1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Kuwa Kitwana Kondo alikuwa Special Branch yeye mwenyewe akinieleza na watu wote wanajua.
Hakuna ubishi katika hili midhali kakueleza. Hapa ndipo swali lililpo, je, alichokuwa anafanya ni kupigania uhuru au kupigana dhidi ya Uhuru? Na huyu si mzee wako kwa Maana ya Muislam?
Je, hakuwa anahujumu watu wake yeye na Mwinyi Tambwe?
Je, Kitwana na A.M. Tambwe hawakuhusika na kuwachomea akina Nyerere na pengine kuwaletea kesi? Katika Uislam hili linaitwajwe? Ushujaa, unafiki au uzandiki?
Mimi siku zote naandika lile ninalolijua na simlazimishi mtu kuniamini.
Hakika ni vema ndio maana tunakueleza haya tukiyasoma std 6 enzi hizo '' not every flower is a rose'
Naam Kitwana Kondo alikuwa Special Branch wala hili halina shaka kama unavyoona hapa nalizungumza kwa wote kusoma na kujua.

Hii ndiyo historia ya TANU.

Nimekueleza kuwa mmoja wa wazee wangu alikuwa rafiki mkubwa wa Kimche ningekaa kimya usingejua lakini ningekuwa nimeifanyia khiyana historia ya mapinduzi.

Nimekueleza pia mkutano wa Nansio kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes Ali Mwinyi akiwapo kumjadili Nyerere kumtia kwenye uongozi wa TAA 1953.

Nimekueleza Abdul na Dossa kumpeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume hii 1954.
Hayahusiani na hoja, Mohamed ni mgumu sana katika kujibu hoja
Kuisaidia ASP aliyeaminiwa kupeleka mifuko ya fedha kwa Karume alikuwa Abbas Sykes.
Hili sikulisema alipokuwa hai.
Sawa sawa ! halafu unamalumu Nyerere wakati kazi imefanywa na wazee wako. Unamlaumu Nyerere na Wamakonde wakati kazi imefanywa na wazee wako! hakuna siku walijutia hayo
Mapinduzi Daima leo unasema ni haramu ! haramu ya wazee wako!
Nimeishi maisha yangu yote ya ukubwani pembeni ya Bwana Abbas na hakupenda kabisa yale yaliyotokea Zanzibar.
Hakupenda lakini alishiriki, wamakonde wanasingiziwa
Nilistahi sana hisia zake.

Uandishi huu wa ukweli ndiyo kwa hakika uliojenga historia hii ya wazee wangu ipendeze na kuvutia wengi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Vyombo vya habari vinapopishana mlangoni pangu haya ndiyo wanayotafuta kutoka kwangu.

Mimi naijua historia hii kwa kuwa ni historia ya baba zangu.
Ndiyo maana na wewe hubanduki kwangu.
Mimi nimekuita uone jinsi ulivyodumaza vijana kwa kutoweza kufikiri. Katika uzi huu vijana wanakunuu tu ukiwauliza ilikuwaje wanasema 'Mohamed kasema'' hakuna critical thinking wanameza kila kitu, hakuna kutafuna mwisho matumbo yanawavurugika na kutuharibia ukumbi

Nipo hapa siku zote kuweka sawa mambo ya upotoshaji. Hili la Abbas Sykes ni la sita katia yale niliyokueleza yanatokana na mnakasha

Ninatatizika sana pale unapoulizwa kitu na kujibu kingine, hakuna summary wala 'concise'
Hili lifanyie kazi Mo, maana kama ni Mwl wanafunzi wako watafeli sana, samahani ni ukweli
Nimekuteka na elimu yangu.
Hauko peke yako.

Mtaani kwangu wajukuu zangu vitoto vya mtaani kwangu wakimuona Mzungu haraka wanamuonyesha nyumba yangu.

Wanajua watu wa sampuli hii huja kwa babu.

Hawa wanafunzi Ph. D. kutoka kwingi akina Ann Lee Grimstad, James Brennan, James ''Sheikh Ahmed'' Brendon kwa kuwataja wachache.

Niliwajua wakiwa watoto wadogo wamenifata Tanga na ''backpack'' zao nimekwenda Amerika nimewakuta watu wazima maprofesa wanasomesha hii historia ya uhuru wa Tanganyika kama walivyopokea kwangu na kama walivyosoma katika kitabu cha Abdul Sykes.

Huu ndiyo urithi niliopokea kutoka kwa wazee wangu hawa.

Picha zangu kidogo zinakuudhi lakini nakuwekea kwani picha inazunguza maneno 1000 na kuna vijana huniuliza, ''Hivi kweli Mzee Mohamed uliwajua hawa watu waliofanya haya yote?''

View attachment 2060411
Abbas Sykes nikimfanyia mahojiano ya TV nyumbani kwake Sea View 2012.

Ni kweli zinaudhi kwasababu hazihusiani na majadala. Nimekuuliza Fitna za Kitwana Kondo na Ali Mwinyi Tambwe wewe unamleta Abbas , inahusu nini ! unaleta wanafunzi wakizungu wakiwa na backpack yahusu nini.
 
Hakuna ubishi katika hili midhali kakueleza. Hapa ndipo swali lililpo, je, alichokuwa anafanya ni kupigania uhuru au kupigana dhidi ya Uhuru? Na huyu si mzee wako kwa Maana ya Muislam?
Je, hakuwa anahujumu watu wake yeye na Mwinyi Tambwe?
Je, Kitwana na A.M. Tambwe hawakuhusika na kuwachomea akina Nyerere na pengine kuwaletea kesi? Katika Uislam hili linaitwajwe? Ushujaa, unafiki au uzandiki?

Hakika ni vema ndio maana tunakueleza haya tukiyasoma std 6 enzi hizo '' not every flower is a rose'

Hayahusiani na hoja, Mohamed ni mgumu sana katika kujibu hoja

Sawa sawa ! halafu unamalumu Nyerere wakati kazi imefanywa na wazee wako. Unamlaumu Nyerere na Wamakonde wakati kazi imefanywa na wazee wako! hakuna siku walijutia hayo
Mapinduzi Daima leo unasema ni haramu ! haramu ya wazee wako!

Hakupenda lakini alishiriki, wamakonde wanasingiziwa

Mimi nimekuita uone jinsi ulivyodumaza vijana kwa kutoweza kufikiri. Katika uzi huu vijana wanakunuu tu ukiwauliza ilikuwaje wanasema 'Mohamed kasema'' hakuna critical thinking wanameza kila kitu, hakuna kutafuna mwisho matumbo yanawavurugika na kutuharibia ukumbi

Nipo hapa siku zote kuweka sawa mambo ya upotoshaji. Hili la Abbas Sykes ni la sita katia yale niliyokueleza yanatokana na mnakasha

Ninatatizika sana pale unapoulizwa kitu na kujibu kingine, hakuna summary wala 'concise'
Hili lifanyie kazi Mo, maana kama ni Mwl wanafunzi wako watafeli sana, samahani ni ukweli

Ni kweli zinaudhi kwasababu hazihusiani na majadala. Nimekuuliza Fitna za Kitwana Kondo na Ali Mwinyi Tambwe wewe unamleta Abbas , inahusu nini ! unaleta wanafunzi wakizungu wakiwa na backpack yahusu nini.
Nguruvi,
Nakupa historia kwa ukweli wake.
Tatizo liko wapi?

Mimi naijua historia ya Tanganyika na Zanzibar na naieleza kwa utafiti niliofanya na kwa kauli za walioshiriki.

Ikiwa nakutaabisha si acha kunisoma?
Kwani unalazimishwa?

Nyerere nimlaumu nini mimi?

Nimemweleza kama alivyokuwa kuwa historia ya Tanganyika dhidi ya Ukoloni haianzi na yeye.

Mengine ya Zanzibar nimeyaeleza kama yalivyokuwa.

