HANGAYA THE CHIEF
JF-Expert Member
- Sep 10, 2021
- 330
- 962
KURA YANGU NI KURA YA UPENDO KWA TANGANYIKA:
Kwa kuwa mihimili inayoongoza nchi yetu imetoa baraka, kwa maana ya serikali, kupitia ikulu imebariki, bunge kwa mbwembwe na bashasha imebariki, na mahakama imeshindwa kutoa msimamo wake kwa kuogopa kuingia madaraka.
Sihitaji kuungwa mkono, wala kumshawishi mtu aungane nami, ili nafsi yangu ipate amani na niwe sehemu ya raia wema walioshiriki kwa vitendo kutetea rasilimali za Tanganyika yangu, kwa vizazi vijavyo, ahadi yangu kwa Mungu wangu aliyenipa uhai na kupenda nizaliwe Tanganyika ni Kura yangu kwa rasilimali za tanganyika. kwa lengo la kutanza amana alizotupa Mungu, kama wazee wetu wakina nyerere walivyoona thamani ya rasilimali zetu, nitapiga kura ya upendo kwa tanganyika, kwa ajili ya sisi tuliopo na watako kuja.
Nitampigia Rais mwenye uwezo wa kutunza, kutetea rasilimali za Tanganyika kwa ajili UPENDO wa kunufaisha vizazi vyetu na vijavyo, itakuwa kura ya ahadi kwa Mungu, sitaangalia chama, sitaangalia, sitaangalia sura, nitaangalia Rais mwenye upendo na wivu wa rasilimali zetu kwa ajili ya wote.
Nitakwenda kupiga kura, hata kama ikiibiwa, ikipotea, ikivurugwa, lakini ili kusahifisha nafsi yangu mbele ya Mungu na mapenzi kwa nchi yangu ya Tanganyika, hiyo ndio ahadi yangu kwa Mungu wangu akiniweka hai mpaka 2025 kwamba kura yangu ni kura ya Upendo kwa Tanganyika.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanganyika