Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #61
ZeMarcopolo ahsante sana kwa mchango wako. Tutarejea kujadili hoja zako
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vyama vya upinzani Tanzania havijajenga uhuru wa mawazo unaoruhusu ushindani wa kisiasa ndani ya vyama hivyo, ndio maana mashabiki wa vyama vya upinzani wanapata shida kuelewa kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kumtafuta mgombea wake wa urais.
CCM imefanya kazi nzuri kuliongoza taifa letu na imeweka misingi ya fursa kwa kila mwenye bidii. Tanzania ni taifa la kutolewa mfano barani Afrika kutokana na kazi nzuri ya CCM.
Lakini ni wajibu wa wanaCCM kukiri kuwa kwa kiwango fulani chama kimetoka nje ya misingi iliyokiasisi.
Vipo viashiria vingi lakini kimoja ni Lowassa kufikiriwa kuwa atapitishwa kugombea urais. Iwapo chama kingekuwa imara kwenye misingi ya uadilifu, mtu kama Lowassa hata asingefikiria kuchukua fomu.
Lowassa anamwaga mapesa kwa wajumbe na makada kwa vile anajua ndani ya chama cha mapinduzi siku hizi pesa ndiyo inayoamua nani awe kiongozi.
Hii ni hatari na vijana lazima wawe mstari wa mbele kulisema hili kwa sauti kuu.
Rushwa ikishamiri kwenye chama itaingia serikalini. Itafikia wakati ukuu wa shule utakuwa unauzwa, ukuu wa idara utapangiwa bei, na huo ndio utakuwa mwisho wa ufanisi. Nchi itaporomoka na hakutakuwa na jinsi ya kuzuia kuporomoka huko.
Lowassa kawaahidi watu wengi vyeo serikalini iwapo atakuwa Rais. Je, nani atasimamia na kukagua ufanisi wa watu walioingizwa kisiasa na mkuu wa nchi? Hawa hawatagusika. Mtu wa namna hii anapofikiriwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM basi ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha dalili za kukinzana na malengo ya kuasisiwa kwake.
CCM imekataa kubadilika kwenye rushwa, hasahasa rushwa za uchaguzi. Rushwa za uchaguzi huzaa viongozi wasiowajibika kwa watu. Kwanini CCM inachagua kutoa viongozi wanaowajibika kwa pesa za uchuuzi?
Viongozi wasiowajibika kwa watu hufanya watu hao wakichoke chama.
Ndio maana kundi la vijana ambao wanaisema vibaya CCM linaongezeka kila baada ya uchaguzi. Ugomvi wao na CCM sio kwa sababu ina sera mbaya na sio sababu haijajenga nchi, ila kwa sababu viongozi wanaotokana na CCM hawaonyeshi udhati wao kwenye kushughulikia masuala yanayoikera jamii kama hili la ufisadi.
Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM.
Bahati ya mtende kuota jangwani ndio inayofanya CCM iendelee kubaki madarakani. Hakuna Chama cha upinzani chenye infrastructure ya kuongoza nchi. Ndio maana watanzania wataendelea kuichagua CCM. Wanaichagua CCM kwa shingo upande huku wakijua they deserve better, but better is not available.
Good news kwa CCM ni kwamba watanzania wanaipa nafasi ya kujirekebisha. Now it's up to CCM kama itajirekebisha au itaendelea kutegemea udhaifu wa wapinzani. Wakati huohuo wapinzani pia wamekuwa wakitegemea udhaifu wa CCM kujitwalia majimbo na kata lakini kwenye Urais ni tofauti.
Vijana wanaokumbatia rushwa za uchaguzi ni vipofu wa fikra, kwa sababu wanachofanya ni kuharakisha tu process ya CCM kuwa chama cha upinzani. Wanajiharibia wenyewe future yao kwa tamaa za muda mfupi.
Mabadiliko ya kweli si lele mama...