Ningependa kukufahamisha kuwa hakuna wa kunifunza kitu katika historia hii.

Nadhani unajua vipi nilivyosuhubiana na hawa wahusika kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Wewe mchango wako hapa barzani ni kuniuliza mimi maswali.

Unalo la zaidi ya hilo?
 
Walaa huntaabishi kabisa, nipo nawe miaka mingi sana tukijadili hizi Ngano
Nyerere nimlaumu nini mimi?
Si ndiye aliyepeleka wamakonde Zanziabr ambao huwezi kueleza kwanini wamakonde na si askari
Leo unaeleza wazee wako akina Sykes walihusika katika mapinduzi unayosema ni haramu

Tunajua historia imeanza hata Nyerere hajazaliwa, hiyo haiondoi mchango wake katika wakati wowote wa historia uwe mdogo au mkubwa na hasa ukweli kuwa alikuwa Rais wa Tanganyika si Abdul

Fundi Mchundo kakueleza wazi kwamba wewe unataka kuchukua umiliki wa historia , si kweli.
Historia ni mkusanyiko wa habari zinazotoka katika sources tofauti. Hadi leo watu wanatafiti historia ya Uingereza seuse wewe na Sykes ya juzi

Ukinywa chai nao si ushahidi maana Fundi Mchundo kakuonyesha wazi wakati yakitokea hukuwepo na uliyokuwepo ulikuwa mtoto. Kakupa facts

Ahaaa! maswali yanayofikirisha na kuonyesha matundu ya historia . Kupitia hayo maswali wanaofikiri (siyo kumeza) wanajiuliza ' wait a minute' halafu wanatafuta ukweli.
Kuna text nazipata ' umetufumbua n.k.'
Unalo la zaidi ya hilo?
Yes
1. Familia ya Sykes ilihusika na mapinduzi ya Zanzibar unayoita haramu
watu wakisema Nyerere lanatullah basi wasikomee hapo, waendelee Sykes, Kitwana na Tambwe

2. Kitwana Kondo na AM Tambwe walihujumu harakati wakiwa wazee wako(waislam), fitna
3. Huna majibu kwanini wamakonde wa Kipumbwi na si askari- ngano na tamthilia
4. Hukuhoji wanampainduzi kwa kisingizio cha kusubiri wafariki ili utuletee picha ...
5. Umetafiti kwa bias, hivi unamhoji Jamsheed au waziri wake ukitegemea akwambie nini kuhusu mapinduzi ya Unguja.
6. Abdul Sykes hakuwahi kufanya mkutano wowote na popote Tanganyika nje ya Tandamti na kipata
 
Bahati mbaya ni bazazi mkosa Adabu, ndani ya mijadala ya KIELIMU anaingiza majivuno na kutweza wengine, utamuona mara kadhaa akitumia kiingereza kama limbukeni kisha achanganya na kiswahili, sijapato kufahamu ni msomi wa kiwango gani hasa, kushindwa kutambua hilo, hebu ajikite kwenye hoja hasa nini hasa tatizo? Uandishi wako uliojumuisha vyanzo mbalimbali vya taarifa? Wewe kuwa muislam? Au historia kuwa imegubikwa na uislamu na waislamu wengi
 
Ukienda kwenye Kitabu cha muandishi kama "Walter Rodney" utakuta mifano mingi kutoka mahali ambako wengi ni waislam, atakutajia mifano ya Timbuktu University, Kilwa empire, Mali, atakutajia mifano kadhaa kutoka Afrika kaskazini na huko magharibi ambako huko kote wako waislam, sasa mfano wa watu kama huyu samaki Lazima ataghadhibika kuona Walter kawaanika mabazazi wa kizungu walivyorejesha nyuma Maendeleo ya mam Afrika
 
Walaa huntaabishi kabisa, nipo nawe miaka mingi sana tukijadili hizi Ngano

Si ndiye aliyepeleka wamakonde Zanziabr ambao huwezi kueleza kwanini wamakonde na si askari
Leo unaeleza wazee wako akina Sykes walihusika katika mapinduzi unayosema ni haramu

Tunajua historia imeanza hata Nyerere hajazaliwa, hiyo haiondoi mchango wake katika wakati wowote wa historia uwe mdogo au mkubwa na hasa ukweli kuwa alikuwa Rais wa Tanganyika si Abdul

Fundi Mchundo kakueleza wazi kwamba wewe unataka kuchukua umiliki wa historia , si kweli.
Historia ni mkusanyiko wa habari zinazotoka katika sources tofauti. Hadi leo watu wanatafiti historia ya Uingereza seuse wewe na Sykes ya juzi

Ukinywa chai nao si ushahidi maana Fundi Mchundo kakuonyesha wazi wakati yakitokea hukuwepo na uliyokuwepo ulikuwa mtoto. Kakupa facts

Ahaaa! maswali yanayofikirisha na kuonyesha matundu ya historia . Kupitia hayo maswali wanaofikiri (siyo kumeza) wanajiuliza ' wait a minute' halafu wanatafuta ukweli.
Kuna text nazipata ' umetufumbua n.k.'

Yes
1. Familia ya Sykes ilihusika na mapinduzi ya Zanzibar unayoita haramu
watu wakisema Nyerere lanatullah basi wasikomee hapo, waendelee Sykes, Kitwana na Tambwe

2. Kitwana Kondo na AM Tambwe walihujumu harakati wakiwa wazee wako(waislam), fitna
3. Huna majibu kwanini wamakonde wa Kipumbwi na si askari- ngano na tamthilia
4. Hukuhoji wanampainduzi kwa kisingizio cha kusubiri wafariki ili utuletee picha ...
5. Umetafiti kwa bias, hivi unamhoji Jamsheed au waziri wake ukitegemea akwambie nini kuhusu mapinduzi ya Unguja.
6. Abdul Sykes hakuwahi kufanya mkutano wowote na popote Tanganyika nje ya Tandamti na kipata
Nguruvi3,
Mimi nimeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes unaita ngano.
Sawa ni ngano lakini bado unataka kujadili ngano na mwandishi wa ngano.

Ngano zinapuuzwa hazijadiliwi.
Hakuna cha kujadili kwenye porojo.

Waze wangu wote walikuwa TANU na ASP hili wala silikatai.

Nimekueleza hapa kuwa baba yangu marafiki zake wakubwa walikuwa Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala.

Hawa ni ASP kindakindaki na wana mapinduzi na kulikuwa na picha sebuleni kwetu ya hawa pamoja na baba yangu.

Picha hii ilitunguliwa walipouawa.
Baba yangu kwa uchungu wa kuuliwa rafiki zake hakuwa na moyo wa kuitazama hii picha.

Kuna mambo mengine mimi nakunyamazia sijibu kwa kuwa sipendi ubishi nakuachia useme upendavyo.

Wapi nimesema Abdul alikuwa Rais?

Nikisema hivyo si nitachekesha barza?

Unapenda hii ''chai,'' unairudia mara nyngi tu.

Kejeli na kebehi.

Sawa.
Ndicho ulichonacho.

Wewe unapata ''text,'' ziweke hapa tuzisome.

Mimi niko katika Dictionary of African Biography, Nyerere Biography, Cambridge Journal of African History, Library of Congress, kitabu cha Abdul Sykes kinasomeshwa vyuo kadhaa Ulaya na Marekani, nimezungumza vyuo kadhaa Afrika na Marekani, nimeandika vitabu 10 nimezunguka ulimwengu si kwa lolote ila kwa kalamu yangu.

Nadhani unajua kuwa nimetunukiwa ''cerificate,'' hapa JF.

Wewe unatamba na ''text.''
Sawa ndicho ulichojaaliwa.

Lakini hata mimi napata ''text.''

Umesoma mara kadha nikikuambia kuwa sitakuita muongo kwa kuwa najua hujui.

Fanya ''search,'' na rejea kusoma maneno hayo.

