2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

.......
Hapo kuna hoja zifuatazo. Je, umejadiliwa katika mukatadha wa kimuungano?
Je, kura za mswada kuamua kuhusu mafuta na gesi zimefikiwa kwa kuzingantia 2/3 ya pande husika?

Maswali zaidi, je, iwapo Zanzibar imeondoa katika muungano, wale wabunge wa Zanzibar katika JMT wanajadili nini?

Maana si suala la muungano kwa mujibu wao. Mijadala yao ni sawa na kuita Wakenya wajadili. Ndivyo livyo sasa

Pamoja na hayo, naibu waziri Nchemba ametangaza kuwepo kwa account mbili chini ya BoT.
Tunafahamu BoT ni ya muungano. Sasa account za kupokea mapato na account za kutunza mapato ni za sehemu gani ya muungano?

Je, account hizo zitahusu gesi na mafuta yatakayopataikana Zanzibar?
Kama jibu ni hapana , ni kwanini rasilimali za upande mmoja (Tanganyika) ndizo zichangie JMT?......

Nimepitia ile sheria ya mafuta (Petroleum Act, 2015) kwa haraka, inasomeka hivi kwenye ukurasa wa 29 wa pdf iliyowekwa jamvini na JF.

Establishment of the Board of PURA (Petroleum Upstream RegulatoryAuthority):-

18.-(1) There shall be the Board of PURA to oversee the operation of PURA.

(2) The Board shall consist of five members who are citizens of Tanzania of moral character, proven integrity
and professional competence.

--------------------
Hao wajumbe watano watatoka Tanganyika (Tanzania Bara) ama Zanziber (Tanzania Visiwani) ama watatoka pande zote mbili.?

Kiukweli, kizungumkuti cha katiba ya Zanzibar kilitakiwa kuwekwa sawa, ili mambo haya yapatiwe ufumbuzi kwa wepesi zaidi. Na uharaka huu ndiyo unaozidisha mashaka, juu ya nia ya wale wanaoharakisha masuala haya. Kuna jambo haliko sawa!!!
 
Yes hapa kuna tatizo. Hizo ni bodi za Tanzania na hivyo wazanzibar watahitaji ajira tu kwasababu ni shughuli za muungano.

Hivyo nafasi za Watanganyika kusimamia rasilimali zao zitageuzwa kua ajira za kisiasa kwa wznz na kupoteza maana nzima.

Kumbuka huko znz hakuna Mtanganyika katika bodi yao.

Anyways, haya ni mambo yanayotakiwa yaangaliwe kwa kina si kukimbiza mswada kibusa bubusa tu

Na hili walitakiwa walione wabunge wa CCM. Inashngaza sana hawaoni haya

Hoja kubwa hapa ni kuwa uchaguzi wa mwaka huu wananchi waamke.

Wanaona jinsi nchi inavyouzwa watu wakipiga makofi. CCM wametufikisha mahali hata vitu vidogo kama hivyo hawawezi kufikiri

Kama wananchi hawaoni haja ya mabadiliko, wawe tayari kuishi na maumivu kwa muda mrefu nchi ikiuzwa na wao wakiwa ni bidhaa
 
What is in air is anger, watu wameichukia sana CCM lakini bado tatizo letu ni kutokuwa na mwamko wa kutosha. Bado tunadanganyika kirahisi sana.
 
Bongolander , tunadanyika kirahisi.
Siku zote husema,Watanzania ni watu wa ajabu kidogo, ni wazuri wa kulalama na wepesi sana wakusahau

Tunajua kila uchaguzi huambatana na mambo ‘maovu'

Siku za nyuma tumeona ya Kagoda n.k. bado hatuamshi vichwana kujiuliza, hii miswad inayokimbizwa bungeni kukiwa hakuna wabunge si wapinzani tu hata wa CCM ina heri na taifa hili.

Na iweje miaka 10 miswada hiyo ilikuwa chini ya kapeti na sasa inaibuliwa kwa hati za dharura

Huu wa gesi na mafuta una usiri tusioujua. Hili lilikuwa jambo la kitaifa,kwaninii limeharakishwa hivi?

Hata wabunge waliobaki bungeni nakuhakikishia zaidi ya asilimia 70 hawajui miswada hiyo ina nini, imekusudia nini na ina tija gani kwa wananchi

Lakini pia inaweza kutumika katika hoja za uchaguzi. Tunajua matatizo yaliyotokea mikoa ya kusini hadi askari wa jeshi
Upo uwezekano ni njia ya kutafuta hoja wakati wa kampeni

Ni hoja kama hizo tumeona kesi zikichukua miaka 8 kuamlizika kuelekea uchaguzi.

Na sasa zinatumika kuonyesha CCM inachukizwa na rushwa.

Wakati huo huo kuna lundo la rushwa kama za escrow zikimezewa tu, achilia mbali viporo vya ufisaidi visivyo na majibu

Wananchi walitakiwa waunge mkono hoja za wapinzani na upinzani kwa ujumla.
Hakuna litalofanyika katika muundo wa serikali ya sasa au bunge la sasa

Hao wagombea wa CCM hawana jipya. Kila mmoja anasifu mafasnikio ya awamu ya nne.

Halafu anasemaatasimama kidete kupinga rushwa.
Yaani wanakubali rushwa ni tatizo bado wanasifu serikali iliyopo imefanya vema

Tumeangalia madahalo wa JF na Maria Saraungi. Watia nia wanatetea deni la taifa.
Tatizo si kukopa, bali kwanini tunakopa kiasi hicho.

Tunapokopa na pesa kuishia mikononi mwa mafisadi wachache ni kuwabebesha mzigo watu wasiofaidika na mikopo hiyo.

Mfano, misamaha ya kodi peke yake ni Trilioni1, pesa za ufujaji za taarifa ya CAG, wizi na shugguli zisizo na manufaa kwa wananchi. Ni kiasi kikubwa sana

Utashangaa katika udanganyifu huu bado wananchi wanadhani wapo malaika ndani ya CCM wanaoweza kuwa mworabaini

Kenya walisimama nakusema hapana. Leo wametoka kundi la nchi masikini sana.

Tanzania bado tunaaminibaada ya miaka 50 ya umasikini ipo 5 inayokuja na malaika anayesubiriwakutangazwa Dodoma.

Kama hatubadiliki na kujiuliza, miaka 50 ijayo tutakuwa tumesimama hapa hapa

Tusemezane
 
Bongolander , tunadanyika kirahisi.
Siku zote husema,Watanzania ni watu wa ajabu kidogo, ni wazuri wa kulalama na wepesi sana wakusahau

Tunajua kila uchaguzi huambatana na mambo ‘maovu'

Siku za nyuma tumeona ya Kagoda n.k. bado hatuamshi vichwana kujiuliza, hii miswad inayokimbizwa bungeni kukiwa hakuna wabunge si wapinzani tu hata wa CCM ina heri na taifa hili.

Na iweje miaka 10 miswada hiyo ilikuwa chini ya kapeti na sasa inaibuliwa kwa hati za dharura

Huu wa gesi na mafuta una usiri tusioujua. Hili lilikuwa jambo la kitaifa,kwaninii limeharakishwa hivi?

Hata wabunge waliobaki bungeni nakuhakikishia
zaidi ya asilimia 70 hawajui miswada hiyo ina nini, imekusudia nini na ina tija gani kwa wananchi

Lakini pia inaweza kutumika katika hoja za uchaguzi. Tunajua matatizo yaliyotokea mikoa ya kusini hadi askari wa jeshi
Upo uwezekano ni njia ya kutafuta hoja wakati wa kampeni

Ni hoja kama hizo tumeona kesi zikichukua miaka 8 kuamlizika kuelekea uchaguzi.

Na sasa zinatumika kuonyesha CCM inachukizwa na rushwa.

Wakati huo huo kuna lundo la rushwa kama za escrow zikimezewa tu, achilia mbali viporo vya ufisaidi visivyo na majibu

Wananchi walitakiwa waunge mkono hoja za wapinzani na upinzani kwa ujumla.
Hakuna litalofanyika katika muundo wa serikali ya sasa au bunge la sasa

Hao wagombea wa CCM hawana jipya. Kila mmoja anasifu mafasnikio ya awamu ya nne.

Halafu anasemaatasimama kidete kupinga rushwa.
Yaani wanakubali rushwa ni tatizo bado wanasifu serikali iliyopo imefanya vema

Tumeangalia madahalo wa JF na Maria Saraungi. Watia nia wanatetea deni la taifa.
Tatizo si kukopa, bali kwanini tunakopa kiasi hicho.

Tunapokopa na pesa kuishia mikononi mwa mafisadi wachache ni kuwabebesha mzigo watu wasiofaidika na mikopo hiyo.

Mfano, misamaha ya kodi peke yake ni Trilioni1, pesa za ufujaji za taarifa ya CAG, wizi na shugguli zisizo na manufaa kwa wananchi. Ni kiasi kikubwa sana

Utashangaa katika udanganyifu huu bado wananchi wanadhani wapo malaika ndani ya CCM wanaoweza kuwa mworabaini

Kenya walisimama nakusema hapana. Leo wametoka kundi la nchi masikini sana.

Tanzania bado tunaaminibaada ya miaka 50 ya umasikini ipo 5 inayokuja na malaika anayesubiriwakutangazwa Dodoma.

Kama hatubadiliki na kujiuliza, miaka 50 ijayo tutakuwa tumesimama hapa hapa

Tusemezane

Mkuu wabunge wetu wengi kweli wanasikitisha. Lakini hata Spika mwenyewe ni wa ajabu, nadhani she is the worst speaker we have ever had, na bunge lenyewe ni bunge ambalo ni ovyo kabisa kuliko yote. NIdhamu hakuna, lakini hata umakini kwa kazi haonekani. Ninachoona ni wapinzani kufanya kazi yao kwa kujitahidi sana, lakini walio wengi ni kama wingi wao umewafanya wabweteke.

Tukiangalia tangu 2005 hadi sasa kwa hali ya kawaida CCM ilitakiwa kuaga, lakini nashangaa kuona uchaguzi wa ndani wa CCM unakuwa na umuhimu hata kuliko mengine yote.

Nakubaliana na wewe watanzania tunatakiwa kusemezana zaidi.
 
Mkuu kuhusu spika, wengine tulielewa ni tatizo tangu mwanzo.

Ilipoletwa hoja ya kuchagua kwakuwa ni mwanamke tukajua nchi imefika pabaya.
Tunajua uwezo wake na yote yanayotokea si bahati mbaya

Hatuwezi kumweka katika kapu moja na akina Sapi, Mang'enya, Msekwa hata kidogo.
Yote haya ni zao la CCM kwa kutumia wingi wao

Wabunge wa CCM wanasikitisha sana. Kuna nyakati nawaangalia na kujisema pembeni, pesa ina taabu.

Hivi mtu anasimamaje bungeni akilalamika kijiji hakina maji, halafu anamalizia kwa kuipongeza serikali inayosikiliza watu, inayoleta maendeleo na kisha kukubaliana na hoja? Kuna chembe fikra kweli

Ndio wale wanaosema pesa imeshuka thamani kwasababu ya kuweka picha. Huyo hana tofauti na yule msomi wa uzamivu anayekalishwa kitako na kuambiwa akubali yote ya chama. Kwamba msimamo wa chama ni mmoja hata kama nchi inauzwa

Hapa ndipo tunawakumbusha wananchi, waulizeni CCM wenye wingi, je kuna lipi la maana wanalifanya?

Waulizeni mswaada wa gesi na mafuta umelenga nini?

Waulizeni, zile pesa za bunge la katiba zilitoka wapi maana ninyi mnaambiwa hakuna fungu

Kama wananchi wa Tanzania wangekuwa na uchungu na maisha yao, wangekuwa na uchungu na vizazi vyao, CCM ingekuwa maktaba muda mrefu sana.

Kwa bahat mbaya na nzuri kwa CCM, Wananchi wanapenda amani na utulivu, yaani wanaibiwa kwa escrow wanasema hewala, wakipandishiwa kodi kufidia escrow wanasema hewala, wakipandishiwa umeme wanasema tumwachie mungu ni kazi yake

Leo lazima warauke saa 10 usiku kupigania mabasi, ukiwaambia kuna zaidi ya trilioni 2 zimepotea kwa wizi wanasema hayo yamepita, mungu anajua.

Kwa kuelewa Watanzania ni watu wa ajabu , kuna wagombea 40 wa CCM.

Kila mmoja anaamini anaweza kuwa rais, si wameona ? sasa nini kinawashinda.

