Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Jamani hili ni jukwaa la GT hivyo naomba tuwe serious kidogo tunapoongelea hatma ya nchi, tuache utani na kuleta mambo yasiyo na maana. Kwa nini nasema hivyo? Nimeona kuna watu wanaleta ulinganisho wa watangaza nia CCM na kuwafananisha watangaza nia wa vyama vya Marekani. Kweli pamoja na akili zetu timamu tunaanza kulinganisha siasa za Marekani na hizi zetu za Bongo!
Hivi leo tumebakiza siku 138 (sawa na miezi minne na siku 18) tuingie katika Uchaguzi Mkuu. Hadi sasa kitaifa hatujui hata kwa kukadiria idadi ya wapiga kura, idadi ya wagombea na hata idadi ya vyama vitakavyoshiriki. Kichama hatujui idadi ya wagombea katika ngazi zote; Uraisi, ubunge na hata Udiwani, are we really serious? Is there any right thinking individual who can understand us or even condone what we are doing?
Halafu tunajilinganisha na Marekani. Marekani bado siku 500 (sawa na mwaka moja, miezi minne na siku 16) hadi wafanye Uchaguzi wao Mkuu. Kitaifa tayari wamekadiria idadi ya wapiga kura (ambao ni mara tatu ya idadi ya Watanzania wote kuanzia vichanga hadi vikongwe) Tayari mchakato wa kupata wagombea katika nafasi mbali mbali umepamba moto na kitakachotoa mchujo kwa wagombea ni wanavyokubalika kwa kupigiwa kura na wananchi.
Mtangaza nia Marekani akijipima akaona hafui dafu, anajiondoa mwenyewe na kumuachia anayekubalika zaidi aendelee. Hakuna kikao kinachokaa na kuamua yupi agombee na yupi jina lake likatwe. Kama anatokea mwenye nia na haungi mkono msimamo wa chama anao uhuru wa kujitosa kama mgombea binafsi. Katika misingi hii kweli inaingia akilini mtu kufikia hatua ya kujaribu kulinganisha ndimu na mananasi? Kwa vituko hatujambo!
Kila Mmarekani ana uhuru wa kujitosa katika kinyang'anyiro isipokuwa pale tu kwamba hana sifa na hizo sifa haziishii tu kwenye siasa, ni kwenye nyanja zote za maisha. Kwamba wakati zimebaki miezi minne na ndio idadi ya watangaza nia inaongezeka ni kichekesho lakini kwa Tanzania haishangazi hata kidogo. Katika jamii ambamo wahalifu wanaweza kutetewa na kupewa uongozi bila wananchi kusema hapana, Watanzania hawana mfano.