2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

Mkuu Mag3

Ninaziangalia hoja zako kwa sura mbili

1 kukubaliana nawe:
Katika bandiko moja nyuma, tumeeleza Watanzania ni
watu wa ajabu sana. Ni wepesiwa kusahau, wazuri wa kulalamika n.k.Miaka 50 na maumivu yote bado hawaoni tatizo. Wanaibiwa na pesa zinatumika kuwanunua bado hawaoni tatizo na hao wanaowaibia leo wanachukua fomu wakisindikizwa na waliobiwa

Ndipo tunakubaliana nawe kuwa Watanzania ni watu wa ajabu kwa hoja yako kuwa wanajua watashindwa lakini bado wapo tu katika uchaguzi. Ni kweli kuna ajabu Fulani

2 Tumeeleza pia , lazima wapinzani wawe na plan A1 (kutwaa dola) na A2( kumilikibunge) na si A na B.

Maana ya
hiini kuwa jitihada za plan A1 iwe imefanikiwa au la, zina impact katika plan A2.

Hii plan A2 ina sehemu mbili

Kwanza, kumiliki bunge kabisa, na pili kuzuia 2/3 ya CCM

Jambo hilo litasaidia kuweka ‘level filed' kwa siku zaijazo.Unafahamu CCM inamiliki vyombo vyote vya dola na Bunge.

Tunafahamu CCM haina nguvu kama chama chenye dola. Mbinu inayotumika ni wingi wa CCM ndani ya bunge kupitisha shaeria haramu kwa njia halali ya 2/3. Tuangalie mifano

1 Sheria ya mchakato wa katiba ilipitishwa na wabunge 100 ikawa halali si kwasababu ni halali bali ilijengewa uhalali na CCM majority iliyosaidiwa na vibaraka kama Mrema

2 Sheria ya mtandao na zingine nyingi zimetumia mfumo huohuo kushinikizwa.
Leo serikali inapeleka mswada wa kusikiliza habari za TBCikijua ina 2/3 majority

3. Bunge la katiba nalo lilitaka kutumia 2/3 kutupa katiba iliyoandikwa na mafisadi.

Bahati nzuri sana, wapinzani walitusikiliza wananchi tulipowataka watoke wasijenge uhalali wa kitu wanachojua kinapikwa.

Hapa kuna contradiction na hoja yako kuwa uchaguzi utahalalisha serikali ya CCM kuendelea na mabavu na ubabe.
Kuna sababu

a) Kutoka nje BMK kwa wapinzani kulisaidia sana 2/3 isipatikane.Mchakato umeahirishwa kwasababu hiyo, BVR inatumika tu kama kisingizio. CCMwanajua hawakuwa na 2/3 mbele ya uso wa dunia. Hili halikuwezekana bila sacrifice ya wapinzani

b) Kususia uchaguzi bado kutakuwa na uhalali ule ule wa vibaraka

c) Watanzania hawawezi kusimama kuhesabiwa kupinga uhuni.Ndivyo walivyo, na hapa tunaungana nawe, hatujui ni uzezeta au ni woga au ubinadamu uliopotiliza

Mkuu unakumbuka shinikizo la tume huru linavyozuiliwa na CCM na Bunge kwa kutumia sheria kama jambo halali?

Tukiangalia mfano wa Kenya tunaweza kujifunza. Kuna wakati(Keneth Marende) Bunge linamilikiwa na upande mmoja , upande mwingine niserikali.

Hilo liliwezesha kujenga mazingira ya kuzuia sheria za kihuni, kufuta sheria za kihuni na kuuweka uwanja sawa(level field) . Unaona hali ya kisiasailivyobadilika

Tumalizie kwa kusema, ngamia aliyepo ni mkubwa sana. Ilikukabiliana naye, kuwe na plan A1 na Plan A2.

Plan A2 inalenga kuvunja mgongo ili ngamia apige magoti kabla ya kummaliza.

Kama tulivyosema sote, Watanzania ni watu wa ajabu sana .Kuwabadilisha kwa ‘radical changes' is something next to impossible. Je,hatuwezi kufikiria ''passive changes' ambayo wanaweza kushiriki katika hali waliyo nayo?
 
Nadhani wananchi bado hawana imani na wapinzani, bado wana imani na CCM ingawa ina mapungufu mengi na imeshindwa kuleta mabadiliko ndani ya miaka 50 kama alivyofafanua Nguruvi3 hapo juu. Ni wajibu wa vyama vya upinzani kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mabadiliko hasa katika kipindi hiki. Wengi wana hofu wakiangalia candidates wa urais katika upinzani wakilinganisha na watangaza nia wa CCM wanaona kama vile upinzani hawana watu wenye uwezo.

Wananchi gani unaowaongelea? Wananchi wengi sana wamekata tamaa. Hasa walio vijijini, hawana matumaini ya maisha. Usichukulie sample ya watu wachache ofisini ukadhani watanzania wote. Hali ni mbaya sana huku field.
 
Last edited by a moderator:
Hatusikik chochote kuhusu "Tume huru" sasa sijui wanasubiri baada ya matokeo ndo waanze zile hadithi zao za tumeibiwa kura?!

Ndio maana sasa siwaelewi wapinzani wanapata wapi hopes hizi

Obviously; Bila haya mambo matatu wapinzani wameshashindwa;

  1. Tume huru ya Uchaguzi
  2. Ushindi wa Rais kuweza kuhojiwa mahakamani
  3. Ushindi wa Rais kwa kura 50+1%
 
Mag3 asante sana

Hadi pale tutakapong'amua Root cause ya matatizo yetu watanzania ndipo tutaweza kujikomboa

Hapa tulipo tunajua kabisa kuwa kuna tatizo...But how comes hakuna hata mmoja kati yetu anayeonesha nia ya kupambana na hayo matatizo...sisi wenyewe tunaishia kuandika tu kwenye key board.

Watanzania tuko wazuri sana wa kulalamika na kuongea maneno mengi.,..na hicho ndicho tunachokifanya siku zote.Likija suala la kutenda wote tuko walewale hakuna kitu,...sio upinzani sio chama tawala.

Pia tukubali kuwa viongozi tunaowapata ni zao la jamii tuliyomo...tukipata viongozi wala rushwa maana yake ni jamii inapenda rushwa...Tukipata viongozi porojo wasioweza kutenda maana yake ni zao la jamii yetu.

Tutaweza kutoka hapa pale ambapo tukiweza kubadili culture yetu
 
Last edited by a moderator:
Alinda,

..Waswahili wana msemo wao, " mwenye shibe hamjui mwenye njaa."

..wapinzani wasitegemee hata siku moja kwamba CCM na serikali yake wataleta tume huru ya uchaguzi.

..kitu cha msingi ni kuilazimisha tume hii hii ambayo siyo huru kutangaza matokeo halali ambayo yanaiondoa CCM madarakani.

..Now, u may ask me how do u do that?? Jibu ni kwamba, lazima wapinzani wahakikishe kwamba wanapata ushindi wa kishindo. Yaani ushindi wao uwe ni mkubwa kiasi kwamba haina maana tena kwa tume au CCM kuchezea matokeo.

..Je, inawezekana? Jibu ni kwamba, inawezekana ikiwa wapinzani watawaelimisha vya kutosha wananchi. Kuna majimbo hapa Tz ambayo ktk uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa wananchi wamechagua wapinzani kwa zaidi ya asilimia 80.

..Nigeria wananchi walimpigia kura mgombea wa upinzani kiasi kwamba ikashindikana kuiba zile kura. Yaani ilifika mahali viongozi wa chama tawala wakawa wanalalamika, lakini tume ilishindwa "kufanya-fanya" ikabidi wamtangaze mshindi halali.

cc Nguruvi3, Freeland, Mag3, Bulldog
 
Last edited by a moderator:
Mag3 asante sana

Hadi pale tutakapong'amua Root cause ya matatizo yetu watanzania ndipo tutaweza kujikomboa

Hapa tulipo tunajua kabisa kuwa kuna tatizo...But how comes hakuna hata mmoja kati yetu anayeonesha nia ya kupambana na hayo matatizo...sisi wenyewe tunaishia kuandika tu kwenye key board.

Watanzania tuko wazuri sana wa kulalamika na kuongea maneno mengi.,..na hicho ndicho tunachokifanya siku zote.Likija suala la kutenda wote tuko walewale hakuna kitu,...sio upinzani sio chama tawala.

Pia tukubali kuwa viongozi tunaowapata ni zao la jamii tuliyomo...tukipata viongozi wala rushwa maana yake ni jamii inapenda rushwa...Tukipata viongozi porojo wasioweza kutenda maana yake ni zao la jamii yetu.

Tutaweza kutoka hapa pale ambapo tukiweza kubadili culture yetu

..I am 50/50 na huu mtizamo wako.

..let me tell u the 50% that disagrees with u.

..I dont think wa-Tz wanapenda rushwa na ufisadi.

..pia sidhani kama viongozi tunaowapata ni reflection ya wa-Tz.

..nasema hivi, kwasababu siamini kama kuna chama cha upinzani Tz kinaweza kumsimamisha fisadi kuliko mafisadi wote halafu kikawashinda CCM.

..wapinzani wamekuwa wanashindwa kwasababu hawajafanya juhudi za kutosha kujitangaza kwa wananchi huko vijijini ambako ndiko kura za ushindi zilipo.

..CCM wako kitaasisi zaidi ya upinzani. Wako makini ktk hatua zote za kuelekea uchaguzi, kuanzia kuandikisha wapiga kura, kutunza vitambulisho vya kupiga kura, kufanya kampeni, na mwisho kwenda kwa wingi vituoni.

..Kwenye kila uchaguzi, wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wamewekewa malengo maalumu ya idadi ya wanachama ambao wanapaswa kuhakikisha wamekwenda kupiga kura.

..Wapinzani wanatakiwa nao kuwa na mpango kazi mzuri zaidi ya ule wa CCM kwa hatua zote za kuelekea ktk uchaguzi mkuu.

cc Bulldog, Alinda, Nguruvi3, Mag3
 
Last edited by a moderator:
jitegemee #31
......

Nasi tuna jukumu la kuwaambia ili wasijifiche kwa kelele za makofi ya wapambe wao.

Mkuu, umeweka msisitizo mzuri sana. shukrani kwa hilo
---------------------------------------------------------------
Sahihisho: siyo 'jitegemee' bali TUJITEGEMEE
----------------------------------------------------------------

.....
.

Pia tukubali kuwa viongozi tunaowapata ni zao la jamii tuliyomo..(1).tukipata viongozi wala rushwa maana yake ni jamii inapenda rushwa...Tukipata viongozi porojo wasioweza kutenda maana yake ni zao la jamii yetu.....
(1) Ni kweli kwa kiasi fulani kwamba jamii(jamii nikiwa na maana ya watanzania) yetu ndiyo inayozaa wala rushwa lakini nadhani si kweli kuwa jamii hiyo imejaa wapenda rushwa tu kisa imezaa wala rushwa..!!. Jamii yetu imegawanyika katika makundi yafuatayo ukiingalia kupitia kona ya masuala ya rushwa:

baadhi ya watanzania wameanza kuzoea harafu inayonuka ya rushwa hasa wengi wao wako kwenye nyazifa za kiutawala; mfano unakuta baadhi wameshiriki kwenye mikataba tata ya ununuzi wa rada, wameshiriki EPA, wameshiriki, Dowans, wameshiriki Escrow, na sasa wameshiriki kwenye upotevu wa zaidi ya bilioni mia tatu kwenye uchapishaji wa vocha 'jero jero'.

pia kuna wengine ambao wana matatizo ya kutambua harufu inayonuka ya rushwa (pua hazifanyi kazi) na hii imetokana na kukosa elimu ya kutambua haki zao. Mfano dereva wa pikipiki (bodaboda) anakubali kutoa ela (2000 mpaka 10000/=)na kumpa askari wa barabari ambaye ,askari huyo, baada ya kuona dereva huyu wa bodaboda kakamilisha kila kitu kinachohitajika awapo barabarani; anamtaka aonyeshe cheti cha chuo aliposomea udereva wakati tayari kashaonyeshwa leseni ya udereva!!.