Wanajua mbinu zote za kulaanisha Watanzania, kucheza na maneno, kukimbia kimbia ofisini n.k, kupanga maneno matamu matamu. Wanajua kazi ya Urais haihitaji akili ni ujanja janja tu nchi inaendelea kuwepo

Leo wenzetu wote majiranii, wanakimbia, sisi tumebaki tumechuchumaa . Wananchi hawaoni hili

Dodoma, kinachotokea wananchi, ni wezi kuchagua mwizi mwenzao. Hofu inapaswa kuwa kwa familia za wezi

Nashangaa eti anayedhulumiwa naye ana hofu, kubwa gani la maadui litapewa kiti.

Watanzania imefika mahali mujiulize, mna matatizo gani

Tusemezane jamani
 
Kwa bahat mbaya na nzuri kwa CCM, Wananchi wanapenda amani na utulivu, yaani wanaibiwa kwa escrow wanasema hewala, wakipandishiwa kodi kufidia escrow wanasema hewala, wakipandishiwa umeme wanasema tumwachie mungu ni kazi yake

Leo wenzetu wote majiranii, wanakimbia, sisi tumebaki tumechuchumaa . Wananchi hawaoni hili

Dodoma, kinachotokea wananchi, ni wezi kuchagua mwizi mwenzao. Hofu inapaswa kuwa kwa familia za wezi

Nashangaa eti anayedhulumiwa naye ana hofu, kubwa gani la maadui litapewa kiti.

Watanzania imefika mahali mujiulize, mna matatizo gani

Tusemezane jamani

Mkuu Nguruvi hapa tuko pamoja kabisa. Kama utakuwa umenisoma vizuri kwenye mabandiko yangu, huwa nasema Tanzania tumekumbwa na tatizo la Stockholm Syndrome...CCM licha ya maudhi yote na mabaya inayotufanyia, EPA, Richmond, Radar, Escrow etc etc kweli watu wanasimama na kusema kidumu chama cha mapinduzi. Sielewi maana yake nini.

Kweli ukiangalia Kenya, imepiga hatua mara mbili zaidi ya Tanzania, ukiangalia Rwanda pamoja na udogo wake inapiga hatua kuliko TZ, Uganda ukiangalia inajitahidi sana....sisi wenzetu ni burundi tu, nao siku si nyingi watauacha.

Lazima tusemezane ili tuamshane na kuwafanya viongozi wetu walete msukumo wa maendeleo ya nchi, si yao binafsi. Tanzania inatakiwa kuwa ya kwanza, this is what God has given us, we need to take care of Tanzania.
 
Na siyo maudhi peke yake, imefikia mahali udanganyifu unafanyika wazi na watu wanakubali.

Kwa mfano, CCM imeshindwa kutatatua tatizo la msongamano wa magari. Wananchi wanaambiwa ongezeko la mgari ni dalili ya kupanda kiwango na ubora wa maisha. Yaani ukufunga lane moja ya barabara automatic maisha yanapanda! na wanakubali

Katika kusemezana, tutaangalia hotuba ya Rais ambayo si mwelekeo wa taifa bali mwanzo wa kampeni.

Tutaiangalia katika bandiko hili kwasababu ni sehemu ya kampeni za uchaguzi na imebeba ilani ya uchaguzi ya CCM.
Ialni itakayobebwa na wababaishaji watarajiwa.

Tutafanya hivyo ili tufunguane macho na tuelezane haya maradhi ya usahlifu, wepesi wa kudanganyika na wazuri wa kubeba maumivu na mizigo isiyotuhusu

Wana duru tutasemezana , msicheze mbali hotuba inafanyiwa tathmini ya kina na uyakinifu
 
HOTUBA YA RAIS YA KUVUNJA BUNGE

VIPINDI VIWILI VYA UTAWALA
MTIZAMO WA HOTUBA KWA JICHO LA PILI

Wanajamvi hotuba inapatikana katika kiunganishi hiki
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/881576-hotuba-ya-rais-kikwete-kuliaga-bunge-09-julai-2015-a.html#post13227584

Shukrani kwa mwajamvi mwenzetu figganigga ambaye situ ametuletea habari katika muda (real time) bali pia hotuba nzima kwa utimilifu wake

Tuiangalie hotuba ya Rais kwa mtazamo mpana. Tutakuwa na mabandiko kadhaa yanayofuata.

UTANGULIZI

Kiongozi ni mtu aanyaeongoza kwa kusikiiliza, kupanga,kushauri, kaumua katika kundi,taasisi au nchi.

Bila kujali kiongozi amefikiaje hatua hiyo, pindi anapopewa nafasi anakuwa ni wa watuwote, waliomchagua na waliompinga

Jukumu muhimu la kiongozi ni kuwaunganisha watu katika kusukuma mbele agenda.

Kiunganishi kimoja kati ya vingi ni lugha ya wingi na si umoja ili kuwaleta wananchi wa itikadi, asili na Imani zote pamoja

Kiongozi huongelea mafanikio na changamoto kama mambo ya pamoja.Ili kufanikisha dhana ya umoja, aghalabu utawasikia wakisema ‘tumefanikiwa,tumeshindwa au tunaendelea n.k. bila kuleta hisia za ubaguzi kwa namna yoyote

Kulinganisha mafnikio au changamoto kwa nyakati au uongozi mwingine ni dalili za kujenga hisia za ubaguzi, dharau au chuki. Mara nyingi hisia hizo humweka kiongozi katika wakati mgumu( vulnerable) ‘kushambuliwa'' kwa hoja kwasababu tayari ameshajenga daraja lisilokuwa la lazima

Kati ya misingi inayotawala uongozi, ni kusimamia taratibu,sheria na kanuni
Kiongozi anatakiwa awe mkweli na mwenye msimamo wa kile anachoamini.

Kufikia azma hiyo, zipo nyakati hulazimika kwenda kinyume na matakwa yake na hubidi iwe hivyo

Kiongozi ni taswira na hivyo, hupaswa kuwa mfano wa tabia,mwendeno, maono, misimamo na nguzo katika jamii husika

Maswali yanayogonga akili za Watanzania kwa sasa ni;

Je,hotuba yam h Rais imewaleta Watanzania pamoja?

Je, amewaeleza Watanzania kuhusu mafanikio na changamoto zinazowakabili kwa ukweli?

Je,hotuba yake imekidhi haja ya kile wananchi walichotakiwa kuelewa kuhusu nchi yao?

Je, ameeleza ukweli na ukweli mtupu usio na chembe ya shaka?

Je, hotuba yake ilikuwa ni dira ya taifa au ni mwanzo wakampeni za uchaguzi?

Je, imekuwaje tumefika mahali makundi ya jamii yantishia taasisi kama ya Urais?

Haya na mengine tutayaangalia kwa kuongozwa na hotuba yam h Rais Bungeni

Itaendelea…
 
Shemu ya I

UMOJA , AMANI NA USALAMA

Mh Rais ameongelea umoja wa taifa kuwa imara. Akasema ''yamekuwepo matukio makuba na madogo ya kuvunjika kwa umoja kutoka kwa watu wasiotutakia mema.

Ametaja baadhi kama muungano wa Tanganyika na Zanzibar, suala la Imani nachuki za eneo moja na jingine

Hoja yetu:
Ni kweli hayo ni miongoni mwa mambo yanayotishia umoja wa taifa. Hata hivyo, tunajiuliza kama yanasababishwa na watu wasioitakia mema nchi hii?

Kwa mfano, suala la muungano ni la kihistoria. Mh Rais anaelewa, matatizo ya muungano si watu wa je wala wandani.
Ni muundo uliojenga muungano huo.

Tofauti za mitazamo haziwezi kuchukuliwa kama hoja ya watu wasioutakia muungano heri.
Kusema hivyo nikuwabagua wale wenye maono na maoni tofauti juu ya muungano.

Hili linazidikujenga hisia za ubaguzi miongoni mwa makundi ya jamii.
Hatuamini kuwa kutofautiana kimawazo ni suala la kutoitakia nchi hii mema

Pili, suala la Imani.
Nalo pia hatuwezi kufunika vichwa mchangani tukitafuta sababu nje ya zile zinazotuhusu.

Tumeona chokochoko za wanasiasakuchonganisha wananchi kwa misingi ya vyama vya kikabila na kidini.

Si wananchi bali wanasiasa, wengine wakikaa meza moja na mh Rais.
Waziri wa serikali yake anapokwenda msikitini au kanisani kuzungumzia katiba ya nchi kwa misingi ya udini ni tatizo la serikali, si watu wa nje au wenye wivu na nchi hii. Huu niukweli aliotakiwa si kuusema bali kuukabili

Je, alichukua hatua gani kuziba ufa uliosababishwa na wanasiasa wengi akiwa nao meza moja.
Je, alipeleka ujumbe gani pale alipomwacha waziri wake aliyehubiri siasa kanisani kuhusu katiba ya nchi?

Tatu, chokochoko za eneo moja na jingine.
Hapa mh Raisametuunga mkono tunaokemea viongozi wa kisiasa wanaopandikiza mbegu za ukabila na ukanda.
Hata hivyo, wananchi wangefarijika kama kiongozi wao angesimama kukemea hayo kwa wakati na si kusubiri wakati anaondoka madarakani

Pamoja na hayo, mh Rais hakuzungumzia mgawanyiko mkubwa wa kisiasa uliopo nchini.
Kushindwa kwa bunge la katiba ni kielelezo kizuri.Kuvurugwa kwa bunge la katiba ni matokeo ya kukosa uongozi, kutoheshimu sheria nahata kanuni.

Je, Rais alionyesha mfano pale paliotokea matatizo ya nani aanze kuhutubia bunge kati yake na mwenyekiti wa tume?

Tunachoelewa serikali yake ilichagiza kuvurugwa kwa kanuni zilizokuwepo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa

Zaidi ya hapo, tumeona wabunge wakifukuzwa bungeni kutokanana kusimamia kanuni na sheria.

Wingi umetumika kufikia maamuzi na si hoja
zinazoongozwa na kanuni, sheria na taratibu.
Mfano, miswada ya mwisho wa bunge hili, je, imepitia taratibu zilizowekwa?

Tumeshuhudia wabunge wa CCM waliobaki bungeni wakishinikiza serikali iangalie masilahi yao ili kumsikiliza Rais.
Kinyume chake, wabunge hao walitishia kususia hotuba yake

Kwa kuangalia pande mbili, wale wa upinzani walifukuzwa ilimaradi serikali ikamilishe azma yake na si azma ya wananchi.

Hawa wa CC Milibidi wasikilizwe kwa kuahirishwa bunge. Kwa mtazamo wa haraka,kilichofanyika ni kutenga makundi, wapinzani na wa CCM chini ya serikali hii. Je,hili si tatizo kubwa kuliko la Imani au ukabila?

Tunawezaje kusema umoja wa kitaifa ni imara, ikiwa sehemu muhimu na yenye ushawishi ya wanasiasa haipo pamoja, si baii yao bali hata na serikali?

Hoja ya umoja wa kitaifa haikuongelewa katika ukweli wake,imeongelewa katika funika kombe na kuwapamba wananchi.

Ukweli ni kuwa upo ufa mkubwa katika jamii, na serikali yake ilipaswa kuona hilo na kulizuia.

Je,tukubali kuwa tuwa wamoja ili kufurahisha nafasi zetu hata kama tunajua upo ufa?

Inaendele sehemu ya II
 
Inaendelea.. Sehemu ya II

''Katika kuzungumzia umoja wa nchi, Rais ameonyesha kutatuliwa kwa kero za muungano kutoka 13 hadi 3 ziliZoanishwa na tume ya Shelukindo. Hivyo, majibu ya matatizo yote yalikuwepo ndani ya tume''

Hoja yetu
Muungano umepitiwa na tume za Nyalali, Kisanga, Warioba 1 , Amina Salum, Shamhuna, Tume ya katiba kwa uchache wa kuzitaja. Kila tume imekuja na mapendekezo , nyingi zikishauri muundo wa muungano utazamwe upya.

