2025 Kampeni zake itakuwa, Nipeni kura nikarudishe nchi mikononi mwenu, huku ni kusema ccm imeturudisha utumwani!

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Tulizoea kuona kila chama kikija na mikakati ya kuboresha maisha ya watanzania, ya kuwatoa mahali walipo na kuwasogeza pahala!

Kwa sasa jambo kubwa kabisa ambalo litakuwa kuanza kuzungumziwa kwenye Kampeni za 2025, itakuwa ni hilo ndipo yafuate mengine,

Hii ni sawa na kusema! Ccm imetuuza tena kwa mwarabu, nchi inahitaji ukombozi wa maeneo yetu

Anayeipinga kusema sisi kwa sasa sio watumwa wa mwarabu abishe hapa kwa hoja,

Inakuwaje baadhi ya maeneo yetu yawe chini ya mwarabu Milele? Huku siyo kuwa chini ya utumwa?

Maana yake 2025 tunahitaji vyama vitakavyoweka mikakati ya kuhakikisha vinakwenda kupambana ili kurudisha nchi yetu mikononi mwetu. Siyo??
 
apo kwenye vyama apo 🙄🤔
 
Kipimo cha akili ya Mtanganyika ni uchaguzi ujao,nawambia kama watanganyika akili mnazo au Hamnazo ni next Election. Yangu macho!!
 
Katiba Mpya! Katiba Mpya! Katiba Mpya!

Mengine yote, ikiwa ni pamoja na uchaguzi mkuu, yaje baada ya kupatikana hiyo katiba.

Nje au kinyume na hilo ni kujidanganya na kujilisha upepo.
 
Hakuna uchaguzi Tanzania boss, na dhalimu alikuja kumaliza imani kidogo ya box la kura iliyokuwepo. Zungumzia machafuko au mapinduzi ya kijeshi zaidi, sio uchaguzi. Hakuna mtu mwenye akili timamu atapoteza muda wake kwenda kusimama kwenye mstari wa kura wakati box la kura haliheshimiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…