Sijui ni uhuru gani unaoongelea, tunadhani unaongelea mheshimiwa kiongozi mkuu kutimuliwa kutoka upinzani.ZeMarcopolo;12947791]Vyama vya upinzani Tanzania havijajenga uhuru wa mawazo unaoruhusu ushindani wa kisiasa ndani ya vyama hivyo, ndio maana mashabiki wa vyama vya upinzani wanapata shida kuelewa kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kumtafuta mgombea wake wa urais.
Ndugu yangu nakuomba kwa hisani uwe na kaibu kidogo. Hatuwezi kuwa nchi masikini kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.CCM imefanya kazi nzuri kuliongoza taifa letu na imeweka misingi ya fursa kwa kila mwenye bidii.
Tanzania ni taifa la kutolewa mfano barani Afrika kutokana na kazi nzuri ya CCM.
Sijui kama ni chama au ni NGO.Lakini ni wajibu wa wanaCCM kukiri kuwa kwa kiwango fulani chama kimetoka nje ya misingi iliyokiasisi.
Umeliona hili, lakini nani msafi ndani ya CCM? Hivi unawezaje kulelewa katika familia kisha ukasema ni familia mbovu?Vipo viashiria vingi lakini kimoja ni Lowassa kufikiriwa kuwa atapitishwa kugombea urais.
Iwapo chama kingekuwa imara kwenye misingi ya uadilifu, mtu kama Lowassa hata asingefikiria kuchukua fomu.
Na tusipobadilika, Watanzania tutaongozwa na wanunuzi, wachuuzi wa nchi. Nani katufikisha hapa, CCMLowassa anamwaga mapesa kwa wajumbe na makada kwa vile anajua ndani ya chama cha mapinduzi siku hizi pesa ndiyo inayoamua nani awe kiongozi.
Na kulikataa si kulisema tu.Hii ni hatari na vijana lazima wawe mstari wa mbele kulisema hili kwa sauti kuu.
Haa, hivi unadhani haipo serikalini! Tunadhani CCM ni safi kuliko serikali yake.Rushwa ikishamiri kwenye chama itaingia serikalini. Itafikia wakati ukuu wa shule utakuwa unauzwa, ukuu wa idara utapangiwa bei, na huo ndio utakuwa mwisho wa ufanisi. Nchi itaporomoka na hakutakuwa na jinsi ya kuzuia kuporomoka huko.
Unaona mtandao unavyotesa nchi.Lowassa kawaahidi watu wengi vyeo serikalini iwapo atakuwa Rais. Je, nani atasimamia na kukagua ufanisi wa watu walioingizwa kisiasa na mkuu wa nchi? Hawa hawatagusika. Mtu wa namna hii anapofikiriwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM basi ni ishara tosha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha dalili za kukinzana na malengo ya kuasisiwa kwake.
Unakubaliana nasi kuwa CCM haijaleta maendeleo uliyosema mwanzoni, haitoi fursa sawa kwasababu kama huna pesa, si lolote si chochote, subiri kofia, tshirt na khanga. Fursa uliyosema ipo CCM iko wapi mkuu?CCM imekataa kubadilika kwenye rushwa, hasahasa rushwa za uchaguzi. Rushwa za uchaguzi huzaa viongozi wasiowajibika kwa watu. Kwanini CCM inachagua kutoa viongozi wanaowajibika kwa pesa za uchuuzi?
Mkuu hawa wamewekeza , wana muda gani wa kusikiliza wananchi? Wanachokifanya ni kuangalia return ya uwekezaji waoNdio maana kundi la vijana ambao wanaisema vibaya CCM linaongezeka kila baada ya uchaguzi. Ugomvi wao na CCM sio kwa sababu ina sera mbaya na sio sababu haijajenga nchi, ila kwa sababu viongozi wanaotokana na CCM hawaonyeshi udhati wao kwenye kushughulikia masuala yanayoikera jamii kama hili la ufisadi
Hao wanaoamua nani awe mbeba bendera wa CCM ni mafisadi.Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM
Hili swala mimi ndio nimelifatilia zaidiTutakuwa na mfululizo wa mabandiko kuangali uchaguzi kwa ujumlawake.
Mtazamo wa wagombea watarajiwa katikahatua za awali. Hali ya chamatawala baada ya miaka50
Sijui ni uhuru gani unaoongelea, tunadhani unaongelea mheshimiwa kiongozi mkuu kutimuliwa kutoka upinzani.
Wengine wametimuliwa kutoka vyama ikiwemo CCM.CCM ingekuwa na uhuru wa mawazo, vipi Mansour Himid aliyetoa mawazo yake alitendwaje? Nassoro Moyo amepewa uhuru gani wa mawazo?
CCM kuzuia wanachama wasiingie midahalo ndio uhuru wenyewe?
Kuhusu upinzani ndani ya CCM, nakuhakikishia si suala la demokrasia wala uhuru. Ni suala la masilahi binafsi. Hilo safari hii linaitesa sana CCM na huenda ikiwa ni catalyst nzuri tu ya kupoteza. Nitajadili kwa undani katika mabandiko yanayofuata. Ndugu yangu nakuomba kwa hisani uwe na kaibu kidogo. Hatuwezi kuwa nchi masikini kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.
Hatuwezi kutegemea wafadhaili kwa baJeti kwa miaka 50 ukasema ni kazi nzuri.
Hatuwezi kuwa nyuma ya Korea, Malaysia, China tuliokuwa karibu nao miaka 50 sasa tofauti yetu ni masikini na wenye uwezo
Hatuwezi kuwakomboa Msumbiji, wakaingia vitani miaka 20 na sasa ni juu yetu.
Hatuwezi kukomboa Botswana wenye rasilimali kama sisi, wakawa kundi jingine tukabaki na nafasi ya 25 masikini sana duniani, eti tutembee vifua mbele CCM inafanya kazi nzuri!!
Fursa unazoongelea ni kwa walioko ndani ya CCM. Nakubaliana nawe ukifanya bidii ukaingia katika system utafanikiwa.
Huko utaruhusiwa kuiba na kusafishwa na ofisi kubwa. Huko utaingia Stanbic na kiroba kitupu ukitoka kimjaa, naam fursa kwa wote.
Fursa ni za wale wanaokwenda kucheki Mimba India, kutibiwa mabusha London, na kuondolewa chunusi South Africa
Mama anayezalia juu ya Tenga miaka 50 baada ya uhuru haoni fursa, anaona moto
Miaka ya 1970 niliona miji ikiwa na Ambulance katika halmashauri. Vituo vya afya vikiwa na usafiri.
Leo tunashushudia watu wakisimama barabarani kuomba msaada wa bajaji kwasababu mtu kapata ajali.
Hakuna Ambulance na hao Polisi hawana vitendea kazi vya kufika maeneo kwa wakati. Kundi hili halina fursa lina maamivu makali
Fursa ni kwa wale wanaopiga kodi za walalahoi ili watoto wakasome nje ya nchi kuanzia kindergaten hadi mwisho.
Wale wasioweza hata kununua sare za shule za kata hawaoni fursa,wanaona moto kila kukicha. Sijui kama ni chama au ni NGO.
CCM inayojulikana si hii ya leo, kama huna mshiko wewe subiri kupiga kura tu. Utaletewa jina likiambatanishwa na khanga au kofia. Hiyo ndiyo fursa yako Umeliona hili, lakini nani msafi ndani ya CCM? Hivi unawezaje kulelewa katika familia kisha ukasema ni familia mbovu?
Nani msafi, nani amesimama na kusema hapana, CCM inakwenda kubaya. Na tusipobadilika, Watanzania tutaongozwa na wanunuzi, wachuuzi wa nchi. Nani katufikisha hapa, CCM Na kulikataa si kulisema tu.
Kukataa ni kupinga kwa nguvu na vitendo nchi kununuliwa na wafanyabiashara wakitumia wachuuzi wa CCM. Haa, hivi unadhani haipo serikalini! Tunadhani CCM ni safi kuliko serikali yake.
Huoni kila mgombea aliye waziri au kiongozi kila mmoja anasema serikali imejaa rushwa.