Hatujui kwanini Serikali ilipitia tume ya Shelukindo na kuifanya kama standard.
Hapa kulikuwa na upendeleo wa kuchagua tume yenye majibu wanayotaka si yenye ufumbuzi

Umoja wa kitaifa kuhusu muungano unatishiwa sana. Pamoja na kudai kero zimepunguzwa, kwa upande mmoja, kusikiliza na kutekeleza matakwa ya wzn si suluhu. Muungano upo katika hali mbaya kuliko wakati mwingine

Ufa baina ya Tanganyika na Zanzibar umepanuka,suluhu si kuwafurahisha upande mmoja bali kutafuta suluhu ya jumla. Awamu haikutoa suluhu bali kuhamisha tatizo kwa awamu ya 5

Katika kero 13 hakuna iliyohusu Tanganyika. Maana yake, serikali ya JK imechochea hisia za Utanganyika na Uzanzibar Muungano si salama tofauti na tunavyoambiwa

Hoja ya umoja wa taifa, kuvunjika kwa bunge la katiba ni ushahidi tumepoteza thamani zinazotuunganisha( social fabric) chini ya uangalizi wa serikali hii. Ni legacy ya Jk kushindwa kusimamia taifa kuandika nyaraka yetu.
Ni failure kwa kiongozi yoyote na itabaki kuwa legacy yake daima dawamu

AMANI

Rais amezungumzia nchi yetu kuwa na amani. Na kwamba, ulinzi na usalama wa nchi upo imara. \
Jeshi lipo tayari na limeimarishwa kiulinzi kwa utayari wa aina yoyote

Hoja yetu

Ulinzi wa taifa ni muhimu na muafaka kueleza wananchi. Ulinzi wa nchi si jeshi, ni pamoja na diplomasia na uchumi.

Tunafahamu matatizo ya mipaka na jirani zetu yaliyoleta tension miaka miwili iliyopita.
Rais hakueleza ni hatua gani zimefikiwa kwa mzozo wa Malawi kidiplomasia

Kwa upande wa uchumi, je usalama wetu kiuchumi upoje? Uchumi na ulinzi na usalama ni vitu visivyotenganishwa katika dunia ya leo. Hilo halikusikika na kuacha maswali zaidi ya majibu

Rais alizungumzia kupungua kwa matendo ya ujambazi zaidi ya wakati alipoingia.
Hapa ndipo Rais alipoanza kuingia katika eneo linalomweka katika wakati mgumu(vulnerable)

Kwanza, tunaona akilinganisha nyakati, hivyo ni vema kila alilosema liwekwe kwa kulinganisha na nyakati
Hilo si jambo jema kwasababu sisi ni taifa, husimama na kuangauka pamoja.

Rais alichaguliwa kutafuta suluhu ya matatizo si kumyooshea kidole fulani.
Kuzungumzia wimbi la ujambazi kwa kipindi chake vs Mkapa ni kujenga taswira mbaya kwa mtangulizi BM

Hata hivyo, hatudhani matukio ya ujambazi yamepungua.
Kwa kutazama namba inaweza kuonekana haraka haraka kuna ukweli.
Kwa kutumia taThmini, matukio ya ujambazi katika awamu ya nne yanatisha

Tumeona Polisi wakiuawa katika vituo vyao. Hili halikuwahi kutokea katika awamu za nyuma. Walinzi wa taifa wanauawa na silaha kuporwa, ni kuonyesha ukubwa wa tatizo. Hatuwezi kusema matukio yamepungua, tunaweza kusema yanatisha sana.

Mfano, uhalaifu wa mabomu mara mbili Arusha, hakuna chanzo wala wahusika.
Tunawezaje kusema tupo salama ikiwa hatujui nani ni adui yetu miongoni mwa jamii?

KIUCHUMI

Matukio kama ya biashara baina yetu na Kenya yameonuesha udhaifu mkubwa. Kwamba, tunategemea nchi jirani kwa usafiri wa anga, si jambo la usalama hata kidogo.

Rais angetueleza ni hatua gani zimechukuliwa kuhakikisha kuwa ulinzi wetu kiuchumi upo imara?

Hatuwezi kuwa 'mateka' katika uchumi tukajinasibu tupo salama kwa amani.
Ndipo tunakuja katika swali letu bandiko la utangulizi, Je Rais alisema ukweli usio na shaka?

Tutaendelea kuangalia hoja ...
 
Sehemu ya II

AJALI ZA BARABARANI

Rais alisema ''ajali za barabarani ni eneo ambalo hakufanikiwa '' Hakueleza zaidi ya hapo

Hoja yetu
Ajali za barabarani zipo tangu mzee Malecela akiwa waziri mkuu. Ndiye aliyezuia mabasi kusaifiri usiku.
Tunakumbuka speed gavana zama za Sumaye.

Rais alikuwa kiongozi katika serikali na hivyo maamuzi mengi yanayohusu tatizo la ajali nchini anayafahamu vema

Miaka 10 madarakani ni mingi ya kutumia wataalamu kupata suluhu. Inasikitisha, tatizo alilolikuta likiongezeka kuliko wakati mwingine, anaondoka bila kuwa na suluhu nalo. Miaka 10 haikutupa majibu ya tatizo! Ni muda mrefu kwa maisha yetu

KATIBA
Rais anaipongeza tume ya Warioba na BMLK kwa kazi kubwa na nzuri. Tunajua, Rais hakupendezwa na tume ya Warioba na wala katiba inayopendekezwa si zao la tume ya Warioba.

Katiba imependekezwa imepatikana katika njia za aibu,inashangaza kwanini Rais azungumzie jambo la namna hiyo

Kuahirishwa kwa kura ya maoni ya CCM kulitokana na ukweli wananchi walisusia , maandalizi hafifu na kukosekana kwa muafaka wa kitaifa. Rais anaposema suala lililobaki ni kura ya maoni, inatia shaka kama anaeleza kilicho cha kweli

Hakuna kura ya maoni ya katiba pendekezwa kwasababu sheria muhimu zinazohusu kura ya maoni lazima ziandikwe upya.
Hivyo bunge lijalo litaanza upya katika kuandika taratibu na si suala la kuendelea Rais alipokomea

Uwezekano wa katiba pendekezwa kutupwa ni mkubwa kuliko wakati mwingine.
Na uwezekano wa Rasimu kurudishwa ni mkubwa kuliko wakati wote.

Uchaguzi una kila dalili ya CCM kupoteza 2/3 bungei.Hatuna uhakika kama alizungumzia bila chembe ya shaka!

Katiba ni zoezi lililoshindwa na kielelezo cha serikali kushindwa kusimamia masilahi ya taifa, sifa muhimu ya kuongoza

Kwa mlinganisho wa awamu, tunajiuliza, hivi serikali hii iliyoshindwa kuleta watu pamoja kuandika katiba ingeweza kutuongoza kupata uhuru kama awamu ya 1? Ingeweza kutuongoza katika vita na Idd Amin?

Ingeweza kutuongoza katika mabadiliko ya uchumi kama awamu ya 2? Na ingeweza kusimamia ukuaji wa uchumi kama awamu ya 3?
Serikali iliyoshindwa kusimamaia uandikaji wa taratibu zetu wenyewe, inawezaje kutushawishi kuwa ilikuwa makini?

RUSHWA

Rais anasema 'ni eneo waliloshikia njuga. Yapo mafanikio kama utungwaji wa sheria.
Kwamba Bilioni 87.8 zimeokolewa na kesi zimeongezeka kutoka 50 wakati anaingia hadi 1,700''

Hoja yetu

Rushwa si jambo geni, sheria zilikuwepo. Wala ongezeko la sheria halimaanishi mafanikio, pengine linaeleza ukubwa wa tatizo
Kwa mfano, mwaka 2005 kesi zililzokuwepo ni 50. Inawezakana kulikuwa hakuna rushwa kiasi cha kuwa na kesi 1900 za sasa.
Hivyo namba hazielezi kitu bila kuwa na tathmini.

Idadi ya 1900 ni wala rushwa ndogo ndogo, mahakimu, wauguzi na makarani. Katika kipindi cha miaka 10 taifa limeshuhudia rushwa za kimataifa, zilizo katika mitandao mingine hatari.

Katika kipindi hicho, tumeona rushwa ikilindwa na vyombo vya serikali, kigugumizi cha kushughulikia wala rushwa na kuwalinda

Hadi leo hatuna majibu ya rushwa nzito kama za Richmond, Meremeta, Tangold, Escrow na nyingine nyingi.

Ni Rais huyu ndiye alisimama kuwaomba wezi warudishe pesa katika kupambana na rushwa

Ni awamu hii katibu mkuu alishikwa akitoa rushwa hadharani na kuachwa astaafu.

Ni awamu ambayo rushwa imerasimishwa kama mfumo maalumu wa utawala wetu.

Watia nia wa CCM wote wanafahamu ukubwa wa tatizo, inaposemwa kulikuwa na jitihada, tunarudi kuuliza lile swali, hivi hotuba ilikuwa na ukweli bila chembe za shaka?

Tutaendelea..
 
Sehemu ya III

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Rais anasema, kipindi chake wameimarisha uhuru wa vyombo vyahabari. Magazeti ya kila siku ni 16, kila wiki 62, vituovya radio 115 na TV 29

Hoja yetu

Uhuru wa vyombo vya habari si wingi wa vyombo hivyo. Ni uhuru wa kutoa na kupokea habari bila kukwazo, kuchujwa au kubughudhiwa.

Tumeona sheria za kuzuia na kupokea habari chini ya sheriaya Mtandao. Tunaona TV zikiwekewa mizengwe

Waandishi wakiteswa hata kuuawa kesi . Ndio maana tunauliza, hivi hotuba ya Mh ni ukweli usio na chembe ya shaka?

UTAWALA NA KODI

Rais amezungumzia ongezeko la makusanyo akilinganisha na wakati anaingia madarakani.

Hoja yetu
Namba za makusanyo ya pesa peke yake hazielezi ongezeko la ukasanyaji wa kodi au miashahara.
Bila kuangalia thamani ya pesa na mfumuko wabei, namba hazitoi jibu sahihi

Mfano, wakati anaingia madarakani dola moja ilikuwa katika kiwango cha takribani Tsh 1000.
Kwa sasa kiwango hicho kimefikia 1700 hadi 2000kwa nyakati.
Je,hilo haliwezi kuwa tatizo katika kutahamanisha shughuli, mapatoau mishahara?

Je, mfumuko wa bei kwa nyakati za kuingia na kutoka madarakani ulikuwa sawa?

PATO LA TAIFA
Rais anasema pato limeongezeka kwa mtanzania, tumepunguza utegemezi kutoka asilimia 42 hadi asilimia 6, na uchumi umekuwa katika kiwangocha asilimia 7.Nchi yetu ni moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani

Hoja yetu

Ingezeko la pato la taifa lina maana hali nzuri kwa wananchi. Swali la kujiuliza, je, ongezeko hilo limekwenda sambamba na ubora wahuduma zetu? Kule hospitali Muhimbili walikoshindwa kulipa pesa kwa ajili ya dawa, tunaweza kusema kuna akisi ongezeko la uchumi, pato , makusanyo n.k.?

Wakati huo huo Rais anasema tatizo la BRN ni ukosefu wa fedha.
Endapo tumeacha utegemezi, inakywaje mpango kama wa BRN ukose fedha?

Inaendelea..
 
Shemu ya IV

''Rais anasema ' nimeamua kuanzisha mkoa wa Songwe kutokaMbeya, na kuongeza idadi ya wilaya (Kibiti,Ubungo, Kigamboni, Tanganyika na Malinyi''

Hoja yetu
Kwa maneno yake, uanzishwaji wa mikoa na Wilaya ni jitihada zake mwenyewe.
Hatudhani kuongeza mikoa au wilaya ni suala la kisiasa.Je, wataalamu walishirikishwa au serikali ilishiriki ?

Pengine hili linaeleza hoja iliyojificha. Tunajua kuna maeneo yamepewa hadhi za manispaa.
Moja ni eneo la Chalinze. Manispaa ina hadhi kuliko Wilaya, na hutkuona mantiki ya kutaja Wilaya bila kuzungumzia manispaa zenye hadhi na gharama zaidi

Swali la kujiuliza, hivi Chalinze imewezaje kufikia hatua ya manispaa haraka kiasi hicho?
Kuna miji kama wa Musoma imechukua miaka mingi kufikia hapo. Kuna miji ya zamani kama Korogwe na mingine haikuapata nafasi ya Chalinze kwa urahisi

Ni kwanini eneo hilo limepewa hadhi ya haraka haraka namna hiyo?Na kwanini hotuba ilitaja Wilaya na kuacha manispaa zenyehadhi kubwa

Lakini pia kuna hoja nyingine. Ongezeko la miji, Wilaya,manispaa na mikoa linakwenda sambamba na ongezeko la gharama.

Tunakumbuka CCM ilikataa rasimu ya Warioba kwa madai ya kuongeza gharama.
Je, hizi za sasa siyo zigo kwa walipa kodi kama ilivyokuwa inadaiwa katika rasimu?

