2021 AFCON Special Thread

Mkuu Nigendako pole aisee ndo naona saa hii. Duuh! Ilikuwaje tena?

Mi mwenyewe nilikuwa na kaunaijeria kidogo kwani walau niliwaona wana uhai.
Nigeria jana tumeingia mchezoni tukiwa tumejiamini kupita kiasi, tulilewa sifa kwenye game za makundi tukawachukulia poa Tunisia..

Mwisho wa siku tukapigwa na kitu kizito [emoji3]

Tupeane pole Shadeeya umetoka Algeria ukahamia Nigeria, sasa hivi unaenda wapi tena [emoji3]
 
Hamna jinsi kwa kweli zaidi ya kupeana pole japo imejua kutuangusha bana.

Sasa hivi nahamia kwa wenyeji. Hahahahaaaa.
Wakitolewa ntachagua ingine mpaka mashindano yanakwisha.
 
We ndio unabakia huna timu ama? Hahahaaaa.
 
Mlisema kwa nigeria, sasa kwa Ivory coast 😆 hivi unazichukuliaje timu kama Morocco, egypt na Tunisia? Morocco or Tunisia wanabeba, mark my words
Tokea nimeumbwa timu zangu zifuatazo Africa Ivory Coast na ikizingua huwa nawaamini sana Algeria. World Cup France. Huko kungine ni Arsenal na Simba
 
Fatilia kwanza mwenendo wa hali za vikosi
Hii AfCON haina vikosi na ingekuwa hivyo Malawi wasingekuwepo bali Ghana,Gabon na Nigeria wangebaki hadi mda huu. Awali niliwapa sana nafasi Algeria ila sioni wakifanya maajabu yoyote yale. Kandanda safi limebaki kwa Burkina na Cod'voir lakini kikubwa zaidi fighting spirit yao is very high na mchezo huwa wanautaka. Narudia tena leo Gambia na Cameroon out
 
Magolikipa wa Comoro wana corona hivyo mchezaji wa ndani atalazimika kwenda kudaka...kama ni kweli Cameroon safari nyeupe robo
 
Mpira wa miguu una siri kubwa sana
Pana mdau siku zilizopita alitahadharisha kuwa timu kubwa zinapoanza kwa kujikongoja baadae hubadilika pana baadhi ya wadau wakabisha nakumbuka miaka ilopita kwa ulaya timu za italy na ujerumani ilikuwa wana kawaida hiyo mkiwaacha wakapenya kwa taabu na dhiki baadae wana ng'ang'ania inakuwa mbinde kuwatoa nadhani bado pana sintofahamu nyingi zitajitokeza. Kwa Nigeria kwa kuwa ni majirani hata kwa mguu watarudi nyumbani kama bado hawajaanza safari.
 
Tunaoenda na Cameroon Tujuane mapema kabisaaaaa sio tukishapiga mtu 4G ndio mjitokeze!
Cameroon kafanyia wenzake figisu kwa mgongo wa corona.Huu uenyeji unamfanya awe na mbinu nyingi nje ya uwanja.maana haiwezekani comoro kacheza vizuri makundi sasa hivi ndo linaibuka la corona.ila ngoja tuone itakavyokua.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…