Wote, watia nia wanakiri serikali ya JK imejaa rushwa na nia zao ni kuiondoa. Wanasema wenyewe! Unaona mtandao unavyotesa nchi.
Mwaka 2005 ni mtandao uliomwingiza mtu pale magogoni. Wanamtandao wakiiba, kazi ya kusafishwa inafanyika pale pale walipowekeza. CCM unayosema imetoa fursa imebaki kuwa kijibwa koko, inabweka tu. Wenye nchi wanatenda yao kwa msaada wa ofisi waliyoipigania Unakubaliana nasi kuwa CCM haijaleta maendeleo uliyosema mwanzoni, haitoi fursa sawa kwasababu kama huna pesa, si lolote si chochote, subiri kofia, tshirt na khanga. Fursa uliyosema ipo CCM iko wapi mkuu? Mkuu hawa wamewekeza , wana muda gani wa kusikiliza wananchi? Wanachokifanya ni kuangalia return ya uwekezaji wao
Huu ndio utamaduni wa CCM uliopo siku hizi. Na hapa tena unarudi kule kule, hao vijana wanaichukiaje CCM ikiwa unadai inatoa fursa sawa kwa wote? Kwanini wakimbilie upinzani na wasikae na fursa ndani ya CCM? Hao wanaoamua nani awe mbeba bendera wa CCM ni mafisadi.
Sasa nani amfunge paka kengele. Wanajua wazi baada ya muda wataondoka, lazima waweke mtu wa kulinda masilahi yao.
Ni yale ya Kagoda, Meremeta, Tangold n.k. kulindana, utamaduni wa CCM na wenye fursa ndio wanaosema, CCM njema!
Mkuu ukisoma nilichoandika, sikwenda kwa wapinzani uliko jadili. Nilikuwa nataka nitenganishe kwasababu hoja zako juu ya wapinzani zina uzito. Umeniwahi tu, lakini nitazijadili vema.Mkuu Nguruvi,
Nilitegemea uje na jibu, lakini umekataa kuja na jibu au kutoa changamoto, badala yake unetafuta tu maneno mengine ya kusema kilekile nilichoandika.
Hata hivyo nimeipenda post yako kwa vile imeendorse nilichoandika.
Msingi wa ninachpjadili ni kuwa at any time t lazima ikulu iwe occupied. Ikulu haiwezi kuwa vacant hata kwa siku moja. Sasa our situation ni kwamba tuna CCM na wapinzani. CCM is bad wapinzani are worse. CCM is slow wapinzani are slower, CCM is weak, wapinzani are weaker.
Mabaya yote uliyotaja ya CCM happy juu ni ya ukweli. Hujakosea, actually ndio msingi wa hoja yangu, kuwa CCM is not clean ila ina bahati ya mtende inayotokana na udhaifu wa wapinzani hasahasa kwenye nafasi ya urais.
Hata hivyo, ukisema CCM haijafanya kitu chochote chenye manufaa unanisababisha nisijibu zaidi kwa sababu ya aina ya jukwaa tulilopo. Hoja kama hiyo naweza kuijibu kule mchafukoge kwa style inayostahili. Kwa huku nakaa kimya.
Mkuu hakika wameanza kujinasibisha na jamii. Agenda ya ufisadi na wizi si ya CCM, lakini kila mmoja anayetia nia anaitaja. Wanajua ni namba moja katika matatizo ya taifa. Swali linakuja, hao wanaolaani ufisadi wakiwa ndani ya CCM wanatenda kwa dhati au ndio kujiunga na jamii? Watawezaje kufumua mfumo uliowalea kwa miaka yote tena wakiwa kimya?zeMarcopolo
Agenda kuu katika uchaguzi wa mwaka huu ni UFISADI. Je, vigezo vya kumpata mgombea wa CCM vinazingatia hili? Kutokuzingatia hili ni kujitenga na jamii na kuifanya wasiipende CCM.
Bahati ya mtende kuota jangwani ndio inayofanya CCM iendelee kubaki madarakani. Hakuna Chama cha upinzani chenye infrastructure ya kuongoza nchi. Ndio maana watanzania wataendelea kuichagua CCM. Wanaichagua CCM kwa shingo upande huku wakijua they deserve better, but better is not available.