Tunajiuliza, kupeleka huduma kwa wananchi ni kugawa maeneo au ni kuongeza miundo mbinu na ufanisi wa kazi?

Kama tunaweza kuwa na mkongo wataifa, ni kwanini tusiweze kutumia teknolojia hiyo na miundo mbinu mingine kuleta ukaribu kwa wananchi?

Tunafikra kidogo kuhusu kugawa maeneo. Nchi kubwa kamaCanada au Marekani hazina maeneo madogo ya kiutawala.

Jimbo moja la Marekani laweza kuwa sawa na nchi ya Tanzania. Nchi za Australia na Canada hazina zaidi ya majimbo15 licha ya eneo lao kubwa. Je, tunagawa maeneo kwa njia za kitaalamu au kwa kutumia siasa?

Kwanini tunaongeza ukubwa wa serikali badala ya kutazama ufanisi wetu?

ELIMU NA AFYA
Rais ameonyesha takwimu za kuongezeka kwa huduma katika maeneo hayo kama udahili wa wanafunzi, ongezeko la vyuo vikuu, na huduma za afya kama uwepo wa mashine za kisasa

Hoja yetu
Je, ongezeko la huduma hizo limekwenda sambamba na ubora wake.
Tunaweza kuwa na vyuo vikuu 200 kwa siku moja. Hoja ya msingi, vyuo hivyo vina ubora au ni bora vyuo?

Tunaweza kuweka mashine na kuanzisha vitengo vya afya. Je,tunapata ubora uliotarajiwa?

Inakuwaje endapo huduma za afya zimeiarika tunaona bado Waheshimiwa wakienda kutibiwa nje?

Ni huduma gani tofauti na zile bora za nchi wanazofuata nje kwa gharama ya wananchi?

Inaendelea…
 
Mkuu Nguruvi3 naomba nichepuke kidogo kutoka uchambuzi wa hotuba ya mkuu wa nchi, can w discuss a little bit kinachomalizikia Dodoma? Pamoja na misukosuko ya Dodoma, CCM sasa wanajinasibu kwamba wako wamoja( wametoka wamoja Dodoma) na kwa kutumia kete ya Mgufuli watawapiga UKAWA sana na kwa kura nyingi. Najiuliza kweli watanzania wanasahau mapema kiasi hicho? Watafanya maamuzi kwa sababu ya mtu na sio kwamba system nzima ya CCM amabayo kwao wanaona ni utata??

Nina hamu sana ya kujua uchaguzi wa mwaka huu pamoja na mazingira ya kiuchaguzi, nione maamuzi ya watanzania yako influenced na jambo gani na je wanaangalia hali halisi ya maisha yao???
 
Mkuu , hoja yako imezangatiwa na tunafanyia kazi

YANAYOTEA DODOMA NA HATMA YA UCHAGUZI
WAPINZANI WAKIJIPANGA , MABADILIKO YANAWEZEKANA

Inafuata
 
YALITOKEA DODOMA NA HATMA YA UCHAGUZI
WAPINZANI WAKIJIPANGA , MABADILIKO YATATOKEA

Marejeo: Katika mabandiko yetu , tulisema, pamoja na kuwa na makundi makali, CCM watakuwa wamoja.Tulieleza sababu
CCM haina timbwili la kuongoza nchi, ina mtafaraku wa kupata viongozi wa kulinda masilahi(interest) na mfumo uliopo(status quo). Tutafafanua

MAKUNDI NA KAMBI

Uchaguzi ndani ya CCM umegubikwa na hali tofatuti na ile ya mwaka2005.
Mwaka 1995 kulikuwa na vita kati ya makundi ya wazee. Mwaka 2005 kulikuwana makundi ya wazee na vijana.
Kundi la vijana ndilo lililotengeneza mtandao

Mwaka 2015, kundi la mtandao limegawanyika katika makundi yavijana.
Kumekuwepo na kundi la kichini chini la akina mama wakitaka nafasi. Hivyo makundi halisi ni haya

1 Kundi la vijana

2 Kundi la akina mama

3 Kundi la wazee ambalo halitajwi kama wazee ili kukwepa ‘stigma'ya wazee

‘Tension' ya uchaguzi ni kutokana na uwepo wa kambi kuumbili. Kambi ya Lowassa, na kambi ya Membe.
Kambi hazikuwa na ushwawishi, bali ushawishiwa kimasilahi.

Hapa ndipo tunajibu hoja ya awali kuwa kuondoka kwa kina Lowassa na Membe hakuwezi kuwagawa CCM kwasababu ‘wafanyakazi' wa makundi hayo na watafuta masilahi tayari wamesha waacha ''watu wao'' wenyewe na kuhamia kambi zenye mwelekeo wa ushindi kwasababu ile ile, ya kulinda masilahi na mfumo

Leo simu wanazopigiwa akina Memba, lowassa , January n.k. nichache. Ni zile za watu wa karibu wenye matumaini kuwa watu hao watakuwepo serikalini kama CCM itashinda

Vinginevyo,‘wafanyakazi' wadogo wadogo tayari wamehamisha kambi

TANO NA TATU YA WAGOMBEA IMAPATIKANAJE?

Hali ya kisiasa nchini imebadilika. Udhaifu wa CCM hauwezi kuhimili dalili za mbadiliko

1 Wananchi wana uelewa mzuri kidogo wa nchi yao kuliko siku za nyuma. Hali ya uchaguzi ‘demography' ikimaanisha changing structure of human population imeabadilika. Kundi la wazee sasa ni dogo ukilinganisha na la vijanana akina mama

2. Uelewa wa matatizo yetu katika sehemu ya jamii ni mkubwa
ukilinganisha na siku za nyuma. Masula kama umasikini, ufisadi ni sehemu ya agenda za mazungumzo ya wananchi

3. Tishio la muungano linaongeza joto zaidi katika kuchuja wagombea'vetting'

4 Ongezeko la nguvu ya wapinzani linailazmisha CCMkufuata mkondo wa uchaguzi kwa kuiangalia jamii.
Kupoteza chaguzi ndogo na zileza mitaa kumeibadilisha CCM

Haya ni baadhi ya mambo yaliyochagiza kupata tatu inayosemwa

Tatizo linalojitokeza ni moja, je mambo hayo yamesaidia CCM kupata tatu itakyiotoa mgombea sahihi kwa nchi hii wa kupambana na mgombea wa upinzani?

