2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

Vyama vya upinzani Tanzania havijajenga uhuru wa mawazo unaoruhusu ushindani wa kisiasa ndani ya vyama hivyo, ndio maana mashabiki wa vyama vya upinzani wanapata shida kuelewa kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kumtafuta mgombea wake wa urais.

CCM imefanya kazi nzuri kuliongoza taifa letu na imeweka misingi ya fursa kwa kila mwenye bidii. Tanzania ni taifa la kutolewa mfano barani Afrika kutokana na kazi nzuri ya CCM.

Lakini ni wajibu wa wanaCCM kukiri kuwa kwa kiwango fulani chama kimetoka nje ya misingi iliyokiasisi.

Vipo viashiria vingi lakini kimoja ni Lowassa kufikiriwa kuwa atapitishwa kugombea urais. Iwapo chama kingekuwa imara kwenye misingi ya uadilifu, mtu kama Lowassa hata asingefikiria kuchukua fomu.

Lowassa anamwaga mapesa kwa wajumbe na makada kwa vile anajua ndani ya chama cha mapinduzi siku hizi pesa ndiyo inayoamua nani awe kiongozi.

Hii ni hatari na vijana lazima wawe mstari wa mbele kulisema hili kwa sauti kuu.

Rushwa ikishamiri kwenye chama itaingia serikalini. Itafikia wakati ukuu wa shule utakuwa unauzwa, ukuu wa idara utapangiwa bei, na huo ndio utakuwa mwisho wa ufanisi. Nchi itaporomoka na hakutakuwa na jinsi ya kuzuia kuporomoka huko.

Lowassa kawaahidi watu wengi vyeo serikalini iwapo atakuwa Rais. Je, nani atasimamia na kukagua ufanisi wa watu walioingizwa kisiasa na mkuu wa nchi? Hawa hawatagusika. Mtu wa namna hii anapofikiriwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM basi ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha dalili za kukinzana na malengo ya kuasisiwa kwake.

CCM imekataa kubadilika kwenye rushwa, hasahasa rushwa za uchaguzi. Rushwa za uchaguzi huzaa viongozi wasiowajibika kwa watu. Kwanini CCM inachagua kutoa viongozi wanaowajibika kwa pesa za uchuuzi?

Viongozi wasiowajibika kwa watu hufanya watu hao wakichoke chama.

Ndio maana kundi la vijana ambao wanaisema vibaya CCM linaongezeka kila baada ya uchaguzi. Ugomvi wao na CCM sio kwa sababu ina sera mbaya na sio sababu haijajenga nchi, ila kwa sababu viongozi wanaotokana na CCM hawaonyeshi udhati wao kwenye kushughulikia masuala yanayoikera jamii kama hili la ufisadi.

Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM.

Bahati ya mtende kuota jangwani ndio inayofanya CCM iendelee kubaki madarakani. Hakuna Chama cha upinzani chenye infrastructure ya kuongoza nchi. Ndio maana watanzania wataendelea kuichagua CCM. Wanaichagua CCM kwa shingo upande huku wakijua they deserve better, but better is not available.

Good news kwa CCM ni kwamba watanzania wanaipa nafasi ya kujirekebisha. Now it's up to CCM kama itajirekebisha au itaendelea kutegemea udhaifu wa wapinzani. Wakati huohuo wapinzani pia wamekuwa wakitegemea udhaifu wa CCM kujitwalia majimbo na kata lakini kwenye Urais ni tofauti.

Vijana wanaokumbatia rushwa za uchaguzi ni vipofu wa fikra, kwa sababu wanachofanya ni kuharakisha tu process ya CCM kuwa chama cha upinzani. Wanajiharibia wenyewe future yao kwa tamaa za muda mfupi.

Mabadiliko ya kweli si lele mama...

Hakika umenena vyema,Tatizo la RUSHWA za Uchaguzi ni janga la kitaifa
 
ZeMarcopolo;12947791]Vyama vya upinzani Tanzania havijajenga uhuru wa mawazo unaoruhusu ushindani wa kisiasa ndani ya vyama hivyo, ndio maana mashabiki wa vyama vya upinzani wanapata shida kuelewa kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kumtafuta mgombea wake wa urais.
Sijui ni uhuru gani unaoongelea, tunadhani unaongelea mheshimiwa kiongozi mkuu kutimuliwa kutoka upinzani.

Wengine wametimuliwa kutoka vyama ikiwemo CCM.CCM ingekuwa na uhuru wa mawazo, vipi Mansour Himid aliyetoa mawazo yake alitendwaje? Nassoro Moyo amepewa uhuru gani wa mawazo?
CCM kuzuia wanachama wasiingie midahalo ndio uhuru wenyewe?

Kuhusu upinzani ndani ya CCM, nakuhakikishia si suala la demokrasia wala uhuru. Ni suala la masilahi binafsi. Hilo safari hii linaitesa sana CCM na huenda ikiwa ni catalyst nzuri tu ya kupoteza. Nitajadili kwa undani katika mabandiko yanayofuata.
CCM imefanya kazi nzuri kuliongoza taifa letu na imeweka misingi ya fursa kwa kila mwenye bidii.
Tanzania ni taifa la kutolewa mfano barani Afrika kutokana na kazi nzuri ya CCM.
Ndugu yangu nakuomba kwa hisani uwe na kaibu kidogo. Hatuwezi kuwa nchi masikini kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.

Hatuwezi kutegemea wafadhaili kwa baJeti kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.

Hatuwezi kuwa nyuma ya Korea, Malaysia, China tuliokuwa karibu nao miaka 50 sasa tofauti yetu ni masikini na wenye uwezo

Hatuwezi kuwakomboa Msumbiji, wakaingia vitani miaka 20 na sasa ni juu yetu.

Hatuwezi kukomboa Botswana wenye rasilimali kama sisi, wakawa kundi jingine tukabaki na nafasi ya 25 masikini sana duniani, eti tutembee vifua mbele CCM inafanya kazi nzuri!!

Fursa unazoongelea ni kwa walioko ndani ya CCM. Nakubaliana nawe ukifanya bidii ukaingia katika system utafanikiwa.

Huko utaruhusiwa kuiba na kusafishwa na ofisi kubwa. Huko utaingia Stanbic na kiroba kitupu ukitoka kimjaa, naam fursa kwa wote.

Fursa ni za wale wanaokwenda kucheki Mimba India, kutibiwa mabusha London, na kuondolewa chunusi South Africa

Mama anayezalia juu ya Tenga miaka 50 baada ya uhuru haoni fursa, anaona moto

Miaka ya 1970 niliona miji ikiwa na Ambulance katika halmashauri. Vituo vya afya vikiwa na usafiri.

Leo tunashushudia watu wakisimama barabarani kuomba msaada wa bajaji kwasababu mtu kapata ajali.

Hakuna Ambulance na hao Polisi hawana vitendea kazi vya kufika maeneo kwa wakati. Kundi hili halina fursa lina maamivu makali

Fursa ni kwa wale wanaopiga kodi za walalahoi ili watoto wakasome nje ya nchi kuanzia kindergaten hadi mwisho.

Wale wasioweza hata kununua sare za shule za kata hawaoni fursa,wanaona moto kila kukicha.
Lakini ni wajibu wa wanaCCM kukiri kuwa kwa kiwango fulani chama kimetoka nje ya misingi iliyokiasisi.
Sijui kama ni chama au ni NGO.

CCM inayojulikana si hii ya leo, kama huna mshiko wewe subiri kupiga kura tu. Utaletewa jina likiambatanishwa na khanga au kofia. Hiyo ndiyo fursa yako
Vipo viashiria vingi lakini kimoja ni Lowassa kufikiriwa kuwa atapitishwa kugombea urais.
Iwapo chama kingekuwa imara kwenye misingi ya uadilifu, mtu kama Lowassa hata asingefikiria kuchukua fomu.
Umeliona hili, lakini nani msafi ndani ya CCM? Hivi unawezaje kulelewa katika familia kisha ukasema ni familia mbovu?

Nani msafi, nani amesimama na kusema hapana, CCM inakwenda kubaya.
Lowassa anamwaga mapesa kwa wajumbe na makada kwa vile anajua ndani ya chama cha mapinduzi siku hizi pesa ndiyo inayoamua nani awe kiongozi.
Na tusipobadilika, Watanzania tutaongozwa na wanunuzi, wachuuzi wa nchi. Nani katufikisha hapa, CCM
Hii ni hatari na vijana lazima wawe mstari wa mbele kulisema hili kwa sauti kuu.
Na kulikataa si kulisema tu.

Kukataa ni kupinga kwa nguvu na vitendo nchi kununuliwa na wafanyabiashara wakitumia wachuuzi wa CCM.
Rushwa ikishamiri kwenye chama itaingia serikalini. Itafikia wakati ukuu wa shule utakuwa unauzwa, ukuu wa idara utapangiwa bei, na huo ndio utakuwa mwisho wa ufanisi. Nchi itaporomoka na hakutakuwa na jinsi ya kuzuia kuporomoka huko.
Haa, hivi unadhani haipo serikalini! Tunadhani CCM ni safi kuliko serikali yake.

