2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

Wabunge wa upinzani hawajawai kua tofauti na CCM siku zote,ukikutana na waziri/mbunge ukimuuliza umefanya nini miaka mitano atakuambia nilikuta shule mbili,sasa hivi zipo ishirini,zahanati moja sasa hivi kila kata kuna zahanati,ukikutana na mbunge wa upinzani ukimuuliza amefanya nini, utasikia nilikuta shule moja,sasa hivi zipo kumi,rejea makala zilizokua zinatoka gazeti la mwananchi likihoji wabunge.
Rejea mshahara wa wabunge,umeshaona wabunge wa upinzani wakipaza sauti kugomea,au mafao(kiinuaa mgongo) juzi walichopandishiwa wabunge mbunge gani amelipinga hili,wanapiga kelele katika mambo ambao hata sisi Jamiiforums tunaandika na kusema na kusema.wabunge wote bila kujali CHAMA chochote,hawapo kwa ajili ya wananchi,afadhari ata sisi huku JF tunatetea maslai ya wananchi bila kupewa posho.
Nb.Wabunge wengi hawaitaki katiba Tume ya Warioba,sababu inaweka ukomo wa ubunge,kuwajibishwa na wananchi,kiwango cha elimu,hivi ni vikwazo kwao,walivyotoka bungeni ukawa sio sababu ya wananchi wala nini,kina Mbowe walijua hii itakua msumeno kwao,hawakua upande wa wananchi hata kidogo,walimuingiza chaka Lipumba ambae hafikilii kua Mbunge.
Kama kung'atuka katika vyama vyao vita watakubali kuachia ubunge kisa ukomo,ile plan ya kutoka si maslai ya wananchi,umeshawi kumsikia ikieleza kwa undani Rasimu ya pili ya katiba ya Warioba.
Wapiganaji wa kweli wapo JF maana wengi wetu tunanunua bando kwa fedha zetu,ili kuitetea Tanzania
 
Asante sana @Nguruvi3 kwa uchambuzi wako uliokwenda shule..

Kwa kweli siasa za Tanznia ni umiza kichwa.. Wanasiasa wetu tena wote wanawaza kujaza matumbo yao kuliko kumkomboa mwananchi wa kawaida. Mpaka hivi sasa kwa watu wote waliotangaza nia hakuna mtu hata mmoja anayetangaza nia ya kuwania urais anayesukumwa na matatizo ya mtanzania hayupo..

Kama hawa watu wangekuwa wanasukumwa na matatizo ya mtanzania basi kwa nafasi zao walizonazo huko serikalini,wangekuwa wanatuorodheshea mafanikio yao, na wapi wanataka kutupeleka lakini matokeo yake kila anayetangaza nia anataka tuanze upya as if hajawahi kufanya kazi katika serikali hiyo hiyo ambayo inatakiwa ifanye anayoyasema.

Mathalani MH: Wassira anasema yeye ataendeleza sekta ya kilimo.. Huyu Wassira ni waziri wa Kilimo sasa ukijiuliza ni nini kilichomfanya hasiendeleze sekta ya kilimo akiwa waziri wa kilimo hila ataweza tu pale hatakapo kuwa rais hupati jibu.
Huyu Mh. hana cha kujivunia katika hiyo wizara maana kama angekuwa nacho angetwambia ni yapi mafanikio yake na anataka kutupeleka wapi na vipi tutafika huko.. Huyu mtu kafanya kazi serikalini zaidi ya miaka 30 leo hii ndo anaona makosa aliyoyafanya/waliyoyafanya na kutaka kufanya kitu kipya.. Hivi kweli hizi ni akili?

Ukija kwa Mwigulu Nchemba naye story ni zile zile. Ukosefu wa ajira, umaskini, mikopo ya wanafunzi anavielewa sana kama anavyojinadi, lakini ana miaka 5 Bungeni, hawezi kusimama na kutwambia katika miaka 5 hiyo amefanya nini katika jimbo lake ili kuondokana na tatizo la ajira au amefanya nini katika katika swala zima la wananchi wa jimbo hilo kuondokana na umasikini, au kama Naibu wa fedha kwa kipindi kifupi alichokaa katika hiyo wizara amewasaidije hawa wanafuzi katika swala zima la mikopo.

Ila mtu huyu huyu ambaye hawezi kujibu haya maswali anataka tumwamini kwa hotuba yake nzuri na tumpe kura za urais.. Hivyo tu na kwa bahati mbaya kuna wanajf waliisifia ile hotuba kwa umahiri na uzuri wake.. Jamani hivi kuna watu wenye maneno mazuri kama wanasiasa? Hivi mtu apewa nchi kwa vile ameandika hotuba nzuri? kwangu mie nina sema hapana, kura yangu inakwenda kwa yule mtu ambaye ananitajia mafanikio yake kwa kipindi chote alichofanya kazi sehemu husika na mie nitaangalia kama ni kweli huyu mtu akafanya haya kweli au la? si hotuba nzuri..

Tukirudi kwa Ukawa/wapinzani tunakumbana na tatizo ile ile ya kupenda madaraka bila kuwekeza.. Wakati baadhi ya vyama vikiwa katika mikoa mbali mbali kuhamasisha uandikishwaji katika daftari la wapiga kura, kuna baadhi ya wanasiasa wako busy na kutangaza nia. Hivi unapokaa studio kwenye viyoyozi na kutangaza nia na ukitoka hapo unakwenda nyumbani kwako kulala unafikiri ni nani atakuchangua kama husipokwenda kuhamasisha wananchi kujiandikisha?

