2019 FIFA Women's World Cup

2019 FIFA Women's World Cup

Duh! Hii mechi ya Scotland a Argentina hadi dakika ya 73 Scotland walikuwa mbele 3-0. Dakika 17 zilizobaki Argentina wakafunga goli 3 za haraka haraka kwenye dakika ya 74, 78 na penalty dakika za nyongeza 94 na mchezo kumalizika 3-3.
Mchezo ulinickekesha sana kwa vile Argentina ilifuta matumaini ya Scotland to advance, yaani ule mchezo tukose wote, kwani Argentina ililazimisha nchi zote mbili zifunge virago; yenyewe haikuwa na matumani kabisa.
 
Baada ya ya mchezo yote ya group D; yaani Canada vs Netherlands ambapo Canada ililambwa 2-1, na Cameroun Vs Newzalan ambapo Cameroun iliwalamba New Zealand 2-1 basi timu za Canada, Netherlands na Cemerorn zimefuzu kuingia kwenye kundi la 16. Mchezo ulionisisimua zaidi ni ule wa Cameroun dhidi ya New Zealand kwa jinsi Cameorun ilivyokuwa ikicheza kwa nguvu utadhani ni wanaume. Kwa muda mrefu walikuwa wakiongoza kwa 1-0, na New Zealand walionekana wakicheza kulinda zaidi ya kushambulia kwa sababu mashambulizi ya Cameroun yalikuwa mengi sana. Hata hivyo kwenye kipindi cha pili, mlinzi mmoja wa Cameroun alikuwa akitaka kutoa mpira nje ili iwe kona, lakini mpira huo haukutoka nje ya goli na hivyo kujikuta amejifunga bao mwenyewe. Hiyo iliwapa matumaini mapya na nguvu New Zealand na kuwavunja moyo sanaa Cameroun. Mwanya huo ulionyesha kuanza kutumiwa na New Zealand kwa wao pia kuoaza kushambulia wakitegemea angalu goli moja kabla Cameorunhawajaamka kwenye majonzii, hata hivyo haikupita hata dakika tano, Cameroun wakaamka tena na kuanza mashambulizi mapya. Dakika mbili kabla ya mpira kuisha wakati wa dakika za majeruhi, Cameroun wakafunga bao moja la ufundi sana, na kuweza kujipatia sifa ya kuingi kwenye grupu la 16.



 
Michezo wa mwisho kwenye makundi ilikuwa ni ya kundi F wakati miamba wawili wa USA na Sweden walipokutana na USA kuibuka kidedea kwa mabao 2-0, na vile vile Chile ilipopambana na Thailand ambapo Chile iliibuka kidedea kwa bao 2-0 pia. Kwenye mchezo baina ya USA na Sweden pande zote mbile zilicheza kwa nguvu na kwa ufundi ila USA ilikuwa ikishambulia zaidi, na vile vile defense yake iliweza kudhibi sana mashamabulizi ya Sweden; hasa kipa wa USA alizuia mashuti kadhaa ya uhakika kutoka Sweden.



Mchezo niliokuwa nikiangalia kwa hamu kubwa ni ule wa Chile dhidi ya Thailand kwa sababu ndio uliokuwa unaamua iwapo Nigeria itaendelea kwenye kundi la 16 au vipi. Chile ilitakiwa ifunge mabao matatu kwa bila, na isipate zaidi ya yellow card mbili. Kwa bahati mbaya pamoja kuishinda Thailand, hawakuweza kuvusha lengo la mabao matatu, na hivyo kumfanya Christiane Endler na timu yake warudi Santiago mapema. Golikipa Endler atakumbukwa sana na watazamaji wa mashindano haya kwa umahiri wake wa kulinda goli. Chile itajilaumu zaidi baada ya kusindwa kufunga penalty kwa kupiga kwenye mwamba ingawa ilikuwa inajulikana kuwa golikipa wa Thailand siyo imara sana wa kuweza kuzuia penalty yoyote ile. Kwa matokeo haya, kutoka Afrika ni Nigeria na Cameroun ndizo zimefuzu kuendelea kwenye kundi la 16.

