Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Uchaguzi wa Oktoba 2015 utakuwa ni uchaguzi wa kumi na moja wa rais na wabunge tangia uhuru. Tangia uhuru, Chaguzi Sita zilifanyika wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa (TANU/CCM), na chaguzi nne zilifanyika chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi wa mwaka huu (2015) utakuwa ni uchaguzi wa tano chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Suala la kujadili ni je, kwa kipindi chote hiki, msukumo wa wananchi kujitokeza kupiga kura umekuwa ni kwa matarajio yepi?
Tangia uhuru (1961), chaguzi kuu zimekuwa kama ifuatavyo:
1. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Uchaguzi chini wa mfumo wa chama kimoja ambapo voters turn out ilikuwa 77%.
2. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1970 chini ya mfumo wa chama kimoja, voters turnout was 72%
3. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975 - chama kimoja, turnout was 81%
4. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1980 Chama kimoja, turnout was 75%
5. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985 Chama kimoja, turnout was 75%
6. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1990 Chama kimoja, turnout was 74%
7. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 Vyama vingi, turnout was 77%
8. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 Vyama vingi turnout was 84% (record breaking highest in history)
9. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 vyama vingi turnout was 72%
10. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Vyama vingi turnout was 42% (record breaking Lowest in history)
11. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ??????????
Muhimu:
1. Uchaguzi mkuu wa 1965 ulikuwa ni uchaguzi wa kwanza wa Tanganyika as a STATE, ambapo kabla, Tanganyika was a TERRITORY.
2. Uchaguzi huu (1965) ulikuja baada ya mfumo wa vyama vingi kufutwa na kubakisha TANU peke yake kama chama cha Siasa nchini Tanganyika (na Tanzania hata baada ya Muungano.
3. Uchaguzi huu (1965) ulihusisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na sio Jamhuri ya Tanganyika. Waafrika wa Tanganyika waliipigania Tanganyika kufa na kupna na hatimaye kuikomboa chini ya TANU, lakini uchaguzi mkuu wa kwanza baaada ya mafanikio hayo ukahusisha Tanzania.
Harakati za TANU kuelekea uhuru, muungano na uchaguzi mkuu wa kwanza wa Tanganyika as a STATE:
Kabla ya uhuru, muungano na uchaguzi mkuu wa kwanza wa chama kimoja 1965, TANU haikuwa chama cha siasa (political party) bali a political movement (vuguvugu la kisiasa).
TANU ilijihusisha zaidi na harakati za kudai uhuru, harakati zilizodumu kwa miaka karibia saba (1954-1961). Kipindi kabla ya kuzaliwa kwa kwa TANU kulikuwa na harakati nyingine za waafrika ambazo zililenda zaidi kudai haki na fursa sawa hasa za kibiashara, kiuchumi na kijamii kwa mfano mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi, fursa za elimu n.k. Ujio wa TANU ukapanua zaidi wigo wa harakati za waafrika na sasa lengo kuu likawa Demand for Self- Determination and Demand for Self-Rule. TANU ikaahidi to break the colonial past (kimfumo) and then recreate a future of Tanganyika. Mafanikio ya TANU yalitokana zaidi na ukweli kwamba TANU wasnt a political party bali a political movement. Kwa maana nyingine, mabadiliko ya kweli yalihitaji a political movement, na sio political party(s). Swali:
Je, mabadiliko ya kweli kwa wananchi leo yanahitaji political parties au political movements? Zipo tofauti kubwa baina ya political parties & political movements. Kwa mujibu wa Goran Hyden (2006), tofauti baina ya political movement & political party ni kama ifuatavyo:
Political Movement Political Party Orientation Cause Issues Level of Operations Regime Government Main Arena of Operation Society Parliament Method of Operation Mobilization Persuasion Member Orientation Diffuse Specific Claims of Resources No formal limits Constrained by Law
TANU as a political movement led to the emergence of Tanganyika as a new state. Kabla ya hapo, Tanganyika was not a STATE, but rather, a TERRITORY. Swali:
· How does a state arise?
A state emerges in response to needs that groups in particular society have. These needs may arise from problems with security (not peace), welfare or resolving conflicting demands on scarce resources.
Maswali:
· For the past 50 years, have we resolved the challenges of insecurity, welfare and conflicting demands on resources?
· Are these parts of issues that voters have in mind whenever they turn out to vote in every election?
· Is this state (Tanzania) the kind of state that wananchi were promised before uhuru?
· Is this state (Tanzania) the kind of state they wananchi envisaged before uhuru?
· Is it the kind of state that they want for the next 50 years?
Tanganyika/Tanzania as a state has gone through three main phases:
1. Party State 1961 to 1964
2. Developmental State 1965 to 1985
3. Contracting state 1986 to present
Kwa kipindi cha mwaka 1961-1964, the state was TANGANYIKA na kwa kipindi cha mwaka 1961-2009, the state was TANZANIA. Kwa kipindi cha 2010 (kufuatia mabadiliko ya katiba ya Zanzibar), utambulisho wa Tanzania as a state haueleweki. Swali:
· Katika hali hii, wananchi wamekuwa wanajitokeza kupiga kura kutimiza malengo gani?
