2021 AFCON Special Thread

Hahahaha mambo ya kuombeana njaa haya Egypt wako vipi sijasikia ukiwaongelea
 
Ligi ya Tanzania ni ya 8 Afrika kwa ubora.
Jifariji tu na takwimu za kuliwaza. Wachezaji hao wenye uafadhali wa kiuchezaji ni raia wazalendo au wachezaji wa kigeni?

Tunapokuwa na mechi za kimataifa na wazalendo wetu huwa tunatoboa au tunabaki kiichwa cha mwendawazimu?

Hiyo kuwa namba 8 kwa ubora wa ligi Afrika ni kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.

Kubali tu bado uendashaji wetu wa soka unatakiwa ushirikishwaji mkubwa wenye maono mujarabu ili kuwa na matokeo chanya Kimataifa. Vinginevyo itakuwa Yanga, Simba,Azam kila siku miaka nenda rudi bila kuwa na timu bora ya taifa na tishio Afrika na Duniani.
 
Udini unakusumbua, na haukusaidii chochote.
 
sijapinga popote nimekueleza tuu kwamba ni ya 8 kitakwimu wewe ulisema ni ya mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…