Makala...
Kama nilivyokuambia kiasi cha siku mbili zilizopita kuwa subiri.
Mimi nishahitimisha.
Kitabu kipo huu sasa tunaingia mwaka wa 23 na nimeandika vitabu vingine katika kipindi hiki lakini hiki kitabu cha Abdul Sykes bado kinajadiliwa sasa miongo miwili tumeingia wa tatu.
Bado kitabu kinafanyiwa ''mapitio.''
Kama vile yale yaliyomo katika Cambridge Journal of African History hayajatosheleza.
Naam bado kinapitiwa na haya mapitio ndiyo yanakipa uhai kitabu hiki na sasa In Shaa Allah tutakwenda toleo la tano.
Kila siku napokea salaam na watu hata siwajui wananieleza kuwa wamekinunua kitabu changu na wanakisoma.
Kila msomaji anasema wanayosoma hawakupatapo kuyasoma popote si shule ya msingi, sekondari wala chuo kikuu.
Huyu ndiye Allah ana njia zake za ajabu sana.
Sikutegemea haya hata kwa mbali kuwa kitabu hiki kitakuja kuwa maarufu kwa kiasi hiki na kitabadili historia yote ya uhuru wa Tanganyika.
Anaetaka ugomvi na agombane na hawa wasomaji wa kitabu hiki si mimi.
Huku kwetu kwa kawaida kitabu baada ya mwaka maisha yake yanakuwa yamekwisha.
Si kitabu hiki.
Kitabu hiki mimi nimekitoa wakfu sichukui mrabaha.
Chapa uza chukua fedha.
Kuna msemo wa Kiingereza unasema, ''Silence is golden because it can never be repeated.''
Nawakalia kimya na pembeni.
Nitakuwa nakupa yale niyajuayo ili wewe ndugu yangu unufaike na yale ambayo huyajui.
Narudia kukuambia kuwa nimeshahitimisha na wewe nakuomba usubiri patulie.
In Shaa Allah tutarejea.
Nimeweka picha ya Buckingham Palace, London nimekaa kitako kwenye uzio wake.
Naamini unaelewa kwa nini nimekuwekea hii picha.
Watu huniambia kuwa walivyonidhani sivyo hadi walipoona picha zangu.
Kuna uhusiano wa mbali na hili gumzo letu baina yangu na wewe.
Kuna msemaji aimwambia mchoraji wa picha yake, ''Paint me as I am if you miss a single wrinkle I wont pay you a penny.''
Tuingie katika darsa kidogo.
Kitabu hiki ''A History of Tanzania,'' (1969) nimekuwekea picha yake hapo chini kimehaririwa na IN Kimambo na AJ Temu.
Kitabu hiki chote karibu kurasa 300 hakuna popote alipotajwa Abdul Sykes ingawa TAA na TANU zimetajwa.
Vipi utakuwa na TAA na TANU na Nyerere ndani ya kitabu chako bila ya Abdul Sykes?
Hii ndiyo historia yetu iliyo rasmi.
Lakini kitabu hiki ndicho kilichokuwa kikisomeshwa na kufanyiwa rejea na walimu wa historia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Mimi siwalaumu nawachukulia kuwa hawajui na kama hawajui wajibu na dhima iliyokuwa juu yangu ilikuwa kuwasomesha walimu wangu historia ya wazee wangu.
Mwalimu wangu akipenda sana majibu ya yangu katika ''essay,''yaani insha.
Siku moja baada ya kuandika insha kuhusu vyama vya wafanyakazi na nikamtaja babu yangu na Kassanga Tumbo aliniita ofisini kwake.
Mwalimu wangu huyu alikuwa kijana na kutoka bara akaniuliza huku insha yangu iko mikononi mwake, ''Mohamed wewe unaandika maneno haya wewe huogopi?''
Naamini umenielewa.
Mwalimu huyu akinipa alama za juu sana katika somo lake.
Laiti nisingeandika kitabu hiki historia ya uhuru wa Tanganyika ingekuwa hii ya Kimambo na Temu.
View attachment 2063431
Buckingham Palace London 1992
View attachment 2063449