Hebu niambie wasomaji wangapi wapo katika uzi huu?

Unadhani wanakuja kukusoma wewe na kejeli na kebehi zako?

Umepata kuandika kitabu chochote, paper, kualikwa kwenye vyuo?

Unaandika umejificha.

Mohamed Said yuko hapa in ''flesh and blood.''

Atakae kuhojiana na yeye na ajitokeze.

Sijajificha.
Sijifichi kwa kuwa nasema kweli.

Jitokeze hapa nikuone na wasomaji wakuone.

Huwezi.
Muoga.

Babu yangu Salum Abdallah kapigania uhuru wa Tanganyika lau baba yake babu yangu mkuu Samitungo Muyukwa Mwekapopo kaingia Germany Ostafrika akitokea Belgian Congo amebeba bunduki na jeshi la Wajerumani kuja kupigana na Waafrika wenzake - Mtwa Mkwawa na Abushiri bin Salim Al Harith.

Hii ni historia ya babu zangu siikatai kwani ndiyo ukweli wenyewe.

Wala siionei aibu kwani hii ni changamoto katika changamoto za ukoloni.

Nacheka.

Abdul Sykes na mikutano ya Tandamti.

Kejeli na kebehi kwa wazee wangu.

Sawa.

Mkutano na Jomo Kenyatta, Peter Mbiu Koinange, Kung'u Karumba, Bildad Kaggia, Paul Ngei na viongozi wengine wa KAU hii kwako si lolote.

Au hujui kama hii ndiyo ile timu ya Kapenguria?

Wasomaji wangu wa maana historia hii huwashangaza.

Choyo, chuki, hasad na wivu vimekutawaleni mnafikia hata kubadili historia za watu na kupenyeza uongo.

Nani mjanja aliyefutiwa historia ya wazee wake au yule aliyeirejesha?
Naam historia hii ilifutwa na mimi nimeiandika na sasa tunaijadili.

Lakini Prof. Haroub aliposoma kitabu cha Abdul Sykes na cha Sheikh Ali Muhsin Barwani, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumwambia kuwa Mwalimu na wewe lazima uandike ueleze upande wako kwani Mohamed Said kasema mengi ambayo yamepindua historia yako yote na ''legacy,'' yako.

Hakuishia hapo alikwenda kwa Ahmed Rashad kuuliza historia ya Abdul Sykes.

Wazee wangu wote kama nilivyokueleza walikuwa TANU na ASP na najua ushiriki wao katika mapinduzi ya Zanzibar.

Leo Abdul Sykes hakuna asiyejua historia yake katika uhuru wa Tanganyika na yeye na mdogo wake Ally wametunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru ingawa baada ya miaka 50.

Picha kidogo:

1640709270197.png

Kulia Sheikh Ahmed Islam, Ahmed Rashad na Prof. Haroub Othman Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere safari ya Jeddah 1997.

Nilikuwa na hawa wazee safari moja Jeddah, Makka na Madina na ilikuwa nafasi kubwa kwetu sote kuulizana mengi.
 
Nimepata kusoma moja ya kitabu alichoandika huyu Mzee Erasto Mang'enya kinaitwa " Displine and Tears".ni kitabu kizuri Kwa kweli kikielezea uzoefu wake kama mwalimu kipindi cha ukoloni mpaka Uhuru.
 
Mang'enya alikuja kupewa uchifu WA heshima WA kibondei baadae baada ya kuhaso Sana kama mwalimu akizunguka Tanzania.Si kama 'machifu' hao uwazaniao.tafuta kitabu chake cha Displine and Tears utapata uhalisia humo
 
Umeandika Kwa utulivu,kiutu uzima,kikomavu,Kwa upeo WA mbali na Kwa uwazi na ukweli..post hii moja inatosha kabisa kufunga huu mjadala.
 
Nguruvi3,
Waze wangu wote walikuwa TANU na ASP hili wala silikatai.
Kwahiyo kumsema Nyerere vibaya ni fitna !
Wapi nimesema Abdul alikuwa Rais?Nikisema hivyo si nitachekesha barza?
Nakukumbusha tu Sheikh, Abdul hata apakwe rangi na Nyerere apakwe matope historia inaeleza, Nyerere alikuwa Rais wa Tanganyika huru, Abdul Sykes hakuwahi
Mimi niko katika Dictionary of African Biography, Nyerere Biography, Cambridge Journal of African History, kitabu cha Abdul Sykes kinasomeshwa vyuo kadhaa Ulaya na Marekani, nimezungumza vyuo kadhaa Afrika na Marekani, nimeandika vitabu 10 nimezunguka ulimwengu si kwa lolote ila kwa kalamu yangu.
Mashallah hizo ni neghma za Mwenyezi. Penye matundu tutakuonyesha tu hapa sivyo, hili kweli lile ngano. Hizo ndizo changanoto za kuwa ''academician' wa kweli
Umesoma mara kadha nikikuambia kuwa sitakuita muongo kwa kuwa najua hujui.
Fanya ''search,'' na rejea kusoma maneno hayo.
Sheikh kwani kutokujua ni kosa au laana. Punguza ghadhabu muungwana.
Sindano zauma lakini ndio dawa ivo!
Hebu niambie wasomaji wangapi wapo katika uzi huu?
Unadhani wanakuja kukusoma wewe na kejeli na kebehi zako?
kheri
Umepata kuandika kitabu chochote, paper, kualikwa kwenye vyuo?
Unaandika umejificha.

Mohamed Said yuko hapa in ''flesh and blood.''
Atakae kuhojiana na yeye na ajitokeze.

Sijajificha.
Sijifichi kwa kuwa nasema kweli.

Jitokeze hapa nikuone na wasomaji wakuone.

Huwezi.
Muoga.
Hapa umepata ghadhabu weli, pata funda la maji kaa kitako halafu tuongee sheikh.
Starehe ya mnakasha ni kuridhiana , laa kwasasa nakusihi upumue kidogo funda lititie tumboni
Babu yangu Salum Abdallah kapigania uhuru wa Tanganyika lau baba yake babu yangu mkuu Samitungo Muyukwa Mwekapopo kaingia Germany Ostafrika akitokea Belgian Congo amebeba bunduki na jeshi la Wajerumani kuja kupigana na Waafrika wenzake - Mtwa Mkwawa na Abushiri bin Salim Al Harith.

Hii ni historia ya babu zangu siikatai kwani ndiyo ukweli wenyewe.
Wala siionei aibu kwani hii ni changamoto katika changamoto za Ukoloni.
Ndio na huo ni ukweli. Akina Sykes walikuja kama Babu Mwekapopo
Abdul Sykes na mikutano ya Tandamti.
ndiyo Tandamti na Kipata
Sawa.

Mkutano na Jomo Kenyatta, Peter Mbiu Koinange, Kung'u Karumba, Bildad Kaggia, Paul Ngei na viongozi wengine wa KAU hii kwako si lolote.
Nilikuuliza Tanganyika, huko ulikotaja ni Kenya. Tuonyeshe eneo moja nje ya Tandamti, Kipata au new street ambako Abdul aliwahi kufanya mkutano hata mmoja,
Au hujui kama hii ndiyo ile timu ya Kapenguria?
Kapenguria siyo Tanganyika
Choyo, chuki, hasad na wivu vimekutawaleni mnafikia hata kubadili historia za watu.
Nani mjanja aliyefutia historia ya wazee wake au yule aliyeirejesha.
Seheikh Mohmed ghadhabu haifai, kaa chini pata funda la maji.
Wazee wangu wote kama nilivyokueleza walikuwa TANU na ASP na najua ushiriki wao katika mapinduzi ya Zanzibar.
Basi ikipigwa Nyerere laanatullah, watu wasisahau 'wazee wa Mohamed laatutllah'
Wote waliunga mkono Mapinduzi daima chini ya ASP.