Awali tumeona voters turn out katika chaguzi kuu zote tangia uhuru.
TANGANYIKA AND PARTY STATE POLITICS 1961-1966
Kipindi cha 1961-1966 kilikuwa ni kipindi cha PARTY STATE. Kuelekea uhuru wa Tanganyika 1964, common enemy wa watu wote weusi alikuwa ni mmoja tu, colonial power. Hali hii ikarahisisha sana kazi ya TANU kujijenga as a single dominant political movement in Tanganyika Territory. Baada ya uhuru, kwa kipindi cha Party State (1961-1964), ultimate aim of politics was to Create and Sustain a New Order. Mwalimu Nyerere alikuwa very optimistic about the future, lakini hakuwa na uzoefu wa kuwa na madaraka makubwa kiasi kile. Kwahiyo he was very anxious to create his own position at the helm of the state (Tanganyika), na ndio maana kukawa na haja ya Party State politics in the said period.
Mwaka mmoja baadae (1965), emphasis ikaondoka kwenye party state na kuhamia kwenye Developmental State. Na katika kipindi hiki hiki, matukio makuu manne yakajitokeza:
(1) Kufutwa kwa mfumo wa vyama vingi
(2) Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar
(3) Maandalizi ya kuelekea ujamaa.
(4) Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya uhuru.
TANU ilihitaji kuonyesha wananchi kwamba chama kilikuwa kimejiandaa kwa matatu:
1. Kuonyesha wananchi kwamba walikuwa wamefanya uamuzi sahihi kuunga mkono TANU.
2. Increase popular participation kupitia chaguzi za mara kwa mara ili wananchi waone kwamba wanashirikishwa katika utawala na maamuzi.
3. Deliver promises za mabadiliko kwa wananchi kiuchumi kufuatia ukombozi wa Tanganyika.
DEVELOPMENTAL STATE 1967-1985.
Katika Uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1965, wananchi walienda kupigia kura mafaniko ya TANU. Kwa mujibu wa gazeti la The Standard, Katibu mkuu wa TANU wa wakati ule Marehemu Hashim Mbita alitoa Radio broadcast tarehe 21 October na kunukuliwa na Gazeti la The Standard kwamba:
He appealed to voters to turn out on the Election Day and vote for president Nyerere .He said that the party was therefore appealing to all registered voters in Tanzania to vote for president Nyerere because of his contribution to the nation during which he has been president of TANU.
Pia uchaguzi huu ulitawaliwa na dhana ya matumaini ya Taifa jipya miongoni mwa wananchi, hasa matarajio ya kula matunda ya uhuru. Ni katika muktadha huu, Azimio la Arusha became imminent. Matokeo yake ikawa kwamba, emphasis and objective shifted from sustenance of order (1961-1966) chini ya PARTY STATE POLITICS, to Development (1967-1985). TANU na mwalimu wakatambua kwamba they needed to show their ability to develop the new state and improve the living conditions of the majority.Wananchi walihitaji kuona matunda ya uhuru sasa na sio baadae. In the process Mwalimu had to grab control of the state so as to guide progress, hence the birth of Azimio la Arusha in 1967. Katika Chaguzi kuu zilizofuatia yani (1970, 1975, 1980 & 1985), wananchi walienda kupigia kura MATUMAINI na IMANI kubwa waliyokuwa nayo juu ya Mwalimu Nyerere katika muktadha wa Azimio la Arusha.
Uchaguzi Mkuu wa 1985
Mwalimu Nyerere alingatuka mwaka 1985. Kufikia kipindi hicho (miaka 24 ya uhuru), wananchi wengi walikuwa bado wanasubiria matunda ya uhuru, hasa kiuchumi. Uchaguzi wa 1985 ulifanyika chini ya third phase of Tanganyika as a state THE CONTRACTING STATE. Hii ilitokana na haja ya kukabiliana na failures and challenges za party state & developmental state tulizojadili awali.
CONTRACTING STATE 1985 to present
Challenges and failures of party state and developmental state necessitated contracting state. Serikali ikaanza kujiondoa katika shughuli za moja kwa moja za kiuchumi na kuachia nguvu za soko zitawale. Mageuzi ya kiuchumi ndio yaliyoanza na baadae kufuatiwa na mageuzi ya kisiasa. Katika mageuzi ya kiuchumi, wananchi walishtukizwa na hawakuwa wamejiandaa kuondokana na misingi ya ujamaa chini ya azimio la arusha. Baadae azimio la Zanzibar likatangazwa kisirisiri Zanzibar, na wachache (hasa wanasiasa/viongozi) ndio wakalitumia kikamilifu kujiendeleza kiuchumi kwani ni wao ndio walikuwa kwenye ajira zenye mishahara lakini muhimu zaidi, kwenye nafasi za uongozi ambazo walizitumia kuanza kujitafutia hisa kwenye kampuni binafsi, kutengeneza mazingira ya kupokea mshahara zaidi ya mmoja na kuwekeza kwenye ardhi walizochukua ili kuwa na nyumba za kupangisha, PER Azimio la Zanzibar. Katika chaguzi kuu zilizofuatia, yani 1990-2010, wananchi wengi wamekuwa waki endorse yote haya kupitia sanduku la kura.