Nilitegemea kuona vyama vyote vinne wakiwa kazini wakihamasisha watu kujiandikisha katika daftari ya wapiga kura na katika mikoa mbali mbali lakini tunachokiona ni Cuf na Chadema ndo wako kazini hali NCCR na NLD (tena bora NLD tunaweza kusema hawana fedha) wako busy na kuwapangia wanaukawa nani awe rais na kwanini awe rais (rejea thread ya Mweyekiti wa Vijana NCCR).. Hii ni aibu, huu ni jinga, na huu ndo ule usaka tonge alosema Zitto.

Hivi chama cha NCCR kinashindwa kufanya mkutano walua kwa mwezi mara moja? NCCR kina ruzuku kina wabunge wanne hivi hawa wabunge wameshindwa kubuni mkakati wa kutangaza hiki chama? Leo hii ukiniuliza ni nina Katibu mkuu wa NCCR au mweka hazina au Mweyekiti wa baraza la wanawake au Katibu wa baraza la vijana (kama yapo) hawafahamiki zaidi ya Mbatia na wabunge wake 3. Hii ni aibu kwa hawa wabunge wanatakiwa kujenga chama chao nchi nzima Si Kigoma na Vunjo tu.

Tukirudi kwa wenyeviti wote ni wapenda madaraka.. Nimesikia Pro. Lipumba anatangaza nia, Si vibaya kwani ni haki yake ya msingi lakini kitu cha kujiuliza hivi CUF kuna Pro. Lipumba peke yake?

kama akichanguliwa na Ukawa itakuwa ni mara yake ya 5 kugombea urais hivi jamani kuna nia ya kweli ya kuelekea Ilkulu? kama watu wale wale wamekukataa mara ya 1, mara ya 2, mara 3, mara 4, hivi unategemea matokea tofauti kwa mara ya 5? Hivi hakuna mtu mwingine anayeweza zaidi ya watu wale wale, majina yale yale, sera zile zile miaka nenda miaka rudi? CUF kina wanachama zaidi ya laki 5. hivi katika hawa wanachama hakuna mtu yeyote zaidi ya Pro. Lipumba?

Tukija kwa Chadema wao kidogo wanakaunafuu maana Mbowe na Slaa wamegombea mara moja, na kwa sasa sijasikia nani anatangaza nia kati ya Mbowe au Slaa au mtu mwingine sio lazima awe Slaa maana tumeona unapomwachia mtu mwingine inaleta mawazo mapya mtazamo mpya na chama kinaimarika (ingawaje si lazima) Hivyo basi nategemea hata kwa Chadema kuleta sura mpya si watu wale wale.
 
Bulldog kuna tatizo katika kambi ya upinzani hasa katika maono na mikakati

Adharusi ukilinganisha wapinzani na wale wa tawala kwa vigezo unavyosema upo sahihi.
Hata hivyo, huyu aliyesema anachukizwa na akatamka ni bora kuliko yule aliyejificha nyuma ya chama.

Hawa akina Wasira si ndio walikataa Escow zisichunguzwe, hivi tunaweza kuwalinganisha na Kafulila katika uchungu?

Alinda kuna mengi umeongea, nitarejea. Kwa uchache, hivi Sumaye aliyekuwa waziri mkuu miaka 10 ana kipi kipya anachotaka kufanya zaidi ya majibu aliyotoa kama tulivyoonyesha akaongezea Ritz , kwamba PM hajui BoT inafanyaje kazi!
Hajui uhusiano wa waziri mkuu na BoT. Huyu alikuwa waziri mkuu wetu!

Kitu kimoja nilichokiona kwa Watangaza nia, wote wanasema kuna tatizo la RUSHWA na UMASIKINI.

Kwa maneno mengine wanatueleza kuwa mfumo wa JK ni wa rushwa na umasikini umeongezeka.

Kumbuka hawa wapo ndani ya sytem na sasa wanatoka kutueleza wazi.
Wanajua rushwa kwa ukamilifu na jinsi serikali inavyosiamamia kushamiri kwa rushwa

Wote wametaja Rushwa.
 
Alinda tunashangaa sana kusikia Mwigulu Nchemba akizungumzia mikopo kwa wanafunzi
Mikopo kwa wanafunzi halijawa tatizo hata kidogo. Zipo pesa , tatizo ni uthubutu wa kuzipata

Mwigulu akiwa naibu waziri wa fedha, na naibu katibu mkuu ni mtu mwenye ushawishi ndani na nje ya serikali

Leo kuna kampuni ya simu imekwepa kodi ya bilioni zaidi ya 300. Mambo yanafunikwa, wafanyabiashara wanahishwa kufunuika kombe. Walioshirikiana nao kule TRA wanadunda.

Bilioni 300 kwa mjadala tu, zinatosha kudhamini wanafunzi 300 katika kiwango cha milioni 10 kwa mwaka mmoja
Kumbuka hizi ni pesa tunazoweza kusema ni nje ya bajeti kwa maana kuwa leo hazipo na bajeti ipo pale pale,
Zimekwenda na maji.

Misamaha ya kodi inafikia Trilioni 1, misamaha isiyo na tija. Kiwango hicho ni sawa na bajeti nzima ya wizara ya elimu
Mwigulu alitakiwa atueleza hayo na jinsi atakavyokabiliana na mapapa wanaotesa

Tunaposikia eti mikopo ni tatizo si kweli, tatizo hakuna mtu mwenye uthubutu wa kukusanya pesa isipokuwa kwa wafanyakazi wa umma na masikini.

Kuna sababu gani za kujenga maabara kwa kuchangisha wananchi wakati CAG anaonyesha pesa zilizotafunwa huko halmashauri na serikalini zingeweza kujenga maabara hizo na vifaa vya kisasa!

Tunasema, hizi si zama za kuorodhesha matatizo.

Hatukubali aina hii ya uongozi wa kuvizia na kujificha nyuma ya chama.Kama hawezi kusema leo, atawezaje akiwa Rais?
 
Tunajiuliza, lini hawa watangaza nia wamesimama na kuhesabiwa wakikemea rushwa? Leo wanaposema rushwa ni tatizo, wapi wanapata ushujaa huo?