Ila Kitwana na Ali waliokuwa special branch walikuwa fitna wakimpinga Nyerere kwa kutumika na wakoloni. Halafu vijana wako wanasema Nyerere alikuwa kibaraka, kumbe kuna watu waliokuwa na Fitna . Hili nalo umetusaidia kujua na hapa ndio nakupa credit kama Makala josee anavyosema. Hatukujua hawa watu walikuwa na Fitna sana

Mohamed, kama ningalikuwa kule Magila Mission au Ngamiani barabara ya II kwetu ningekuambia maneno machache sijui kama hayataudhi ' tupumzike kidogo ili urudishe moyo, nshakusamhe ulipo ghafilika, hakika sisi ni viumbe dhaifu kusameheana ndio uungwana
 
Kwahiyo kumsema Nyerere vibaya ni fitna !

Nakukumbusha tu Sheikh, Abdul hata apakwe rangi na Nyerere apakwe matope historia inaeleza, Nyerere alikuwa Rais wa Tanganyika huru, Abdul Sykes hakuwahi

Mashallah hizo ni neghma za Mwenyezi. Penye matundu tutakuonyesha tu hapa sivyo, hili kweli lile ngano. Hizo ndizo changanoto za kuwa ''academician' wa kweli

Sheikh kwani kutokujua ni kosa au laana. Punguza ghadhabu muungwana.
Sindano zauma lakini ndio dawa ivo!

kheri

Hapa umepata ghadhabu weli, pata funda la maji kaa kitako halafu tuongee sheikh.
Starehe ya mnakasha ni kuridhiana , laa kwasasa nakusihi upumue kidogo funda lititie tumboni

Ndio na huo ni ukweli. Akina Sykes walikuja kama Babu Mwekapopo

ndiyo Tandamti na Kipata

Nilikuuliza Tanganyika, huko ulikotaja ni Kenya. Tuonyeshe eneo moja nje ya Tandamti, Kipata au new street ambako Abdul aliwahi kufanya mkutano hata mmoja,

Kapenguria siyo Tanganyika

Seheikh Mohmed ghadhabu haifai, kaa chini pata funda la maji.

Basi ikipigwa Nyerere laanatullah, watu wasisahau 'wazee wa Mohamed laatutllah'
Wote waliunga mkono Mapinduzi daima chini ya ASP.

Ila Kitwana na Ali waliokuwa special branch walikuwa fitna wakimpinga Nyerere kwa kutumika na wakoloni. Halafu vijana wako wanasema Nyerere alikuwa kibaraka, kumbe kuna watu waliokuwa na Fitna . Hili nalo umetusaidia kujua na hapa ndio nakupa credit kama Makala josee anavyosema. Hatukujua hawa watu walikuwa na Fitna sana

Mohamed, kama ningalikuwa kule Magila Mission au Ngamiani barabara ya II kwetu ningekuambia maneno machache sijui kama hayataudhi ' tupumzike kidogo ili urudishe moyo, nshakusamhe ulipo ghafilika, hakika sisi ni viumbe dhaifu kusameheana ndio uungwana
Nguruvi 3,
Kuna mtu kasema Bwana Mkush kwangu mimi niloyosema yametosha kufunga mjadala.

Nimefuata ushauri wake.
 
"This book is not about TANU, nor even about the struggle for Uhuru in Tanganyika; it is about the part that Sykes and his Muslim associates played in that struggle. It suggests (incidentally, not deliberately) what might have happened if the TAA (Tanganyika African Association) had not handed over to the TANU (Tanganyika African National Union) and Sykes to Nyerere in 1953. At that moment there was lift-off and Nyerere began nation-building."

Nguruvi3

Amandla.......
 
Review by Brian Eccles (Zanzibar & Tanganyika 1952-61)

1640752738359.png
This book is not about TANU, nor even about the struggle for Uhuru in Tanganyika; it is about the part that Sykes and his Muslim associates played in that struggle. It suggests (incidentally, not deliberately) what might have happened if the TAA (Tanganyika African Association) had not handed over to the TANU (Tanganyika African National Union) and Sykes to Nyerere in 1953. At that moment there was lift-off and Nyerere began nation-building.0B
This book divides itself into four parts. The first is concerned with the Kleist family history, their coming from Mozambique to settle in Arab-dominated but German-ruled Dar es Salaam. The second part concerns Kleist's father's role in Dar es Salaam docks and the son's assumption at the age of 24 of the General Secretaryship of the Dockworkers Union. (The family name was Kleist in German Colonial times, it was Sykes in British Colonial times).
Five years' later Abdulwahid was manoeuvring to get Nyerere, a Christian, to run the Tanganyika African Association (TAA) which he had built on the foundation of the Dockworkers Union. A National party needed the support of up-country Christians and what the author calls 'Nyerere intellectuals'. This was Abdulwahid's great decision. It is the theme of the third part of the book.
The fourth part is concerned with the author's second thoughts; should not Mrima (the coastal area) have remained the effective power base (which colonialism - whether Arab, German or British - had made it) in Tanganyika? Union with Zanzibar was to create additional problems.
The book's sub-title is "the untold story of the Muslim struggle against British Colonialism in Tanganyika". Nyerere embarks on more than that. For him, a man from the Lake Victoria area, Tanganyika was more than the Mrima area, indirect rule was an old-fashioned colonial concept. The new Tanganyika needed direct rule (a concept that it was more difficult to impose on Zanzibar and Pemba).
How little we British knew of the aspirations of Tanganyika politicians (still less understood or sympathised with them). Nyerere changed this, whereas Abdulwahid went on ploughing his lonely furrow.
After the 1958 election the author admits that "the Muslims who had sacrificed a lot in the struggle... began to lose control of policies, and were consequently marginalised, never again to regain their political power". This was the equality of opportunity for which Nyerere had worked but about which Sykes had reservations.
This is a fascinating if erratic book for those of us who were participants or even bystanders.

Ndugu zanguni huu mjadala kwa upande wangu nilishauhitimisha.
Hapa nazungumza na Bwana Brian Eccles mwandishi wa review ya kitabu cha Abdul Sykes.

Kwa makusudi kabisa nimeweka review yake yote ili usihadaike na kipande kifupi kilichowekwa.

Kipande hicho kimenikumbusha mzee wangu Aboud Jumbe alipokuwa ananihadithia yale yaliyotokea Dodoma na kusabisha yeye kujiuzulu.

Anasema Mwalimu alikuwa anasoma kutoka barua yake zile sehemu ambazo yeye Mwalimu alikuwa anazipenda.

Jumbe akimwambia asome na hizo sehemu nyingine Mwalimu alikuwa anakataa kusoma anashikilia hapo hapo kama mtoto aliyepewa pipi na sasa anataka kunyang’anywa.

Brian Eccles anasema kitabu kina sehemu nne.
Si kweli kitabu cha Abdul Sykes kina sehemu tatu.

Lakini sitamuita muongo nataka niwe na dhana nzuri na yeye.

Namchukulia kuwa labda hakukisoma kitabu au si mtu makini kahemkwa na kuona kitabu kimetaja, ‘’…the untold story of the Muslim Struggle Against British Colonialism…’’

Hili la Uislam kama kawaida limemuudhi ndipo akafungua andiko lake kwa kusema kuwa kitabu hiki hakihusu TANU wala harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na akaendelea na maneno mengine.

Naamini wasomaji wangu sihitaji hapa mimi kusherehesha chochote kwani kitabu hiki ni maarufu na waliokisoma wanajua nini kilichopo ndani yake.

Lakini sitamwita muongo.

Namchukulia kama ninavyowachukulia wengine kuwa hajui kitu anahangaishwa na mhemko.

Anaendelea kusema kipi kingetokea iwapo harakati zisingepewa Nyerere nk. nk.
Sasa haya si maneno yake haya maneno kayachukua kutoka kwangu.