Huoni kila mgombea aliye waziri au kiongozi kila mmoja anasema serikali imejaa rushwa.
Wote, watia nia wanakiri serikali ya JK imejaa rushwa na nia zao ni kuiondoa. Wanasema wenyewe!
Lowassa kawaahidi watu wengi vyeo serikalini iwapo atakuwa Rais. Je, nani atasimamia na kukagua ufanisi wa watu walioingizwa kisiasa na mkuu wa nchi? Hawa hawatagusika. Mtu wa namna hii anapofikiriwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM basi ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha dalili za kukinzana na malengo ya kuasisiwa kwake.
Unaona mtandao unavyotesa nchi.
Mwaka 2005 ni mtandao uliomwingiza mtu pale magogoni. Wanamtandao wakiiba, kazi ya kusafishwa inafanyika pale pale walipowekeza. CCM unayosema imetoa fursa imebaki kuwa kijibwa koko, inabweka tu. Wenye nchi wanatenda yao kwa msaada wa ofisi waliyoipigania
CCM imekataa kubadilika kwenye rushwa, hasahasa rushwa za uchaguzi. Rushwa za uchaguzi huzaa viongozi wasiowajibika kwa watu. Kwanini CCM inachagua kutoa viongozi wanaowajibika kwa pesa za uchuuzi?
Unakubaliana nasi kuwa CCM haijaleta maendeleo uliyosema mwanzoni, haitoi fursa sawa kwasababu kama huna pesa, si lolote si chochote, subiri kofia, tshirt na khanga. Fursa uliyosema ipo CCM iko wapi mkuu?
Ndio maana kundi la vijana ambao wanaisema vibaya CCM linaongezeka kila baada ya uchaguzi. Ugomvi wao na CCM sio kwa sababu ina sera mbaya na sio sababu haijajenga nchi, ila kwa sababu viongozi wanaotokana na CCM hawaonyeshi udhati wao kwenye kushughulikia masuala yanayoikera jamii kama hili la ufisadi
Mkuu hawa wamewekeza , wana muda gani wa kusikiliza wananchi? Wanachokifanya ni kuangalia return ya uwekezaji wao

Huu ndio utamaduni wa CCM uliopo siku hizi. Na hapa tena unarudi kule kule, hao vijana wanaichukiaje CCM ikiwa unadai inatoa fursa sawa kwa wote? Kwanini wakimbilie upinzani na wasikae na fursa ndani ya CCM?
Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM
Hao wanaoamua nani awe mbeba bendera wa CCM ni mafisadi.
Sasa nani amfunge paka kengele. Wanajua wazi baada ya muda wataondoka, lazima waweke mtu wa kulinda masilahi yao.

Ni yale ya Kagoda, Meremeta, Tangold n.k. kulindana, utamaduni wa CCM na wenye fursa ndio wanaosema, CCM njema!
 
Tutakuwa na mfululizo wa mabandiko kuangali uchaguzi kwa ujumlawake.

Mtazamo wa wagombea watarajiwa katikahatua za awali. Hali ya chamatawala baada ya miaka50
Hili swala mimi ndio nimelifatilia zaidi

Kinachojitokeza dhahiri asilimia kubwa ya matatizo ya taifa yanachangiwa na vyama vya siasa. Unaweza kuvisamehe vyama vya upinzani kwa uchanga wake; lakini si CCM hawa wamekuwa na zaidi ya miaka 50 ya work experience ya uendeshaji wa serikari katika muda huo wamepata mafanikio vilevile wameona makosa yao katika kuendesha serikari na sasa walitakiwa kuwa ni mashine ya kutoa viongozi waliokomaa walau kutorudia tena makosa yale yale yanayo julikana.

Aiwezekani leo tulalame ubovu wa uendeshwaji wa mashirika ya umma kama nyakati za Mwalimu miaka ya sabini wakati yeye alikubali tatizo lilikuwa ni uwezo wa wawafanyakazi na mbinu hafifu za usimamizi miaka 40 baadae ripoti ya CAG irudi na kitu kile kile safari hii jumlisha na ufisadi wa kutupa juu. CCM amekuwa kaka mmbaya kama mfano wa kuigwa na kaweka kiwango cha chini sana katika siasa zetu, kiwango cha chini katika kuangalia kiongozi bora na kiwango cha chini kwenye kufikiria maendeleo.

Kinachovunja moyo ni muundo wenyewe wa CCM na possibility za kubadilika anytime soon uelewa wa chama cha siasa unataka kujua nguvu zake za maamuzi zilipo na si vyama vyote vipo sawa au demokrasia inaangaliwa kwa jicho moja katika vyama tofauti kutokana na asili ya kuanzishwa kwake.

CCM ya leo imefanana na chama cha ushirika kuliko chama cha siasa; kwa sababu chama cha ushirika ndio maamuzi ya kimkakati yanaweza pangwa na watu wasiokuwa viongozi na kuchagua mtu wa kusimamia tu na yeye ana majukumu ya kupanga safu ya uongozi ndio CCM na ilani yake. To give credit kwa vyama vya ushirika walau they will take the trouble to ensure wanachagua kiongozi mwenye track record sio CCM yeyote mwenye kudhani ajitokeze in the name of democracy thereafter he is entrusted with unquestionable authority.

Hii sio namna sahihi kabisa kwa siasa za wenzetu vyama vya siasa kwanza vinafaya thathmini ya ilani yao iliyopita, social scanning, challenges za ilani iliyopita; hali ya usalama wa taifa, afya ya chama na mengineo. Kikwetu mifano michache ninayoifikiria ingekuwa:
· Budget shortfall na kutafutia ufumbuzi wake kwa mbinu zenye maelezo sio hadithi
· Social disintegration udini unaoibuka na makundi yanayoibuka yanatishia usalama wa taifa
· Discipline ya chama na kuwaweka baadhi ya wanachama ndani ya mstari, maadili ya uongozi
· Usimamizi mmbovu wa sera za serikari
· Kupwaya kwa uelewa kwa baadhi ya mawaziri kwenye kusimamia wizara walizokabiliwa
· Ajira
· Kupanda kwa gharama za maisha
· Kushuka kwa thamani ya fedha
· Mitaji ya mikopo
· Amount of players to increase competition in some sectors to benefit consumers
· Elimu

Mlolongo ni mrefu wa mifano lakini mwisho wa siku chama kinaangalia vipaumbele kama ni usalama basi ilo linakuwa wazi kiongozi ajaye lazima awe na sifa ya intellegensia au uwezo na mbinu, kama ni uchumi basi lazima waangalie ni nani na chama akifichi hakuna cha siri hawa ndio tunaowataka, demokrasia ya kugombea kwa wengine ni procedure tu au an act of rebellion to upset the higher hierarchy: baada ya hapo sasa ndio ilani inaandikwa kwa mlengo wa chama na kiongozi akishiriki kusaidiana na team ya chama.

Na ndio mantiki ya kiongozi kupewa powers za kuteua kwa sababu ya kuwa nahodha wa kile alichokileta mezani na utapimwa kwa mafanikio yake ndani ya chama na impact ya sera utakazo tunga kwa hivyo jukumu la nani anakufaa nani afai pia lako kwenye kukusaidia lakini challenge zipo wazi isije tena baadae udai ujui kwanini kitu fulani ni tatizo.

Haya CCM tayari wana ilani wanatafuta kiongozi kila mtu anakuja akifikiri tatizo ni ili si lile wamepishana kimtazamo utadhani wanatoka vyama tofauti.

Chama akijaifanya nafasi ya uraisi na uenyekiti wa chama ionekane kwa ugumu kuna watu awajaingia ofisi za CCM miaka mingi atakama bado wanachama leo wanataka wapewe nafasi ya uenyekiti na uraisi yani wameifanya nafasi ionekane nyepesi na yeyote mzenye kadi anazewa imudu not special at all. Pamoja na siasa kwa ujumla za taifa anything goes kufikia malengo uchawi; rushwa, makundi yasiyopishana kimtazo kwenye kutekeleza thatmini za chama bali kuunga tu mkono kwa sababu wazijuazo wao hii si democracy bali anarchy at earliest stages misingi aliyoiacha mwalimu JKN ni wazi sasa ni nyufa ndani ya chama na usalama wa taifa kwa ujumla wake.
 
Eric Cartmanahsante. CCM iliyojaa maprofesa, miaka 50 haina excuse yoyote.

Akina Nyerere walianza pagumu sana, hawakuwa na wizi tunaouona na walifanya mengi ya maana

Nimesikia Rais akisema, wakati anaingia kulikuwa na vyuovikuu 26 sasa ni 52.
Hata kabla ya kujua ubora, hivi kweli kuna mtu alitaraji Nyerere angejenga vyuo hata viwili kwa changamoto alizokuwa nazo.

Huyo anayesema, kasomeshwa na Nyerere.

Kwa umri 50 CCM si ya kuongelea ufisadi. Ilipaswa kuongelea namna gani wananchi wanaondoka katika middle class kwenda juu kama ilivyo Malaysia

50 hawakuweza kukomesha rushwa, watawezaje ndani ya miaka 5.

Miaka 50 hawana la maana la kuwaeleza wananchi! Bado watu wanakaa kitako kuwasikiliza

Kuhusu vigezo wananchi wanavyotakiwa kuviangalia kama ulivyosema

1 Ilani imetimizwa kwa kiasi gani. Ilani ya uchaguzi ndiyoilikiweka chama madarakani.
Je, kile walichouziwa wananchi, ndicho walichopata?

2 ‘Bajeti ya nchi. Je, tumeweza kujitegemea? Upungufu wabajeti unakabiliwaje na kwa kutumia rasilimali zipi?
Tupunguze ukubwa waserikali? Tuwe na bajeti inayolingana na matumizi yetu, tuzuie wizi na ufisadi,tupate wapi vyanzo vingine?

Je, tumetumia rasilimali zetu katika kiwango?Tumetafuta vyanzo vingine mbadala?
Tunabana vipi misamaha ya hovyo ya kodi?Wanopaswa kulipa kodi wanalipa?

3 Je, umoja wa kitaifa upo? Kama unaondoka ni kwanini nanini kifanyike?

4Huduma zetu zipi zipewe kipaumbele, kwanini na kwa muda gani

5 Tunakabilianaje na vitu kama mifumuko ya bei, kushuka thamani kwa pesa

6 Tuna vyanzo gani vya nishati, tunaitumiaje

Orodha inaendelea, inatosha kusema kuwa, CCM haijaweza ku-balance budget kwa miaka 10 tu iliyopita.
Hao wagombea wanaoongelea rushwa,wanaongelea ili iweje.

Maana yetu ni kuwa CCM inatumia rushwa kutafuta huruma kwawananchi.