 
Michezo ya kundi la 16 ni kama ifuatavyo;
1133382


Ulaya ina timu 8: Germany, Sweden, Englan, Italy, France, Netherlands, Spain, Norway
North America ina timu 2: Canada, USA
Africa ina timu 2, Nigeria, Cameroun
Asia ina timu 2: China, Japan
South America in timu 1: Brazil
Oceania ina timu 1: Australia
 
Mchezo baina ya germany na Nigeria ulikuwa na misisimko pia, ingawa Ugerumani ilishinda, haikushindwa kwa ufundi kama ambavyo watu wanadai. Ilifunga bao moja la kona ambayo labda ndiyo iliyokuwa na ufundi tu, gori moja lilikuwa la pebnalty na moja lilitokana na makosa ya mlinzi mmoja wa Nigeria. Ujerumani haikuwa na ushambuliaji mkalia ambao ungetegemea kwa kulingana na invyosifiwa, ingawa Nigeria nayo hawakuwa na ball control nzuri



Kwa upande wa Noray na Australia, kwa kweli mchezo ulikuwa mgumu sana. Timu zote mbili zilicheza kwa ustadi mkubwa na kumaliza dakika tisini za kwanza zikiwa sare 1-1. Australia ilionyesha ushambuliaji mkubwa sana lakini haikufanikiwa kupata goli la pili. Kuna wakati mchezaji wao maarufu Kennedy alipewa red card na kuiacha Australia ikiwa na wachezaji kumi tu. Hata hivyo upungufu huo haukuzaa matunda kwa Norway hivyo mchezo ukaamuliwa kwa penalty. Hapa ndipo Australia ilivuruga sana kwani kapteni alianza kwa kupiga penalty nje, halafu mchezaji wa pili akapiga shuti ambalo lilipanguliwa na kipa wa Norway. mashuti yote ya Norway waliingia gorini, na hivyo baada ya Norway kupata mashuti manne, mcehzo ukasimamishwa, na Norway kupewa ushind wa 1 (4)-1(1) ingawa record hiyo siyo fair kwani Australia ilipiga penalty tatu tu wakati Norway ilipiga nne; ushindi sahihi ungekuwa ama 1(4)-1(2) au 1(3)-1(1)

 
Mchezo baina ya Brazil na France unaendelea, bado wako 0-0; sasa nyie akina Marco Polo na Rural Swagga msikae kumduwalia macho golikipa wa Brazili tu. Alifungwa bao kwa kugongwa kichwa kwenye maziwa na kunyang'anywa mpira aliokuwa anazuwia, kwa hiyo bao hilo likakataliwa. Ila golikipa huyo ana tatoo tumbo zima mpaka mapajani.
 
Hawa wanawake wanacheza vizuri kuliko hata ile timu yetu

Ova
 
England illifunga Cameroun 3-0, ila uamuzi wa katika mchezo ule uliwajenga wasichana wa Cameroun kuwa na hasira, kwa vile walionewa kwa kukataliwa bao walilokuwa wamefunga kihalali kabisa. Wasichana wale walitaka hata kususia mchezo mzima ila wakaombwa sana waendelee, ndipo walipoingia tena uwanjani baada ya tafarani ya kama dakika sita hivi. Sasa kama unavyoelewa, hasira hasara; kwa hiyo walipendelea na mchezo walicheza kwa hasira sana. Ingawa mcghezo ulikuwa mzuri sana na watoto wale walicheza kwa nguvu na kwa kujiamni, haikuwa siku yao.



