Mkuu wabunge wetu wengi kweli wanasikitisha. Lakini hata Spika mwenyewe ni wa ajabu, nadhani she is the worst speaker we have ever had, na bunge lenyewe ni bunge ambalo ni ovyo kabisa kuliko yote. NIdhamu hakuna, lakini hata umakini kwa kazi haonekani. Ninachoona ni wapinzani kufanya kazi yao kwa kujitahidi sana, lakini walio wengi ni kama wingi wao umewafanya wabweteke.
Tukiangalia tangu 2005 hadi sasa kwa hali ya kawaida CCM ilitakiwa kuaga, lakini nashangaa kuona uchaguzi wa ndani wa CCM unakuwa na umuhimu hata kuliko mengine yote.
Nakubaliana na wewe watanzania tunatakiwa kusemezana zaidi.

Mkuu kuhusu spika, wengine tulielewa ni tatizo tangu mwanzo.
Ilipoletwa hoja ya kuchagua kwakuwa ni mwanamke tukajua nchi imefika pabaya.
Tunajua uwezo wake na yote yanayotokea si bahati mbaya
Hatuwezi kumweka katika kapu moja na akina Sapi, Mang'enya, Msekwa hata kidogo.
Yote haya ni zao la CCM kwa kutumia wingi wao
Wabunge wa CCM wanasikitisha sana. Kuna nyakati nawaangalia na kujisema pembeni, pesa ina taabu.
Hivi mtu anasimamaje bungeni akilalamika kijiji hakina maji, halafu anamalizia kwa kuipongeza serikali inayosikiliza watu, inayoleta maendeleo na kisha kukubaliana na hoja? Kuna chembe fikra kweli
Ndio wale wanaosema pesa imeshuka thamani kwasababu ya kuweka picha. Huyo hana tofauti na yule msomi wa uzamivu anayekalishwa kitako na kuambiwa akubali yote ya chama. Kwamba msimamo wa chama ni mmoja hata kama nchi inauzwa
Hapa ndipo tunawakumbusha wananchi, waulizeni CCM wenye wingi, je kuna lipi la maana wanalifanya?
Waulizeni mswaada wa gesi na mafuta umelenga nini?
Waulizeni, zile pesa za bunge la katiba zilitoka wapi maana ninyi mnaambiwa hakuna fungu
Kama wananchi wa Tanzania wangekuwa na uchungu na maisha yao, wangekuwa na uchungu na vizazi vyao, CCM ingekuwa maktaba muda mrefu sana.
Kwa bahat mbaya na nzuri kwa CCM, Wananchi wanapenda amani na utulivu, yaani wanaibiwa kwa escrow wanasema hewala, wakipandishiwa kodi kufidia escrow wanasema hewala, wakipandishiwa umeme wanasema tumwachie mungu ni kazi yake
Leo lazima warauke saa 10 usiku kupigania mabasi, ukiwaambia kuna zaidi ya trilioni 2 zimepotea kwa wizi wanasema hayo yamepita, mungu anajua.
Kwa kuelewa Watanzania ni watu wa ajabu , kuna wagombea 40 wa CCM.
Kila mmoja anaamini anaweza kuwa rais, si wameona ? sasa nini kinawashinda.
Wanajua mbinu zote za kulaanisha Watanzania, kucheza na maneno, kukimbia kimbia ofisini n.k, kupanga maneno matamu matamu. Wanajua kazi ya Urais haihitaji akili ni ujanja janja tu nchi inaendelea kuwepo
Leo wenzetu wote majiranii, wanakimbia, sisi tumebaki tumechuchumaa . Wananchi hawaoni hili
Dodoma, kinachotokea wananchi, ni wezi kuchagua mwizi mwenzao. Hofu inapaswa kuwa kwa familia za wezi
Nashangaa eti anayedhulumiwa naye ana hofu, kubwa gani la maadui litapewa kiti.
Watanzania imefika mahali mujiulize, mna matatizo gani
Tusemezane jamani