20,20,60 na namna inavyofanya kazi katika maisha

20,20,60 na namna inavyofanya kazi katika maisha

meliyasumu

Member
Joined
Jul 20, 2021
Posts
16
Reaction score
9
Kwanza tumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai,afya silika na tabia njema
Miongoni mwa vitu jamii nyingi inavikosa ni kulazimisha kupendwa/kukubarika katika kila hatua anayopitia, na hali hii huleta msongo wa mawazo pale inapotokea hilo hitaji lako linapokutana na vikwazo na kupelekea kujihisi una udhaifu sehemu,
Njia hii ya 20,20,60 itakutoa huko na kukufanya ujione na kujivunia lolote litakalotokea katika mipango yako.
20% ya kwanza hawa ni watu ambao hawatakukubali hata ufanye nini, yani wapo tayari hata kutunga uongo ili wakutie hatiani na kukufedhehesha, hawana shukrani na wapo tayari hata kununua na kutumia pesa ili wahakikishe hufanikiwi, watatumia kila NJIA wakutoe kwenye reli na wanasiasa hii inawahusu sana. Kazi yao duniani ni kukupinga tu na kutafuta maeneo ya kimkakati ili kufanikisha agenda zao. Watakusema hadharani na sirini, wataunda vikundi vya kutengeneza propaganda ili kukudhoofisha na wapo tayari kutoa hata ushaidi wa uongo ili wafanikiwe kukutia hatiani.
20% ya pili hawa ni wale wanaokukubali kufa au kupona kwa ajili yako, watakutetea kwa chochote kinachotokea na wapo tayari muda na saa yoyote kukulinda, na kundi hili huwa hata tayari kukupa taarifa nzuri na mbaya ili ujipange kukabiliana nazo na watatumia hadi gharama zao kuhakikisha kila baya halikufikii.
Kundi hili ni mtaji mkubwa sana katika mafanikio yako kwani huhitajiki kutumia nguvu kulimiliki maana lipo tayari kukusaidia kwa gharama yoyote, mkizama mtazama nalo, mkiibuka mtaibuka nalo lipo tayari muda na saa yoyote kwa ajili yako
60% ya mwisho hawa ni wale wasio na msimamo wowote, vijana wanawaita oyaoya huku wapo huku wapo, hawana msimamo wowote wanayumba yumba kama bendera fata upepo, wakiambiwa hv sawa, wakiambiwa vile pia sawa
Nini namaanisha?
Kama wewe unataka kufanikiwa usihangaike na 20% inayokukubali wala 20% inayokukataa
20% inayokukubali tayari ipo hangaika na lile kundi la 60% (wazee wa oyaoya au sigara kali nyuma inawashwa na mbele inawashwa) kama utafanikiwa kushawishi 40% ya lile kundi la 60% maana yake utakuwa na 20% ya wanaokukubali+40% ya wale oyaoya= 60% hivyo mpinzani wako atabaki na 40% na wewe utakuwa mshindi
USHAURI WANGU:
Wote wenye mamlaka kuanzia ngazi ya juu hadi chini wachukue hii kama mfano, hangaika zaidi na kundi la 60% sababu kwalo ndilo litakalokupa ushindi, achana na kushawishi 20% ya wasiokukubali maana hutawabadilisha wameumbwa hivyo na nature inawaongoza hivyo, hata Yesu/ Mohamed hilo kundi lilimpinga hata baada ya kufanya makubwa katika jamii zao, ngazi ya juu mlione hili na mlifanyie kazi
Nimalize kwa kusisitiza, VIONGOZI AFANYE KAZI SANA KULISHAWISHI KUNDI LA 60% MALI NDIO IPO HAPA
Ni mimi
MELI YA SUMU ILIYOPATA AJALI BAHARINI, SAMAKI WOTE WANAELEA
 
Back
Top Bottom