Mpambano baina ya Brazil na France ulikuwa mgumu sana. Hadi dakika ya tisisni timu zote zilikuwa sare 1-1; ila katika dakika ya 104 wakati wa nyongeza, Brazili ilikosa bao la wazi kabisa lililuiliwa mstalini na mchezaji namba 11 wa Ufaransa baada ya kipa kuwa keshapigwa chenga. Muda mfupi baadaye dakika ya 106, Ufaransa ikapata bao la pili na ushindi. Kwa waliongalia mchezo huu nadhani ilikuwa ni burudani nzuri sana. Nadhani akina Marco Polo na Rural Swagga watamkosa sana Barbara, kipa wa Brazili kwa vile sasa hivi yuko njianai kurudi Rio de Janeiro

 
Mchezo baina ua USA na Spain umekwisha huku USA ikiibuka kidedea 2-1; hata hivyo ingawa USA ilitawala mchezo huo kwa kila kipimo: ball possession 54%-46%, pass accuracy 78%-72% pamoja na vipimo vinginevyo vyote, Spain ilicheza mchezo mzuri sana kuliko USA. Spain ilikuwa na spidi, halafu aggressive katika kushambulia kuliko USA. Maoli yote ya USA yamepatikana kwa njia ya penaly, huku goli la Spain lilipatikana kwa uzembe wa golikipa na defender ,mmoja wa USA mbele ya mshambuliaji hatari wa Spain. Well, ushindi ni magoli, kwa hiyo Spain inabidi wapande treni kurudi Barcelona usiku huu. Sasa USA itapambana na France, na nina wasiwasi watatolewa na France iwapo hawatabadili uchezaji.



Kwa jumla timu ya spain ilcheza vizuri sana kuliko hata Arsenal
 
Mpira wa wanawake umeharibiwa sana na VAR na maamuzi mabovu ya referees. Mtu akiguswa kidogo penalty, Sijui kwanini hawakuchukua waamuzi wa kiume wawasaidie.

Timu inapambana ila inakuja kuangushwa na maamuzi ya refa kwa kutoa penalty rahisi rahisi. I feel Sorry for Spain. Penati ya pili wameonewa.
 
Bingwa France au USA
Kulingana na jinsi mchezo unavyokwenda, nina mashaka na uwezo wa USA iwapo kweli wataweza kuchukua ubingwa mwaka huu. Kwa karibu sana utaona kuwa style ya USA na Canada havitofautiani sana. Wanaceza pasi fupi fupi lakini hawana spidi sana, wakati timu nyingi za Europe zinapenda pasi ndefu ndefu halafu kwa spidi kali sana. Ni rahisi sana wao kuhamisha mpira kutoka golini kwao a hadi golini kwa adui wakati USA na Canada zinajivuta. Kama ambavyo Canada imetolewa leo na Sweden ndivyo ninavyoona jinsi USA itakavyotolewa na Ufaransa tarehe 28 June unless wabadilishe style. Nafasi inayoshikiliwa sasa na Megan Rapinoe inabidi apewe Jessica McDonald katika kipindi cha kwanza; Rapinoe hana kasi inayotakiwa katika mashindano haya kwa sasa kama ile ile MacDonald.
 
World cup imebaki kuwa baina ya USA na Europe. Timu zote nje ya Europe zimeshatolewa isipokuwa USA. Hata hivyo survival ya USA iko mashakani sana hasa baada ya kuhangaika sana kuifunga Spain kwa penalty, timu ambayo haikuwa tishio kwa timu za Ujerumani, France na England. Kwa hiyo mchezo wa Kesho baina ya USA na France ndio utakaomua future ya USA. Iwapo USA itaweza kuitoa France, basi inakuwa karibu na ubingwa tena, ila chances za kuifunga Ufaranza ni ndogo sana.

Kwenye mechi ya leo baina ya England na Norway, ingawa Norway ilicheza kwa ufundi na nguvu sana, haikuwa riziki yao kwani waliishia kubugizwa mabao 3-0. Ila golikipa wao aliwasaidia kwa kupangua bao moja la penalty.



Kitu nilichoona kwenye michezo hii, magolikipa wa kike wako sharp sana kuzuia penalty. Tangu michezo hii ianze, wameshuzuia zaidi penalties sita ukichanganya na zile zilizokataliwa kutokana ni hii sheria mbovu ya VAR.
 
World cup imebaki kuwa baina ya USA na Europe. Timu zote nje ya Europe zimeshatolewa isipokuwa USA. Hata hivyo survival ya USA iko mashakani sana hasa baada ya kuhangaika sana kuifunga Spain kwa penalty, timu ambayo haikuwa tishio kwa timu za Ujerumani, France na England. Kwa hiyo mchezo wa Kesho baina ya USA na France ndio utakaomua future ya USA. Iwapo USA itaweza kuitoa France, basi inakuwa karibu na ubingwa tena, ila chances za kuifunga Ufaranza ni ndogo sana.

Kwenye mechi ya leo baina ya England na Norway, ingawa Norway ilicheza kwa ufundi na nguvu sana, haikuwa riziki yao kwani waliishia kubugizwa mabao 3-0. Ila golikipa wao aliwasaidia kwa kupangua bao moja la penalty.



Kitu nilichoona kwenye michezo hii, magolikipa wa kike wako sharp sana kuzuia penalty. Tangu michezo hii ianze, wameshuzuia zaidi penalties sita ukichanganya na zile zilizokataliwa kutokana ni hii sheria mbovu ya VAR.
Game Kali sana France vs USA. Mpira unapigwa mwingi sanaa mpaka unainjoi.
 
Game Kali sana France vs USA. Mpira unapigwa mwingi sanaa mpaka unainjoi.
Dk.33 France ameshalizwa moja Ila wana forward yao anaitwa diani huyu Dada anacheza sana.kwa kifupi mechi Kali sana sina mpango wa kuangilia mechi ya south Africa na Namibia maana sitainjoi kama hiii maana najua mechi itajaa butua butua tu
 
Timu ya ya wanawake ya Ufaransa inaelekea kuja kuwa tishio kubwa kwa marekani, kwani watoto hao nililiwaona wana ball controll ya hali ya juu sana. Ingawa wachina wamefungwa na ujerumani, ni dhahiri kuwa walikuwa na resistance kubwa na ujerumani ilicheza mchezo wa hali ya chini sana.

Dada zetu wa Banyana Banyana wa South Africa walianza vizuri na kuwapa wakati mgtumu Spain lakini wamekuwa wakielemea sana kadri muda unavyokwenda na dakika hihi hihii wamefungwa goli la pili; sijui kama watakata tamaa.

Ratiba kamili ya michezo yote iko hapa Paris France

Updates: Banyana Banyana wameishiwa sana pumzi dakika za mwisho na kuishia kufungwa 3-1
Wananichukiza nimeacha kuangalia mechi zao,yaani mchezaji anafunga goli la ushindi dakika ya 90 halafu havui jezi wakati wa kushangilia (Joke)😂😂😂
 
Dk.33 France ameshalizwa moja Ila wana forward yao anaitwa diani huyu Dada anacheza sana.kwa kifupi mechi Kali sana sina mpango wa kuangilia mechi ya south Africa na Namibia maana sitainjoi kama hiii maana najua mechi itajaa butua butua tu
USA kashinda lakini mechi ilikua nzuri sana.France wamecheza mno bahati haikuwa yao
 
Mtanange baina ya USA na France ulikuwa Mkali sana; France walicheza kandanda la hali ya juu sana huku USA ikiwa na ball control ya hali ya chini sana kiasi kuwa walikuwa wakinyang'anywa au kupoteza mipira yao kirahisi wa Ufaransa. Kuna mchezaji wao machachari Diani alikuwa hatari sana kwa USA. Hata hivyo USA walicheza kwa kulenga goli vizuri sana na kwa makali sana kiashi cha kuweza kuibuka kidedea 2-1. Golikipa wa zamani wa USA amekiri kuwa USA imeshinda kwa bahati tu, hawakuonyesha mchezo wa kibingwa. Ball possession France 60%, USA 40%, lakini hata hivyo ushindi ni mabao, siyo chenga.

 
Back
Top Bottom