Wananchi wawaulize tuliyosema na mengine kwanza.
Waulize, nikipi kipya CCM watafanya kukabaliana na rushwa ambacho sasa hivi hakipo?

Walipokataa rasimu ya Warioba na kuondoa maadili walikuwa wanapigana au wanaunga mkono rushwa?

Walisema rasimu ya Warioba itaongeza mzigo, je tume ya uchaguzi inayogawa majimbo kusaidia CCM kupata 2/3 inapunguza gharama?
 
Sijui ni uhuru gani unaoongelea, tunadhani unaongelea mheshimiwa kiongozi mkuu kutimuliwa kutoka upinzani.

Wengine wametimuliwa kutoka vyama ikiwemo CCM.CCM ingekuwa na uhuru wa mawazo, vipi Mansour Himid aliyetoa mawazo yake alitendwaje? Nassoro Moyo amepewa uhuru gani wa mawazo?
CCM kuzuia wanachama wasiingie midahalo ndio uhuru wenyewe?

Kuhusu upinzani ndani ya CCM, nakuhakikishia si suala la demokrasia wala uhuru. Ni suala la masilahi binafsi. Hilo safari hii linaitesa sana CCM na huenda ikiwa ni catalyst nzuri tu ya kupoteza. Nitajadili kwa undani katika mabandiko yanayofuata. Ndugu yangu nakuomba kwa hisani uwe na kaibu kidogo. Hatuwezi kuwa nchi masikini kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.

Hatuwezi kutegemea wafadhaili kwa baJeti kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.

Hatuwezi kuwa nyuma ya Korea, Malaysia, China tuliokuwa karibu nao miaka 50 sasa tofauti yetu ni masikini na wenye uwezo

Hatuwezi kuwakomboa Msumbiji, wakaingia vitani miaka 20 na sasa ni juu yetu.

Hatuwezi kukomboa Botswana wenye rasilimali kama sisi, wakawa kundi jingine tukabaki na nafasi ya 25 masikini sana duniani, eti tutembee vifua mbele CCM inafanya kazi nzuri!!

Fursa unazoongelea ni kwa walioko ndani ya CCM. Nakubaliana nawe ukifanya bidii ukaingia katika system utafanikiwa.

Huko utaruhusiwa kuiba na kusafishwa na ofisi kubwa. Huko utaingia Stanbic na kiroba kitupu ukitoka kimjaa, naam fursa kwa wote.

Fursa ni za wale wanaokwenda kucheki Mimba India, kutibiwa mabusha London, na kuondolewa chunusi South Africa

Mama anayezalia juu ya Tenga miaka 50 baada ya uhuru haoni fursa, anaona moto

Miaka ya 1970 niliona miji ikiwa na Ambulance katika halmashauri. Vituo vya afya vikiwa na usafiri.

Leo tunashushudia watu wakisimama barabarani kuomba msaada wa bajaji kwasababu mtu kapata ajali.

Hakuna Ambulance na hao Polisi hawana vitendea kazi vya kufika maeneo kwa wakati. Kundi hili halina fursa lina maamivu makali

Fursa ni kwa wale wanaopiga kodi za walalahoi ili watoto wakasome nje ya nchi kuanzia kindergaten hadi mwisho.

Wale wasioweza hata kununua sare za shule za kata hawaoni fursa,wanaona moto kila kukicha. Sijui kama ni chama au ni NGO.

CCM inayojulikana si hii ya leo, kama huna mshiko wewe subiri kupiga kura tu. Utaletewa jina likiambatanishwa na khanga au kofia. Hiyo ndiyo fursa yako Umeliona hili, lakini nani msafi ndani ya CCM? Hivi unawezaje kulelewa katika familia kisha ukasema ni familia mbovu?

Nani msafi, nani amesimama na kusema hapana, CCM inakwenda kubaya. Na tusipobadilika, Watanzania tutaongozwa na wanunuzi, wachuuzi wa nchi. Nani katufikisha hapa, CCM Na kulikataa si kulisema tu.

Kukataa ni kupinga kwa nguvu na vitendo nchi kununuliwa na wafanyabiashara wakitumia wachuuzi wa CCM. Haa, hivi unadhani haipo serikalini! Tunadhani CCM ni safi kuliko serikali yake.

Huoni kila mgombea aliye waziri au kiongozi kila mmoja anasema serikali imejaa rushwa.
Wote, watia nia wanakiri serikali ya JK imejaa rushwa na nia zao ni kuiondoa. Wanasema wenyewe! Unaona mtandao unavyotesa nchi.
Mwaka 2005 ni mtandao uliomwingiza mtu pale magogoni. Wanamtandao wakiiba, kazi ya kusafishwa inafanyika pale pale walipowekeza. CCM unayosema imetoa fursa imebaki kuwa kijibwa koko, inabweka tu. Wenye nchi wanatenda yao kwa msaada wa ofisi waliyoipigania Unakubaliana nasi kuwa CCM haijaleta maendeleo uliyosema mwanzoni, haitoi fursa sawa kwasababu kama huna pesa, si lolote si chochote, subiri kofia, tshirt na khanga. Fursa uliyosema ipo CCM iko wapi mkuu? Mkuu hawa wamewekeza , wana muda gani wa kusikiliza wananchi? Wanachokifanya ni kuangalia return ya uwekezaji wao

Huu ndio utamaduni wa CCM uliopo siku hizi. Na hapa tena unarudi kule kule, hao vijana wanaichukiaje CCM ikiwa unadai inatoa fursa sawa kwa wote? Kwanini wakimbilie upinzani na wasikae na fursa ndani ya CCM? Hao wanaoamua nani awe mbeba bendera wa CCM ni mafisadi.
Sasa nani amfunge paka kengele. Wanajua wazi baada ya muda wataondoka, lazima waweke mtu wa kulinda masilahi yao.

Ni yale ya Kagoda, Meremeta, Tangold n.k. kulindana, utamaduni wa CCM na wenye fursa ndio wanaosema, CCM njema!

Mkuu Nguruvi,

Nilitegemea uje na jibu, lakini umekataa kuja na jibu au kutoa changamoto, badala yake unetafuta tu maneno mengine ya kusema kilekile nilichoandika.
Hata hivyo nimeipenda post yako kwa vile imeendorse nilichoandika.

Msingi wa ninachpjadili ni kuwa at any time t lazima ikulu iwe occupied. Ikulu haiwezi kuwa vacant hata kwa siku moja. Sasa our situation ni kwamba tuna CCM na wapinzani. CCM is bad wapinzani are worse. CCM is slow wapinzani are slower, CCM is weak, wapinzani are weaker.

Mabaya yote uliyotaja ya CCM happy juu ni ya ukweli. Hujakosea, actually ndio msingi wa hoja yangu, kuwa CCM is not clean ila ina bahati ya mtende inayotokana na udhaifu wa wapinzani hasahasa kwenye nafasi ya urais.

Hata hivyo, ukisema CCM haijafanya kitu chochote chenye manufaa unanisababisha nisijibu zaidi kwa sababu ya aina ya jukwaa tulilopo. Hoja kama hiyo naweza kuijibu kule mchafukoge kwa style inayostahili. Kwa huku nakaa kimya.
 
Mkuu ukisoma nilichoandika, sikwenda kwa wapinzani uliko jadili. Nilikuwa nataka nitenganishe kwasababu hoja zako juu ya wapinzani zina uzito. Umeniwahi tu, lakini nitazijadili vema.

Pengine ni changamoto nzuri sana kwa wapinzani na nitashangaa kama yupo mpinzani atasoma kwa mtazamo tofauti
Kwangu ulichosema ni challenge kwao. Nitajadili
 
zeMarcopolo

Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM.

Bahati ya mtende kuota jangwani ndio inayofanya CCM iendelee kubaki madarakani. Hakuna Chama cha upinzani chenye infrastructure ya kuongoza nchi. Ndio maana watanzania wataendelea kuichagua CCM. Wanaichagua CCM kwa shingo upande huku wakijua they deserve better, but better is not available.

Good news kwa CCM ni kwamba watanzania wanaipa nafasi ya kujirekebisha. Now it's up to CCM kama itajirekebisha au itaendelea kutegemea udhaifu wa wapinzani. Wakati huohuo wapinzani pia wamekuwa wakitegemea udhaifu wa CCM kujitwalia majimbo na kata lakini kwenye Urais ni tofauti.

Vijana wanaokumbatia rushwa za uchaguzi ni vipofu wa fikra, kwa sababu wanachofanya ni kuharakisha tu process ya CCM kuwa chama cha upinzani. Wanajiharibia wenyewe future yao kwa tamaa za muda mfupi. Mabadiliko ya kweli si lele mama
Mkuu hakika wameanza kujinasibisha na jamii. Agenda ya ufisadi na wizi si ya CCM, lakini kila mmoja anayetia nia anaitaja. Wanajua ni namba moja katika matatizo ya taifa. Swali linakuja, hao wanaolaani ufisadi wakiwa ndani ya CCM wanatenda kwa dhati au ndio kujiunga na jamii? Watawezaje kufumua mfumo uliowalea kwa miaka yote tena wakiwa kimya?

Kumpata mgombea wa CCM asiye na unasaba na Ufisadi haiwezekani. Mtu msafi kabisa ndani ya CCM bado ni mchafu wa ufisadi. Sababu kubwa ni moja, nani amesimama na kuisema serikali ya CCM kuhusu ufisadi ? Hakuna jibu, wote wanautumikia mfumo, na itakuwa ajabu akitokea mtu na kutuambia tofauti

Kuhusu wananchi, taratibu wanatambua mabadiliko ni muhimu. Kwanza, walikuwa na hofu ya amani kwavile mfumo wa vyama vingi haukuwepo. Tulianza na wabunge 5 nadhani, taratibu wameongezeka.
Kasi ya kuongezeka si ya kuridhisha, hata hivyo lazima tukubali kuwa mazingira yaliyotengenezwa na CCM hayawezi kutoa fursa

Jukumu la mabadiliko limerudi kwa wananchi. Unaona serikali za mitaa watu 12 huko kijijini wameshika bendera wanashangilia ushindi wa kitongoji kwa wapinzani. Hii maana yake wananchi wana kiu ya mbadiliko, wapo tayari. Swali, je wanakuwa motivated kiasi cha kutosha?