Kundi la tatu ni wale ambao wanachukia kweli kweli harufu inayonuka ya rushwa na ni wachache sana waliopo katika nyazifa za kiutawala na kiasi ni baadhi yetu sisi raia wa kawaida. Kundi hili linaanza kupata kuungwa mkono na wale ambao hapo awali walikosa elimu ya haki zao; baada ya kutambua haki zao sasa wanakerwa na harufu ya rushwa. Lakini kundi hili pia linakumbana na hujuma, vitisho wakati mwingine hata mauaji kutoka kwa kundi lile la kwanza. Kuna tetesi ya mifano mingi ya wanajamii (wahandishi, wahandisi,'wabunge','mawaziri', 'wanausalama','wanasheria' raia wa kawaida na kadhalika ) kudhuriwa afya zao,kupotezwa, kuuliwa na mengine kama hayo.

NINI KIFANYIKE? Kwa kuanza,tuliunge mkono kundi la tatu, kwa kuhakikisha tunatoa elimu ya kutosha juu ya haki za kila raia ambao hawajui haki zao; kiasi cha kuona kutoa malipo kwa haki yako ni makosa. Pia tutoe msaada wa haraka pale tunapoona raia anaelekea kuhujumiwa kisa anapinga vitendo vya rushwa ili tumuepushe na hujuma hiyo. Hili linaweza kufanyika kwa kueleza kwa uwazi mbele ya umma hujuma inayopangwa na wahusika wanaopanga hujuma hiyo. Na kisha kuwachukulia hatua za kisheria hao wahujumu.

Hicho hapo juu na mengine ya namna hiyo yatawezeka endapo tuboresha mifumo na mbinu za kupambana tukiwa na dhamira ya kushinda vita dhidi ya rushwa. Maana Ukweli ni kuwa mifumo na mbinu tunazotumia kwa sasa kwa jinsi zilivyo hazikidhi kiu ya kupambana na kushinda vita dhidi ya rushwa.
 
..I am 50/50 na huu mtizamo wako.

..let me tell u the 50% that disagrees with u.

..I dont think wa-Tz wanapenda rushwa na ufisadi.

..pia sidhani kama viongozi tunaowapata ni reflection ya wa-Tz.

..nasema hivi, kwasababu siamini kama kuna chama cha upinzani Tz kinaweza kumsimamisha fisadi kuliko mafisadi wote halafu kikawashinda CCM.

..wapinzani wamekuwa wanashindwa kwasababu hawajafanya juhudi za kutosha kujitangaza kwa wananchi huko vijijini ambako ndiko kura za ushindi zilipo.

..CCM wako kitaasisi zaidi ya upinzani. Wako makini ktk hatua zote za kuelekea uchaguzi, kuanzia kuandikisha wapiga kura, kutunza vitambulisho vya kupiga kura, kufanya kampeni, na mwisho kwenda kwa wingi vituoni.

..Kwenye kila uchaguzi, wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wamewekewa malengo maalumu ya idadi ya wanachama ambao wanapaswa kuhakikisha wamekwenda kupiga kura.

..Wapinzani wanatakiwa nao kuwa na mpango kazi mzuri zaidi ya ule wa CCM kwa hatua zote za kuelekea ktk uchaguzi mkuu.

cc Bulldog, Alinda, Nguruvi3, Mag3
JokaKuu, pamoja na yote ukweli usiopingika ni kwamba Upinzani hapa nchini unafanya kazi katika hali ngumu sana na kuwa mpinzani Tanzania kunataka moyo. Kuwa mpinzani ni sawa kutangaza vita dhidi ya utawala ulioko madarakani na hivyo kuwa tayari kuyaonja machungu mikononi mwa vyombo vya dola. Hebu shuhudia visa hivi viwili;

1. said:
WAKATI Jeshi la Polisi mkoani Iringa likimkamata na kumshikilia kwa muda wa saa tano kisha kumwachia huru Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, pamoja na wabunge watatu, kiongozi huyo amesema kuwa endepo kesi hiyo itafikishwa mahakamani itakuwa ya 10 kufunguliwa na jeshi hilo.

Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na vilevile mbunge wa Hai alikamatwa jana asubuhi pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Diwani wa Kata ya Mitimirefu, Frank Nyalusi, wakidaiwa kuzidisha muda wa mkutano.

Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao, kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi, alisema kuwa walizidisha muda wa mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika viwanja vya Mwembetogwa kwa zaidi ya dakika 25.

SAM_1251.JPG

Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa.

4.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na wanachama wa CCM Wilayani Nzega kwa kumpokea vyema na kumtakia heri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha chama nchini. Kinana alikuwa akiwahutubia wananchi hao saa nne usiku.

JokaKuu, katika mazingira kama haya, Upinzani wanatakiwa wafanye nini? Wapambane na vyombo vya dola? Huko Iringa mwandishi moja wa habari aliyethubutu kumhoji Kamanda wa Polisi wa Mkoa hivi sasa ni marehemu. Haya yote yanapotokea, sisi wananchi kwa kunyamaza ni kama tunawapa baraka hawa mafashisti wazidi kutunyanyasa. Kwa kweli nashindwa kuwaelewa Watanzania!
 