Nimeeleza katika kitabu kuwa baada ya serikali kutoa Government Circular No. 1 August 1, 1953 kuwakumbusha wafanyakazi wa serikali kutojihusisha na siasa mambo ndiyo yakapamba moto.

Kuna mengii hapa siwezi kuyaeleza yote itoshe tu kusema kuwa kipindi hiki President wa TAA alikuwa Julius Kambarage Nyerere na Makamu wa Rais Abdulwahid Kleist Sykes wanaelekea kwenye kuunda TANU.

Bwana Eccles anazungumza kuhusu, ‘’Nyerere intellectuals.’’
Hakuna neno hilo katika kitabu changu.

Nimetumia neno, ‘’Makerere Intellectuals,’’ na hilo neno nimelipata kutoka kwa Judith Listowel katika kitabu chake, ‘’The Making of Tanganyika,’’ (1965).

Kutoka hapa ndipo Eccles anazungumza sehemu ya nne ya kitabu cha Abdul Sykes ambayo haipo.

Sina la kusema kwa uchovu.

Hapa nafunga mdomo wangu na kalamu yangu naiweka chini kwa kuwa siwezi kuandika kuhusu kitu kisichokuwapo.

Wala sioni sababu ya kugusa makosa yake katika uandishi.
Hajui wapi kwa kuweka herufi kubwa wapi herufi ndogo.

Haya ndiyo ya Bwana Brian Eccles yaliyowekwa hapa niliyoletewa.
Huyu Eccles mimi nimesoma miaka 22 iliyopita na nikampuuza.

Waswahili tuna msemo ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.

Haya mambo yanataka sana subra.
Kazi kwenu wasomaji wangu.

Lakini Mzungu ni Mzungu hata akiwa wa karata.
Mtaka nyingi nasaba humkuta mwingi msiba.

Kataka kadha kapata kadha wa kadha.

1640753662793.png
 
Review by Brian Eccles (Zanzibar & Tanganyika 1952-61)

View attachment 2061301

View attachment 2061307
Ni vizuri kuwa umejibu review ya Eccles na umeweka wazi mapungufu yake. Lakini ukweli bado ni kuwa ulicho andika ni historia ya Abdulwahid Sykes na sio historia ya TANU. Kwa kufanya hivyo umeangalia zaidi mchango wake katika uanzishwaji wa TANU na haukuangalia sana michango ya wengine. Aidha, umeangalia pia kile unachoona ni kusahauliwa kwa mchango wa waislamu katika mapambano dhidi ya ukoloni wa muingereza. Hiki sisi hatuna shida nacho. Ni haki yako na unastahili pongezi kwa kufanya hivo.

Tunachopinga ( kama alivyosema Eccles) ni kutaka kuifanya historia ya Abdulwahid Sykes ndio historia ya TANU na kutaka kutuaminisha kuwa waislamu ( hususan wale wa Gerezani) hawakutendewa haki kwa maksudi ingawa wao ndio walioongoza mpambano. Sisi tunaona huu ni uongo kwa sababu vita dhidi ya ukoloni haikupiganwa kwa msingi wa udini au ukabila. Na kuna waislamu waliwapinga wale waliotaka kuingiza udini katika vita ile. Hili mara nyingi linakuwa wazi kwenye mabandiko yako na kwenye mafundisho yako kwa waislamu wenzako. Huu ni udini na unalenga katika kulets mpasuko katika jamii.

Vita ya Maumau iliyowahusisha wakina Kenyatta ilikuwa inapigania haki za wakikuyu zaidi ya haki ya wakenya kwa ujumla. Hii imechangia sana ukabila uliopo Kenya hadi leo. Lakini wakina Sykes ( Btw Sykes alikutana na wakina Kenyatta mwaka 1950 kwa sababu wakati ule ndoto ilikuwa ni panafricanism na aliona ni wajibu wa watanganyika na waganda kusaidia Kenya African Union katika mpambano yao na waingereza) walitambua kuwa ni lazima washirikiane na watu kutoka sehemu za Tanganyika na wa dini nyingine ili uhuru wa nchi yao uweze kupatikana. Ndio maana toka mwanzo walishirikiana na wakina Martin Kayamba msomi wa Oxford kutoka Tanga ambae mwaka 1922 aliyeanzisha the Tanganyika Territorial African Civil Servants Association na kwa kiasi kikubwa kiliwezesha kuanzishwa kwa Tanganyika African Association na wakina Kleist Sykes, Cecil Matola na wengine mwaka 1929 baada ya kushauriwa kufanya hivyo na Dr. James Aggrey kutoka Ghana.

Ni ukweli kuwa ingawa makao makuu yalikuwa Dar, ni matawi ya Dodoma na Bukoba ndio yalikuwa radical. Dar es Salaam walijikita zaidi katika mambo social na kutafuta uwakilishi katika serikali ya kikoloni. Wakina Erica Fiah walipingwa walipotaka kukifanya chama kuwa radical zaidi. Ni wazi kuwa wakina Sykes, Vedasto Kyaruzi na vijana wengine walileta mapinduzi katika TAA kwa kuwaondoa wazee wao wakina Kleist na Cecil katika sehemu za uongozi. Kila siku unazungumzia wakina Sykes kumpokea Nyerere alipokuja Dar kama vile wao ndio walimuingiza katika siasa za TAA. Hiki si kweli kwa sababu Nyerere alijiunga na TAA mwaka 1945 na alianzisha tawi Makerere alipokuwa anasoma na wakina Andrew Tibandebage na Hamza Kibwana Mwapachu baada ya kuanzisha nao the Tanganyika African Welfare Association.

Madai ya uhuru hayakuwa ya watu weusi peke yao, kuna wazungu kama Tom Tyrrell ( Tanganyika European Council, Capricorn Africa Association, United Tanganyika Party), wakulima Derek Bryceson na Lady Chesham ambao waliungwa mkono na TANU katika uchaguzi wa 1958-59. Lady Chesham alianzisha the Community Development Trust of Tanganyika mwaka 1962 na Bryceson alikuwa mbunge na waziri katika serikali baada ya uhuru. Kuna wahindi kama Amir Jamal na Abdulkarim Karimjee ambao waliunga mkono TANU. Kilichokuwa wazi ni kuwa wazee wetu walifanya juhudi za ziada kuvuka mipaka ya udini, ukabila na urangi katika jitihada zao za kupigania uhuru wa Tanganyika. Haikuwa one man show ya Abdul Sykes na Nyerere. Haikuwa ya wakina Dossa Aziz wa Gerezani peke yao. Haikuwa ya wagalatia wakina Oscar, Dennis, Andrew peke yao. Ilikuwa ya watanganyika, period. Wakina Sykes na Nyerere walikuwa viongozi lakini bila ridhaa ya watanganyika kutoka bara na mrima, wa makabila yote, wa dini zote wasingeambulia kitu.

Naona katika kum beza Eccles umewakandia wazungu wote ukisahau kuwa kwa kiasi kikubwa maandiko yako yametokana na maandiko ya wakina John Iliffe na shule unazotambia kuwa zimekupa heshima ni za wazungu.

Nimekushangaa pia kukusikia kuwa hamna mtu wa kukufundisha kuhusu historia ya Tanganyika kana vile wewe ndio Alfa na Omega katika suala hilo wakati ni wakina Ilife, Kimambo na wengine nao wamechangia sana katika uelewa wetu wa historia yetu. Unakuwa kama yule kipofu aliyegusa mkia wa tembo na akajiaminisha kuwa mkia ndio tembo na hakutaka kusikia habari za mkonga na mengine. Unachofanya kwa selective reading ya historia yetu ni hatari sana kwa afya ya nchi yetu. Kwa sababu hiyo, unastahili kupingwa kwa nguvu zote.

Amandla...
 
Ndugu zanguni kwanza napenda nikufahamisheni kuwa mjadala ule nimeuhitimisha sina la kuongeza.