Hapa ndipo wapinzani wanapokuwa slow kama ulivyosema. Tunajua hakuna uwezekano wa kupata haki na usawa. Ni wajibu wa wapinzani kuhakikisha wanatafuta njia ya kuvunja mgongo wa ngamia
Ndio maana nilisema ziwepo plan A1 na A2

A1 ni kupata kiongozi wa dola. Hilo linataka ushindi wa Chiluba ambao Kenneth Kaunda hakuweza kuufanyia kazi maabara. Ilikuwa haiwezekani.

A2 kutokana na mwamko wa A1 upo uwezekano wa kufikia idadi ya wabunge itakayoondoa 2/3 ya ccm.
Watu hawafahamu kuwa CCM inatumia sheria 'haramu'' kutokana na 2/3 tu. Mifano tumeiona. Ikiwezekana kuvunja 2/3, hapo utakuwa mwanzo wa kubadili mwelekeo wa nchi.

CCM wanajua kuwa uwezekano wa kupoteza 2/3 ni mkubwa sana. Ndio maana wametangaza majimbo mapya kupitia ytawi lao la ''tume ya uchaguzi'' Hizi ni mbinu za woga, wapinzani wanatakiwa wajue hilo. Kazi uya upinzani ilikuwa ku take advantage hiyo kuongeza wabunge. Wasilalamike kuongezwa majimbo, bali wapiganie kutwaa majimbo hayo

Je, wapinzani wanaweza. Yes, inawezekana kama ilivyotokea kwingine. Muhimu ni kuwa na mbinu na mikakati. Moja, kuhamasisha wananchi kupiga kura, pili, kuwafikia na kuwapa ujumbe unaolingana na hali ya maisha yakiwemo majawabu, tatu, juwaweka CCM katika 'defence zone''

Leo wapinzani hawana mkakati na kule wasikofanikiwa. Hakuna dalili kama wana mkakati.
Wananchi wanawasubiri, tatizo hawana mbinu za kuwafikia.

Mbinu mojawapo, viongozi wa UKAWA wasambae kila mahali wakiwa na ujumbe na si kelele.
Viongozi wa UKAWA washiriki kama wabunge ili kuongoza nguvu kwa kutumia umaarufu wao

Waende ngazi za chini na vijijini kuwafikia wananchi. Wahamasishe kulinda kura! yes, inawezekana mbona serikali za mitaa CCM walishindwa kuiba?

Endapo uchaguzi wa serikali za mitaa CCM imepoteza kwa 20% ikiwa na kila sababu ya kushinda kwa hila na mbinu, ni dalili kuwa huko chini wamehasika!

cc
MJINI CHAI
 
Ni kweli kuwa ufisadi inaonekana kama agenda ya wapinzani, lakini si kweli kuwa rushwa na ufisadi ni agenda ya wapinzani.

Sokoine anasifika kwa kupiga vita ufisadi. Kipindi cha Sokoine hakukuwa na upinzani. Sio kweli kwamba rushwa na ufisadi ni kitu kipya. Ilikuwepo, ipo na kwa kiwango fulani lazima itaendelea kuwepo. Lengo sio kueliminate rushwa ila ni kuwa na no tolerance policy INAYOTEKELEZWA.

Tofauti kati ya wapinzani na CCM ni kuwa mpinzani ana uhuru wa kusema mapungufu ya serikali hadharani bila kujidhuru kisiasa. Ndio maana watangaza nia hawajawahi kusema haya wanayosema hadharani. Kwenye vikao vya ndani wanasema.

Tukisema CCM imekataa kubadilika kuhusu rushwa ya uchaguzi, hatumaanishi kuwa kila mtu CCM anapenda na kuunga mkono rushwa, ila tunasema matendo ya rushwa yanavumiliwa. Kama CCM wanashaurika basi angalau kwa nafasi ya Urais wawe wakali. Waseme kwa urais mtoa rushwa fomu yake hata haifunguliwi ukurusa wa pili. Na wawe serious kwenye hilo.

Rais anayepatikana kwa njia hiyo ana uwezekano mkubwa wa kuwasikiliza na kuwajali wananchi kuliko Rais aliyeanzia mkakati wa uchaguzi kwenye vibaraza vya wachuuzi.

Lowassa ni icon ya ufisadi nchini, kitendo cha yeye kushabikiwa na viongozi wa chama mikoani ni ishara kuwa CCM imekataa kujirekebisha. Lakini hii ni ishara tu, maamuzi ya kamati kuu na NEC yatatoa jibu la uhakika. Baada ya maamuzi yao hatutazungumzia tena ishara, tutakuwa tumejulishwa ufisadi unachukuliwaje na mainstream CCM.
 
Article hii ya kiongozi wa Chadema ni ishara tosha kuwa hata UKAWA wanatafuta Rais toka CCM...

Katika article hii, pamoja na mambo mengine, utaona ukweli kuwa rushwa si agenda mpya na si agenda ya upinzani kama jinsi wapinzani wengi wanavyotaka ieleweke.

Kwa kifupi, wapinzani hawana agenda mpya. Na hiyo ni bahati ya mtende ya CCM...

Na Fred Mpendazoe

SIKU Edward Lowassa alipotangaza rasmi kugombea urais wa Tanzania nilibahatika kumsikiliza na nilishuhudia umati mkubwa wa watu waliofurika kumsikiliza. Ni kweli yalikuwa ni mafuriko ya watu. Sijui kama walikwenda kwa hiari yao au walilipwa ili waende kwenye mkutano huo.

Hilo sijui wala si ajenda yangu kwenye makala hii. Jambo ambalo ninataka wasomaji wa makala hii walizingatie ni aina ya watu waliokuwepo kwenye mafuriko hayo, kwani ndege wenye manyoa yanayofanana ndiyo wanaoruka pamoja. Watanzania wajiridhishe bila shaka yoyote Lowassa ni nani. Na je anaweza kukabiliana na changamoto zinazolikabili Taifa letu hasa ufisadi, rushwa na kuporomoka kwa maadili.

Mwalimu Nyerere katika kitabu chake, Nyufa, cha mwaka 1995, alisema: “Sasa Tanzania inanuka rushwa… tunataka kiongozi anayejua hivyo, ambaye atasema rushwa kwangu mwiko, mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa na… watoa rushwa watamjua hivyo. Lakini hatutaki aishie hapo tu, maana haitoshi wewe mwenyewe uwe mwaminifu… Unaweza ukawa wewe mwaminifu kabisa kabisa, lakini una shinikizo la ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako.

“Kwa hiyo si inatosha wewe kuwa mwaminifu tu, lakini uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa zako kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena. Unawaambia jamaa na rafiki zako kwa dhati kabisa… Ikulu ni mahali patakatifu, mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza pango la walanguzi na hakuna serikali yoyote duniani inayoongozwa bila miiko”.
Zipo taarifa zinazoeleza kwamba fedha nyingi zimetumika katika kufanya maandalizi ya mkutano wa Arusha uliosababisha mafuriko ya watu. Aidha, ndugu Lowassa mara kadhaa amekiri kwamba marafiki zake ndio wanaomchangia kufanikisha safari yake ya matumaini.
Hivyo fedha nyingi anazochangia kwenye harambee kwenye misikiti na makanisani nyingine anatoa yeye na nyingine anachangiwa na hawa marafiki zake ambao wengi wao ni wafanya biashara matajiri na wengi wao ni wale waliotajwa kwenye kashfa za ufisadi natuhuma mbalimbali.

Hawa marafiki zake Lowassa wamesaidia sana kumjua Lowassa ni nani, kwani wahenga walisema, “Nionyeshe marafiki zako na mimi nitakuambia wewe ni nani au wewe una tabia gani”.
Hawa marafiki zake na Lowassa wanaweza kuwasababisha Watanzania wamtilie shaka Lowassa kama anaweza kuwa safi na kustahili kupewa dhamana ya kuongoza nchi. Naomba niwakumbushe kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu mmoja wa wagombea urais kwenye NEC Dodoma mwaka 1995, “Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi”.
“Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe nae chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni, Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike”.

“Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba si kweli. Lakini Kaisari bado akamwacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine wasafi ambao hawana tuhuma.

“Kama mtamteua huyu mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu nimwombee kura. Hapana kabisa . Huyu najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu”.

Aidha, mtakumbuka pia kuwa mwaka 1995, kundi la Vijana lilimtaka Lowassa ateuliwe kugombea urais wa Tanzania. Hata hivyo, ilitolewa kauli kuwa Lowassa alikuwa na tuhuma za rushwa, kujilimbikizia mali na kupungukiwa na maadili, kinyume na katiba ya CCM na kanuni za chama hicho.

Kamati Kuu ilipopeleka mapendekezo ya kutompendekeza kugombea urais, Lowassa alitetewa kwa makelele, kihuni, bila kufuata taratibu za kikao cha NEC Dodoma. Kundi moja lilikuwa limejiandaa kumpitisha kwa hoja ya nguvu na si kwa nguvu ya hoja.

Waliyatetea maelezo ya Kamati Kuu, lakini waliyakataa yale ya nyongeza aliyoyatoa Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi (Rais wa wakati huo) ambaye alielezea tuhuma hizo zilizokuwa zinamkabili Lowassa. Hivyo, naomba kusisitiza kwamba Lowassa hakuwa chaguo la CCM katika uchaguzi wa mwaka 1995.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu, Mwalimu Nyerere aliamua kusaidia kikao kwa kutoa maelezo ya nyongeza. Aliwauliza wajumbe wa NEC maswali, kwamba wao ni wahuni au ni viongozi wa CCM? Ikiwa wao ni viongozi wa CCM, je, hivyo ndivyo wanavyopaswa kumtafuta mgombea wa urais, kwa makelele?

