Namshukuru MUNGU ameniwezesha kuwasaidia watu katika magonjwa na misiba ambapo niliweza kusaidia misiba miwili kijijini kwetu kikamilifu kwa kuchangia gharama za mochwari,usafiri ,mazishi na chakula.
Pia niliweza kusaidia matibabu ya wagonjwa kadhaa wa kijijini kwetu kwa kuchangia matibabu katika dawa ,usafiri na chakula kwa wagonjwa.
Na bila kusahau wanafunzi mbalimbali hasa wa shule za msingi na sekondari waliokuwa wanaanza masomo yao kwa kuchangia nauli, sare na madaftari.
Namshukuru sana MUNGU wetu kunipa ujasiri wa kutochangia sherehe mbalimbali kama vile sendoff,harusi,kipaimala,birthday,n.k.
Nimefarijika sana kwa hili na Mungu atubariki wote wenye moyo kama huu kiachana na masheikh,wachungaji,maaskofu,nk wanaofuga matumbo yao kwa kiwanyonya maskini ambao hawawachangii katika matatizo yao.