Uchaguzi 2020 2020 Urais: Twende na Prof. Assad

Uchaguzi 2020 2020 Urais: Twende na Prof. Assad

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Sasa ni muda mwafaka kwa profesa Assad kugombea urais 2020 kwa chama chochote tofauti na kile chama kingine

Profesa kwenye kipindi chake amesimamia ukweli na kama ni uzalendo ameuonyesha hadharani kuliko bwana yule

Profesa karibu kwenye siasa,wananchi wanakupenda,wameona,wewe ndo mkombozi wa nchi hii,kila mtu ameona juhudi zako za kufichua zile trillion na kilichotokea baada ya kuunyoshea kidole ule mhimili

2020 twende na Assad,Mungu pamoja nawe
 
2020 twende na cutelove, Mimi na familia yangu nakuhahakishia kura za ndio ukiamua kugombea urais
 
Prof Assad (Assad = Simba) amelitendea haki jina lake na elimu yake, amethubutu kusimamia ukweli kwa maslahi ya taifa tena bila kuogopa muhimili wowote ule nchi hii. Sio wale wanaoteuliwa halafu badala ya kufanya kazi wana kutetea ugali wao (Kama yule wa bungeni, mnene mnene hivi halafu mfupi kama kiroba cha mahindi. Na yule mwingine ana hips kuliko hata mke wake).

Hii nchi Prof Assad angepata support na ruhusa ya kukagua miradi yote mpaka ile aliozuiluwa asikague mahesabu yake (ATCL, STIEGLERS, WIZARA YA MADINI) basi angetoa wadudu yakutisha.

Ila ni kawaida kwa nchi yetu yule bwana kupiga kelele eti "MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUGU", ila wale wanaosema ukweli ndio anaowaona hawafai kwenye uongozi huu, wanaofaa ni wale wakuunga mkono juhudi na waongo kama wamebatizwa.

Charles Kichere eti kateuliwa kua CAG, wakati hata ubalozi wa nyumba kumi hawezi. Aibu kweli.
 
Mwacheni mzee apumzike, hizo siasa zenu uchwara komaeni wenyewe.!
 
Sasa ni muda mwafaka kwa profesa Assad kugombea urais 2020 kwa chama chochote tofauti na kile chama kingine

Profesa kwenye kipindi chake amesimamia ukweli na kama ni uzalendo ameuonyesha hadharani kuliko bwana yule

Profesa karibu kwenye siasa,wananchi wanakupenda,wameona,wewe ndo mkombozi wa nchi hii,kila mtu ameona juhudi zako za kufichua zile trillion na kilichotokea baada ya kuunyoshea kidole ule mhimili

2020 twende na Assad,Mungu pamoja nawe
Bakwata zamu yao ni 2025 kwa mujibu wa utaratibu wa CCM!
 
Prof Asad ni presidential material. Lkn atapenyea wapi ili kuifikia ikulu? Maana dikteta uchwara ameifanya nchi kuwa mali yake.

Marais wastaafu wakiongea anasema wanawashwa washwa.

Wakiongea makatibu wastaafu wa ccm wakilalamika kwa waraka wanageuka kuwa maadui na wanarekodiwa mpk sauti zao

Waandiahi, waoinzani na wanaharakati wakiandika ama wakisema kwa kukosoa wanapotezwa, wanapigwa risasi, wanauawa ama kupewa kesi za uhujumu uchumi. Nchi imetekwa hii
 
Prof Assas ana kaliba ya Prof Kigoma Malima, na akiingia kwenye siasa atapata wafuasi wengi Waislam walio wengi ambao wanaamini bado tz kuna chembechembe za ubaguzi.

Ataweza pia kuunganisha upinzani kwa ambao wanamuamini na walimuunga mkono wakati wa timbili kati yake na ngundai
 
Back
Top Bottom