Good news kwa CCM ni kwamba watanzania wanaipa nafasi ya kujirekebisha. Now it's up to CCM kama itajirekebisha au itaendelea kutegemea udhaifu wa wapinzani. Wakati huohuo wapinzani pia wamekuwa wakitegemea udhaifu wa CCM kujitwalia majimbo na kata lakini kwenye Urais ni tofauti.
Vijana wanaokumbatia rushwa za uchaguzi ni vipofu wa fikra, kwa sababu wanachofanya ni kuharakisha tu process ya CCM kuwa chama cha upinzani. Wanajiharibia wenyewe future yao kwa tamaa za muda mfupi. Mabadiliko ya kweli si lele mama
Mkuu hakika wameanza kujinasibisha na jamii. Agenda ya ufisadi na wizi si ya CCM, lakini kila mmoja anayetia nia anaitaja. Wanajua ni namba moja katika matatizo ya taifa. Swali linakuja, hao wanaolaani ufisadi wakiwa ndani ya CCM wanatenda kwa dhati au ndio kujiunga na jamii? Watawezaje kufumua mfumo uliowalea kwa miaka yote tena wakiwa kimya?
Kumpata mgombea wa CCM asiye na unasaba na Ufisadi haiwezekani. Mtu msafi kabisa ndani ya CCM bado ni mchafu wa ufisadi. Sababu kubwa ni moja, nani amesimama na kuisema serikali ya CCM kuhusu ufisadi ? Hakuna jibu, wote wanautumikia mfumo, na itakuwa ajabu akitokea mtu na kutuambia tofauti
Kuhusu wananchi, taratibu wanatambua mabadiliko ni muhimu. Kwanza, walikuwa na hofu ya amani kwavile mfumo wa vyama vingi haukuwepo. Tulianza na wabunge 5 nadhani, taratibu wameongezeka.
Kasi ya kuongezeka si ya kuridhisha, hata hivyo lazima tukubali kuwa mazingira yaliyotengenezwa na CCM hayawezi kutoa fursa
Jukumu la mabadiliko limerudi kwa wananchi. Unaona serikali za mitaa watu 12 huko kijijini wameshika bendera wanashangilia ushindi wa kitongoji kwa wapinzani. Hii maana yake wananchi wana kiu ya mbadiliko, wapo tayari. Swali, je wanakuwa motivated kiasi cha kutosha?
Hapa ndipo wapinzani wanapokuwa slow kama ulivyosema. Tunajua hakuna uwezekano wa kupata haki na usawa. Ni wajibu wa wapinzani kuhakikisha wanatafuta njia ya kuvunja mgongo wa ngamia
Ndio maana nilisema ziwepo plan A1 na A2
A1 ni kupata kiongozi wa dola. Hilo linataka ushindi wa Chiluba ambao Kenneth Kaunda hakuweza kuufanyia kazi maabara. Ilikuwa haiwezekani.
A2 kutokana na mwamko wa A1 upo uwezekano wa kufikia idadi ya wabunge itakayoondoa 2/3 ya ccm.
Watu hawafahamu kuwa CCM inatumia sheria 'haramu'' kutokana na 2/3 tu. Mifano tumeiona. Ikiwezekana kuvunja 2/3, hapo utakuwa mwanzo wa kubadili mwelekeo wa nchi.
CCM wanajua kuwa uwezekano wa kupoteza 2/3 ni mkubwa sana. Ndio maana wametangaza majimbo mapya kupitia ytawi lao la ''tume ya uchaguzi'' Hizi ni mbinu za woga, wapinzani wanatakiwa wajue hilo. Kazi uya upinzani ilikuwa ku take advantage hiyo kuongeza wabunge. Wasilalamike kuongezwa majimbo, bali wapiganie kutwaa majimbo hayo
Je, wapinzani wanaweza. Yes, inawezekana kama ilivyotokea kwingine. Muhimu ni kuwa na mbinu na mikakati. Moja, kuhamasisha wananchi kupiga kura, pili, kuwafikia na kuwapa ujumbe unaolingana na hali ya maisha yakiwemo majawabu, tatu, juwaweka CCM katika 'defence zone''
Leo wapinzani hawana mkakati na kule wasikofanikiwa. Hakuna dalili kama wana mkakati.
Wananchi wanawasubiri, tatizo hawana mbinu za kuwafikia.
Mbinu mojawapo, viongozi wa UKAWA wasambae kila mahali wakiwa na ujumbe na si kelele.
Viongozi wa UKAWA washiriki kama wabunge ili kuongoza nguvu kwa kutumia umaarufu wao
Waende ngazi za chini na vijijini kuwafikia wananchi. Wahamasishe kulinda kura! yes, inawezekana mbona serikali za mitaa CCM walishindwa kuiba?
Endapo uchaguzi wa serikali za mitaa CCM imepoteza kwa 20% ikiwa na kila sababu ya kushinda kwa hila na mbinu, ni dalili kuwa huko chini wamehasika!
cc
MJINI CHAI
ZeMarcopolo ishu ya ufisadi hisio na ushahidi itabaki kua majungu tu,kama ni tuuma za ufisadi hakuna ambae hajaguswa,Kuanzia CHAMA kiongozi mpaka vyama vya upinzani kuna ufisadi,ndio mana nasema tatizo la ufisadi si la CHAMA, ni watu(Wanachama),ukienda upinzani watu wanachota ruzuku(wanakula urefu wa kamba yao),huku CHAMA kiongozi ufisadi upo katika serikali,sio katika CHAMA, na baadhi ya watendaji hawana CHAMA,mfano yule CEO wa Vodacom,sio CCM, alioshirikiana ni watendaji wa serikali ambao ndani yake wapo wasiokua na vyama.
NB.CCM ikipata vijana 50 level Mwigullu Nchemba katika ubunge,30 level ya Deo Filukunjombe,20 level Ester Bullaya jumla wakawa 100 pale bungeni CCM haitafanya kazi kwa mazoea kuanzia katika CHAMA mpaka Serikalini,upinzani utokuwa na kazi tena
Tuhuma ambazo hazichukuliwi hatua yoyote ile na vyombo vya dola vinavyohusika hatuwezi kuziita ni majungu!ZeMarcopolo ishu ya ufisadi hisio na ushahidi itabaki kua majungu tu,kama ni tuuma za ufisadi hakuna ambae hajaguswa,Kuanzia CHAMA kiongozi mpaka vyama vya upinzani kuna ufisadi,ndio mana nasema tatizo la ufisadi si la CHAMA, ni watu(Wanachama),ukienda upinzani watu wanachota ruzuku(wanakula urefu wa kamba yao),huku CHAMA kiongozi ufisadi upo katika serikali,sio katika CHAMA, na baadhi ya watendaji hawana CHAMA,mfano yule CEO wa Vodacom,sio CCM, alioshirikiana ni watendaji wa serikali ambao ndani yake wapo wasiokua na vyama.
NB.CCM ikipata vijana 50 level Mwigullu Nchemba katika ubunge,30 level ya Deo Filukunjombe,20 level Ester Bullaya jumla wakawa 100 pale bungeni CCM haitafanya kazi kwa mazoea kuanzia katika CHAMA mpaka Serikalini,upinzani utokuwa na kazi tena
ZeMarcopolo
Marekani inawatu milioni 300, wanaochukua fomu katika vyama vyote, hawazidi wagombe wa CCM.
Uingereza ina watu milioni 80. Wanaochukua fomu hawazidi idadi ya wagombea wa CCM.
Kwamba, Tanzania ina watu 45Milioni ina justify kuchukua fomu kwa mamia, haina mashiko.
Pili,wakatiwa Mwinyi waliochukua fomu hawakuzidi 10.
Wakati Kikwete anagombea hawakuzidi 10 kwa ccm,if memory serves me right
Miaka 10 iliyopita CCM ilikuwa na watu hawa, Dr Salim, SindeWarioba, CD, Msuya, JS Malecela.
Hawa walikuwa na sifa za uongozi kimaadili,kiuzoefu na kitaaluma.
Haina maana hakukuwepo na watu wenye nia, walikuwepo, suala ni kuwa, nani alijipima kupokea kijiti kutoka kwa Nyerere anayekaribia hao?
Katika vifaa hivyo vitano, hakuna aliyekuwa Rais. Hao ndio waliomchagua na kumsaidia Rais kwa kutumia busara zao.
Mwinyi alichaguliwa kwa mtazamo wa busara tukijua alikuwa makamu na suala zima la muungano
Kinachotokea sasa hivi, kwanza, ni udhaifu wa uongozi.
Wanaojitokeza ni wasaidizi wakuu wa Rais aliyepo na ndio wanatuletea kauli mbiuy a rushwa na ufisadi.
Maana yake wanauona udhaifu uliopo. Wengine wanasema elimu au kilimo kwanza. Wanachokifanya ni ku explore weakness ya kiongozi waliomsaidia.
Kila mmoja anaona angeweza kufanya vizuri zaidi. Ni udhaifu tu.
Kundi lingine linatafuta umaarufu. Tumeeleza huko nyuma,Kuga Mziray alihutubia viti.
BMLK alikuwepo kama mpinzani kwasababu uwepo wake ulishaonekana. Hawa wa CCM wanatafuta nafasi tu.
Hoja kuwa ni kupanuka kwa demokrasia ni kweli kwasababu demokrasia ni kitu cha ajabu kidogo.
Inaweza kukupa matokeo mazuri au mabaya.
DemokrasiA ilimtengeneza Lady Thatcher miaka 11ikamuondoa kwa aibu siku moja.
Demokrasis ilimtengeneza Ronald Regan akajenga uchumi waMarekani, ikamleta G.Bush , recession ikaingia
Kupanuka kwa demokrasia kumetupatia Kibajaji wa Dodoma na kupitia kwake tumepata wazo la kuondoa picha za wanyama,' thamani ya pesa yetu ipande''
Bandiko linalofuata tutakuonyesha udhaifu wa uongozi wa CCM unaoleta wingu la watia nia.
Jinsi EL anavyoiyumbisha CCM bila sababu za msingina na jinsi CCM inavyomugopa
Tusemezane
| | Political Movement | Political Party |
| Orientation | Cause | Issues |
| Level of Operations | Regime | Government |
| Main Arena of Operation | Society | Parliament |
| Method of Operation | Mobilization | Persuasion |
| Member Orientation | Diffuse | Specific |
| Claims of Resources | No formal limits | Constrained by Law |
Mchambuzi sijui kama ni makusudi au bahati mbaya lakini kuna ukweli mkubwa umeuacha bila kusema.Uchaguzi wa Oktoba 2015 utakuwa ni uchaguzi wa kumi na moja wa rais na wabunge tangia uhuru. Tangia uhuru, Chaguzi Sita zilifanyika wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa (TANU/CCM), na chaguzi nne zilifanyika chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uchaguzi wa mwaka huu (2015) utakuwa ni uchaguzi wa tano chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Suala la kujadili ni je, kwa kipindi chote hiki, msukumo wa wananchi kujitokeza kupiga kura umekuwa ni kwa matarajio yepi?
Tangia uhuru (1961), chaguzi kuu zimekuwa kama ifuatavyo:
1. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Uchaguzi chini wa mfumo wa chama kimoja ambapo voters turn out ilikuwa 77%.
2. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1970 chini ya mfumo wa chama kimoja, voters turnout was 72%
3. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975 - chama kimoja, turnout was 81%
4. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1980 Chama kimoja, turnout was 75%
5. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985 Chama kimoja, turnout was 75%
6. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1990 Chama kimoja, turnout was 74%
7. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 Vyama vingi, turnout was 77%
8. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 Vyama vingi turnout was 84% (record breaking highest in history)
9. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 vyama vingi turnout was 72%
10. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Vyama vingi turnout was 42% (record breaking Lowest in history)
11. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ??????????