Kama Watanzania wangewaona walivyokuwa wanafanya katika kikao hicho, je, wangeamini kuwa wao ni viongozi kweli? (Wajumbe walibaki kimya). Kisha Mwalimu aliendelea kusisitiza maelezo aliyoyatoa Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi akisema: “Mwinyi amemstahi sana Lowassa”.
Hakuwaambia wajumbe wa NEC baadhi ya tuhuma mbaya kabisa kuhusu Lowassa.
Ikiwa NEC inachoombwa ni kuchagua kati ya wenye tuhuma za rushwa kuchaguliwa kwa nafasi ya urais, na wale wasioitaka, basi huu ni wakati muafaka kwao kuipeleka hoja hiyo mbele ya Watanzania waiamue kwa kuwa ndani ya NEC hakuna mwenye uwezo wa kumfukuza mwenzie, wote ni wajumbe sawa kwa mujibu wa katiba ya CCM”.

Hatimaye kikao cha NEC kiliondoa jina la Lowassa, kikawateua Benjamin William Mkapa, Cleopa David Msuya na Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wagombea. Majina yao yaliwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu ambao ndio uliopaswa kumchagua miongoni mwao kuwa mgombea urais wa CCM.

Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM, wagombea hao watatu walijinadi kwa wajumbe. Kikwete alipokuwa akijinadi aliwaeleza wajumbe kwamba endapo wangempitisha kugombea na akashinda, angemteua Lowassa kuwa Waziri Mkuu wake.

Hata hivyo Kikwete hakuchaguliwa kuwa mgombea urais. Historia hii inatoa mfano hai wa jinsi matatizo yanayolikumba taifa letu yalivyoanza.Ni dhahiri kabisa kuwa watu walewale, wakiongozwa na tamaa zilezile za kuwa matajiri na kutaka urais kwa gharama yoyote hata kuhonga au kutumia fedha, ndio wanaolisumbua taifa letu mpaka sasa.

Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, wale wanaoomba nafasi ya urais hawapaswi kutuhumiwa kwa jambo lolote. Hawapaswi kutiliwa mashaka kuhusu uadilifu wao. Wanapaswa kuaminiwa kuhusu dhamira yao ya kupiga vita ufisadi na rushwa.

Na wagombea hawa tunaweza kuwajua kutokana na hulka au tabia za marafiki zao. Katika mafuriko ya Arusha, baadhi ya walioshiriki mkutano huo walitajwa. Hawa walitajwa kuwa ni marafiki wa Lowassa. Wengine walikuwa wamevaa nguo zilizoandikwa “Marafiki wa Lowassa”.
Baadhi ya marafiki wa Lowassa ni pamoja na Rostam Aziz, Andrew Chenge, Anna Tibaijuka, Cyril Chami, Ezekiel Mayige, David Matayo, Nazir Karamagi na kadhalika.

Baadhi ya marafiki hawa wa Lowassa wengi wao ni wale ambao ama walijiuzuru kwa kupatikana na tuhuma za ufisadi, au wengi wao waliondolewa kwenye nyadhifa zao kwa kashfa za kutokuwa waadilifu.

Na wengi wao ni wafanyabiashara na matajiri. Tunapoliangalia kundi la watu wanaomuunga mkono Lowassa, tunaweza kujua Lowassa ni nani. Tukiliangalia kundi linalomuunga mkono Lowasssa tunaweza kujua kama Lowassa akiingia Ikulu atapambana na rushwa na ufisadi au ataenda kufanya biashara.

Je, marafiki wa Lowassa anaowataja na walioonekana kwenye mafuriko ya Arusha wanakerwa na rushwa na ufisadi kwa dhati?. Ndege wenye manyoya yanayofanana ndio wanaoruka pamoja.
Watanzania tukumbuke kwamba utumishi wa umma ni dhamana na fursa adhimu kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wananchi wote. Haya ni maneno aliyoyasema Rais Barack Obama baada ya kula kiapo cha kuongoza Marekani.

Inawapasa wale wanaopata nafasi za kuchaguliwa wafahamu kwamba wamepewa dhamana ya kuwatumikia wananchi na si nafasi ya kujitajirisha au kumnufaisha ndugu au marafiki. Kutokana na kumomonyoka kwa maadili na moyo wa uzalendo nchini, uongozi umegeuzwa kuwa nafasi ya kujitajirisha. Urais, uimekuwa fursa ya uwekezaji, na wala si fursa ya kuwatumikia wananchi.
Ukweli kwamba kuna matajiri au watu wanaotumia pesa kumiliki siasa na uongozi katika nchi yetu, ni jambo lililo wazi. Zipo taarifa kwamba baadhi ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya watia nia ya urais mfano waliofurika Arusha walinunuliwa waende kwenye mkutano, walilipwa wapige kelele “Rais, Rais”.

Matumizi makubwa ya fedha yalionekana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi huo, Kikwete, alizindua Bunge Desemba 30, 2005 alidhibitisha hili alisema: “Yameanza mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa fedha.

“Tusipokuwa waangalifu, nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo, maana unaweza kufadhiliwa na mtu ili ununue uongozi, ni vema sasa tulishughulikie suala hili”.

Kuna mawazo kwamba sasa Tanzania inahitaji Rais tajiri. Ninapenda niwakumbushe wosia alilowahi kuutoa Mwalim Nyerere wakati wa uhai wake juu ya hatari ya watu wachache wenye pesa kujaribu kutafuta uongozi kwa manufaa yao.
Alisema: “Tanzania halijawa taifa imara sana na adilifu kiasi cha kuruhusu matajiri kuingia kwenye uongozi wa nchi kama ilivyo Marekani na Ulaya. Wakati huo bado uko mbali sana na tukitaka kuuvuta kwa kamba huko ndiko kuliingiza taifa letu changa kwenye kiwango cha ufisadi”.

Mgombea mmoja wa urais amesema bado anasaka utajiri na anaomba aende Ikulu. Je Ikulu kuna biashara gani itakayompatia utajiri? Na wale wanaomuunga mkono atawalipaje akienda Ikulu?
Nchi kuwekwa rehani kwa matajiri ni jambo la hatari sana, kwa maana serikali itaongozwa na matajiri na haitawajibika kwa wananchi. Hili limeanza kujitokeza. Demokrasia itakoma na udikteta utatawala.

Jambo linalojitokeza hapa na ambalo ni matokeo ya matumizi makubwa ya fedha na rushwa kwenye chaguzi, ni kupatikana kwa viongozi ambao hawakuchaguliwa na wananchi bali walinunua uongozi au waliotoa rushwa kushawishi wapiga kura wawape uongozi.
Serikali inayopatikana kwa rushwa haiwajibiki kwa wananchi. Hutumikishwa na matajiri walionunua uongozi na waliotoa rushwa. Serikali hiyo huwaabudu matajiri walioiweka madarakani, haiwezi kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wananchi.

Serikali hiyo hulinda maslahi ya watu wachache, haiwezi kuchukua hatua dhidi ya ufisadi. Baadhi ya maamuzi ambayo yamekuwa yakitolewa na utawala wa awamu ya nne, ripoti ya hivi karibuni ya Ikulu ya TOKOMEZA na ESCROW ni ushahidi wa ninachokieleza.
Tuwe makini na wagombea wanaotumia fedha nyingi na wanaopewa fedha nyingi na marafiki zao katika mchakato wa kutafuta nafasi za kuchaguliwa urais, ubunge na udiwani. Tumejifunza katika utawala wa awamu ya nne. Tusirudie makosa.

Ningependa kusisitiza, Watanzania tunatakiwa tuichukie rushwa ya aina yoyote. Rushwa ni dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti. Rushwa hupofusha macho na moyo. Taifa linaoendekeza rushwa ni taifa ambalo watu wake ni sawa na vipofu na wafu.
Vipofu ambao hawaoni madhara ya rushwa na mioyo yao imekufa. Rushwa inapotolewa na kupokelewa kwa shangwe makanisani na misikitini na wagombea wa vyama vya siasa ni ushahidi wa jambo hili.

Tanzania ina nafasi ya kuwa Taifa linaloheshimika kama tutaichukia rushwa na kukataa kuipokea au kuitoa. Mfalme Suileman aliwahi kusema; “haki huinua taifa bali dhambi na uovu ni aibu ya watu wote”. Rushwa ni dhambi na ni aibu kwa watanzania wote.
Tanzania imepoteza heshima kwa sababu ya rushwa. Pia napenda kusisistiza, Kwenye nchi ambapo rushwa imetawala sauti ya wengi si sauti ya Mungu. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu kwenye nchi ambapo haki, usawa na upendo vinatamalaki.

Mafuriko ya watu kule Arusha kama walilipwa ili waende kwenye mkutano sauti yao si sauti ya Mungu. Na, Je Lowassa ana dhamir ya kweli ya kuchukia rushwa?

Nionyeshe marafiki zake na mimi nitakuambia kama Lowassa ana dhamira ya kweli ya kupiga vita rushwa na ufisadi. Niliposikiliza akisema atapiga vita ufisadi, rushwa na atahakikisha rasilimali za nchi hii zinawanufaisha Watanzania na nilipowangalia marafiki zake ni nani, nilitambua anachokifanya ni usanii. Hana dhamira ya kweli na anachokisema.
Lowassa hafai kuwa Rais -

chanzo raia mwema.
 
Mkuu ZeMarcopolo

Kwanza, nikukumbushe maneno ya Nyerere ''…..katika wakatiwetu haina maana rushwa haukiwepo, hapana! Ilikuwepo. Tofauti na sasa sisi tuliichukiana tuliikemea ….''