Mag3,

..asante kwa post yako hapo juu.

..mimi nadhani njia sahihi ni kuwashtaki CCM kwa wananchi kuhusu UKATILI wanaowafanyia wapinzani.

..mbona CDM imeweza Arusha mjini, Mbeya mjini, Ubungo, etc etc?? Kule jimboni kwa Tundu Lissu CDM imekomba imekomba vijiji 90 nadhani, na kuwaachia CCM vijiji 3.

..Tatizo la CDM ni kwamba chama kilikuwa hakijawekeza vya kutosha maeneo ya vijijini. Tujielekeze ktk kuhakikisha chama kinachoshinda kutokana na kuwa more organized huko vijijini. CCM wanaweza kusimamisha mgombea mbovu lakini wanashinda kwasababu wako more organized na off course wanabebwa na vyombo vya dola.

..Vyombo vya dola huwa ni watu wa mwisho kuunga mkono mageuzi. Kama unakumbuka kilichotokea Tahrir square, polisi walipoamua kuwaunga mkono "kiaina" wale waandamanaji baada ya kuona Hosni Mubarak hana future tena.

..Kwa hiyo CDM lazima wavifikishe vyombo vya dola ktk hatua ambayo wataona kabisa kwamba wananchi wameamua kubadilisha utawala. Hali ikifika hapo nakuhakikishia mtashuhudia polisi nao "wakiwapa shavu" CDM.

..Haya maovu tunayotendewa yawe chachu ya sisi kufanya kazi kwa bidii zaidi.

NB:

..Baada ya vitimbi vilivyofanyika ktk BUNGE MAALUM LA KATIBA nimegundua kwamba hakuna mabadiliko yatakayotokea ikiwa CDM haitakamata ikulu na kuwa na majority mle bungeni.
Alinda, Nguruvi3, TUJITEGEMEE, Freeland
 
Last edited by a moderator:
TUJITEGEMEE mfumo wa rushwa umetengenezwa mahususi , kwamba wananchi wanabaki na uwezo mdogo wa kukabiliana nao. Vyombo muhimu vya kupambanana rushwa vipo chini ya watoarushwa

''Radical changes'ni njia ninayoipenda sana, kwa bahati mbaya haiwezi kufanya kazi Tanzania.
Pengine ni ujinga uliotopea au ubinadamu uliotitia.

Hatujui kwanini Watanzania
wamegeuka mazezeta kiasi cha kuibiwa na kumshangilia mwizi aliyewaibia

Watoa rushwa wanatumia vyombo kama tume ya uchaguzi. Wanatumia Bunge kuondoa hoja na kuzisafisha- serikali.

Tume huru ya uchaguzi ingewezakana kupatikana kwa radical changes
Wananchi
wetu ni mazezeta, hawawezi kuthubutu. Kwa vile tunajua udhaifu wao, na tunajua udhaifu wa madhalimu, kilichopo ni kutumia udhaifu wa pande mbili kutoa matokeo chanya

Udhaifu wa wananchi:
Waelezwe jinsi wanavyodhulumiwa haki zao . Waelezwe tume ya uchaguzi ni tawi la CCM.
Halafu waambiwe kazi ni moja, kuhamasisha uandikishaji kupiga kura na kulinda kura.Tume ya uchaguzi si ya kuamini

Iliwezekana Tarime mara nyingi, ikawezekana Shinyanga, inaonekana Morogoro wameamka.
Kuna uwezekano mkubwa wa kupata
1/3. 2/3 au 1. Hili litatoa uwezakano wa kudhibiti eneo kama bunge linalotumika na CCM kwa 2/3 majority kuendeleza uhuni, ufisadi na wizi.

Na kuanzia hapo uwezekano wa kusema tunataka tume ya uchaguzi huru upo. Ukishakata mirija inayotoa nguvu kwa serikali,
mabadiliko yapo

Bunge la katiba lina mfano mzuri sana. CCM kwa kutumia sheria zao hawakuweza kuburuza umma.
Kwanini tudhani haiwezekani bunge la JMT

Kugawa kwa majimbo ni agenda ya CCM. Ni baada ya kuona 2/3 ina mashaka sana. Wanaongeza majimbo kufidia maeneo wanayoona tayari wamepoteza. Kazi ya wapinzani kama alivyosema JokaKuu ni kwenda kushambulia.

CCM kwasasa haihitaji kushambulia inalinda tu. Wapinzani wana nafasi nzuri ya kushambulia.
Wajiuliulize kama Singida na Mbeya wamepenya, kwanini isiwe Tanga au Morogoro?

Nasi wananchi tunajukumu, kuwaeleza wananchi, hivi hawa walioshindwa miaka 10 tena wakiwa katika mfumo huo , wanawezaje kusema wanaweza?

Wasira ni mmoja wa ‘think tank' ya CCM, leo anawezaje kusema kuna rushwa ikiwa yeye ni mratibu wa jitihada zile zile zilizoshindwa?
 
KUNDI HILI NI TATIZO!

Ni vema kuongelea kila mmoja na mchango wake katika harakati za kulisaidia taifa.

Lipo kundi linalochanganya umma, kwa kutoeleweka. Ni kundi muhimu sana katika taifa.
Lina weledi wa hali ya juu na ni taa
ya taifa.

