Kausha damu lazima wapigwe vita hawa ni wakina mama na dada za watu hivi mabinti na wadogo zao wakiona yanayoendelea wanajifunza nini? Matokeo yake watoto wa kike hawataki shule wala kujishughulisha na shughuli halali za kuwapa kipato wakijua kudanga kunalipa, na tunaongea haya sio kwamba tunawaonea uwivu ila tunawalinda pia huko kwenye viwanja vya starehe mabinti wadogo wanaleweshwa pombe na kuishia kuingiliwa kinyume na maumbile wakiwa hawajielewi hii yote ni kuendekeza vya bure, wangeenda kiwanja kwa gharama zao kuanzia usafiri, chakula, vinywaji n.k wangekua hawafanyiwi haya matendo. Hatuwezi kutengeneza kizazi cha kausha damu eti kwa sababu wanaume wanatoa hela kwa hiyari yao sio wanaume wote wanawapa hela kwa mema wengine lengo lao ni kuwafanyia maovu.. Mwanamke lazima akumbushwe kuwajibika.