Ila nataka nikuongezeeni kitu kuhusu huyu Eccles na mfano wa yeye.

Hawa waandishi Wazungu na mfano wa hawa wakoloni wana na chuki na historia ya wazee wetu.

Sababu ya chuki hizi zinafahamika.

Katika review yake Eccles kataja Dar es Salaam Dockworkers' Union anasema Abdul Sykes aliijenga TAA kutoka chama hiki.

Sitamuita muongo huyu hajui.
Hii ndiyo sifa yake.

Hata hivyo namshukuru kwa kunizindua.

Naona nikuwekeeni hapa utangulizi wa historia hii kisha nitaweka link ili atakae asome kwtaani ni kisa kirefu chenye sehemu tatu kukiweka hapa makala itakuwa ndefu sana:

''Historia ya Dar es Salaam Dockworkers’ Union, yaani Chama Cha Makuli wa Bandari ya Dar es Salam niliisoma mahali kama ilivyoandikwa na mtafiti na mwandishi mmoja Mwingereza lakini kwa kuwa nilishasoma kazi zake nyingi kuhusu historia ya Tanganyika na kwa kuwa sikuridhika na jinsi alivyokuwa anakwepa kueleza mengi yaliyofanywa na Waswahili wa pwani nikamtilia shaka katika maelezo yake ya historia ya chama hiki.

Kwa ajili hii basi nami nikaamua kufanya utafiti wangu niangalie kama na huku nako kafanya kama ilivyo kawaida yake.

Naam na huku nako kafanya yale yale aliyozoea.

Haya hakufanya yeye peke yake.

Hata watafiti wengine waliokuja kuandika baada yake mtindo ulikuwa hivyo.

Watafiti hawa walipokuja kuandika historia ya vyama vya wafanyakazi, historia hii ilipuuzwa.

Nilipokuwa nasomeshwa historia ya vyama vya wafanyakazi Tanzania Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam tulipewa rejea kitabu cha Alfred Tandau, A.C.A. Tandau, Historia ya Kuundwa kwa TFL (1955-1962) na Kuanzishwa kwa NUTA, Dar es Salaam, 1964.

Nimechakura kitabu kizima simuoni babu yangu.

Nikamwambia mwalimu wangu kuwa Tandau hajui historia ya vyama vya wafanyakazi anajiandikia tu.

Mwalimu kapigwa na butwaa ananiuliza kwa nini natoa kauli ile.

Nikamwambia babu yangu Salum Abdallah ni mwasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) mwaka wa 1955 na ameongoza migomo mitatu dhidi ya Waingereza, 1947, 1949 na 1960 na mgomo wa 1960 ulidumu siku 82.

Hii haikupata kutokea.

Tandau hakugusia harakati hizi hata kwa mbali.

Mgomo huu ulivunja rekodi ya mgomo wa Makhan Singh Kenya uliodumu siku 62.

Walimu wakinipenda kwani ilifika mahali wakajua kuwa najua kwa kuwa wazee wangu ndiyo waliopambana na hawa wakoloni.

Hii ndiyo hali ya historia yetu.

Baada ya kumaliza utafiti na kuandika historia ya makuli wa Dar es Salaam ya miaka ya 1940 sikujuta na nilishukuru kuwa nimepata nafasi ya kuinusuru historia hii iliyotukuka ya wazee wangu wenyeji wa Dar es Salaam.

Hii ndiyo historia ya makuli, wazee wetu naeleza hapo chini vipi walikabiliana na dhulma za wakoloni wakati palikuwa hakuna hata chama kimoja cha wafanyakazi Tanganyika.

Prof. Mohamed Bakari amepata kusema kuwa ikiwa kama sisi hatutaandika historia yetu na tukawaachia watu wengine waiandike basi wataandika mambo ambayo sisi hayatatupendeza.

Mfano wa Eccles hata kuandika hajui anataka kuandika review ya kitabu na kuna watu wanamuamini wanamfanyia rejea.

Namshukuru marehemu Mzee Islam Barakat kwa kunisomesha historia hii na Mama Daisy kwa kuniongezea taarifa nyingine.''

Hapo chini nakuwekeeni links ikiwa mnataka kuisoma historia hii nasikitika nimeandika Kiingereza:

1640778951686.png

Prof. Mohamed Bakari ofisini kwake Fath University, Istanbul Turkey 2015
 
Nguruvi3,
Mimi nimeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes unaita ngano.
Sawa ni ngano lakini bado unataka kujadili ngano na mwandishi wa ngano.

Ngano zinapuuzwa hazijadiliwi.
Hakuna cha kujadili kwenye porojo.

Waze wangu wote walikuwa TANU na ASP hili wala silikatai.

Nimekueleza hapa kuwa baba yangu marafiki zake wakubwa walikuwa Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala.

Hawa ni ASP kindakindaki na wana mapinduzi na kulikuwa na picha sebuleni kwetu ya hawa pamoja na baba yangu.

Picha hii ilitunguliwa walipouawa.
Baba yangu kwa uchungu wa kuuliwa rafiki zake hakuwa na moyo wa kuitazama hii picha.

Kuna mambo mengine mimi nakunyamazia sijibu kwa kuwa sipendi ubishi nakuachia useme upendavyo.

Wapi nimesema Abdul alikuwa Rais?

Nikisema hivyo si nitachekesha barza?

Unapenda hii ''chai,'' unairudia mara nyngi tu.

Kejeli na kebehi.

Sawa.
Ndicho ulichonacho.

Wewe unapata ''text,'' ziweke hapa tuzisome.

Mimi niko katika Dictionary of African Biography, Nyerere Biography, Cambridge Journal of African History, Library of Congress, kitabu cha Abdul Sykes kinasomeshwa vyuo kadhaa Ulaya na Marekani, nimezungumza vyuo kadhaa Afrika na Marekani, nimeandika vitabu 10 nimezunguka ulimwengu si kwa lolote ila kwa kalamu yangu.

Nadhani unajua kuwa nimetunukiwa ''cerificate,'' hapa JF.

Wewe unatamba na ''text.''
Sawa ndicho ulichojaaliwa.

Lakini hata mimi napata ''text.''

Umesoma mara kadha nikikuambia kuwa sitakuita muongo kwa kuwa najua hujui.

Fanya ''search,'' na rejea kusoma maneno hayo.

Hebu niambie wasomaji wangapi wapo katika uzi huu?

Unadhani wanakuja kukusoma wewe na kejeli na kebehi zako?

Umepata kuandika kitabu chochote, paper, kualikwa kwenye vyuo?

Unaandika umejificha.

Mohamed Said yuko hapa in ''flesh and blood.''

Atakae kuhojiana na yeye na ajitokeze.

Sijajificha.
Sijifichi kwa kuwa nasema kweli.

Jitokeze hapa nikuone na wasomaji wakuone.

Huwezi.
Muoga.

Babu yangu Salum Abdallah kapigania uhuru wa Tanganyika lau baba yake babu yangu mkuu Samitungo Muyukwa Mwekapopo kaingia Germany Ostafrika akitokea Belgian Congo amebeba bunduki na jeshi la Wajerumani kuja kupigana na Waafrika wenzake - Mtwa Mkwawa na Abushiri bin Salim Al Harith.

Hii ni historia ya babu zangu siikatai kwani ndiyo ukweli wenyewe.

Wala siionei aibu kwani hii ni changamoto katika changamoto za ukoloni.

Nacheka.

Abdul Sykes na mikutano ya Tandamti.

Kejeli na kebehi kwa wazee wangu.

Sawa.

Mkutano na Jomo Kenyatta, Peter Mbiu Koinange, Kung'u Karumba, Bildad Kaggia, Paul Ngei na viongozi wengine wa KAU hii kwako si lolote.

Au hujui kama hii ndiyo ile timu ya Kapenguria?

Wasomaji wangu wa maana historia hii huwashangaza.

Choyo, chuki, hasad na wivu vimekutawaleni mnafikia hata kubadili historia za watu na kupenyeza uongo.

Nani mjanja aliyefutiwa historia ya wazee wake au yule aliyeirejesha?
Naam historia hii ilifutwa na mimi nimeiandika na sasa tunaijadili.

Lakini Prof. Haroub aliposoma kitabu cha Abdul Sykes na cha Sheikh Ali Muhsin Barwani, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumwambia kuwa Mwalimu na wewe lazima uandike ueleze upande wako kwani Mohamed Said kasema mengi ambayo yamepindua historia yako yote na ''legacy,'' yako.

Hakuishia hapo alikwenda kwa Ahmed Rashad kuuliza historia ya Abdul Sykes.

Wazee wangu wote kama nilivyokueleza walikuwa TANU na ASP na najua ushiriki wao katika mapinduzi ya Zanzibar.

Leo Abdul Sykes hakuna asiyejua historia yake katika uhuru wa Tanganyika na yeye na mdogo wake Ally wametunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru ingawa baada ya miaka 50.

Picha kidogo:

View attachment 2060838
Kulia Sheikh Ahmed Islam, Ahmed Rashad na Prof. Haroub Othman Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere safari ya Jeddah 1997.

Nilikuwa na hawa wazee safari moja Jeddah, Makka na Madina na ilikuwa nafasi kubwa kwetu sote kuulizana mengi.
Kaka Mohamed wewe ni wa kipekee sana, narejea ushauri wa Paschal Mayalla hebu uwe na kipindi katika stesheni zetu za ndani kiwe na muendelezo, kuna shule kubwa sana hapa, hata hawa wanaokunakasha usiwapuuze ni watu muhimu sana hasa huyu fundimchundo na bwana Nguruvi3 mwenye mizaha mingi na kuiviza akili yake kwa upumbavu bali wamekuwa wakiibua maswala ya muhimu ambayo kiasi yanatupa wigo wakuwafahamu wa mlengo wa kushoto
 
Makala...
Kaka jambo la kuwa na kipindi cha TV sijalipuuza ila sijui naanzia wapi.

Kwanza tambua mimi si kijana tena nahitaji kuongozwa kwa mambo ya kisasa kama haya.

Ikitokea fursa In Shaa Allah hili tutalifanya.
 
Fundi Mchundo hii kitu haihitaji editing hata mstari mmoja.
Kwa ridhaa yako naomba 'nichafue chafue ' baadhi ya maeneo.
Ni vizuri kuwa umejibu review ya Eccles na umeweka wazi mapungufu yake. Lakini ukweli bado ni kuwa ulicho andika ni historia ya Abdulwahid Sykes na sio historia ya TANU.
Na hapa ndipo hasa tofauti ya wengi na Mohamed nikiwemo inapokuja. Hatuna shida kwa yeye kumuadhimisha Abdul Sykes au Wazee wake wengine. Wapo walioandika historia za koo , makabila au mikoa yao. Tatizo ni pale anapomfanya Abdul Sykes kama TANU na kiongozi wa Uhuru wa Tanganyika peke yake. Historia haionyeshi hivyo
Kwa kufanya hivyo umeangalia zaidi mchango wake katika uanzishwaji wa TANU na haukuangalia sana michango ya wengine. Aidha, umeangalia pia kile unachoona ni kusahauliwa kwa mchango wa waislamu katika mapambano dhidi ya ukoloni wa muingereza. Hiki sisi hatuna shida nacho. Ni haki yako na unastahili pongezi kwa kufanya hivo.
Hili sina shida nalo kabisa kwasababu ni haki pia tukiangalia mchango wa Wahindi au Wazungu au Wenyeji wa miji kama Dar kama sehemu ya Historia. Kuandika Historia ya mchango wa Waislam sioni kama tatizo lakini kuufanya mchango huo kama ndio pekee na ndio Uhuru, kuna shida hapo

Tunachopinga ( kama alivyosema Eccles) ni kutaka kuifanya historia ya Abdulwahid Sykes ndio historia ya TANU na kutaka kutuaminisha kuwa waislamu ( hususan wale wa Gerezani) hawakutendewa haki kwa maksudi ingawa wao ndio walioongoza mpambano. Sisi tunaona huu ni uongo kwa sababu vita dhidi ya ukoloni haikupiganwa kwa msingi wa udini au ukabila. Na kuna waislamu waliwapinga wale waliotaka kuingiza udini katika vita ile. Hili mara nyingi linakuwa wazi kwenye mabandiko yako na kwenye mafundisho yako kwa waislamu wenzako. Huu ni udini na unalenga katika kulets mpasuko katika jamii.
Kuanzia AA na Fundi umetuonyesha chanzo chake kingine cha 'civil servants' utaona kuna watu wa dini zote na rangi zote. Mfano Kleist alifanya kazi na Cecil Matola, akina Abdulwahid walikuwa na V. Kyaruzi hadi Nyerere. Ukiangalia hawa wazee walijali sana mchango wa mtu kuliko imani yake. Wazee walipomkaribisha Nyerere walijua ni Mkatoliki na anafundisha shule ya Wakatoliki.
Kwao ukatoliki halikuwa tatizo walihitaji knowledge ya Mwalimu na kupanua wigo
Vita ya Maumau iliyowahusisha wakina Kenyatta ilikuwa inapigania haki za wakikuyu zaidi ya haki ya wakenya kwa ujumla. Hii imechangia sana ukabila uliopo Kenya hadi leo. Lakini wakina Sykes ( Btw Sykes alikutana na wakina Kenyatta mwaka 1950 kwa sababu wakati ule ndoto ilikuwa ni panafricanism na aliona ni wajibu wa watanganyika na waganda kusaidia Kenya African Union katika mpambano yao na waingereza) walitambua kuwa ni lazima washirikiane na watu kutoka sehemu za Tanganyika na wa dini nyingine ili uhuru wa nchi yao uweze kupatikana. Ndio maana toka mwanzo walishirikiana na wakina Martin Kayamba msomi wa Oxford kutoka Tanga ambae mwaka 1922 aliyeanzisha the Tanganyika Territorial African Civil Servants Association na kwa kiasi kikubwa kiliwezesha kuanzishwa kwa Tanganyika African Association na wakina Kleist Sykes, Cecil Matola na wengine mwaka 1929 baada ya kushauriwa kufanya hivyo na Dr. James Aggrey kutoka Ghana.