Tumeona dana dana za Escrow bungeni, waliokuwa mbele ni akina Wasira na Lukuvi.
Wameliondoa suala hilo bungeni na kwenda kulisafisha wanakojua
Leo Wasira anaposema atapambana na rushwa, ni ipi hiyo tusioijua?

Miaka 30 amekuwa kiongozi tena akawa waziri wa Kilimo. Ni kipi alikiacha kama alama wakati akishughulikia Kilimo?
Ni kipi alikiacha kama sera wakati akiwa waziri wa sera na mipango?

Sumaye, amekuwa waziri mkuu. Mauza uza ya Kagoda, Meremeta, Tangold na mengineyo yametokea machoni mwake akiwa waziri mkuu. Ni rushwa ipi anayoongelea leo ambayo haikuwepo zama hizo?

Muhongo anatuambia amesoma, nchi inahitaji msomi.

Ni lini Tanzania ilikuwa na upungufu wa wasomi?

Na je wasomi ndilo tatizo la nchi? Kumumonyoka kwa maadili hasa rushwa kunafanywa na nani, masikini asiyejua BOT ni nini au hawa wasomi wanaojua kucheza na nyaraka za BoT?

Watia nia , hakuna hata mmoja anayeongelea suala la muungano!

Je hilo hawalioni kama sehemu ya tatizo linalohitaji suluhu ya haraka?

Watasimama wapi na watuambie nini ikiwa walikaa na wala rushwa na kukubali nyaraka ya wala rushwa ituongoze?

Ni kwanini hawa watia nia walimpinga Warioba hata kuondoa vipengele vinavyohusu rushwa.
Leo wanapambana na rushwa kwa nyenzo gani?

Huko Majimboni, waulizeni, lini walikuja kutaka maoni yenu kabla ya kwenda bungeni?

Zile fedha za mfuko wa jimbo zinafanyiwa ukaguzi na nani?
 
Alinda;12895286]Kama hawa watu wangekuwa wanasukumwa na matatizo ya mtanzania basi kwa nafasi zao walizonazo huko serikalini,wangekuwa wanatuorodheshea mafanikio yao, na wapi wanataka kutupeleka lakini matokeo yake kila anayetangaza nia anataka tuanze upya as if hajawahi kufanya kazi katika serikali hiyo hiyo ambayo inatakiwa ifanye anayoyasema.
Ndio maana tunasema, trusingependa waorodheshe matatizo. Tunataka waweke platform zao nje ya ile ya chama kwanza ili tuwajue wanasimama katika nini. Kusubiri ilani ya chama ni kutafuta namna ya kujificha, utaratibu uliozoeleka

Kuhusu uwepo wao serikali, ni mfano mzuri wa Membe. Yupo kama waziri miaka 10.
Masuala mengi yameamuliwa nchini akiwa katika cabinet na Bunge.
Je, nani anaweza kusimama na kusema anajua msimamo wa Membe?

Naye kama Sumaye, atajitokeza na kulaani rushwa. Ni Membe huyo huyo hajatuambia nani amechukua chenji ya Radar.
Alipoulizwa akasema kazi yake ilikuwa kurudisha pesa. Kwamba, anajua tatizo lakini anaficha ili kutoudhi watu.

Hawa wamejaa ndio sababu tunasema, lazima tubadilike. Tunataka watu waweke 'CV' zao nasi tutazipitia
Leo nimstuka niliposikia Mgoni aliyefumaniwa Morogoro naye anataka kuchukua FORM
Mathalani
MH: Wassira anasema yeye ataendeleza sekta ya kilimo.. Huyu Wassira ni waziri wa Kilimo sasa ukijiuliza ni nini kilichomfanya hasiendeleze sekta ya kilimo akiwa waziri wa kilimo hila ataweza tu pale hatakapo kuwa rais hupati jibu.
Huyu Mh. hana cha kujivunia katika hiyo wizara maana kama angekuwa nacho angetwambia ni yapi mafanikio yake na anataka kutupeleka wapi na vipi tutafika huko.. Huyu mtu kafanya kazi serikalini zaidi ya miaka 30 leo hii ndo anaona makosa aliyoyafanya/waliyoyafanya na kutaka kufanya kitu kipya.. Hivi kweli hizi ni akili?
Atueleze, nini alichoshindwa kufanya miaka 30 ambacho sasa anataka kukikamilisha
Ukija kwa Mwigulu Nchemba naye story ni zile zile. Ukosefu wa ajira, umaskini, mikopo ya wanafunzi anavielewa sana kama anavyojinadi, lakini ana miaka 5 Bungeni, hawezi kusimama na kutwambia katika miaka 5 hiyo amefanya nini katika jimbo lake ili kuondokana na tatizo la ajira au amefanya nini katika katika swala zima la wananchi wa jimbo hilo kuondokana na umasikini, au kama Naibu wa fedha kwa kipindi kifupi alichokaa katika hiyo wizara amewasaidije hawa wanafuzi katika swala zima la mikopo.
Ndio maana tumehoji tatizo ni mikopo au upatikanaji wa fedha. Nchemba amefanya nini kuhusu misamaha ya kodi? Amefanya nini kuhusu wakwepa kodi kama ile kampuni ya Shiiv iliyokwapua vocha za uani kukwepa kodi?
Tukirudi kwa Ukawa/wapinzani tunakumbana na tatizo ile ile ya kupenda madaraka bila kuwekeza.. Wakati baadhi ya vyama vikiwa katika mikoa mbali mbali kuhamasisha uandikishwaji katika daftari la wapiga kura, kuna baadhi ya wanasiasa wako busy na kutangaza nia. Hivi unapokaa studio kwenye viyoyozi na kutangaza nia na ukitoka hapo unakwenda nyumbani kwako kulala unafikiri ni nani atakuchangua kama husipokwenda kuhamasisha wananchi kujiandikisha?