Kundi limesambaa nchi
nzima kuanzia nyumba kumi, mtaa hadi taifa.Si jingine ni lile la Walimu

Wiki chache zilizopitawalimu walionekana May Mosi wakiadhimisha siku ya wafanyakazi.
Walibeba bango linalosema ‘Shemeji unatuachaje?' likimaanisha linamatatizo
na kutaka kujua ‘shemeji'anawaachaje

Wiki chache baadaye Rais akalikwa kufunguamkutano wa Walimu.
Rais akasema matatizo ya Walimu ikiwemo malipo yamalizwa kabla hajaondoka ofisini.
Na pia kutaka mswada wa sheria ya kuanzisha baraza kuu la vyama vya Walimu

Wiki iliyopita, mtia nia mh Lowassa akasema,Walimu ni kipaumbele chake atakapochaguliwa kwa kuangalia masilahi yao.

Wote wamelengaWalimu makusudi kabisa kwa kutambua wingi , ushawishi na kusambaa kwao kuanzia vijijini hadi mijini

Wanatambua ni kundi muhimu katika kutafuta kuungwamkono na kura

Walimu wanaonekana kushawishika na kauli hizo.Miaka nendarudi wametumiwa na kuachwanjia panda hadi kusahau taaluma zao na umuhimu wake na kutegemea ushemeji.

Udhaifu huo unapelekea wao kuwa wabeba bendera na wapiga debe, mwisho wa siku wanarudi katika mikutano kujadilimatatizo yao wenyewe

Ni vema Walimu wakajiuliza, hivi miaka 10 serika liilikuwa wapi kushughulikia haki zao?
Ni
lini pesa zimeapatikana ikiwa wafanyakazi wa umma wanapata mishahara kwa kudunduliza ?

Wajiulize ni lini Lowassa akiwa waziri mkuu, waziri wa kawaida au Mbunge , alisimama na kutetea masilahi yao?
Leo ana waona kwa jicho gani lililokuwa halioni
wakati akiwa na nyadhifa?

Wajiulize, iweje wazee wa iliyokuwa EAC wamefariki wakiacha malipo yao nyuma, na kwanini wao wadhani safari hii matatizo yao yatashughulikiwa?

Na Walimu wajiulize,kwanini
si mabwana shamba na mifugo wa kilimo kwanza, kwanini wao ndio wanakuwa walengwa?

Kama hawatajiuliza maswali hayo, tutarudi kule kule kunakoonyesha, Walimu licha ya weledi na umuhimu wao kitaifa, ndilo kundi linalorudisha jitihada za mbadiliko ya kisiasa na kiuchumi kwa kutumika bila kujielewa.

Ndio maanatunasema kundi la Walimu ni tatizo na wakati umefika lijiangalie
lenyewe na kizazi kijacho

Tusemezane
 
..I am 50/50 na huu mtizamo wako.

..let me tell u the 50% that disagrees with u.

..I dont think wa-Tz wanapenda rushwa na ufisadi.

..pia sidhani kama viongozi tunaowapata ni reflection ya wa-Tz.

..nasema hivi, kwasababu siamini kama kuna chama cha upinzani Tz kinaweza kumsimamisha fisadi kuliko mafisadi wote halafu kikawashinda CCM.

..wapinzani wamekuwa wanashindwa kwasababu hawajafanya juhudi za kutosha kujitangaza kwa wananchi huko vijijini ambako ndiko kura za ushindi zilipo.

..CCM wako kitaasisi zaidi ya upinzani. Wako makini ktk hatua zote za kuelekea uchaguzi, kuanzia kuandikisha wapiga kura, kutunza vitambulisho vya kupiga kura, kufanya kampeni, na mwisho kwenda kwa wingi vituoni.

..Kwenye kila uchaguzi, wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wamewekewa malengo maalumu ya idadi ya wanachama ambao wanapaswa kuhakikisha wamekwenda kupiga kura.

..Wapinzani wanatakiwa nao kuwa na mpango kazi mzuri zaidi ya ule wa CCM kwa hatua zote za kuelekea ktk uchaguzi mkuu.

cc Bulldog, Alinda, Nguruvi3, Mag3

Mkuu JokaKuu ahsante kwa mhango wako.

Hivi unajua huku "field " kwa sasa wananchi wameshindwa kutofautisha kati ya wapinzani na CCM.

Huku "field" mtu akipata nafasi serikalini alafu asiibe wananchi "tu/wa namwona " ni mjinga....Huchelewi kusikia kauli za "jamaa ----- kweli" kashindwa kupiga?

Mkuu..Unajua hawa wapinzani walikua na muda wa kutosha sana kuweka presha ya Tume huru,aU TUSEME mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi..Lakini kwa nini hawakufanya hivyo?

Hivi leo ukimuuliza Freeman,Lipumba au James....Wanatarajia kushinda kwa juhudi zipi walizofanya? atakujibu lipi la maana?

Nakubaliana na wewe kwamba Wapinzani hawajajipanga ipasavyo.

Tusigemee matokeo tofauti oktoba
 
Mkuu@Mag3 katoa hojainayohitaji fikra. Kasema Watanzania ni watu wa ajabu, wameweka matumaini kwa viongozi wa siasa na si wao kuwa viongozi wa mageuzi. Maana yake nikuwa shinikizo unalosema lilipaswa kutoka kwaWananchi.

Nasi tukasema Watanzania ni mazezeta au ubinadamu umewazidi.
Unaona
baada ya kushindwa kuleta mabadiliko kama ya tume ya uchaguzi,bado wanafurika kupokea wezi waliowaibia

Hoja hapa ni kuwa mabadiliko hayana mtu yana watu, watu nisisi, yule, wale na wao.
Siyo
sualala Mbowe, Lipumba n.k.

Kuhusu ufisadi, wananchi wanachukia sana. Kinachowakatisha tamaa ni namna unavyoshughulikiwa.

Kuna sababu gani
za wao kupinga ufisadiikiwa serikali yao inalinda mafisadi tena kwa kutumia njia za sheria hata kama kuna uharamu?