Ni ukweli kuwa ingawa makao makuu yalikuwa Dar, ni matawi ya Dodoma na Bukoba ndio yalikuwa radical. Dar es Salaam walijikita zaidi katika mambo social na kutafuta uwakilishi katika serikali ya kikoloni. Wakina Erica Fiah walipingwa walipotaka kukifanya chama kuwa radical zaidi. Ni wazi kuwa wakina Sykes, Vedasto Kyaruzi na vijana wengine walileta mapinduzi katika TAA kwa kuwaondoa wazee wao wakina Kleist na Cecil katika sehemu za uongozi.
Kuntu
Kila siku unazungumzia wakina Sykes kumpokea Nyerere alipokuja Dar kama vile wao ndio walimuingiza katika siasa za TAA. Hiki si kweli kwa sababu Nyerere alijiunga na TAA mwaka 1945 na alianzisha tawi Makerere alipokuwa anasoma na wakina Andrew Tibandebage na Hamza Kibwana Mwapachu baada ya kuanzisha nao the Tanganyika African Welfare Association.
Hili tumejadiliana na Mohamed miaka mingi sana hapa JF tukimweleza wazi kuwa Nyerere hakuanza siasa na Abdul Sykes na wala akina Abdul hawaku 'introduce him' katika siasa.
Mwaka 1948 Nyerere alihudhuria mkutano wa TAA Dar akiwa katibu wa tawi la Tabora.
Ukisoma mabandiko ya Mohamed, lazima atakueleza Nyerere alikuwa anapata wapi lunch na Dinner, hili ni makusudi ili kujenga dhana kwamba alikuja kuingizwa katika siasa na familia ya Sykes. Si kweli, Nyerere alianza siasa miaka mingi kabla ya kkukutana na akina Sykes
Madai ya uhuru hayakuwa ya watu weusi peke yao, kuna wazungu kama Tom Tyrrell ( Tanganyika European Council, Capricorn Africa Association, United Tanganyika Party), wakulima Derek Bryceson na Lady Chesham ambao waliungwa mkono na TANU katika uchaguzi wa 1958-59. Lady Chesham alianzisha the Community Development Trust of Tanganyika mwaka 1962 na Bryceson alikuwa mbunge na waziri katika serikali baada ya uhuru. Kuna wahindi kama Amir Jamal na Abdulkarim Karimäen ambao waliunga mkono TANU. Kilichokuwa wazi ni kuwa wazee wetu walifanya juhudi za ziada kuvuka mipaka ya udini, ukabila na urangi katika jitihada zao za kupigania uhuru wa Tanganyika. Haikuwa one man show ya Abdul Sykes na Nyerere. Haikuwa ya wakina Dossa Aziz wa Gerezani peke yao. Haikuwa ya wagalatia wakina Oscar, Dennis, Andrew peke yao. Ilikuwa ya watanganyika, period. Wakina Sykes na Nyerere walikuwa viongozi lakini bila ridhaa ya watanganyika kutoka bara na mrima, wa makabila yote, wa dini zote wasingeambulia kitu.
Marhumu Alnour Kassam aliyetutoka majuzi tu. Kwa faida ya vijana, huyu Derek Bryceson alikuwa Mbunge na wakati Sinza inaanza kupanuka na kujengwa kuna aina ya mjengo wa nyumba ulipewa jina lake. kuna wazungu wengine kama Dr L.D.Stirling aliyeanzisha Hospitali ya Lulindi na baadaye kuwa waziri wa Afya.
Naona katika kum beza Eccles umewakandia wazungu wote ukisahau kuwa kwa kiasi kikubwa maandiko yako yametokana na maandiko ya wakina John Iliffe na shule unazotambia kuwa zimekupa heshima ni za wazungu.
Huu ni udhaifu wa Mohamed hataki kukoselewa kwasababu ana hati miliki ya Historia ya Tanganyika
Nimekushangaa pia kukusikia kuwa hamna mtu wa kukufundisha kuhusu historia ya Tanganyika kana vile wewe ndio Alfa na Omega katika suala hilo wakati ni wakina Ilife, Kimambo na wengine nao wamechangia sana katika uelewa wetu wa historia yetu. Unakuwa kama yule kipofu aliyegusa mkia wa tembo na akajiaminisha kuwa mkia ndio tembo na hakutaka kusikia habari za mkonga na mengine. Unachofanya kwa selective reading ya historia yetu ni hatari sana kwa afya ya nchi yetu. Kwa sababu hiyo, unastahili kupingwa kwa nguvu zote.

Amandla...
Ahsante Fundi
 
Fundi Mchundo hii kitu haihitaji editing hata mstari mmoja.
Kwa ridhaa yako naomba 'nichafue chafue ' baadhi ya maeneo.

Na hapa ndipo hasa tofauti ya wengi na Mohamed nikiwemo inapokuja. Hatuna shida kwa yeye kumuadhimisha Abdul Sykes au Wazee wake wengine. Wapo walioandika historia za koo , makabila au mikoa yao. Tatizo ni pale anapomfanya Abdul Sykes kama TANU na kiongozi wa Uhuru wa Tanganyika peke yake. Historia haionyeshi hivyo

Hili sina shida nalo kabisa kwasababu ni haki pia tukiangalia mchango wa Wahindi au Wazungu au Wenyeji wa miji kama Dar kama sehemu ya Historia. Kuandika Historia ya mchango wa Waislam sioni kama tatizo lakini kuufanya mchango huo kama ndio pekee na ndio Uhuru, kuna shida hapo

Kuanzia AA na Fundi umetuonyesha chanzo chake kingine cha 'civil servants' utaona kuna watu wa dini zote na rangi zote. Mfano Kleist alifanya kazi na Cecil Matola, akina Abdulwahid walikuwa na V. Kyaruzi hadi Nyerere. Ukiangalia hawa wazee walijali sana mchango wa mtu kuliko imani yake. Wazee walipomkaribisha Nyerere walijua ni Mkatoliki na anafundisha shule ya Wakatoliki.
Kwao ukatoliki halikuwa tatizo walihitaji knowledge ya Mwalimu na kupanua wigo

Kuntu

Hili tumejadiliana na Mohamed miaka mingi sana hapa JF tukimweleza wazi kuwa Nyerere hakuanza siasa na Abdul Sykes na wala akina Abdul hawaku 'introduce him' katika siasa.
Mwaka 1948 Nyerere alihudhuria mkutano wa TAA Dar akiwa katibu wa tawi la Tabora.
Ukisoma mabandiko ya Mohamed, lazima atakueleza Nyerere alikuwa anapata wapi lunch na Dinner, hili ni makusudi ili kujenga dhana kwamba alikuja kuingizwa katika siasa na familia ya Sykes. Si kweli, Nyerere alianza siasa miaka mingi kabla ya kkukutana na akina Sykes

Marhumu Alnour Kassam aliyetutoka majuzi tu. Kwa faida ya vijana, huyu Derek Bryceson alikuwa Mbunge na wakati Sinza inaanza kupanuka na kujengwa kuna aina ya mjengo wa nyumba ulipewa jina lake. kuna wazungu wengine kama Dr L.D.Stirling aliyeanzisha Hospitali ya Lulindi na baadaye kuwa waziri wa Afya.

Huu ni udhaifu wa Mohamed hataki kukoselewa kwasababu ana hati miliki ya Historia ya Tanganyika

Ahsante Fundi
We bwana nguruvi ipi hasa hoja yako? Nikweli huwezi kuanisha 1,23.. Huyu kijana Fundi Mchundo anakuacha mbali sana

Mathalan kuna mahala huko nyuma huyu bwana mdogo alianzisha hoja kwamba Moh si "authority" na kudai kwamba hapaswi kurejewa, jambo liko mbali kabisa na uhalisia, yaani hakuna mahala Mohamed said ame "claim" kwemba yeye ni rejea bali Anaeleza wazi namna alivyohangaishana na wazee wake kina sykes (hadi wakati mwingine wakimpa hela aondoke zake i.e "Mohamed umeshakula? Mzee anatoa pesa mfukoni a nampa" hata yule "zindiki" (K .k Allah Amrahamu) kama waitavyo waarabu, Moh ameonyesha wazi pasina kificho namna alivyomhangaisha kumpekulia mafaili ya "ujasusi" ya wakati huo akiwachimba wapigania Uhuru, badala yake imekuwa hoja kwako samaki kumtandika nayo Moh kwamba wazee wake kama K. K na Ali Tambwe ni fitna na yeye amewaficha, ajabu hakuna mahala Moh kawaficha kwamba walikuwa special branch.

Lakini sasa nataka kukuelewa kwamba Moh si "authority" wewe je ni nan? Hizi kauli unazokariri mara kwa mara kwamba "mimi sina shida napo" au mimi kadhaa, zina maana gani? Ndio maana Moh anakuita Hasidi mwenye choyo, nikirejea kwenye Hoja zako ambazo umekuwa ukijigonga gonga na kuto kubali mchango wa Mohamed Said katika kuwaibua mashujaa waliofichwa kwa makusudi ni Wazi unapwaya, hebu sasa eleza hoja zako mosi, pili kubali mchango wa Moh katika haya ya Msingi kinyume chake karma itakutafuna
 
Back
Top Bottom