Nyerere anakiri rushwa ilikuwepo, ila ilikemewa na kuchukiwa. Na wala hakuna taifa linaloweza kusema ni pristine 100%.

Hata nchi zilizofanikiwa bado rushwa ipo hata kama ni 1%

Unapoongelea Sokoine unachanganya mambo. Kuna grand corruption, corruption, bribery na sabotage.

Kama unakumbu kumbu Sokoine wahusika walisemwa '' racketeer and sabotage'' wahujumu uchumi na magendo.

Racketeer ina maana ya genge la wahalfu(crime syndicate)lenye kufanya uhalifu ikiwemo (hongo) si rushwa katika mtindo wa ima kuzuia haki kutotendeka kwa namna tofauti .

Kwa wakati huo, ukosefu wa bidhaa ulisababisha kuwepo kwa genge linaloficha bidhaa na kuziuza kwa bei ya kuruka.

Wakati wa sokoine hakukuwepo genge la wahalifu wa sasa linalokomba mabilioni kwa kutumia au kupitia mikataba ''halali' ilitotengezwakwa njia haramu.

Ndio maana wahusika ni mawaziri n.k. wakishirikiana na wafanyabiashara.

The whole scam ipokatika top gov level, ikiwa imejengewa mfumo usio rasmi

Hivyo, wakati wa Sokoine si huu na wala hauna mfanano!

Wakati wa Soine kulikuwa na zero tolerance ya rushwa,kwasasa rushwa ni ‘impunity' tena ikilindwa na ofisi zajuu nchini.

Walioleta rushwa kujulikana kwa uwazi wake ni wapinzani.Waliosimama kuikemea ni wapinzani.

Hao CCM wametumika kama kamati za chama bungeni. Hawana sauti kwasababu kukemea rushwa si haki yao ni haki ya chama.Tuseme ukweli bila haya

Kila mwanaCCM katika ngazi za juu ni mla rushwa, hilo halinakificho. Na wala hakuna anayechukia rushwa.

Wangekuwepo wasingeweza kukubali serikali yao isafishe wezi Zaidi ya mara 3 tena ikipinga maazimio ya bunge.

Wamepinga hata katiba ili kulinda masilahi yanayotokana na ufisadi. Hao unaweza kutuambia wanachukia rushwa?

Serikali yao iliyopita ilinunua radar kwa rushwa, hii ikaja na makando kando mengi tu. Hakuna aliyesimama na kusema, enough is enough!

Wotewalikaa kimya sasa wanazungumza ili kuungwa mkono. Hawa ndio unasema wanachukiar ushwa!

Huko kamati kuu na NEC wajumbe wameshanunuliwa, leo unaamini mbegu za mhindi zinaweza kuota kama mchicha! Uchaguzi uliopita wa CCM ilikuwa kupanga safu ambako wajumbe wamenunuliwa. Unategemea miujiza gani?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu zeMarcopolo

Umeuzngumzia rushwa kuongelewa ndani ya vikao vya CCM. Hatudhani kama kuna ukweli wa hili.

Hakuna ushahidi waaina yoyote Zaidi ya kulaghai umma.
Wahusika wote bado ni viongozi wa CCM nawanapeta tu.
Kwani umesahau tuliambiwa kuvua gamba hadi leo imebaki hadithi tamu !

Pili, popote pale penye watu safi, akitokea mmoja mwenye uchafu, huyo hutengwa.
Ndivyo tunasikia wenzetu mbunge fulani kaondolewa katika caucus ya chama chake

Si kwa rushwa tu, hata ikibainika mtu kafumaniwa au kabaka,chama kina muondoa ili kisinasibishwe na uchafu huo.

Tunajua wabunge na mawaziri wote wa Richmond ndio wapiga debe wa mzee.
Tunajua waeba viroba stanbic ndio wapiga debe! Kikao gani cha chama kimezungumzia rushwa?

Kama CCM ingechukia rushwa, waliotajwa kwa wizi na ufisadi wangekuwa nje ya chama.
Nitajie mmoja tu aliyewajibishwa. Hivi kweli kumvua mtu uwaziri, au kumuondoa uenyekiti wa kamati ndiyo adhabu ya
mla!

Umemuongelea EL kwamba hafai hata kushika fomu. Well, kuna Memb anayejua pesa za radar zimetokaje, hatuambiii. Sasa huyu naye utasemaanachukia rushwa

Yupo mzee Wassir aliyesimama kutetea escrow, huyu naye anachukia rushwa?

ZeMarcopolo ishu ya ufisadi hisio na ushahidi itabaki kua majungu tu,kama ni tuuma za ufisadi hakuna ambae hajaguswa,Kuanzia CHAMA kiongozi mpaka vyama vya upinzani kuna ufisadi,ndio mana nasema tatizo la ufisadi si la CHAMA, ni watu(Wanachama),ukienda upinzani watu wanachota ruzuku(wanakula urefu wa kamba yao),huku CHAMA kiongozi ufisadi upo katika serikali,sio katika CHAMA, na baadhi ya watendaji hawana CHAMA,mfano yule CEO wa Vodacom,sio CCM, alioshirikiana ni watendaji wa serikali ambao ndani yake wapo wasiokua na vyama.
NB.CCM ikipata vijana 50 level Mwigullu Nchemba katika ubunge,30 level ya Deo Filukunjombe,20 level Ester Bullaya jumla wakawa 100 pale bungeni CCM haitafanya kazi kwa mazoea kuanzia katika CHAMA mpaka Serikalini,upinzani utokuwa na kazi tena
 
Kiongozi,

Ushahidi ili upatikane ni lazima vyombo vya dola vifanye kazi bila kuingiliwa na wanasiasa. Tumesema kuwa tatizo ni watu kusympathise na wala rushwa. Kwahiyo ushahidi sio kwamba hauwezi kupatikana ila hautafutwi kwa dhati.

Labda nitoe mfano wa kinara wa ufisadi serikalini, Lowassa. Huyu alijiuzuru baada ya kutajwa kwenye uchafu wa Richmond. Mantiki ya kiongozi kuachia ngazi baada ya kutajwa ni za aina tatu:
1. Anavipa fursa vyombo kufanya uchunguzi bila kukwazwa na cheo chake.
2. Anakiri kosa na kuona hastahili kuaminiwa.
3. Amethibitika kuwa msafi lakini amegundua mazingira ya ushirikiano na wenzake yameathiriwa na sakata kwahiyo anatoka ili government iendeshwe smoothly.

Kustaafu kwa Lowassa kunafit kwenye number 1 kwa vile uchunguzi ulikuwa unaendelea na alikataa kukiri kosa, hakuna chombo cha kisheria kilichomsafisha.

Sasa tujiulize, huyu mtu anataka kupewa nafasi kubwa zaidi ambayo itafanya asichunguzwe kabisa. Je, kwanini hakutumia miaka yote tangu ajiuzuru kuweka ushahidi wa usafi wake kwenye vyombo vya sheria athibitike kuwa msafi. Kugombea kwake kunaondoa mantiki ya kujiuzuru kwake. Inaonekana alijiuzuru ili tu kuvuta muda watu wasahau.

Rushwa ya Lowassa sio majungu. Imesemwa Bungeni. Tukisema ni majungu maana yake Bunge ni kijiwe cha majungu.
 
Last edited by a moderator:
ZeMarcopolo ishu ya ufisadi hisio na ushahidi itabaki kua majungu tu,kama ni tuuma za ufisadi hakuna ambae hajaguswa,Kuanzia CHAMA kiongozi mpaka vyama vya upinzani kuna ufisadi,ndio mana nasema tatizo la ufisadi si la CHAMA, ni watu(Wanachama),ukienda upinzani watu wanachota ruzuku(wanakula urefu wa kamba yao),huku CHAMA kiongozi ufisadi upo katika serikali,sio katika CHAMA, na baadhi ya watendaji hawana CHAMA,mfano yule CEO wa Vodacom,sio CCM, alioshirikiana ni watendaji wa serikali ambao ndani yake wapo wasiokua na vyama.
NB.CCM ikipata vijana 50 level Mwigullu Nchemba katika ubunge,30 level ya Deo Filukunjombe,20 level Ester Bullaya jumla wakawa 100 pale bungeni CCM haitafanya kazi kwa mazoea kuanzia katika CHAMA mpaka Serikalini,upinzani utokuwa na kazi tena
Tuhuma ambazo hazichukuliwi hatua yoyote ile na vyombo vya dola vinavyohusika hatuwezi kuziita ni majungu!
 
Kuhusu idadi inayoonekana kubwa ya wachukua fomu wa CCM. Mpaka sasa watu 26 wametangazwa kuchukua fomu. Inategemewa kuwa idadi hii itaongezeka.

Wapo wanaoona idadi ni kubwa na wingi huu unaashiria kudharaulika kwa Urais. Wapo wanaodhani kuwa uchukuaji fomu unatumika kujijengea tu umaarufu.

Hili la kujijengea umaarufu sitalizungumzia zaidi kwa vile kujua dhamira ya mtu ni jambo gumu.

Nchi yetu ina watu wanaokadiriwa kuwa million 45. Katika kundi la watu million 45, lazima kuwepo na mamia ya watu wenye uwezo wa kuwa Rais. Ni kosa kudhani kuwa uwezo wa kuwa Rais unatokana na umaarufu wa kisiasa.

Watu hawa waliojitokeza wanaonyesha ari ya kujiamini. Idadi yao kubwa inafaa kutafsriwa kuwa kiwango cha kujiamini nchini kimeongezeka.

Kuongezeka kwa kujiamini ni matokeo ya uongozi wa kidemokrasia ndani ya CCM. Inastahili kupongezwa badala ya kubeza.

Ni vizuri watu wakaelewa kuwa kazi ya Urais sio ngumu zaidi ya kazi wanazofanya kila siku. Urais ni taasisi na haitegemewi Rais ajue kila kitu.
Vigezo vya kumudu kazi ya Urais ni viwili tu 1. Awe na busara 2. Awe na nia njema.
Yeyote mwenye hivi viwili anaweza kuunda timu nzuri itakayoshirikiana naye kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali. He doesn't need to know all the answers.