Mwaka 1995, taifa lilfanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi baada ya mfumo wa chama kimoja kuishi kwa miaka 30. Ingawa mageuzi ya kiuchumi yalianza mapema zaidi (1986), mageuzi ya kisiasa yaliratibiwa kwa ustadi mkubwa in a top-down fashion ili kuzuia dissapointemtns za wananchi kiuchumi zisihamishiwe kwenye sanduku la kura na wananchi na kukiondoa CCM madarakani.
Tulipo Leo:
Chama tawala kimepoteza kila aina ya uhalali wa kutawala:
1. Ahadi ya matunda ya uhuru zilizotolewa miaka ya 1950s, wananchi walio wengi hadi leo hii hawajaona kitu.
2. Azimio la Arusha ambalo liliwapa wananchi walio wengi matumaini ya Tanzania ya baadae yenye neema, azimio hili liliuliwa na CCM yenyewe mwaka 1991 Zanzibar na kulipisha azimio la Zanzibar ambalo halijali tena wananchi walio wengi.
3. Amani na utulivu (political stability). Hauwezi kuwa na political stability iwapo wananchi walio wengi (micro level households and indigenous businesses do not experience economic stability). The Pre requisite of political stability is economic stability for the majority. Hata Mwalimu alionya miaka zaidi ya 20 iliyopita kwamba wananchi hawa hawawezi kuvumilia moja kwa moja, ipo siku wataamka na kusema basi tumechoka.
4. CCM ilikuwa inathibiti njia kuu muhimu za uchumi kwa maslahi ya walio wengi. Zilikuwepo taasisi na makampuni ya umma ambayo yalijiendesha kwa ufanisi, yalizaa ajira, lakini yote haya yamerudishwa kwa adui Yule Yule aliyepelekea TANU kuunganisha nguvu ya umma kuikomboa nchi (Wakoloni). Adui huyu amekuwa akigawia hisa wanasiasa na viongozi wa CCM na kuacha wananchi wenye mali na rasilimali wakitaabika bila huduma za msingi za kijamii, vipato duni n.k.
Katika mazingira kama haya, kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2015, wapiga kura watajitokeza kwenda kupigia kura CCM kwa kitu gani?
Mchambuzi:
Ulizoandika hapa hizi zote ni longolongo tu za kisiasa na hazina mshiko wowote kwa maisha ya watanzania. Umetumia muda mwingi kueleza jinsi chama tawala kilivyofanya mabadiliko ndani ya nchi.
Ukweli wa mambo, chama tawala kilifanikiwa kwenye kuleta uhuru. Baada ya hapo mipango yote iliyofuatia ilikuwa kama majaribio ya sayansi ya mtoto wa darasa la tatu.
Kitu kilichofanya chama hiki kuendelea kuwa madarakani. Ni upeo mdogo wa kielimu wa wananchi, ulaghahi wa wanasiasa na misaada kutoka nje.
Tanzania ingekuwa na wasomi miaka ya 60 na 70, Nyerere asingeweza kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 10. Toka nchi ipate uhuru, chama tawala ni chama chenye mipango ya kilaghahi. Unatoa mifano ya viwanda. Let's get real. Hivi Tanzania ilikuwa na viwanda gani vya maana vya kuleta ajira?
Hata kama nchi ilikuwa na viwanda, nitajie just five business executives ambao walikuwa uwezo wa kuendesha mashirika ya umma kwa ufanisi. Huwezi kusema kulikuwa na mipango ya kuweka uchumi mikononi mwa wananchi wakati wananchi wenye hawajuhi jinsi ya kuendesha uchumi.
Tukirudi kwenye data zako za uchaguzi, watu walishiriki kwa wingi wakati wa mfumo wa chama kimoja kwa sababu moja kubwa: uchaguzi wa wabunge. Uchaguzi wa wabunge ulikuwa ndio njia pekee ya watu kutumia haki zao za kidemokrasia. Uchaguzi wa rais (ndio au hapana) ulikuwa sio kivutio. Na kama uchaguzi wa rais ungekuwa unafanyika pekee yake, maudhurio ya wapiga kura yangekuwa chini. Hivyo kushiriki kwa wananchi kwa wakati hule haikuwa ni ishara ya mafanikio ya serikali.
Tukirudi kwenye uchaguzi wa 2015, wapiga kura wengi ni vijana. Mtazamo wao ni tofauti na wapiga kura wa 60, 70, 80, na 90. Vijana hawa wanataka viongozi watakaoweza kuja na ufumbuzi wa matatizo yao na ya nchi kwa ujumla. Miaka ya zamani watu walifurahi serikali kuwa na viwanda bila ya wao kufaidika. Siku hizi watu wanataka kuona wanafaidika vipi na rasimali za umma.