Nilitegemea kuona vyama vyote vinne wakiwa kazini wakihamasisha watu kujiandikisha katika daftari ya wapiga kura na katika mikoa mbali mbali lakini tunachokiona ni Cuf na Chadema ndo wako kazini hali NCCR na NLD (tena bora NLD tunaweza kusema hawana fedha) wako busy na kuwapangia wanaukawa nani awe rais na kwanini awe rais (rejea thread ya Mweyekiti wa Vijana NCCR).. Hii ni aibu, huu ni jinga, na huu ndo ule usaka tonge alosema Zitto.

Hivi chama cha NCCR kinashindwa kufanya mkutano walua kwa mwezi mara moja? NCCR kina ruzuku kina wabunge wanne hivi hawa wabunge wameshindwa kubuni mkakati wa kutangaza hiki chama? Leo hii ukiniuliza ni nina Katibu mkuu wa NCCR au mweka hazina au Mweyekiti wa baraza la wanawake au Katibu wa baraza la vijana (kama yapo) hawafahamiki zaidi ya Mbatia na wabunge wake 3. Hii ni aibu kwa hawa wabunge wanatakiwa kujenga chama chao nchi nzima Si Kigoma na Vunjo tu
Tunasikia vijana wa NCCR wanalalamika. Hatujawasikia wakihamasisha uandikishaji au mabadiliko.

Si lazima wawe na fedha, wanaweza kutumia platform za vyama vingine
 
Bulldog kuna tatizo katika kambi ya upinzani hasa katika maono na mikakati

Adharusi ukilinganisha wapinzani na wale wa tawala kwa vigezo unavyosema upo sahihi.
Hata hivyo, huyu aliyesema anachukizwa na akatamka ni bora kuliko yule aliyejificha nyuma ya chama.

Hawa akina Wasira si ndio walikataa Escow zisichunguzwe, hivi tunaweza kuwalinganisha na Kafulila katika uchungu?

Alinda kuna mengi umeongea, nitarejea. Kwa uchache, hivi Sumaye aliyekuwa waziri mkuu miaka 10 ana kipi kipya anachotaka kufanya zaidi ya majibu aliyotoa kama tulivyoonyesha akaongezea Ritz , kwamba PM hajui BoT inafanyaje kazi!
Hajui uhusiano wa waziri mkuu na BoT. Huyu alikuwa waziri mkuu wetu!

Kitu kimoja nilichokiona kwa Watangaza nia, wote wanasema kuna tatizo la RUSHWA na UMASIKINI.

Kwa maneno mengine wanatueleza kuwa mfumo wa JK ni wa rushwa na umasikini umeongezeka.

Kumbuka hawa wapo ndani ya sytem na sasa wanatoka kutueleza wazi.
Wanajua rushwa kwa ukamilifu na jinsi serikali inavyosiamamia kushamiri kwa rushwa

Wote wametaja Rushwa.

Mkuu Nguruvi3 unadhani ni nini kifanyike kuokoa hali hii mbaya?
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 sijui kama huu ni mtazamo wangu wa kihisia tu au hali halisi. Naona kuwa urais sasa unaonekana kuwa ni kitu cha mzaha tu, kila mtu anautaka. CCM ni kama inafanya vichekesho, ukiangalia ndani ya Chama walioonesha nia wana tofauti kubwa sana, hata ni vigumu kujua nani ni nani na kipi hasa kinamsukuma.

Lakini kwa mara ya kwanza naona kama rushwa imebarikiwa, ni kama CCM wanajiweka kwenye wakati mgumu na kuweka mazingira ya watu kuprevail kutokana na rushwa. ajabu sana kusikia Profesa Muhongo anatangaza nia licha ya kashfa ya bilioni iliyomchafua.
 
Mkuu Bongolander

Urais kuonekana jambo rahisiunasababu nyingi, tujadili kidogo
1 Kuna ombwe kubwa la watu wenyesifa kutoka katika jamii na si za kutengeneza.
Wakati wa Nyerere (mfumo wa chamakimoja) watu hawakufikiria nani anaweza kuvaa viatu hata kwa kumpwaya

Ndani ya chama, walikuwepowatu waadilifu kiasi kwamba wezi, mafisadi nawababaishaji walijiona kabla ya kunyooshewa kidole. Nikupe mfano tu rahisi hatakama hauna uhalisia wa wahusika. Yupo Salim Ahmed, J.Maleceal, B.Mkapa, J. Warioba,CD Msuya, Ali Mchumo, Bakari Mwapachu,A.Natepe

2 Urais unaonekana si sifa katikajamii bali uwezo wa ku-organize kelele na waiga debe.
Matumizi ya fedha kununuamedia, wajumbe n.k. Utaratibu ulianza mwaka 2005(mtandao)
Tulionya sana huu utakuwa utaratibu. Ndivyo inaonekana

3 Wengi wameona Urais ni mbinu tuwala si maarifa. Ni ujanja ujanja wa kusema hili leo ,kesho lile keshokutwahili. Ni art ya kucheza na akili za watu kama mazingaombwe na kila mtu anajuaanaweza kuchezesha vidole haraka akaitwa mwanamazingaombwe. Bad precedentiliyowekwa na walioko madarakani

4 ''Attention seekers'' Hawa niwatu wanaotaka kujenga majina ili kujihakikishia nafasi kwa serikalizinazokuja. Unakumbuka Kuga Mziray alikuwa anahutubia sokoni akiwa peke yake.
Bunge la katiba aliteuliwa kwasababu tu ni mwakilishi na ana ''constituent' akaula

Unakumbuka waliokuwa againstBWM walipewa ulaji ili kukata makali. Wanaochukuaform wengine ni ''political stunt' Nikupe mfano, EL akitia nia, kunamwenyekiti wa mkoa wa Geita aliletwa kwa ‘chopa'.

