2019 Africa Cup of Nations Special Thread

2019 Africa Cup of Nations Special Thread

Mimi naona mlio wengi munalaum CCM, mnafikiri kwa kariba ya wachezaji tulionao hata ingelisimamiwa na Chadema tungeshinda?
Acheni kujificha kwenye shamba la Mihogo inayo chipua. Ukweli timu za bongo hazikosi sababu leo hii Jamiiforum ndo kisima cha habari na uchambuzi mzuri tunakuja na hoja au majibu mepesi kabisa. Tumepoteza sababu ya CCM. Mnajua kufuzu tumebebwa na Uganda na baada ya kuongezwa timu kuwa 24.
 
Ishu sio kusimamiwa na vvm wala chadema, timu inatakiwa iwe na mlengo wa kitaifa sio kichama na ndio maana unaona tunalumbana wenyewe
Mimi naona mlio wengi munalaum CCM, mnafikiri kwa kariba ya wachezaji tulionao hata ingelisimamiwa na Chadema tungeshinda?
Acheni kujificha kwenye shamba la Mihogo inayo chipua. Ukweli timu za bongo hazikosi sababu leo hii Jamiiforum ndo kisima cha habari na uchambuzi mzuri tunakuja na hoja au majibu mepesi kabisa. Tumepoteza sababu ya CCM. Mnajua kufuzu tumebebwa na Uganda na baada ya kuongezwa timu kuwa 24.
 
Steve Nyerere pia yupo Egypt,hayo maneno yake ss aah ni hovyoooo.Kamsikili IG Kwa Millard Ayo inashangaza kwakweli
Polepole alisema T stars kwenda afcon ni juhudi za awamu ya Tano.... Kwahiyo tulia hivyohivyo
 
Na TTCL...na mengine mengi...mbele wanatanguliza neno CCM wakati ni mali yetu wote kwa kodi zetu sisi!

Wanakosea sana...watakosa support ya umma wote maana tuna itikadi tofauti!

Michezo waiache,waiendeshe kwa sura ya kitaifa bila siasa ya vyama ndani...

Walivyo sikio la kufa,hawatakaa waelewe chochote!
Kabisa katika mambo yanakera ni haya, mimi sina chama lakini hii tabia ya wanasiasa kuingilia team hasa wanapokuwa wameona kuna fursa itaturudisha nyuma sana na Captain wetu akanasa kwenye mtego akaanza tunaishukuru serikali ya awamu ya tano ya JPM nikajuwa hapo tu basi kwisha kazi. Unamshukuru kwa lipi hebu tumuulize? kawapa pesa no, ndio kwanza bakuli mnatembeza badala ya kushukuru wachezaji na makocha na washabiki unaanza kuleta siasa turudi tukapige kura serikali za mitaa tu. sijawahi kusikia captain wa mfano team ya England akisema tunamshukuru malkia na waziri mkuu ndio level yetu iko wapi siasa za kijinga katika kila kitu. michezo ikae mbali na siasa jamani unataka kuchangia peleka TFF. Mpaka bunge limehamia huko ujinga mtupu na naomba tupigwe mpaka na wakenya ujinga mtupu.
 
MODI UNABOA.. UNAHARIBU MAMBO KWA KUCHANGANYA THREAD..
 
Hii nayo imechangia
FB_IMG_1561357036297.jpeg
 
si tunasema league yetu bora Africa mashariki? Burundi wazuri, Uganda wazuri hata wa Kenya bora kuliko sisi na league zao mbaya kwa mujibu wetu
At least wana wachezaji abroad
Birigimana
Belahino
Ni mfano tu in short wana team nzuri

Sisi ndio tuna league nzuri kwa mafanikio Ya team Kama simba lakini wanaoibeba simba sio mchezaji wa hapa Kagere Kotei Chama Wawa okwi
Yanga makambo tshishimbi
Azam chirwa ngoma wadada yakoub abarola

Hapo umeona mzee
 
Najua wengi mmekata tamaa baada ya kupokea kichapo mujarabu kutoka kwa Senegal, Ila Huwezi amini hii timu itavuka hatua hii ya makundi.

Raundi inayofata Itakuwa Kama ifuatavyo:
Tanzania itashinda 2-0 mechi ya kenya na kuwa na point 3 .

Algeria atamfunga senegal 3-0 na kufikisha point 6

Msimamo utakuwa

1. Algeria 6
2. Senegal 3
3.Tanzania 3
4. Kenya 0


Raundi ya mwisho

Tanzania atadraw bila kufungana na Algera na kufikisha point 4

Kenya atadraw 1-1 na Senegal na kufikisha point 1

Msimamo wa mwisho utakuwa

1.Algeria point 7 goli difference 5
2. Tanzania point 4 goli difference 0
3. Senegal point 4 goli difference -1
4. Kenya point 1 goli difference-4

Hivyo Tanzania itaipita senegal kwa tofauti ya ma goli ya kufunga na kufungwa.


Najua wengi mtabeza lakini mwisho wa siku mtanitafuta ili niwatabirieni mambo yenu yajayo
 
Back
Top Bottom