Wewe umefanya nini?? Au wewe ni Mkenya au Mganda?? Hao wabongo unaowasema na wewe upo humohumo- tabia hizohizo..
Kuhusu Mimi nimefanya nini? swali zuri sana.
Binafsi Mimi huwa sipendi unyonge na nikiona jambo haliko sawa huwa silikalii kimya lazima nitafute namna ya kukabiliana nalo au nimuwajibishe muhusika.
Kuna kipindi mtaani kwetu kulikuwa na wezi sana, watu walikuwa wanavamiwa usiku na vibaka wanaibiwa flat screens zao na wengine mifugo...!!
Wengi walikuwa wanaishia kulalamika tu bila kuchukua hatua yoyote, ikabidi Mimi nimtafute mwenyewe kiti na mtendaji wa kata na kuwashurutisha waitishe kikao Cha nzengo kwa ajili ya majadiliano ya kukomesha huo wizi... Na kweli Hilo likafanyika.
Tukawekeana mkubaliano pale tutafute walinzi tutakaowalipa Kila mwezi na kwa asiyelipa basi yeye atakuwa anaungana na wale walinzi kulinda usiku.
Nililisimamia Hilo zoezi kwa muda wa miezi mitatu na likaleta matokeo chanya, wizi uliisha kabisa ule mtaa mpaka naondoka sikuskia mtu yeyote kaibiwa.
Kwa hiyo unaweza ukaona ni jinsi gani nilivyokuwa na spirit au uthubutu wa kuleta mabadiliko,
Mimi sio mtu wa kulalamika lalamika tu hata kwa jambo ambalo naona linawezekana kutatulika, nitoe kwenye kundi la hao wabongo wanapenda kulalamika bila kuchukua hatua huku wakitegemea sijui huruma ya Mungu.