Yule bwana alikuwa vocal sanakatika vikao. Njia rahisi ni kumweka karibu.
Ikitokea EL akaingia Ikulu ni wazihawezi kumwacha

Kuhusu rushwa, hata watia wotewameliongelea kama tatizo. Maana yake ni kuwa wao wakiwa ndani ya mfumo wameonarushwa ilivyofanywa mfumo rasmi wa maisha yetu
Rushwa ni pamoja na kusafisha walarushwa. Tatizo ni kuwa wale walioachwa watazua balaa.

Tayari tunaona akinaKarag, Anne , na hata mzee Laigw wameshAunda ushirika wao.

CCM ina hiari,wakubaliane na mfumo au wawapige chini nao wajibu mapigo
 
Last edited by a moderator:
Tunajiuliza, lini hawa watangaza nia wamesimama na kuhesabiwa wakikemea rushwa? Leo wanaposema rushwa ni tatizo, wapi wanapata ushujaa huo?
....
Kwanza shukrani kwa uzi huu, ambao nafikiri unalenga kuwapa watanzania kujua uhalisia wa watanzania wenzao wanaotaka (sina hakika kama ni kwa hiari yao) kuwa wawakilishi wao katika nafasi mbalimbali za uongozi wa taifa hili. Wakisha kujua uhalisia wa watanzania wenzao hawa juu ya uhalisia wao (kiuwezo na kidhamira kwa uchache) wa kuwasaidia kupambana na kuzishida changamoto sugu (maradhi, umaskini, ujinga na sasa RUSHWA), watakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi sahihi.

Tulishaelezwa huko siku za nyuma kuwa Rushwa ya Tanzania haina aibu, tena msemaji (Mwl. Nyerere) akaongeza kuwa Tanzania inanuka kwa rushwa kipindi hicho. Kwa sasa inaonekana Watanzania wameanza kuizoe harufu inayonuka ya rushwa (maana harufu inayonuka kwa vyovyote vile utafanya jambo la haraka kuiondoa ama kuikimbia). Watangaza nia hawaonyeshi kukerwa kwa dhati (ili waiondoe) harufu inayonuka ya rushwa wala kuonyesha njia inayoeleweka ya kuwafanya watanzania wote waikimbie rushwa!

Watanganza nia wanaizungumza Rushwa kama jambo la kawaida tu, tena linaloweza kutumika katika kuwarubuni baadhi ya watanzania ili wawape tena ridhaa ya kutawala kwa misingi hiyo hiyo ya kirushwa rushwa. Watangaza nia hawataki kusema ukubwa halisi wa tatizo la Rushwa nchi kwa takwimu, kwa mifano halisi ya namna rushwa inavyotolewa, kwa mifano namna inavyopokelewa, na kwa mifano namna rushwa inavyoombwa katika ngazi zote za utendaji ama ndani ya serikali kuu na serikali za mitaa na mashirika ama wakala zao ama kwenye sekta binafsi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi ngazi ya taifa. Hawataki. Kwa nini? kwa sababu wameishaizoea harufu ya rushwa. Mtangaza nia anatakiwa pia aje na mikakati inayoeleweka namna ya kukomesha Rushwa na aonyeshe kweli mikakati hiyo anao uwezo na dhamira ya kuitekeleza.

Tena watangaza nia wangeweza hata kutumia ripoti za PCCB kutueleza ukubwa wa tatizo na kuonyesha madhaifu ya mifumo yetu ya kupambana na kushinda vita dhidi ya rushwa na kisha watuonyeshe wao watafanyaje ili kuondoa madhaifu hayo. PCCB wametoa 'list of shame' ingawa imejaa zaidi wala na watoa rushwa 'vidagaa', wakati wala na watoa rushwa 'mapapa' hawajawekwa wazi sana. Waweza kufuatilia orodha hiyo ya aibu ya PCCB kwenye links hapa chini

>>>PREVENTION AND COMBATING OF CORRUPTION BUREAU
>>>List of Shame

Hao watanagaza nia pia wakiwa watanzania (raia wa kawaida ama wenye madaraka ) watueleze walijishughulishaje na suala kupambana na kushinda vita dhidi Rushwa na kikwazo kwao kilikuwa nini kiasi cha kushindwa vita hiyo. Maana nadhani 'kupambana bila dhamira ya kushinda vita dhidi ya Rushwa, ni aina nyingine ya Rushwa'.

Hatutaki blah blah !!! Watangaza nia watueleze uhalisia wa ukubwa wa tatizo la rushwa , udhaifu wa mipango ya sasa ya kupambana na kushida vita dhidi ya Rushwa, waonyeshe pia uhalisia wao wa dhamira na uwezo wa kupambana na kushida vita dhidi ya Rushwa kwa kueleza jinsi walivyoshiriki kwenye vita hiyo, vikwazo walivyopambana navyo.
na watuonyeshe mbinu ama mikakati inayotekelezeka watakayo itumia kuondoa udhaifu wa kupambana na kushida vita dhidi ya Rushwa.

Wakifanikiwa kukidhi matakwa haya watakuwa na sifa mojawapo ya msingi ya kupimwa kama wanafaa kuwania nafasi ya Urais ama ubunge ama udiwani, ama uwakilishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuwapime watangaza nia katika utaratibu huu unaohitaji kujua uhalisia wa mtangaza nia kuwa na uwezo na dhamira thabiti kwa vigezo vyote. Nafikiri utaratibu huu unaweza kutupatia Kiongozi bora kwa manufaa ya waafrika wa Tanzania na nchi yetu kwa ujumla.

Ahsanteni kwa kusoma maoni yangu. Na shukrani sana Nguruvi3 kwa kuanzisha uzi huu na wale wote wanaochangia na kusoma mabandiko ya uzi huu.

==========================================================

JAMIIFORUMS.COM iendelee kuwepo
 
Last edited by a moderator:
Tanzania hatuna upinzani wa kuweza kuwasaidia watanzania kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine. Wapinzani wangekuwa na nia ya dhati wangejiunga na umoja wao kama vyama vilivyounda UKAWA na kuhakikisha wanaisimamia serikali kuandikisha watu wote wenye vigezo vya kupiga kura. Hii ingewasaidia sana kuitoa CCM madarakani. Wasimamie zoezi zima la kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.

Nguvu ya umma.
Watanzania ni waoga na wasahaulifu sana. Ukiangalia toka JKikwete aingie madarakani hadi leo madudu mengi yamefanyika, kuna ufisadi wa wazi sana na hadi waziri mkuu kujiuzulu. Lakini sisi tumesahau kiasi kwamba huyo waziri mkuu tunamuona amegeuka lulu.

Maswala nyeti yanayohusu maslahi ya taifa tunayasahau sana. Watu wanaendelea na shughuli zao kana kwamba hayawahusu kumbe wao ndo wahanga wakuu wakubwa.

Binafsi naona dhahiri kuwa ukombozi tunaoudhania utatokea 2015 hautatokea kwasababu wananchi hatujatambua nguvu tulionayo.
Nadhani wananchi bado hawana imani na wapinzani, bado wana imani na CCM ingawa ina mapungufu mengi na imeshindwa kuleta mabadiliko ndani ya miaka 50 kama alivyofafanua Nguruvi3 hapo juu. Ni wajibu wa vyama vya upinzani kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mabadiliko hasa katika kipindi hiki. Wengi wana hofu wakiangalia candidates wa urais katika upinzani wakilinganisha na watangaza nia wa CCM wanaona kama vile upinzani hawana watu wenye uwezo.
 
Last edited by a moderator:
jitegemee #31

Kwasasa tunahitaji siasa za uhalisi na si nadharia. Hayo uliyosema kuhusu rushwa ndiyo haswaa tunayapiga vita
Hao wanaotangaza kupambana na rushwa si kuwa walishiriki, bali hawakuweza kuzuia

Wanafahamu hasira za wananchi ni dhidi ya wala rushwa.
Nao wanataka wawe sehemu ya wananchi midomoni (lip service) mioyoni wanajua chanzo na washiriki hasa wa rushwa

Hiyo orodha ya PCCB ni ya vidagaa ili kujisafisha. Tunajua PCCB ilishapoteza imani yake siku nyingi sana.
Ni chombo cha serikali ambacho hutumika kuficha maovu

Kwa mfano, taarifa ya awali ya PCCB bungeni ilisema Richmond ni deal safi.

Waziri mkuu akisimama na kusema hiyo ndiyo taarifa ya uchunguzi hakuna shaka. Huyo alikuwa EL.
Eddie alifahamu timbwili lote kwasababu washiriki ni washirika wake

Leo tunafahamu ilikuwa ni taarifa ya uongo. Hapo hapo anatokea mtu na kusema atapambana na rushwa!
Huyu aliyetetea uzozo wa PCCB ndiye anatarajiwa kupigana vita ya rushwa(white elephant)

Sumaye anasema kama kuna wala rushwa hiyo ni kazi ya serikali. Wakati rushwa inatendeka yeye alikuwa waziri mkuu vyombo vyote vikiwa chini yake. Sumaye alikaa kimya bungeni wakati akina Mramba wanasema 'Radar itanunuliwa hata kama watu watakula nyasi''

Leo Sumaye anasema, akiwa Rais atashughulikia rushwa wiki mbili akimaanisha matokeo ya uchunguzi na mtu kufikishwa mbele ya sheria. Hakuweza alipokuwa PM anatuaminisha ataweza sasa

Sumaye anasema nyumba za serikali ziliuzwa kwasababu ya gharama kubwa ya kuzikarabati.

Aliyesimamia zoezi hilo bwana Pombe leo amechukua Form ya kugombea Urais.
Wote wawili hakuna anayetueleza, gharama za ukarababti na zile za kuweka mawaziri miezi 3, 4 stars hotel zipoje.

Na katika nyumba hizo hizo za serikali, tatizo si gharama bali rushwa iliyotumika viongozi kujimilikisha wenyewe kwa wenyewe.
Leo wawili hao wanatumabia watapambana na rushwa

Ndio msingi wa kusema, sasa hivi hatutaki siasa za bla bla, tunataka mtu aweke hoja, takwimu na matokeo(results)

Nasi tuna jukumu la kuwaambia ili wasijifiche kwa kelele za makofi ya wapambe wao.
 
KWANINI TUNASISITIZA SIASA ZA KILEO?

Tunaposema watia nia au wagombea watuwekee vielelezo,takwimu na hoja zao tuna hoja muhimu
Yes, tunafahamu kuna platform ya chama itakayokuwa na sera atakazobeba mgombea

Hata hivyo ieleweke kuwa mgombea atakayeteuliwa atakuwa na sehemu kubwa sana ya sera hizo.
Hawezi kuzunguka akiuza kitu asichokijua. Hivyo, mtazamo wa mgombea na hoja zake haziwezi kutengwa na maono yake katika sera atakazo uza

Kuna mfano mzuri umetokea mwaka huu nchini Uingereza. Kwanza, ni kura ya maoni kuhusu mustakabali wa Scotland kujitoa katika himaya ya maliki.

Katika kampeni, waziri mkuu Cameron alisema, masilahi ya washirika yataangaliwa endapo kura ya kukataa kujitenga itashinda. Hapa alimaanisha England, Wales na Ireland nazo zitapewa mamlaka zaidi juu yao wenyewe kama yale ambayo Scotland imepewa. Tulijadili sana hili katika uzi mmoja

Kauli ya pili ya Cameron wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu ilikuwa kura ya maoni ya Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya.

Baada ya kushinda uchaguzi kwa kuwa na wingi katika bunge, waziri mkuu Cameron ameshaanza mchakato wa kutoa mamlaka zaidi kwa England, Wales na Ireland.

Kwa maana kuwa anasimamia kile alichokinadi na kukiuza kwa wananchi
Ameshakwenda SCotland kuwaambia kuwa sasa England, Wales na Ireland zitakuwa na mamlaka kamili

Mfano huo ni kama wetu hapa ambapo Tanganyika inadai kupata mamlaka yake kama ilivyo Zanzibar.

Cameron anazunguka Ulaya kuwaeleza nia ya kura ya maoni na nini hatima ya Uingereza ikitokea A au B

Hizi ndizo siasa za kileo, unaahidi, unatkeleza. hakuna bla bla

Tujiulize CCM na JK waliahidi nini na wametekeleza nini.

Na ndivyo tunavyotaka vyama vya siasa visimame. Kama ni muungano, lazima kila kitu kiwekwe wazi
CCM wakisema watasimamia serikali 2 waeleze na ufumbuzi wa matatizo yanayotokana na hizo serikali

Wapinzani wakisema wanataka utatu wa shirikisho, wasimame waeleze ni kwav vipi na namna gani.

Hizo ndizo siasa za kileo, zile za 'nichagueni nitawaletea maendeleo' tuwaachie akina kibajaj

Tusemezane
 
Nadhani wananchi bado hawana imani na wapinzani, bado wana imani na CCM ingawa ina mapungufu mengi na imeshindwa kuleta mabadiliko ndani ya miaka 50 kama alivyofafanua Nguruvi3 hapo juu. Ni wajibu wa vyama vya upinzani kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mabadiliko hasa katika kipindi hiki. Wengi wana hofu wakiangalia candidates wa urais katika upinzani wakilinganisha na watangaza nia wa CCM wanaona kama vile upinzani hawana watu wenye uwezo.
Katavi, kuna hilo tatizo ulilosema. Ukisoma mabandiko tumewaeleza wazi, ni lazima wawe viongozi wa maono na kutenda na si kusubiri kuongozwa

Hili nitalichangia pamoja na hoja ya Bulldog kuhusu ni kifanyike, ingawa sikumwelewa ilikuwa kwa upande gani
Nitaongelea wapinzani

1. Wana bahati, agenda zimeshatangulia kwa wananchi.
Umasikini, hali ngumu ya miasha
kuzorota kwa huduma za jamii kama afya na elimu
Rushwa iliyojengewa mfumo katika nchi na wizi unaoligharimu taifa
Wananchi wanayajua hayo

2. Kuhsindwa kwa CCM, kwamba miaka 50 tupo hapa tulipo. Wananchi wanalijua hilo

3. Nchi kupoteza ushawishi katika jumuiya ya kimataifa, wanalijua hilo

4 Matatizo yasiyo na majibu kila siku, wananchi wanayajua

Orodha ni ndefu sana, ninachosisitiza ni kuwa agenda zimeshatangulia

2. Wapinzani wanapokelewa na wananchi kila wanapokwenda.
Si kuwa wananchi wanataka kuwaona, bali wana kiu ya kusikia kile wasichokipata kwa muda mrefu. Wana kiu ya mabadiliko

3. Tayari wana mfano.
Wananchi wanaona kazi inayofanywa na wabunge-upinzani. Pamoja na uchache wao lakini wanaweza kutetea hoja zao kwa mantiki

Hivyo, kazi ya Wapinzani si kuweka mezani agenda.

Tayari wananchi wana agenda. Wapinzani wanatakiwa kutumia agenda hizo kuwaondoa wananchi hofu kuhusu ukweli.
Kuwaondoa hofu kuhusu hujuma, udhaifu na uhalifu uliopo

Wapinzani watumie mifano halisi kuonyesha jinsi wanavyoumizwa kwa uzembe wa kundi dogo.

Jinsi wanavyolipa gharama kubwa za maisha yao kwasababu ya kulinda watu wachache.

Kwa mfano, ile kampuni iliyokwepa kodi za Bilioni 300 ni ya watu wachache.
Wakati serikali ikiacha watu hao waendelee kutamba, wagonjwa anakufa muhimbili kwa hosipitali kukosa Bilioni 10.

Kwamba kodi iliyokwepa ni kubwa kuliko bajeti ya Muhimbili. Waonyesheni kwa namba

Waambieni madarasa na maabara za shule wanazochangia si haki yao. Ni haki yao kuwa nazo, si haki kuchangia

Wekeni namba za CGA, kupotea kwa mabilioni ambayo yangeweza kumaliza mradi wa maabara bila mwanacnhi kutoa senti tano

Waelezani wanachi takwimu za uchumi, matatizo yanayowakabili walipo na mnaahidi nini na kwa njia zipi kwa kutumia rasilimali gani kuayamaliza.

Hoja hapa ni kuwa ipo fursa iliyotengenezwa na CCM, wapinzani wanatakiwa kuweka mbolea tu. Hoja tayari zipo

Wapinzani wasambae nchi nzima. Si lazima wote wakae vikao vya kugawana majimbo.

Kuna tech committee za kufanya kazi. Wapinzani waonyeshe UKAWA ipo kote si kwa viongozi tu

Wapinzani wafike maeneo magumu. Hivi kwanini waamini hawawezi kupata kiti mkoa wa Tanga!

Mbona waliweza kupata Mbeya, Shinyanga na kwingineko.