Iwapo Rais atakuwa na vision au ujuzi mkubwa ni bonus, lakini bonus hiyo haina maana bila kuwepo busara na nia njema. Vision inaweza kuundwa na timu ya wataalam, lakini busara haiwezi kufidiwa.

Kwahiyo si sahihi Urais kuonekana kazi ya watu wachache kiasi cha kushtushwa na watu 30 kati ya mil 45.

UKAWA wana mengi ya kujifunza toka CCM, mojawapo ni hili.

Mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM unavyoendeshwa tayari unawaandaa wananchi kisaikolojia kuwa tayari kupata Rais toka CCM. Serikali inahitaji Rais toka CCM.
Wingi wa wagombea unaongeza free coverage kwa chama. In the end hii ni win win win situation kwa CCM, Serikali na Wananchi...
 
ZeMarcopolo

Marekani
inawatu milioni 300, wanaochukua fomu katika vyama vyote, hawazidi wagombe wa CCM.

Uingereza ina watu milioni 80. Wanaochukua fomu hawazidi idadi ya wagombea wa CCM.
Kwamba, Tanzania ina watu 45Milioni ina justify kuchukua fomu kwa mamia, haina mashiko.

Pili,wakatiwa Mwinyi waliochukua fomu hawakuzidi 10.
Wakati Kikwete anagombea hawakuzidi 10
kwa ccm,if memory serves me right

Miaka 10 iliyopita CCM ilikuwa na watu hawa, Dr Salim, SindeWarioba, CD, Msuya, JS Malecela.
Hawa walikuwa na sifa za uongozi kimaadili,kiuzoefu na kitaaluma.

Haina maana hakukuwepo na watu wenye nia, walikuwepo, suala ni kuwa, nani alijipima kupokea kijiti kutoka kwa Nyerere anayekaribia hao?

Katika vifaa hivyo vitano, hakuna aliyekuwa Rais. Hao ndio waliomchagua na kumsaidia Rais kwa kutumia busara zao.

Mwinyi alichaguliwa kwa mtazamo wa busara tukijua alikuwa makamu na suala zima la muungano

Kinachotokea sasa hivi, kwanza, ni udhaifu wa uongozi.

Wanaojitokeza ni wasaidizi wakuu wa Rais aliyepo na ndio wanatuletea kauli mbiuy a rushwa na ufisadi.
Maana yake wanauona udhaifu uliopo. Wengine wanasema elimu au kilimo kwanza. Wanachokifanya ni ku explore weakness ya kiongozi waliomsaidia.

Kila mmoja anaona angeweza kufanya vizuri zaidi. Ni udhaifu tu.

Kundi lingine linatafuta umaarufu. Tumeeleza huko nyuma,Kuga Mziray alihutubia viti.
BMLK alikuwepo kama mpinzani kwasababu uwepo wake ulishaonekana. Hawa wa CCM wanatafuta nafasi tu.

Hoja kuwa ni kupanuka kwa demokrasia ni kweli kwasababu demokrasia ni kitu cha ajabu kidogo.
Inaweza kukupa matokeo mazuri au mabaya.

DemokrasiA ilimtengeneza Lady Thatcher
miaka 11ikamuondoa kwa aibu siku moja.

Demokrasis ilimtengeneza Ronald Regan akajenga uchumi waMarekani, ikamleta G.Bush , recession ikaingia

Kupanuka kwa demokrasia kumetupatia Kibajaji wa Dodoma na kupitia kwake tumepata wazo la kuondoa picha za wanyama,' thamani ya pesa yetu ipande''

Bandiko linalofuata tutakuonyesha udhaifu wa uongozi wa CCM unaoleta wingu la watia nia.

Jinsi EL anavyoiyumbisha CCM bila sababu za msingina na jinsi CCM inavyomugopa

Tusemezane
 
Kabla haujaendelea sana naomba jibu la makadirio yako. Nimekadiria kwamba Tanzania kuna mamia ya watu wenye uwezo wa kuongoza nchi. Je, wewe unakadiria Tanzania nzima kuna watu wangapi wenye uwezo wa kuongoza nchi?
 
Last edited by a moderator:
Uchaguzi wa Oktoba 2015 utakuwa ni uchaguzi wa kumi na moja wa rais na wabunge tangia uhuru. Tangia uhuru, Chaguzi Sita zilifanyika wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa (TANU/CCM), na chaguzi nne zilifanyika chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi wa mwaka huu (2015) utakuwa ni uchaguzi wa tano chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Suala la kujadili ni je, kwa kipindi chote hiki, msukumo wa wananchi kujitokeza kupiga kura umekuwa ni kwa matarajio yepi?

Tangia uhuru (1961), chaguzi kuu zimekuwa kama ifuatavyo:

1. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 – Uchaguzi chini wa mfumo wa chama kimoja ambapo voters’ turn out ilikuwa 77%.
2. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1970 – chini ya mfumo wa chama kimoja, voters’ turnout was 72%
3. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975 - chama kimoja, turnout was 81%
4. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1980 – Chama kimoja, turnout was 75%
5. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985 – Chama kimoja, turnout was 75%
6. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1990 – Chama kimoja, turnout was 74%
7. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 – Vyama vingi, turnout was 77%
8. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 – Vyama vingi turnout was 84% (record breaking – highest in history)
9. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 – vyama vingi turnout was 72%
10. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 – Vyama vingi turnout was 42% (record breaking – Lowest in history)
11. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ??????????

Muhimu:

1. Uchaguzi mkuu wa 1965 ulikuwa ni uchaguzi wa kwanza wa Tanganyika as a “STATE”, ambapo kabla, Tanganyika was a “TERRITORY.”
2. Uchaguzi huu (1965) ulikuja baada ya mfumo wa vyama vingi kufutwa na kubakisha TANU peke yake kama chama cha Siasa nchini Tanganyika (na Tanzania hata baada ya Muungano.
3. Uchaguzi huu (1965) ulihusisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na sio Jamhuri ya Tanganyika. Waafrika wa Tanganyika waliipigania Tanganyika kufa na kupna na hatimaye kuikomboa chini ya TANU, lakini uchaguzi mkuu wa kwanza baaada ya mafanikio hayo ukahusisha “Tanzania”.

Harakati za TANU kuelekea uhuru, muungano na uchaguzi mkuu wa kwanza wa Tanganyika as a “STATE”:

Kabla ya uhuru, muungano na uchaguzi mkuu wa kwanza wa chama kimoja 1965, TANU haikuwa chama cha siasa (political party) bali a “political movement” (vuguvugu la kisiasa).

TANU ilijihusisha zaidi na harakati za kudai uhuru, harakati zilizodumu kwa miaka karibia saba (1954-1961). Kipindi kabla ya kuzaliwa kwa kwa TANU kulikuwa na harakati nyingine za waafrika ambazo zililenda zaidi kudai haki na fursa sawa hasa za kibiashara, kiuchumi na kijamii – kwa mfano mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi, fursa za elimu n.k. Ujio wa TANU ukapanua zaidi wigo wa harakati za waafrika na sasa lengo kuu likawa “Demand for Self- Determination” and “Demand for Self-Rule”. TANU ikaahidi to break the colonial past (kimfumo) and then recreate a future of Tanganyika. Mafanikio ya TANU yalitokana zaidi na ukweli kwamba TANU wasn’t a political party bali a political movement. Kwa maana nyingine, mabadiliko ya kweli yalihitaji a political movement, na sio political party(s). Swali:

Je, mabadiliko ya kweli kwa wananchi leo yanahitaji political parties au political movements? Zipo tofauti kubwa baina ya political parties & political movements. Kwa mujibu wa Goran Hyden (2006), tofauti baina ya ‘political movement’ & ‘political party’ ni kama ifuatavyo:

Political Movement
Political Party
Orientation
Cause
Issues
Level of Operations
Regime
Government
Main Arena of Operation
Society
Parliament
Method of Operation
Mobilization
Persuasion
Member Orientation
Diffuse
Specific
Claims of Resources
No formal limits
Constrained by Law

TANU as a political movement led to the emergence of Tanganyika as a new “state”. Kabla ya hapo, Tanganyika was not a STATE, but rather, a TERRITORY. Swali:

· How does a state arise?
A state emerges in response to needs that groups in particular society have. These needs may arise from problems with security (not peace), welfare or resolving conflicting demands on scarce resources.

Maswali:
· For the past 50 years, have we resolved the challenges of insecurity, welfare and conflicting demands on resources?
· Are these parts of issues that voters have in mind whenever they turn out to vote in every election?
· Is this state (Tanzania) the kind of state that wananchi were promised before uhuru?
· Is this state (Tanzania) the kind of state they wananchi envisaged before uhuru?
· Is it the kind of state that they want for the next 50 years?

Tanganyika/Tanzania as a state has gone through three main phases:

1. Party State – 1961 to 1964
2. Developmental State – 1965 to 1985
3. Contracting state – 1986 to present

Kwa kipindi cha mwaka 1961-1964, the state was TANGANYIKA na kwa kipindi cha mwaka 1961-2009, the state was TANZANIA. Kwa kipindi cha 2010 (kufuatia mabadiliko ya katiba ya Zanzibar), utambulisho wa Tanzania as a “state” haueleweki. Swali:

· Katika hali hii, wananchi wamekuwa wanajitokeza kupiga kura kutimiza malengo gani?

Awali tumeona voters’ turn out katika chaguzi kuu zote tangia uhuru.

TANGANYIKA AND PARTY STATE POLITICS 1961-1966

Kipindi cha 1961-1966 kilikuwa ni kipindi cha “PARTY STATE”. Kuelekea uhuru wa Tanganyika 1964, common enemy wa watu wote weusi alikuwa ni mmoja tu, “colonial power”. Hali hii ikarahisisha sana kazi ya TANU kujijenga as a single dominant political movement in Tanganyika Territory. Baada ya uhuru, kwa kipindi cha Party State (1961-1964), ultimate aim of politics was to “Create and Sustain a New Order”. Mwalimu Nyerere alikuwa very optimistic about the future, lakini hakuwa na uzoefu wa kuwa na madaraka makubwa kiasi kile. Kwahiyo he was very anxious to create his own position at the helm of the state (Tanganyika), na ndio maana kukawa na haja ya “Party State” politics in the said period.

Mwaka mmoja baadae (1965), emphasis ikaondoka kwenye “party state” na kuhamia kwenye “Developmental State”. Na katika kipindi hiki hiki, matukio makuu manne yakajitokeza:

(1) Kufutwa kwa mfumo wa vyama vingi
(2) Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar
(3) Maandalizi ya kuelekea ujamaa.
(4) Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya uhuru.

TANU ilihitaji kuonyesha wananchi kwamba chama kilikuwa kimejiandaa kwa matatu:

1. Kuonyesha wananchi kwamba walikuwa wamefanya uamuzi sahihi kuunga mkono TANU.
2. Increase popular participation kupitia chaguzi za mara kwa mara ili wananchi waone kwamba wanashirikishwa katika utawala na maamuzi.
3. Deliver promises za mabadiliko kwa wananchi kiuchumi kufuatia ukombozi wa Tanganyika.

DEVELOPMENTAL STATE 1967-1985.

Katika Uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1965, wananchi walienda kupigia kura mafaniko ya TANU. Kwa mujibu wa gazeti la “The Standard”, Katibu mkuu wa TANU wa wakati ule Marehemu Hashim Mbita alitoa Radio broadcast tarehe 21 October na kunukuliwa na Gazeti la The Standard kwamba:

“He appealed to voters to turn out on the Election Day and vote for president Nyerere….He said that the party was therefore appealing to all registered voters in Tanzania to vote for president Nyerere because of his contribution to the nation during which he has been president of TANU”.

Pia uchaguzi huu ulitawaliwa na dhana ya matumaini ya Taifa jipya miongoni mwa wananchi, hasa matarajio ya kula matunda ya uhuru. Ni katika muktadha huu, Azimio la Arusha became imminent. Matokeo yake ikawa kwamba, emphasis and objective shifted from sustenance of order (1961-1966) chini ya PARTY STATE POLITICS, to “Development” (1967-1985). TANU na mwalimu wakatambua kwamba they needed to show their ability to develop the new state and improve the living conditions of the majority.Wananchi walihitaji kuona matunda ya uhuru sasa na sio baadae. In the process Mwalimu had to grab control of the state so as to guide progress, hence the birth of Azimio la Arusha in 1967. Katika Chaguzi kuu zilizofuatia – yani (1970, 1975, 1980 & 1985), wananchi walienda kupigia kura “MATUMAINI” na “IMANI” kubwa waliyokuwa nayo juu ya Mwalimu Nyerere katika muktadha wa Azimio la Arusha.

Uchaguzi Mkuu wa 1985

Mwalimu Nyerere alin’gatuka mwaka 1985. Kufikia kipindi hicho (miaka 24 ya uhuru), wananchi wengi walikuwa bado wanasubiria matunda ya uhuru, hasa kiuchumi. Uchaguzi wa 1985 ulifanyika chini ya third phase of Tanganyika as a state – “THE CONTRACTING STATE”. Hii ilitokana na haja ya kukabiliana na failures and challenges za ‘party state’ & ‘developmental state’ tulizojadili awali.

CONTRACTING STATE 1985 – to present

Challenges and failures of party state and developmental state necessitated ‘contracting state’. Serikali ikaanza kujiondoa katika shughuli za moja kwa moja za kiuchumi na kuachia nguvu za soko zitawale. Mageuzi ya kiuchumi ndio yaliyoanza na baadae kufuatiwa na mageuzi ya kisiasa. Katika mageuzi ya kiuchumi, wananchi walishtukizwa na hawakuwa wamejiandaa kuondokana na misingi ya ujamaa chini ya azimio la arusha. Baadae azimio la Zanzibar likatangazwa kisirisiri Zanzibar, na wachache (hasa wanasiasa/viongozi) ndio wakalitumia kikamilifu kujiendeleza kiuchumi kwani ni wao ndio walikuwa kwenye ajira zenye mishahara lakini muhimu zaidi, kwenye nafasi za uongozi ambazo walizitumia kuanza kujitafutia hisa kwenye kampuni binafsi, kutengeneza mazingira ya kupokea mshahara zaidi ya mmoja na kuwekeza kwenye ardhi walizochukua ili kuwa na nyumba za kupangisha, PER Azimio la Zanzibar. Katika chaguzi kuu zilizofuatia, yani 1990-2010, wananchi wengi wamekuwa waki endorse yote haya kupitia sanduku la kura.

Mwaka 1995, taifa lilfanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi baada ya mfumo wa chama kimoja kuishi kwa miaka 30. Ingawa mageuzi ya kiuchumi yalianza mapema zaidi (1986), mageuzi ya kisiasa yaliratibiwa kwa ustadi mkubwa in a top-down fashion ili kuzuia dissapointemtns za wananchi kiuchumi zisihamishiwe kwenye sanduku la kura na wananchi na kukiondoa CCM madarakani.

Tulipo Leo:
Chama tawala kimepoteza kila aina ya uhalali wa kutawala:

1. Ahadi ya matunda ya uhuru zilizotolewa miaka ya 1950s, wananchi walio wengi hadi leo hii hawajaona kitu.

2. Azimio la Arusha ambalo liliwapa wananchi walio wengi matumaini ya Tanzania ya baadae yenye neema, azimio hili liliuliwa na CCM yenyewe mwaka 1991 Zanzibar na kulipisha azimio la Zanzibar ambalo halijali tena wananchi walio wengi.
3. Amani na utulivu (political stability). Hauwezi kuwa na political stability iwapo wananchi walio wengi (micro level – households and indigenous businesses do not experience economic stability). The Pre requisite of political stability is economic stability for the majority. Hata Mwalimu alionya miaka zaidi ya 20 iliyopita kwamba wananchi hawa hawawezi kuvumilia moja kwa moja, ipo siku wataamka na kusema basi tumechoka.

4. CCM ilikuwa inathibiti njia kuu muhimu za uchumi kwa maslahi ya walio wengi. Zilikuwepo taasisi na makampuni ya umma ambayo yalijiendesha kwa ufanisi, yalizaa ajira, lakini yote haya yamerudishwa kwa adui Yule Yule aliyepelekea TANU kuunganisha nguvu ya umma kuikomboa nchi (Wakoloni). Adui huyu amekuwa akigawia hisa wanasiasa na viongozi wa CCM na kuacha wananchi wenye mali na rasilimali wakitaabika bila huduma za msingi za kijamii, vipato duni n.k.

Katika mazingira kama haya, kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2015, wapiga kura watajitokeza kwenda kupigia kura CCM kwa kitu gani?
 
Uchaguzi wa Oktoba 2015 utakuwa ni uchaguzi wa kumi na moja wa rais na wabunge tangia uhuru. Tangia uhuru, Chaguzi Sita zilifanyika wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa (TANU/CCM), na chaguzi nne zilifanyika chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi wa mwaka huu (2015) utakuwa ni uchaguzi wa tano chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Suala la kujadili ni je, kwa kipindi chote hiki, msukumo wa wananchi kujitokeza kupiga kura umekuwa ni kwa matarajio yepi?

Tangia uhuru (1961), chaguzi kuu zimekuwa kama ifuatavyo:

1. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 – Uchaguzi chini wa mfumo wa chama kimoja ambapo voters’ turn out ilikuwa 77%.
2. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1970 – chini ya mfumo wa chama kimoja, voters’ turnout was 72%
3. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975 - chama kimoja, turnout was 81%
4. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1980 – Chama kimoja, turnout was 75%
5. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985 – Chama kimoja, turnout was 75%
6. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1990 – Chama kimoja, turnout was 74%
7. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 – Vyama vingi, turnout was 77%
8. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 – Vyama vingi turnout was 84% (record breaking – highest in history)
9. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 – vyama vingi turnout was 72%
10. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 – Vyama vingi turnout was 42% (record breaking – Lowest in history)
11. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ??????????
Mchambuzi sijui kama ni makusudi au bahati mbaya lakini kuna ukweli mkubwa umeuacha bila kusema.

What is the definition of voter turnout?

Ni asilimia ya waliojiandikisha ambao wamejitokeza kupiga kura. Kwahiyo, kina nani na wangapi waliojiandikisha ni kigezo muhimu sana kwenye kuamua turnout.

Miaka ya nyuma watu walikuwa wanajiandikisha maalum kwa ajili ya kupiga kura. Karatasi/shahada ya kupigia kura haikuwa na shughuli nyingine zaidi ya kupiga kura. Katika mazingira haya it is common sense kuwa wengi wa waliojiandikisha watapiga kura.

Recently, matumizi ya kadi ya kupigia kura yameongezeka. Kadi ya kupigia kura imekuwa ikitumika kama kitambulisho bank na sehemu mbalimbali. Kwa sababu hii, wapo wengi wamejiandikisha kwa lengo tu la kupata kitambulisho. Si jambo la kushangaza kuona turnout imeshuka.

Ingekuwa more interesting ungeenda mbali zaidi. Ungeangalia trend za asilimia ya wenye umri zaidi ya miaka 18 waliojiandikisha kupiga kura. Ungeshangazwa kuona kwenye uchaguzi wa 2010 asilimia hiyo ni kubwa kuliko chaguzi zilizopita. Sababu ni hiyo ya matumizi ya kadi ya mpiga kura kama kitambulisho.

Kwenye tafiti kupata results is one thing and interpretation of the results is another. Results zako ziko sahihi ila kwenye interpretation umeteleza...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom