2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

Jamani hili ni jukwaa la GT hivyo naomba tuwe serious kidogo tunapoongelea hatma ya nchi, tuache utani na kuleta mambo yasiyo na maana. Kwa nini nasema hivyo? Nimeona kuna watu wanaleta ulinganisho wa watangaza nia CCM na kuwafananisha watangaza nia wa vyama vya Marekani. Kweli pamoja na akili zetu timamu tunaanza kulinganisha siasa za Marekani na hizi zetu za Bongo!

Hivi leo tumebakiza siku 138 (sawa na miezi minne na siku 18) tuingie katika Uchaguzi Mkuu. Hadi sasa kitaifa hatujui hata kwa kukadiria idadi ya wapiga kura, idadi ya wagombea na hata idadi ya vyama vitakavyoshiriki. Kichama hatujui idadi ya wagombea katika ngazi zote; Uraisi, ubunge na hata Udiwani, are we really serious? Is there any right thinking individual who can understand us or even condone what we are doing?

Halafu tunajilinganisha na Marekani. Marekani bado siku 500 (sawa na mwaka moja, miezi minne na siku 16) hadi wafanye Uchaguzi wao Mkuu. Kitaifa tayari wamekadiria idadi ya wapiga kura (ambao ni mara tatu ya idadi ya Watanzania wote kuanzia vichanga hadi vikongwe) Tayari mchakato wa kupata wagombea katika nafasi mbali mbali umepamba moto na kitakachotoa mchujo kwa wagombea ni wanavyokubalika kwa kupigiwa kura na wananchi.

Mtangaza nia Marekani akijipima akaona hafui dafu, anajiondoa mwenyewe na kumuachia anayekubalika zaidi aendelee. Hakuna kikao kinachokaa na kuamua yupi agombee na yupi jina lake likatwe. Kama anatokea mwenye nia na haungi mkono msimamo wa chama anao uhuru wa kujitosa kama mgombea binafsi. Katika misingi hii kweli inaingia akilini mtu kufikia hatua ya kujaribu kulinganisha ndimu na mananasi? Kwa vituko hatujambo!

Kila Mmarekani ana uhuru wa kujitosa katika kinyang'anyiro isipokuwa pale tu kwamba hana sifa na hizo sifa haziishii tu kwenye siasa, ni kwenye nyanja zote za maisha. Kwamba wakati zimebaki miezi minne na ndio idadi ya watangaza nia inaongezeka ni kichekesho lakini kwa Tanzania haishangazi hata kidogo. Katika jamii ambamo wahalifu wanaweza kutetewa na kupewa uongozi bila wananchi kusema hapana, Watanzania hawana mfano.
 
Ili bandiko lako ungemtumia PM Nguruvi3 maana yeye ndio alianza kulinganisha,na kushangaa,watu wakachimbua wakaja kusahisha,yeye hapendi kusahishwa,maana mnakasha wake
 
Last edited by a moderator:

Mkuu umemjibu vyema Mag3.

Shukrani.
 
Mag3:

Siasa ni mchezo wa taifa wa Tanzania. Tanzanian people take pride when they engage in unproductive and endless debates.

Kwa maoni yangu binafsi, mfumo wa kisiasa umeundwa hili kulaghai ulimwengu kuwa Tanzania nayo inajishughulisha kwenye demokrasia. Mpaka pale watu watakapojua kuwa demokrasia ni kwa faida yao wenyewe na sio kuwafurahisha wahisani au kuleta ushabiki wa michezo ndipo watu watakapokuwa serious.
 
Tuendelee...
Mchakato wa kutafuta mgombea wa CCM, ambaye pundits wanatoa nafasi kubwa kwa mbali kuwa ndiye atakayekuwa Rais wa awamu ya tano, unachukua sura mpya kila kukicha.

Mpaka jana top five ilikuwa Mwandosya, Membe, Bilal , Sitta na Pinda in random order. Tukio la Jaji Augustino Ramadhani kuchukua fomu linalazimisha mabadiliko kwenye order hiyo ya top 5. Kuna haja ya nguli huyu wa mhimili wa mahakama kuingia top 5.

Hata hivyo kuna mambo ya kuyaangalia;
1. Mkuu wa mahakama anapostaafu na kuvaa shati la kijani watu wanaweza kujiuliza kama huduma za kimahakama hakuziendesha kwa maslahi ya rangi hiyo.

2. Jaji Ramadhani alikuwa kiongozi wa tume za uchaguzi NEC na ZEC kwa nyakati tofauti. Je , ni kweli kuwa tume hizi ni huru. Je , tuna uhakika kuwa mgombea huyu hakuzisuka tume katika mfumo wa kumpatia ushindi. Ni lini alianza kuota Urais, ametumiaje nafasi hiyo kutimiza ndoto ya Urais.
3. Mgombea Urais kwa CCM ni de facto mgombea uenyekiti wa CCM. Nini kimemsukuma jaji ambaye hajawahi hushiriki nafasi yoyote ya uongozi wa chama kutaka kushika nafasi ya uongozi mkuu?

Jaji Ramadhan anafaa kuwa Rais, hata hivyo kugombea kwake kunaacha maswali hayo ambayo akishinda sio lazima yajibiwe ila akishindwa, yataendelea kumpa sura tofauti na aliyokuwa nayo kabla ya kugombea.

Vilevile ni muhimu kukumbushana kuwa Rais ajaye ndio mwenyekiti wa CCM ajaye. Kazi hii ya uenyekiti jaji wetu huyu hataiweza. Iwapo atapitishwa, kunaweza kuonekana haja ya kubadili kanuni ili Rais asiwe mwenyekiti wa CCM.

Tuiombee nchi yetu iendelee kuwa na amani...
 
Kwanza, kufikiria kuwa Rais atatoka CCM ni kuendelea kukubali maradhi yaliyotufikisha hapa miaka 50 sasa. Ni lazima wananchi wajiulize, kufanya jambo lile lile kwa muda mrefu bila matokeo tofauti kunatusaidia?

Je, wananchi wa maeneo mengine waliovunja mwiko kama Zambia na Kenya, ni bora au dhaifu kuliko sisi?
Je, tutaendelea kuishi na serikali iliyojaa ulaghai, isiyojibu hoja za nyakati ikiwemo umasikini, maradhi na ujinga hadi lini?

Na mfano mzuri ni huu wa Jaji. Hatutegemei ikitokea akawa Rais, Jaji anaweza kufanya jambo tofauti na mfumo uliomlea katika maisha ya siri hadi sasa. Kwamba, alikuwa mtumishi wa umma kama Jaji na mkuu wa tume ya uchaguzi na sasa anafikiriwa kuhudumia mfumo ule ule

Hii ni picha nzuri kuwa, hakuna njia ya kufumiua mfumo uliopo isippokuwa moja tu, kubadili mfumo

Je, wananchi wanaweza? Ndiyo wakiamua, hapa wakikumbatia miaka 50
 
Kiongozi, swala la CCM kuendelea kubaki madarakani sio swala la kuamini au kutokuamini, it is a mathematical fact. We can choose to be angry about it, but that won't change the statistics.
 
Mchakato wa kutafuta mgombea wa CCM, ambaye pundits wanatoa nafasi kubwa kwa mbali kuwa ndiye atakayekuwa Rais wa awamu ya tano, unachukua sura mpya kila kukicha.

Mpaka jana top five ilikuwa Mwandosya, Membe, Bilal , Sitta na Pinda in random order. Tukio la Jaji Augustino Ramadhani kuchukua fomu linalazimisha mabadiliko kwenye order hiyo ya top 5. Kuna haja ya nguli huyu wa mhimili wa mahakama kuingia top 5.

Hata hivyo kuna mambo ya kuyaangalia;
1. Mkuu wa mahakama anapostaafu na kuvaa shati la kijani watu wanaweza kujiuliza kama huduma za kimahakama hakuziendesha kwa maslahi ya rangi hiyo.

2. Jaji Ramadhani alikuwa kiongozi wa tume za uchaguzi NEC na ZEC kwa nyakati tofauti. Je , ni kweli kuwa tume hizi ni huru. Je , tuna uhakika kuwa mgombea huyu hakuzisuka tume katika mfumo wa kumpatia ushindi. Ni lini alianza kuota Urais, ametumiaje nafasi hiyo kutimiza ndoto ya Urais.
3. Mgombea Urais kwa CCM ni de facto mgombea uenyekiti wa CCM. Nini kimemsukuma jaji ambaye hajawahi hushiriki nafasi yoyote ya uongozi wa chama kutaka kushika nafasi ya uongozi mkuu?

Jaji Ramadhan anafaa kuwa Rais, hata hivyo kugombea kwake kunaacha maswali hayo ambayo akishinda sio lazima yajibiwe ila akishindwa, yataendelea kumpa sura tofauti na aliyokuwa nayo kabla ya kugombea.

Vilevile ni muhimu kukumbushana kuwa Rais ajaye ndio mwenyekiti wa CCM ajaye. Kazi hii ya uenyekiti jaji wetu huyu hataiweza. Iwapo atapitishwa, kunaweza kuonekana haja ya kubadili kanuni ili Rais asiwe mwenyekiti wa CCM.

Tuiombee nchi yetu iendelee kuwa na amani...

umeniwahi tu mkuu kuhusu hili jambo, nimelijadili kdg kwenye uzi unauhusu mgombea huyu kuchukua fom kule jukwaa la siasa,
binafsi nimeshangazwa sana na kuhuzunika na uamuzi wake na hasa kwa nafasi ambazo amewahi kushik kwenye taifa, kimsingi utumishi wake ulikua ni wa kuwafaa na kuwaamua watu wote sawa, sasa kwa yeye kugombea kwenye chama cha siasa kuna kuna leta maswali na sintofaham nyingi sana.

kimsingi mm nina mtazamo tofauti na wengu, pamoja na kuheshimu sana demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa, lakini kuna baadhi ya nyadhifa kwenye system za nchi mtu akiwa amezitumikia si vem kabisa kujihusisha na siasa au umakundi wowote utakaomdefine tofauti kwenye jamii anayoihudumua au aliyoihudumia.

utumishi kama Ukuu wa majeshi, Majaji, wakuu wa inteligency, CAG, wakuu wa polisi, wakuu au wasimamizi wa uchaguzi na hata central bank governors or financial inteligeng system, hawa wakati na baada ya utumishi wao sio vema na sio busara wakajihusisha na siasa kwa namna yoyote ile maana wata rise a lot of questions including conflict of interest on how wanadeal na maamuzi kwa jamii au walitumika vipi, ili kulinda uadilifu wao na heshima zao, better wakikubali hizo posts wajue siasa kwao mwiko na kwenye taifa nafasi pekee itakayowafaa ni kuwa washauri sio wanasiasa.

inaumiza sana kuona baadhi ya watu kama wakuu wa usalama kwenye nchi eti nao ni wagombea wa siasa, unajiuliza why?? Inamaana walipokua watumishi walikua wanatumikia siasa (chama) au Taifa, utasikia mtu alikua mkuu wa polisi wa nchi au mkoa (IGP or RPC) eti anaenda kugombea ubunge, unajiuliza alikosa nini huyu katika kututumikia mpaka aendelee tena kutaka ubunge? Au mkuu wa majeshi mstaafu anaingia kwenye mchakato wa ubunge kwenye chama cha siasa unabaki kushangaa sana anatafuta nn tena?

Ni hitimishe kwa kusema hata kama hawa wastaafu walitumikia taifa kwa utumishi uliotukuka kiasi gani, si vema kujihusisha na siasa kwa namna yoyote ile hasa kipindi hiki cha democrasia ya vyama vingi, inaleta sintofaham nyingi sana. Atleast wakati wa chama kimoja sawa maana chama na serikali waliku kitu kimoja sio kipindi hiki. ni hayo kwa sasa, tusemezane kwa mitazamo yenu wadau
 
Ni kweli.

Nchi yetu inajifunza as it grows. Wapinzani wetu wamekosa focus. Wanaendeshwa zaidi na matukio bila focus. Juzi walikuwa wanazunguka wakitangaza kuwa Kikwete ana mpango wa kubaki madarakani baada ya muda wake kuisha. Baseless claims zinawapotezea muda na nguvu.

Haya ni mambo ambayo Wapinzani walitakiwa kuyashughulikia kabla ya kukimbilia kugombea urais. Hata kama wakuu hawa wataruhisiwa kugombea lakini ingefaa kuwe na utaratibu wa kudeclare their conflict of interest. Hii itasaidia kwenye mambo fulani wakakubali kuwaachia wengine waamue. Kwa mfano kesi yenye maslahi na CCM haikufaa apewe Agustino Ramadhani iwapo kuna jaji Mwingine.

Kwa mfano Marekani, Rais George Bush senior alikuwa director wa CIA. Lakini alifahamika kuwa ni Republican katika kipindi chake chote. General David Petraeus naye ni Republican na alitajwa kuwa atagombea Urais, akakanusha. Pamoja na kwamba ni Republican lakini Obama alimteua kuwa Director wa CIA kwa vile conflict of interest zake ziko declared.

Kwahiyo viongozi wasiorodheshe mali tu, waorodheshe pia uhusiano wao na vyama vya siasa.
 
Thanks mkuu hoja kuntu,
Soon nitarejea tujadili pamoja hoja zako kwa kirefu, japo kwa kifupi uwanja wa mapambano kwa siasa za Tanzania haupo balanced kiasi cha kulazimisha wakuu wengi wa utumishi wa uma kuwa na kadi za chama mfukoni, wakimaliza tu utumishi wao utakuta wanakuambia mm nilikua mwanachama siku nyingi bila hata kudeclear interest kipindi cha utumishi wao.
 
Mkuu JokaKuu na wadau wengine wa jukwaa hili. Nashauri mada zote zinazohusu uchaguzi tuziweke kwenye thread hii iliyobeba heading general ya uchaguzi. Tukifanya hivyo itakuwa rahisi kufuatilia nani alisema nini baada ya uchaguzi.

Uchaguzi ukiisha wadau wanaweza kuipitia thread yote na kutoa tathmini ambayo inaweza kutuongoza kwenye mijadala inayofuata.

Thanks...
 
Last edited by a moderator:
Binafsi naamini kabisa kwamba Tanzania hatujawa tayari kufanya uchaguzi wa mwaka huu.... unfortunately, this has been crafted by a group of people waliokua na intention ya kuvuruga uchaguzi kwa faida yao

Mbaya zaidi... wameamua hadi kuvuruga mfumo wa uchaguzi ndani ya chama tawala kuhakikisha wanafanikiwa
 
..matatizo yote yanayotokea yawe ni chachu kwa vyama vya upinzani kufanya kazi kwa ari kubwa zaidi.

..something gotta give in this year. ama bunge lichukuliwe na ukawa, au raisi atoke ukawa, au vyote.

..we can not afford kushindwa mwaka huu.

cc Chademakwanza, Ben Saanane, Mohamedi Mtoi,, Mag3
 
CCMINAPOTAFUTA MGMBEA BAADA YA MIAKA 50

MAKUNDI NA WINGI WA WAGOMBEA NI ''KURA YA KUKOSA IMANI''

EL HANA NGUVU INAYOFIKIRIWA

Miaka 50ya kuongoza,CCM inajikuta katika wakati mgumu kupata mgombea.
Kwa chama kikongwe, hilo lisingekuwa tatizo. Pengine wana CCM wangekuwa na wagombea 5 tu wa kufikiriwa.

Utitiri wa wagombea una sababu tulizoeleza huko nyuma.
Kwahali ilivyo, makundi yanayojitojeza kutafuta mgombea wao yapo matatu

Kwanza, lile linalotaka kulinda mfumo uliopo liendeleze hujuma.
Kundi hili lina vigogo wengine wakiwa wafanyabiashara. Ni lile lililoathirika na tuhuma za ufisadi na wizi.

Kundi la pili,ni lile linalotafuta ‘mtu wao' ili kujiweka sawa katika nafasi za uongozi kama uwaziri, ubalozi n.k.
Ni kundi linaloangalia masilahi

Kundi la tatu, ni lile linaloona CCM imepoteza hadhi ya chama na sasa ni NGO.
Linataka kurudisha heshima yake. Hili linaweka mtu wao kama ‘veto' kuzuia makundi mawili hapo juu

Katika makundi hayo, lile la kwanza linaloongozwa na EL linaonekana kuwa na nguvu kiasi cha kuivuruga CCM.

Kiuhalisia kundi hili linataka jambo moja tu, jina la mgombea wao liingie katika NEC na kisha mkutano mkuu

Kundi hili halina ushawishi wa kisiasa kama inavyoonekana.Lina ushawishi wa rasilimali.

Limeachwa kiasi cha ‘kununua' sehemu kubwa ya wanachama.
Kwa mfano, wenyeviti wa mikoa ni wapiga debe. Wajumbe wa NEC wameshawekwa ‘sawa'

Kundi la kwanza lina uwezo wa kununua wanachama na wapigadebe, haliwezi kununuliwa na wanachama.
Kwa maana kuwa kiongozi wao hana ushawishi wa kisera, wala mvuto ‘charisma' achilia mbali makando kando ya kashfa

Mgombea akitemwa, kazi ya pesa itakuwa imefikia hatma yake.
‘Wafanyakazi'watahamia makundi mengine na kumwacha mgombea akisononeka
Kwa maana kuwa kuna mkataba wa kikazi na si wa kiushawishi,sera au kisiasa.

Kwavile CCM ya leo inaongozwa kwa masilahi hakuna ‘think tank' inayoweza kubaini ukweli huu.

Hicho ndicho chanzo cha CCM kubabaika kuhusu nguvu za mgombea fulani.

Ukweli utabaki, mgombe huyo hana nguvu nje yaCCM , kwanini CCM imuone ana nguvu kuliko chama?
Jibu ni rahisi, udhaifu wa CCM na serikali yake

Kutokana na udhaifu huo kuna nafasi muhimu sana kwawapinzani ambayo wakiutumia vema ima watachukua mhimili mmoja wa dola, au dola au kudhibiti sehemu muhimu za utawala kama alivyosema JokaKuu hapo juu

Inaendelea
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea..

Mtifuano ndani ya CCM unahusisha makundi mawili makuu.
Lile lenye mshiko na rasilimali , washiriki wake wengi wanatuhuma za wazi zaufisadi na wizi

Pili, Kundi linalotaka chama kirudi katika mstari wake.

Kundi la pili( masilahi) halina nguvu. Linaweza kujiunga na kambi yoyote ilimradi tu linahakikishiwa masilahi salama.

TUANGALIE KWA NADHARIA TU

(1)Kama mgombea atatoka kundi la kwanza (EL) watu wanaomzunguka wana kashfa nzito za taifa hili.
Mwaziri na viongozi wote waliofukuzwa au kujiuzulu.

CCM itapata tabu kumuuza mgombea wake, na kampeni nzima itahusisha kashfa badala ya sera

Wapinzani wakijipanga, itakuwa fursa nzuri kuihusisha CCM na kundi hilo. Muhimu ni wao kujenga hoja zenye mashiko

(2)Mgombea akitoka kundi la tatu(linalotaka kurejesha CCM yazamani) kazi itakuwa kuwauza wagombea wake.
Mfano, aliyekuwa Jaji mkuu, hakuna anayejua anasimama wapi katika masuala ya kisiasa na kijamii.
Likimchukua Baloziwa UN, hoja itakuwa, ana ufahamu gani wa masuala ya ndani ya nchi

Nayo pia ni nafasi nzuri ya wapinzani kujenga hoja kwa kutumia umaarufu wao kisiasa katika siasa za ndani, na uelewa wao wa mahitajiya Watanzania kwa wakati

Wapinzania waelewe, CCM katika hali yoyote ina nguvu.Uwanja wa mchezo haupo sawa.
CCM ina msaada wa vyombo na taasisi za dola. Hata goli la mkono litahesabiwa kama wanavyo jinasibu

Wapinzani wanachotakiwa ni kuhakikisha pale wanapotaraji kushinda, washinde kwa kishindo.

Pale penye mashaka walete upinzani wa nguvu.Hilo litawezekana kama watakuwa na mkakati.
Moja ya mikakati ni kupata makundi muhimu, kuhakikisha yanapiga kura

1 Kundi la vijana limepoteza Imani na CCM hasa maeneo ya mijini.
Vijana waliobaki CCM ni wale wanaoamini chama hicho kitawainua binafasina si wananchi

2. Kundi la raia wa kawaida. Hili limeanza kupata mwamko na hasa upande wa wanaume.
Mabadiliko ya kijamii hasa katika elimu na ufahamu limeligawa kundi hili baina ya wapinzani na chama tawala

3 Kundi la akina mama. Hili lina watu wengi, lina shamrashamra zinazoleta ushawishi.
Ni kundi tiifu kwa CCM hata kama ndilo waathirikawakubwa wa sera mbovu za CCM

Tatizo linaloonekana kwa wapinzani ni kutokuwa na nguvu au mbadala wa kushindana na kundi la wanawake CCM.

Ukiangalia vyama vya upinzani ni kama vile taasisi za akina mama hazipo.
Kama kuna eneo wapinzani wanatatizo, hili ni mojawapo.

Wapi taasisi za akina mama wa CUF, Chadema, NCCR? Ushawishiwao upo wapi?

Eneo lingine a mkakati ni taasisi za elimu hasa ya juu

Itaendelea…
 
TAASISI ZA ELIMU YA JUU

CCM imepoteza ushawishi. Ni mahali wapinzani wana nafasi nzuri. Taasisi zipo mijini na ushawishi katika jamii zinazozunguka ni mkubwa

CCM wanatambua hilo na watafanya kila mbinu kuhakikisha taasisi hazileti athari zinazotarajiwa.

Mwaka 2010 serikali iliahirisha kwamuda mwaka wa masomo hadi uchaguzi upite.
Athari zake zilikuwa wanafunzi kutopiga kura kwani walikojiandikisha ni vyuoni na wanapoishi ni majimboni

Makakati huo unaweza kurudiwa tena. Wapinzani hawahitaji kupingana na chaguo la CCM.
Iwe kupiga kura vyuoni au katika majimbo yao. Hali yoyote ile inawapa unafuu

Kwa mfano, kufungwa kwa vyuo mwaka 2010 kulisaidia wanafunzi kurudi makwao na kuwa makada wa upinzani . Tuliona matokeo ya kushangaza kutoka maeneo kama Shinyanga na kwingeneko wapinzani walipopata majimbo ya ubunge

Katika kpindi hiki CCM ilipopoteza serikali za mitaa, kurud ikwa vijana kutaleta hamasa na kuwa msaada kwa wapinzani

CCM ikiamua wabaki vyuoni bado utakuwa ni msaada kwa wapinzani.

Tatizo ni moja, je wanafunzi wamejiandikisha katika BVR ? za maeneo gani.
Hatujui mfumo huo unaruhusu kujiandikisha eneo moja na kuweza kupiga kura eneo jingine.

Kusudio la BVR ni kujiandikisha na kupiga kura bila kughushi au kuongeza idadi.
Je, vyuo vitafungwa au utaratibu upi utatumika?

Kwa mwendo huu wa BVR kutumika kama computer za kawaida na kisha majina kuingizwa katika data base na tume kwa wakati wao na namna zao,kuna haja ya wapinzani kufungua macho.

MAENEO SALAMA KWA CCM

Yapo maeneo salama kwa CCM kama vile mikoa ya Tanga,Morogoro, Tabora, Pwani

Mikoa hiyo imekuwa mitiifu kwa kuipa CCM kura. CCM wanajua hilo na hawapotezi muda kufanya kampeni.

Wapinzani wanaonekana kutojua kuwa juhudi zao zilenge kuwaweka CCM mchaka mchaka.

Kwa maneno mengine wapinzani wanalinda majimbo yao (defensive) badala ya kushambulia maeneo wasio nauwakilishi( offensive)

Kama lipo eneo wapinzani wanatkiwa kuliangalia ni hili la maeneo salama ya CCM.

Kinyume chake, eneo hilo litawaumiza katika ubunge na Urais.

Swali la kuwauliza wapinzani, ni kipi wanachoshindwa kuwashawishi wananchiwa maeneo hayo?

Tusemezane
 
Baada ya dhuluma ambazo wapinzani wanafanyiwa kwenye chaguzi nyingi hasa zilizopita wameshindwa kukaa na kutatua hayo matatizo.

Kwanza ni kushinikiza kuwa na tume ya huru na haki. Hapa ndo sehemu muhimu sana ambayo wapinzani wanakumbuka wakati wanaingia kwenye uchaguzi ili hali walikuwa ba miaka 5 ya kujipanga na kutatua hili tatizo.

Pili kuhakikisha vyombo muhimu vya maamuzi havipo chini ya CCM kama mahakama. Sheria inasema rais akishatangazwa hakuna kupinga matokeo. Hili ni kosa kubwa sana, kwasababu mahakama na tume watatumia huu mwanya kuwakamdamiza wapinzani.

Tatu, vyombo vya ulinzi, wapinzani walitakiwa wanahakikisha polisi wanasimamia haki kwa vyama vyote na si kukaa kusubiri muujiza wa chama tawala kuacha kuvitumia kukandamiza wapinzani.
 
..tume ya uchaguzi na jeshi la polisi hawawezi kubadilika bila kuwaondoa CCM madarakani.

..wanachopaswa kufanya wapinzani ni kuhakikisha wanapata ushindi wa KISHINDO ili kuondoka uwezekano wa tume kuchakachua matokeo.

..wagombea wote wa UKAWA wahakikishe wanapata ushindi kama wa Joshua Nassari na tume itakuwa haina jinsi ila kutangaza mshindi halali.

cc Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
YANAYOTOKEA DODOMA SI UONEVU

NI UJUMBE KWA WATANZANIA UIWSUKUMA KUKUMBTIA MABADLIKO

HOJA SI KUONEWA, NI KUTAFSIRI UJUMBE HUO MZITO ULIOWFIKIA KWA NJIA YA BUNGE

Bunge limeingiwa na sintofahamu baada ya wabunge wa UKAWA kupinga miswada ya dharura inayopelekwa bungeni

Hoja kubwa ya UKAWA ni kukiukwa kwa taratibu za uwasilishajiwa miswada kwa njia ya dharura, kukiukwa kwa taratibu za kujadili miswada na muda mdogo wa kujadili vifungu zaidi ya 2000 vinavyohusu nyaraka muhimu kama hiyo

Kwa mtazamo wetu, hakuna sababu yoyote ya hati ya dharura.Matatizo ya gesi na mafuta yapo siku nyingi.
Hayahitaji kujadiliwa kimchezo mchezo kwani hiyo ndiyo dira na muongozo wa mikataba mingi itakayofuata.

Wananchi wanapaswa kushirikishwa kujua nini kinaendelea katika mustakabali wa rasiilimali zao.
Sheria zitawagusa na kugusa masilahiyao, hakuna sababu ya kufanya mchezo wa kitoto

Spika ametumia maguvu k, huku akitaka UKAWA watoke ili wapitishe miswaada kwa njia wanazotaka wao(CCM)

Kwa wabunge wa CCM , masilahi yao ya kwanza ni kutafuta nafasi za kuteuliwa si kutetea masilahi ya nchi.
Ndio maana wapo tayari kukubali chochote bila kukisoma au kutafakari.

Wananchi wanapaswa kuona kile tunachokisema kila siku.Kwamba, nguvu ya ushawishi ya CCM imekwisha.
Hawana sera wala ushawishi kwaj amii. Nguvu yao imebaki sehemu moja, bungeni. Huko ndiko wanatumia sheria kuhalalalisha hata kilicho haramu kwa kutumia wingi wao

Kitendo cha UKAWA kufukuzwa kina maana moja. Kwamba, CCM itapata 2/3 ya kupitisha miswaada yao.
Hii inaeleza hoja zetu kuwa wananchi wakitaka kuibadili nchi hii na kuondokana na uzezeta na dhalili hii ya miaka 50 yapo maeneo mawili makubwa

Kwanza kubadili dola, pili kumiliki bungeni.
Ni kwa mtazamo huo, ile hoja yetu ya UKAWA kuwa na vipaumbele A1 na A2 inakuwa na nguvu.

Wananchi waone yanayotokea na wajue, wakifanya upuuzi tena CCM itaendele na upuuzi huo huo kwa miaka 5.
Wakati Kenya wakiingia uchumi wa kati sisi tunabaki kundi maskini. Sababu ni hizi hizi za CCM

Ujumbe unaopatikana ni kuwa wananchi zuia CCM bungeni au ondoa dola. Njia ipo kama nia ipo.

Na hili linawagusa sana wananchi wote. Lakini wale wa Mtwarana Lindi waelewe mswada huo hawakushiriki.

Wasije shangaa siku wakihamishwa kupisha wawekezaji kwa sheria hii hii

Jukumu la wananchi wote kwa sasa ni kuwaunga mkono UKAWA waliofukuzwa.

Na hao wabunge wa UKAWA sasa waanze kampeni na agenda ya kwanza ni uhuni huu na jinsi utakavyoangimiza taifa.

Hilo waanze kesho

Tusemezane
 
MSWADA WA GESI NA MAFUTA

UMEHARAKISHWA BILA KUANGALIA ‘FUTURE'

LINI MAFUTA NA GESI YAMEMULIWA KATIKA JICHO LA MUUNGANO?

Mswada wa gesi na mafuta umewasilishwa baada ya wapinzani kuzuiliwa kushiriki

Hakuna anayeweza kueleza kwanini umeharakishwa.Yapo yanayotia shaka yakijenga wingu kubwa mbele ya safari

Mafuta na gesi ni rasilimali zenye matatizo kwa nchi nyingi. Mikataba inahusisha mataifa yenye uwezo wa utafiti na uchimbaji. Mikataba inatakiwa iwe inayoeleweka na iliyochambuliwa kwa kina na uayakinifu

Tanzania ina viashairia kwamba gesi na mafuta zitaleta matatizo mbele ya safari. Tumeona ya mikoa ya kusini

Tunafahamu muungano umetishiwa sana na suala la mafuta na gesi.
Ingawa Zanzibar imeondoa suala hilo , kisheria hakuna nyaraka inayoonyesha si suala la muungano

Kauli ya Rais tu, haiwezi kuwa ni sheria hadi itakapopata uhalali wa kisheria. Hivyo, kwa mujibu wa katiba ya 1977 gesi na mafuta bado ni mambo ya muungano.

Hapo kuna hoja zifuatazo. Je, umejadiliwa katika mukatadha wa kimuungano?
Je, kura za mswada kuamua kuhusu mafuta na gesi zimefikiwa kwa kuzingantia 2/3 ya pande husika?

Maswali zaidi, je, iwapo Zanzibar imeondoa katika muungano, wale wabunge wa Zanzibar katika JMT wanajadili nini?

Maana si suala la muungano kwa mujibu wao. Mijadala yao ni sawa na kuita Wakenya wajadili. Ndivyo livyo sasa

Pamoja na hayo, naibu waziri Nchemba ametangaza kuwepo kwa account mbili chini ya BoT.
Tunafahamu BoT ni ya muungano. Sasa account za kupokea mapato na account za kutunza mapato ni za sehemu gani ya muungano?

Je, account hizo zitahusu gesi na mafuta yatakayopataikana Zanzibar?
Kama jibu ni hapana , ni kwanini rasilimali za upande mmoja (Tanganyika) ndizo zichangie JMT?

Suala la uharaka wa mswada, linaeleza matatizo yaliyo mbele ya safari. Ilibidi kuwepo muafaka wa suala hilo katika ngazi ya muungano. Kwa mwendo ulivyo, maswali yataibuka na ipo siku rasilimali hiyo ikahitimisha muungano

Haieleweki kwanini CCM hawaoni vitu rahisi kama hivyo. Leo Tanganyika wakisema wanaingiliwa na Wazanzibar nani atakana? Leo Watanganyika wakisema rasilimali zao zinatumika kuhudumia muungano watakuwa wamekosea?

Ni kwa msingi huo, wananchi hawapaswi kugawanywa kwa makundi ya uchama.

Duru tunadhani wapinzani wana hoja nzito, mswada huu umeharikishwa bila sababu za maana na kutengeneza mazingira mazuri ya vurugu siku zijazo

Ni wakati wananchi wasimame na kuona hoja za wapinzani

Na pia wananchi waone umuhimu wa mbadiliko ya kisiasa.

Miaka50 ya kuburuzwa bungeni na watu wasio na ufahamu sasa ikomea.

Hivi ni viashiria tu kuwa uchaguzi wa mwaka huu uwe wakuirudisha nchi katika mstari

Kinyume chake tutaendelea kuishi na dude hili lisilo namaono kwa miaka mingi ijayo

Tusemezane
 
Back
Top Bottom