Hawa wa sh 100 si tatizo ni njaa, tatizo nigenge linalohangaisha umma wa watu milioni45.

Sina uhakika unaongeleaeneo lipi, bribery, corruptions au grand corruptions and sabotage
 
JokaKuu, pamoja na yote ukweli usiopingika ni kwamba Upinzani hapa nchini unafanya kazi katika hali ngumu sana na kuwa mpinzani Tanzania kunataka moyo. Kuwa mpinzani ni sawa kutangaza vita dhidi ya utawala ulioko madarakani na hivyo kuwa tayari kuyaonja machungu mikononi mwa vyombo vya dola. Hebu shuhudia visa hivi viwili;

SAM_1251.JPG

Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa.

4.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na wanachama wa CCM Wilayani Nzega kwa kumpokea vyema na kumtakia heri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha chama nchini. Kinana alikuwa akiwahutubia wananchi hao saa nne usiku.

JokaKuu, katika mazingira kama haya, Upinzani wanatakiwa wafanye nini? Wapambane na vyombo vya dola? Huko Iringa mwandishi moja wa habari aliyethubutu kumhoji Kamanda wa Polisi wa Mkoa hivi sasa ni marehemu. Haya yote yanapotokea, sisi wananchi kwa kunyamaza ni kama tunawapa baraka hawa mafashisti wazidi kutunyanyasa. Kwa kweli nashindwa kuwaelewa Watanzania!

Hii nchi kwakweli inasikitisha
 
Mkuu@Mag3 katoa hojainayohitaji fikra. Kasema Watanzania ni watu wa ajabu, wameweka matumaini kwa viongozi wa siasa na si wao kuwa viongozi wa mageuzi. Maana yake nikuwa shinikizo unalosema lilipaswa kutoka kwaWananchi.

Nasi tukasema Watanzania ni mazezeta au ubinadamu umewazidi.
Unaona
baada ya kushindwa kuleta mabadiliko kama ya tume ya uchaguzi,bado wanafurika kupokea wezi waliowaibia

Hoja hapa ni kuwa mabadiliko hayana mtu yana watu, watu nisisi, yule, wale na wao.
Siyo
sualala Mbowe, Lipumba n.k.

Kuhusu ufisadi, wananchi wanachukia sana. Kinachowakatisha tamaa ni namna unavyoshughulikiwa.

Kuna sababu gani
za wao kupinga ufisadiikiwa serikali yao inalinda mafisadi tena kwa kutumia njia za sheria hata kama kuna uharamu?

Hawa wa sh 100 si tatizo ni njaa, tatizo nigenge linalohangaisha umma wa watu milioni45.

Sina uhakika unaongeleaeneo lipi, bribery, corruptions au grand corruptions and sabotage

Ahsante mkuu Nguruvi3 Nakubaliana na wewe kwamba watanzania ni specie ya ajabu kabisa labda inayohitaji uchunguzi wa kisayansi kujua tofauti yetu na binadamu wengine.

Pia,Mkuu katika mabadiliko yoyote lazima yawe na kiongozi....Kiongozi ndiye anayeonesha njia wengine wanafuatia...lazima kuwe na mwonyesha njia.

Hapa kwetu "tulidhani" wapinzani watakuwa wanatuelekeza njia inayoeleweka...lakini wameshindwa kuifanya kazi hiyo ipasavyo.

Inapotokea CCM inakataliwa ni kwa sababu ya watu kuwa na hasira nayo ila sio kwa sababu wapinzani wameonesha wao ni bora zaidi.

Tunawaongelea wapinzani kwa sababu tunawaona wao ndio viongozi katika mabadiliko tunayoyataka...Ndio maana lazima tumuongelee Ibrahim kama kiongozi,Freeman Kama kiongozi na James kama kiongozi.

Katika suala la wananchi kuuchukia ufisadi...sian uhakika kama umefanya utafiti mdogo tu hata huku "mtaani"

Watanzania (wengi wao) hawajui ufisadi ni nini...na hawajui athari zake kwao....kwa hio kwa wao hawawezi kukichuia kitu ambacho hawakijui.......Mimi nikiiba serikalini huku mtaani ntaonekana "Hero"....na nitasifiwa......

Hapa tunaongelea Grand Corruption....na corruption ya kawaida
 
Mh MAKAMBA NA Mh MEMBE WATANGAZA

Wote wameongelea rushwa kama tatizokubwa.Viongozi, waliotangaza na wanaotangaza nia, wanaelewa rushwa ni tatizo.

Hapa ndipo tunaposema nani msafi ndaniya CCM? Tunasema kwasababu wote wanaona tatizo la rushwa.

Wote ni system ile wanayoilaumu.Wanatumbia wanakokaa katika chama, bunge au baraza la mawaziri rushwa wanajua ipo

Swali,wao kama viongozi wamefanya nini kuzuia rushwa? Kwanini waone rushwa katika majukwaana si katika chama, bunge , serikali au cabinet pale Ikulu?Usafi wao upo wapi?Nani msafi ndani ya CCM?

Memba amejinasibu ni mwadilifu. Uadilifu hauishii kwa kutotoa rushwa.
Kukaa kimya uhalifu ukitendeka ni sehemu ya ukosefu wa maadili.

Mh Membe ni mjumbe wa baraza lamawaziri. Lini amesimama na kupinga rushwa kwenye chama auserikali?

Miaka kadhaa akiwa naibu na waziri alikuwa kimya rushwa ikistawi, leo anapata wapi ushujaa wa kusema ni mwadilifu?

Tena Mh Membe ndiye aliyerudisha pesa za radar,hatujui zilitokaje,hatuambii.

Uadilifu wa Membe upo wapi? Alisem atatueleza nani wamechukua pesa, hadi sasa hatujui ingawa anajua.
Uadilifu wake upo wapi? Je, kukaa kimya si ‘conspiracy''

Mh Makamba, yeye hakuzungumizia kwa undani. Tunajua alikuwa mshauri wa Rais Ikulu, vipi, hakuona ya Richmond, Meremeta, Tangold, Dowans namengine?

Mh January ina maana hajui mzazi wake alikuwa kundi gani wakati wa sakata la Richmond ?

Na kwamba, yeye alipokuwa kamati ya nishati,alifanya nini kuhusu tatizo la rushwa katika nishati ambalo si kuwa liliisha bali limendelea hadi kufikia escrow?
 
JANUARY BADO HAJALIONA TATIZO

Katika kuzindua nia yake Janury Makamba tofauti na wagombea wengine amejaribu kuonyesha namna gani atapata mapato yatakayo muewezesha kutimiza malengo

Pengine anapata credit si kama waorodhesha matatizo bila kutuambia wanatumia rasilimali gani, kwa utaratibu upi

Hata hivyo Makamba ana maungufu makubwa. Ukiacha lile tunalisema la ‘hakuna msafi ndani yaCCM'' upungufu mwingine ni wa kukwepa hoja nzito

Kwanza ukiangallia mchanganuo wake, atapataTrilioni 3 kwa vyanzo alivyotaja.

Bado nchi yetu vyanzo vya mapatoni vingi sana kama angetulia. Hajaongelea utalii na jinsi unavyoweza kuchangia pato la taifa. Uvuvi ameongelea meli bila kueleza uvuvi wenyewe unachangiaje pato la taifa

Makamba ameacha eneo muhimu sana linaloumiza taifa, ukubwawa serikali na matumizi ya hovyo ya serikali.

Hili tu lingeweza kumsaidia kupata pato kubwa kuliko lile la nyuki.

Mh hajaeleza matumizi mabaya kama CAG anavyoonyesha, kubana matumizi kulingana na bajeti, kupunguza muda wa bunge,kufuta pesa za mifuko ya wabunge, kuondoa allowance za wabunge kukaa katika viti vyao n.k.

Makamba hajaonelea mchango wa Kilimo katika pato la taifa tukijua kilimo ni sehemu kubwa ya uchumi wetu.

Makamba hajaeleza mchango wa mashirika ya nje na ndani katika pato la taifa.
Tunajua zipo corporate tax, hizo anazizungumziaje

Eneo la madini hajalizungumzia kwa uyakinifu, eneo linaloweza kusaidia sana katika pato la taifa

Ukiangalia haraka, hesabu zake zinaonyesha ni kama Trilioni3 katika bajeti ya leo.

Hata hivyo, kwa umakini angeweza kupata Trilioni 6 ambazo zingefidia nakisi ya bajeti a leo.
Hata kama si kwa ujumla, lingeondoa asilimia 40 ya utegemezi

Makamba akumbuke , hata kama atakusanya Trilioni 30, hakuna kitakachofanikiwa ikiwa rushwa ipo.

Kuna mradi uliofanyika Ethiopia unaofanana na ule wa Kenya.

Gharama za Ethiopia zilikuwa chini sana kulingana na za Kenya.

Waziri mmoja akualiza kwanini iwe hivyo? Waziri mwenzake wa Ethiopia akajibu, gharama ni kubwa Kenya kwasababu kuna rushwa, Ethiopia gharama ni ndogo hakuna rushwa

NB

Makamba alikuwa 'mshauri wa Rais wa serikali hii''

Ni mwanachama wa CCM le ile yenye rushwa!

Tusemezane
 
Hii nchi kwakweli inasikitisha

Inasikitisha nini,Haki inatakiwa ianzie katika familia zetu,vyama vyetu,Taifa,Mara ngapi CHADEMA inanyanyasa wanachama wake sababu ya kutofautiana mtizamo,kumbuka mwigamba alivyopigwa tofari,huku Mbowe akiangalia,kumbuka mlichofanyia mlinzi wa Dr Slaa,Tulitakiwa tulaani sote,nachukia kuona polisi ikinyanyasa upinzani,na kuibeba CCM pale inapopitiliza mda wa kibali,ila haki lazima iwepo katika vyama vyetu
 
Alinda,

..wapinzani wasitegemee hata siku moja kwamba CCM na serikali yake wataleta tume huru ya uchaguzi.

..kitu cha msingi ni kuilazimisha tume hii hii ambayo siyo huru kutangaza matokeo halali ambayo yanaiondoa CCM madarakani.

..Now, u may ask me how do u do that?? Jibu ni kwamba, lazima wapinzani wahakikishe kwamba wanapata ushindi wa kishindo. Yaani ushindi wao uwe ni mkubwa kiasi kwamba haina maana tena kwa tume au CCM kuchezea matokeo.

..Je, inawezekana? Jibu ni kwamba, inawezekana ikiwa wapinzani watawaelimisha vya kutosha wananchi. Kuna majimbo hapa Tz ambayo ktk uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa wananchi wamechagua wapinzani kwa zaidi ya asilimia 80.

..Nigeria wananchi walimpigia kura mgombea wa upinzani kiasi kwamba ikashindikana kuiba zile kura. Yaani ilifika mahali viongozi wa chama tawala wakawa wanalalamika, lakini tume ilishindwa "kufanya-fanya" ikabidi wamtangaze mshindi halali.
Mkuu hapa kuna hoja,tutete kidogo

Suala la tume huru yauchaguzi, kuhoji mahakamani na 50.1% ya matokeo ni vitu ambavyo wapinzani walitakiwa kuvisimamia kwa msaada wa wananchi. Tuliwaeleza

Hayo yalidhaniwa yangetokea katika katiba. CCM wakagundua na kuvuruga mchakato

Kwa wananchi wa Tanzania ‘radical changes' tunazoziona kwingine duniani ni suala lisiloeleweka.
Ndio maana tunasema ni ima mazezeta au binadamu saana

Hapo ndipo nakubaliana nawe kuwa hata siku moja CCM haiwezi kubadili tume ya uchaguzi.
Kwani watu hawaoni kila analosema JK ndilo analiotangaza yule Jaji?

Mfano wako wa serikali za mitaa ni mzuri sana. Huu ni uchaguzi unaosimamiwa na CCM ikishirikiana na Polisi, wakuu wa Wilaya n.k.Bado wananchi katika maeneo yasiyofikiwa na Wapinzani walisimama kukataa kudhulumiwa

Kwavile hakuna kinachoweza kutokea kwa muda huu na tunajua Watanzania walivyo, kuna nafasi ya kutoa elimu kwa njia nyingine. Moja ni hiyo ya kuwaambia wapinzani ushindi wao usiwe wa kubabaisha, uwe ushindi ambao CC waone haya
Inawezekana hiyo, mbona Tarime , Mbeya, Mwanza, wanaweza?

Njia ya pili ni kuwaelimisha wananchi kuwa mabadiliko wanayo wenyewe.
Ikiwezekana kuzuia 2/3 ya CCM, ngamia atakuwa amepiga magoti.

Hata CCM wanafahamu wapinzani wakijipanga hali mbaya. Ndio maana watia nia wote wameteka agenda za wapinzani,wanazungumzia rushwa ile ile waliyoitetea miaka 10, wanazungumzia afya na elimu mambo yale yale waliyoyapa kisogo miaka 10. Wamefikia kukiri serikaliyao imejaa rushwa, na inahitaji kiongozi imara, wakimaanisha kuna udhaifu

CCM wanajau wazi hawana kauli za kuuza tena kwa kutumia sera na ilani yao ya uichaguzi.

Wanachokifanya ni kufuata upepo ambao ni kuungana na wananchi katika hasira utadhani wao ndio wapinzani.
 
Vyama vya upinzani Tanzania havijajenga uhuru wa mawazo unaoruhusu ushindani wa kisiasa ndani ya vyama hivyo, ndio maana mashabiki wa vyama vya upinzani wanapata shida kuelewa kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kumtafuta mgombea wake wa urais.

CCM imefanya kazi nzuri kuliongoza taifa letu na imeweka misingi ya fursa kwa kila mwenye bidii. Tanzania ni taifa la kutolewa mfano barani Afrika kutokana na kazi nzuri ya CCM.

Lakini ni wajibu wa wanaCCM kukiri kuwa kwa kiwango fulani chama kimetoka nje ya misingi iliyokiasisi.

Vipo viashiria vingi lakini kimoja ni Lowassa kufikiriwa kuwa atapitishwa kugombea urais. Iwapo chama kingekuwa imara kwenye misingi ya uadilifu, mtu kama Lowassa hata asingefikiria kuchukua fomu.

Lowassa anamwaga mapesa kwa wajumbe na makada kwa vile anajua ndani ya chama cha mapinduzi siku hizi pesa ndiyo inayoamua nani awe kiongozi.

Hii ni hatari na vijana lazima wawe mstari wa mbele kulisema hili kwa sauti kuu.

Rushwa ikishamiri kwenye chama itaingia serikalini. Itafikia wakati ukuu wa shule utakuwa unauzwa, ukuu wa idara utapangiwa bei, na huo ndio utakuwa mwisho wa ufanisi. Nchi itaporomoka na hakutakuwa na jinsi ya kuzuia kuporomoka huko.

Lowassa kawaahidi watu wengi vyeo serikalini iwapo atakuwa Rais. Je, nani atasimamia na kukagua ufanisi wa watu walioingizwa kisiasa na mkuu wa nchi? Hawa hawatagusika. Mtu wa namna hii anapofikiriwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM basi ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha dalili za kukinzana na malengo ya kuasisiwa kwake.

CCM imekataa kubadilika kwenye rushwa, hasahasa rushwa za uchaguzi. Rushwa za uchaguzi huzaa viongozi wasiowajibika kwa watu. Kwanini CCM inachagua kutoa viongozi wanaowajibika kwa pesa za uchuuzi?

Viongozi wasiowajibika kwa watu hufanya watu hao wakichoke chama.

Ndio maana kundi la vijana ambao wanaisema vibaya CCM linaongezeka kila baada ya uchaguzi. Ugomvi wao na CCM sio kwa sababu ina sera mbaya na sio sababu haijajenga nchi, ila kwa sababu viongozi wanaotokana na CCM hawaonyeshi udhati wao kwenye kushughulikia masuala yanayoikera jamii kama hili la ufisadi.

Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM.

Bahati ya mtende kuota jangwani ndio inayofanya CCM iendelee kubaki madarakani. Hakuna Chama cha upinzani chenye infrastructure ya kuongoza nchi. Ndio maana watanzania wataendelea kuichagua CCM. Wanaichagua CCM kwa shingo upande huku wakijua they deserve better, but better is not available.

Good news kwa CCM ni kwamba watanzania wanaipa nafasi ya kujirekebisha. Now it's up to CCM kama itajirekebisha au itaendelea kutegemea udhaifu wa wapinzani. Wakati huohuo wapinzani pia wamekuwa wakitegemea udhaifu wa CCM kujitwalia majimbo na kata lakini kwenye Urais ni tofauti.

Vijana wanaokumbatia rushwa za uchaguzi ni vipofu wa fikra, kwa sababu wanachofanya ni kuharakisha tu process ya CCM kuwa chama cha upinzani. Wanajiharibia wenyewe future yao kwa tamaa za muda mfupi.

Mabadiliko ya kweli si lele mama...
 
Back
Top Bottom