Mchezo ulinickekesha sana kwa vile Argentina ilifuta matumaini ya Scotland to advance, yaani ule mchezo tukose wote, kwani Argentina ililazimisha nchi zote mbili zifunge virago; yenyewe haikuwa na matumani kabisa.Duh! Hii mechi ya Scotland a Argentina hadi dakika ya 73 Scotland walikuwa mbele 3-0. Dakika 17 zilizobaki Argentina wakafunga goli 3 za haraka haraka kwenye dakika ya 74, 78 na penalty dakika za nyongeza 94 na mchezo kumalizika 3-3.
Nitajie majina yao mkuuHata kipa wa South Africa ana kishundu na hips moja matata mnooooo....Kiboko kipa wa Jamaica bana
Kulingana na jinsi mchezo unavyokwenda, nina mashaka na uwezo wa USA iwapo kweli wataweza kuchukua ubingwa mwaka huu. Kwa karibu sana utaona kuwa style ya USA na Canada havitofautiani sana. Wanaceza pasi fupi fupi lakini hawana spidi sana, wakati timu nyingi za Europe zinapenda pasi ndefu ndefu halafu kwa spidi kali sana. Ni rahisi sana wao kuhamisha mpira kutoka golini kwao a hadi golini kwa adui wakati USA na Canada zinajivuta. Kama ambavyo Canada imetolewa leo na Sweden ndivyo ninavyoona jinsi USA itakavyotolewa na Ufaransa tarehe 28 June unless wabadilishe style. Nafasi inayoshikiliwa sasa na Megan Rapinoe inabidi apewe Jessica McDonald katika kipindi cha kwanza; Rapinoe hana kasi inayotakiwa katika mashindano haya kwa sasa kama ile ile MacDonald.Bingwa France au USA
Game Kali sana France vs USA. Mpira unapigwa mwingi sanaa mpaka unainjoi.World cup imebaki kuwa baina ya USA na Europe. Timu zote nje ya Europe zimeshatolewa isipokuwa USA. Hata hivyo survival ya USA iko mashakani sana hasa baada ya kuhangaika sana kuifunga Spain kwa penalty, timu ambayo haikuwa tishio kwa timu za Ujerumani, France na England. Kwa hiyo mchezo wa Kesho baina ya USA na France ndio utakaomua future ya USA. Iwapo USA itaweza kuitoa France, basi inakuwa karibu na ubingwa tena, ila chances za kuifunga Ufaranza ni ndogo sana.
Kwenye mechi ya leo baina ya England na Norway, ingawa Norway ilicheza kwa ufundi na nguvu sana, haikuwa riziki yao kwani waliishia kubugizwa mabao 3-0. Ila golikipa wao aliwasaidia kwa kupangua bao moja la penalty.
Kitu nilichoona kwenye michezo hii, magolikipa wa kike wako sharp sana kuzuia penalty. Tangu michezo hii ianze, wameshuzuia zaidi penalties sita ukichanganya na zile zilizokataliwa kutokana ni hii sheria mbovu ya VAR.
Dk.33 France ameshalizwa moja Ila wana forward yao anaitwa diani huyu Dada anacheza sana.kwa kifupi mechi Kali sana sina mpango wa kuangilia mechi ya south Africa na Namibia maana sitainjoi kama hiii maana najua mechi itajaa butua butua tuGame Kali sana France vs USA. Mpira unapigwa mwingi sanaa mpaka unainjoi.
Wananichukiza nimeacha kuangalia mechi zao,yaani mchezaji anafunga goli la ushindi dakika ya 90 halafu havui jezi wakati wa kushangilia (Joke)πππTimu ya ya wanawake ya Ufaransa inaelekea kuja kuwa tishio kubwa kwa marekani, kwani watoto hao nililiwaona wana ball controll ya hali ya juu sana. Ingawa wachina wamefungwa na ujerumani, ni dhahiri kuwa walikuwa na resistance kubwa na ujerumani ilicheza mchezo wa hali ya chini sana.
Dada zetu wa Banyana Banyana wa South Africa walianza vizuri na kuwapa wakati mgtumu Spain lakini wamekuwa wakielemea sana kadri muda unavyokwenda na dakika hihi hihii wamefungwa goli la pili; sijui kama watakata tamaa.
Ratiba kamili ya michezo yote iko hapa Paris France
Updates: Banyana Banyana wameishiwa sana pumzi dakika za mwisho na kuishia kufungwa 3-1
USA kashinda lakini mechi ilikua nzuri sana.France wamecheza mno bahati haikuwa yaoDk.33 France ameshalizwa moja Ila wana forward yao anaitwa diani huyu Dada anacheza sana.kwa kifupi mechi Kali sana sina mpango wa kuangilia mechi ya south Africa na Namibia maana sitainjoi kama hiii maana najua mechi itajaa butua butua tu