Inaendelea…
 
Tutanakufuatilia mkuu, ukimaliza nitachangia kidogo, hususan ulaghai unaotaka kufanywa especial kwa kuwaaminisha wananchi kwamba wanawaletea mgombea bora wa kuwaunganisha, while kiukweli the whole system is fractured and w need a new vehicle to revive our country.
 
TANO YA CCM

Kutokana na mabadiliko ya kijamii kwa wapiga kura,udhaifu wa CCM na nguvu ya upinzani nchini, CCM ilitumia njia ya kushinda ‘win' makundi badala ya kutafuta mgombea mwenye uwezo.
Baadhi ya wenye uwezo wakawa ni wahanga wa utaratibu huo

1 Mawaziri wakuu waliondolewa ili kupooza nguvu za EL.Wengine kama Mheshimiwa Pinda waliondolewa kwasababu za kimitego. Udhaifu wakewa kusimamia serikali ni moja kati ya mengi.
Mh alikaa kimya ili kutoudhi makundi ya CCM ndani ya bunge, kinyume chake akaonyesha udhaifu

2 Wazee akina Wasira, Sitta n.k. waliondolewa katika kuangalia kizazi kilichopo na mwelekeo wa kura za makundi ya kijamii

3 Vijana ndio wanaonekana kuwa tatizo. Kuondolea kwao kunabaki tatizo la chini chini

Hivyo, tano bora ikapatikana kwa kuangalia haya

1 Membe- akiwakilisha kundi la kati baina ya wazee na vijana

2 January- Akiwalilisha kundi la vijana

3. Amina Ali-akiwakilisha kundi la muungano

4. Asha Rose- akiwakilisha akina mama

5. JP Magufuli- akiwakilisha kundi la kati lakini likiwa la wasiona makando kando

TATU YA CCM
Kuondolewa kwa EL kulizua hisia za kubebwa Mh membe. Kura ndani ya NEC ikazingatia hasira.
Team EL ikahamishia nguvu kwa wahombea wengine.January akawa mhanga wa ‘bifu' lake na EL

Waliopatikana ni Magufuli, Amina S. Ali na Asha Rose Migiro

Hadi hapa uchaguzi wa CCM haukuzingatia weledi, ukomavu au uongozi.
Umeongozwa na hofu ya uchaguzi mkuu dhidi ya Upinzani.

Tumeona wagombea wakijieleza, hakuna shaka ilikuwa ni disappointment kubwa sana.

Endapo CCM itashinda, basi Watanzania wategemee ubovu zaidi ya uliopo. Huu ni ukweli hata kama unauma.

Pamoja na hayo, CCM itaondoka Dodoma ikiwa ni moja. Makundi yatajielekeza katika masilahi na hayawezi kufanya kazi nje ya CCM.

Ni ukweli kuwa wagombea wa CCM wamepatikana kwa bahatinasibu na si vigezo vya mtu anayechukua uongozi wa nchi

Katika kutibitisha hili, haiwezekani wagombea wasiulizwemaswali hata moja.

Hii maana yake ni kuwa tayari makundi yalishafikia uamuzikilichokuwa kinasubiriwa ni kura tu.

Kwa mwendo huu upatikanaji wa uongozi ‘vettingsystem' ya CCM ni mbovu kwa uchaguzi na kama watashinda kwa nchi

Kitakachotokea ni makundi husika kujipenyeza katika serikali. Mfumo wa CCM utabaki kama ulivyo

Hata hivyo, CCM imefanikiwa Dodoma

Inaendelea…
 
CCM WAMEFANIKIWA

WAPINZANI WAJITATHMINI

Kutoka Dodoma , kwa takribani wiki mbili habari kubwa imekuwani uchaguzi wa CCM wa ndani.

Habari zilizotanda katika vyombo vyote ni kuhusu uchaguzi wa CCM. Kama kawaida Watanzania ni wazuri sana wa kufuatilia matukio,si kwa kubaini bali ushabiki

Katika media coverage waliyopata CCM, hakuna shaka wamepata uenezi ‘publicity' kubwa na hivyo tayari wana Mileage katika uchaguziwa Oktoba. Hili wamefanikiwa sana.

Kwa bahati mbaya , wapinzani nao kama wananchi wengine wakasitisha shughuli za kuzuia publicity hiyo.

Kuelekea Oktoba, mgombea wa CCM anatambulika haraka hadi hapo wapinzani watakapo badilisha mbinu ‘equation'

Suala la CCM kupasuka halipo kwasababu ni nani atakayeweza kuwa nje ya mfumo unaomjua na unaomlinda akabaki salama? Kila mmoja atajiunga na kambi ya CCM si kwa masilahi ya nchi bali ya mtu au watu binafasi

NINI KINATARAJIWA
Saa nne asubuhi upo uwezekano mkubwa wa Magufuli kukabidhiwa

ilani ya CCM. Tunasema ‘uwezekano' kwa kuzingatia hali halisi iliyopo Dodoma

Kwanini Magufuli

1 Katika udhaifu wawagombea wa CCM(3) yeye ni bora

2 Taratibu zisizo rasmi za uongozi wa nchi zinampa ‘advantage'

3 Kundi la EL limekosa ‘leadership' kila mtu kivyake nawengi wataegemea kwa JP

4. Makundi ya vijana yamepigwa na butwaa, kila mmoja kivyake

5 Asha Migiro na Amina wanaonekana si sehemu ya ‘inner cicrcle ' ya akina mama, hawaonekani kupewa advantage hiyo

KITAKACHOFUATA

Mgombea mwenza lazima atoke Zanzibar. Uwezekano wa wagombea wenza

1 Shamsa Vuai – kwasababu ya misimamo yake juu ya muungano

2. Amina S. Ali – Kwa nafasi yake aliyofikia katika uchaguzi

3. Seif Idd – Ni mwiba mkali wa wapinzani wa CCM visiwani

3 Mohamed Seif Khtaibu- Kama mtetezi wa muungano

Itashangaza sana kama Magufuli si mbeba bendera. Ukiangalia safu yawagombea wenza, tuna rudi kule kule, kwamba iwapo CCM watashinda, tutabaki tulipo

Wapinzani nao hali ikoje?

Inaendelea sehemu ya mwisho
 
Back
Top Bottom