Ni lazima wawafikie wananchi wakiwa na ujumbe wa kuamsha matumaini, kuonyesha njia na kueleza namna gani wananchi watafika huko
 
Huko Majimboni, waulizeni, lini walikuja kutaka maoni yenu kabla ya kwenda bungeni?
Zile fedha za mfuko wa jimbo zinafanyiwa ukaguzi na nani?
Hapa naona unawasurubu mpaka Tundu Lissu,Lema wabunge wote kwa ujumla,kwa ufupi hawastahili kurudi mjengoni tena
 
Kwahiyo unataka na upinzani waendelee kurodhesha matatizo duu,wakati umeshasema wananchi hawataki orodha ya matatizo,naomba Nguruvi3 Sababu unakiu ya mabadiriko ungewaambia upinzani wanatakiwa kufanya nini,ili kuondoa kwwenda kuorodhesha matukio,vinginevyo icho unachofikilia wapinzani hawataweza kufanya maana wenyewe ni sehemu ya wabunge,wamekua wakiungana na CCM katika kufaidi keki ya Taifa,wanajiongezea tu mafao
Wapinzani wetu ni wasanii tu,mfano Dr Slaa wakati aliwahaidi watanzania kua akienda ikulu yupo tayali kula mihogo,wakati ndani ya CHAMA chake kawawekea masharti,uchaguzi ukiisha,sababu yeye atokua mbunge basi alipwe kama mbunge, hivi na yeye atapokea kiinua mgongo chake mwezi 7
 
Adharusi, soma kwa uyakinifu usiwe na prejudice. Nimeeleza hapo juu, waende kueleza wananchi kwanini tupo hapa, wanafikiria nini kutuondoa hapa, kwa njia gani na rasilimali gani

Nguruvi :

Waelezani wananchi takwimu za uchumi, matatizo yanayowakabili, walipo na mnadhidi nini na kwa njia zipi kwa kutumia rasilimali gani kuayamaliza.

Sikusema waorodheshe matatizo, hebu soma hiyo quote kwa undani uelewe.
Kwa mwendo unaokwenda nao wa kupinga bila kujadili, hakika hutajifunza, hutaelewa na hutaeleweka.
 
Hapa naona unawasurubu mpaka Tundu Lissu,Lema wabunge wote kwa ujumla,kwa ufupi hawastahili kurudi mjengoni tena
Nadhani unapaswa kuchangia hoja, unachokifanya ni vioja. Je umesoma mabandiko yote ? umeelewa?
Kwanini usijibu hoja kwa hoja? Kwani kuna tatizo gani endapo huna hoja ukakaa kimya?
 
Naomba nitoke kidogo tu nje ya mada...kwangu Watanzania nimewachoka. Nimejaribu kukuna kichwa nimeshindwa kung'amua tatizo letu hasa ni nini...je tatizo letu ni Utanzania au ubinadamu? Je sisi ni viumbe tofauti na binadamu wengine? Je tatizo letu linatokana na werevu wetu au ujinga wetu? Ingawa kila mtu anajua tunalo tatizo kubwa la kiutaratibu, kisheria, kikanuni na kimaadili katika namna tunavyoendesha mambo yetu kisiasa, kiutamaduni, kijamii na kiuchuni lakini kama mbuni vichwa tumevichimbia mchangani. Ama hatujui au kwa makusudi, pamoja na kujua, hatujali tukijiaminisha kwamba, hata bila tahadhari, kila kitu ni salama huko nje, hakuna hatari!

Mathalani kila moja wetu anajua kuwa uchaguzi tunaodai kuufanya kila baada ya miaka mitano ni kiini macho tu kwani tunaingia kwenye uchaguzi tukijua wazi kabisa kura zetu pekee hazitatupa kiongozi tunayemtaka. Tunajua kabisa kwamba chama tawala hakiwezi kushindwa kikitaka na kwamba kiwango cha ushindi kinaamuliwa mezani na si kwenye kituo cha kura. Tunajua kabisa sababu za chama tawala kutokuwa tayari kushindwa lakini bado tunakubali kushiriki na hivyo kuwapa uhalali wa kubaki madarakani. Ajabu ni kwamba pamoja na kujua namna ya kuwaondoa madarakani na kwamba uwezo huo tunao, tunawaruhusu kufanya wanavyotaka na baadaye tunaanza kulalamika.

Tunavyo vyama vya siasa na ingawa tunajua kabisa kwamba hivi vyama haviwezi kushinda uchaguzi, tunaendelea kuvishabikia tukiviruhusu vitusimamie badala ya sisi kuvisimamia. Kama tungeamua kuvisimamia hatungekaa kimya vinaponyanyaswa na badala yake tungevitetea kwa sababu ni vyetu, hatungeruhusu vipigwe mabomu kwani vikipigwa mabomu tunaovuja damu ni sisi. Tumewatosa wachache wenye moyo, tumekuwa watazamaji tukiangalia wanavyohangaika juani ili tuje tule kivulini...Duniani kuna watumwa wa aina mbili;wanaotekwa na kufanywa watumwa na wanaoutamani utumwa kwa sababu wametosheka kwa kutupiwa makombo, hawataki kuhangaika.

Nilisema zamani na leo kurudia, CCM haitatolewa madarakani kwa njia ya kura. CCM tumewaruhusu wamewekeza na wamewekeza kweli kweli na kwa baraka zetu. Ni kama vile tumefanya nao mkataba, tumewapa nchi kwa mkataba kwamba wale mpaka washibe bila kujiuliza je shibe ina mwisho? Wakishiba leo je kesho hawatakuwa na njaa? Halafu wanakuja wanamageuzi wanadai mabadiliko, wanataka kuukatiza mkataba! Je kwa miaka hamsini walikuwa wapi? CCM kwa ujanja kumbe waliweka kipengele cha uchaguzi lakini kwa sharti moja kuu, wao ndio wawe watunga kanuni, wasimamizi, waamuzi wa zoezi zima...tukaafiki fisi kukabidhiwa ulinzi wa bucha! Halafu tunalalamika!

Haya tuendelee na mada kama ilivyoletwa; 2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi
 
Back
Top Bottom