ''backpack'' zao nimekwenda Amerika nimewakuta watu wazima maprofesa wanasomesha hii historia ya uhuru wa Tanganyika kama walivyopokea kwangu na kama walivyosoma katika kitabu cha Abdul Sykes.

Huu ndiyo urithi niliopokea kutoka kwa wazee wangu hawa.

Picha zangu kidogo zinakuudhi lakini nakuwekea kwani picha inazunguza maneno 1000 na kuna vijana huniuliza, ''Hivi kweli Mzee Mohamed uliwajua hawa watu waliofanya haya yote?''

1640683401429.png

Abbas Sykes nikimfanyia mahojiano ya TV nyumbani kwake Sea View 2012.
 
Naweza kukubaliana na wewe nusu kwa nusu.

Tungefanya pamoja uvivu haungewepo si ni kila mtu au familia na kipande chake?
Kwenye makaratasi ipo vizuri, maana tofauti ya masikini na tajiri inakuwa ndogo sana, mali zote ni mali za uma, shule ni za uma zinaboreshwa, hakuna mtoto wa tajiri na masikini watoto wote wanasoma shule za uma n.k.....

Kwenye makaratasi ni nzuri sana ila ukirudi kwenye uhalisia wote mnakuwa masikini kwa sababu binadamu hawafanani kiu ya mafanikio, hawafanani kuridhika, hawafanani uchapaji kazi sasa ukilazimisha akili ya modewj ifanane na akili ya Irene uwoya kiutendaji na kimapato kinachotokea ni ambao wangepambana kuleta mafanikio nchini wanahama kutafuta fursa sehemu zingine halafu nchi inabaki na lia lia wa kutaka kila kitu kifanywe na serikali.
 
Hivi nyinyi vijana hata tukiwaomba mfanye majadiliano ya wazi na moh mtaweza? Hivi kwanini mnajadili zaidi moh na si alichokiandika? Hizi kasumba zitawatafuna
Makala...
Madaktari wana kitu wanakiita, ''Denial,'' yaani kukataa.

Madaktari pale wanapomwabia mgonjwa maradhi yake hasa kama ni makubwa wao hujua mgonjwa atapokeaje.

Kwanza mgonjwa atakuwa kama vile haamini na nafsi inakataa kuwa ni kweli kisha baadae ndiyo akili ikitulia anakubali.

Hawa ndugu zangu wamesomeshwa historia ya uhuru wao wanaelezwa Nyerere kaunda TANU nk. nk. miaka nenda miaka rudi.

Siku jarida la Africa Events lilipochapa makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' (1988) nikasimulia historia ya TANU na mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika, ilikuwa kizaazaa.

Mshtuko mkubwa.
Magazeti yakakusanywa.

Kisha likaja jibu kali likiwa na vitisho dhidi yangu kutoka CCM Dodoma katika toleo lililofuatia.

Mwandishi Dr. Mayanja Kiwanuka.

Sasa angalia jamaa yangu hapa.
Kauliza mkutano aliofanya Abdul Sykes Tanganyika.

Nimemwekea taarifa ya Special Branch kuhusu Abdul Sykes na mkutano wake na Jomo Kenyatta.

Haamini kuwa ni kweli.
Hawaamini Special Branch au mimi nimeghushi.

Abdul hakufanya hayo yote.
Mimi ni muongo.

Chuki, hasad, choyo na wivu inawatia upofu hata wakionyeshwa kweli akili zao zinakataa.
Kwa nini haya wamejaaliwa wazee wake Mohamed kuyafanya?

Kwa nini neema hii haukuletwa kwetu?
Mimi namuhurumia kwani hasad ni katika maradhi makubwa ya nafsi.

Kwa kawaida ninapowaonyesha watafiti nyaraka hizi huwa wanapigwa na mshtuko mkubwa, ''Mohamed is this true 1950 a young boy from Dar es Salaam is having a secret meeting with Jomo Kenyatta in Nairobi?''

Prof. Haroub Othman yeye mshtuko wake wala siwezi kueleza.

Tusimame hapa yapo mengi yalitokea TANU yenyewe ilipoamua kuandika historia yake mara tu baada ya uhuru waandishi wakiwa Abdul Sykes na Dr. Wilbard Klerruu.

Picha kama kawaida kunogesha makala:

1640688378476.png

Mwandishi Akiwa Amesimama Nje ya Ofisi za Africa Events London, 1991

Ingia hapo chini:

Kwenye makaratasi ipo vizuri, maana tofauti ya masikini na tajiri inakuwa ndogo sana, mali zote ni mali za uma, shule ni za uma zinaboreshwa, hakuna mtoto wa tajiri na masikini watoto wote wanasoma shule za uma n.k.....

Kwenye makaratasi ni nzuri sana ila ukirudi kwenye uhalisia wote mnakuwa masikini kwa sababu binadamu hawafanani kiu ya mafanikio, hawafanani kuridhika, hawafanani uchapaji kazi sasa ukilazimisha akili ya modewj ifanane na akili ya Irene uwoya kiutendaji na kimapato kinachotokea ni ambao wangepambana kuleta mafanikio nchini wanahama kutafuta fursa sehemu zingine halafu nchi inabaki na lia lia wa kutaka kila kitu kifanywe na serikali.
Hata moo na uyoya wangekuwa originated from one source wangefanana tu.
 
Back
Top Bottom