Samahani hapo unaweza kunikadiria gharama za Ujenzi wa msingi (foundation) kiwanja tambarare
View attachment 3524595
Okeey
Mi sio Architect ila Hii Ramani yako nikama inavipengele
.
1. Jamaa alie iandaa Alimaliza kuichora kwanza then aka type hizo dimensions. Madhara yake ni kwamba ukiinput hizo dimensions shape ya jengo inaweza change. Pia baadhi ya dimensions hapo ni kubwa sana kwa normal standard dimension za vyumba
Yaan house of two bedrooms Ina bedroom yenye 4 kwa 6m?!
2. Kwanini sebule ina Entrance mbili?! Ndo umetaka iwe hivyo?!
3. Hio Utilities hapo inakazi gani?!
Kwa experience ndogo
Hio duct huwa tunaweka kwenye ghorofa kwaajili ya kupitisha pipes za maji taka na safi kupeleka floors za juu
Ama ku cover downpipes zinazotoa maji kutokea kwenye roof juu kuleta chini.
Ingeweza kutumika kwa kuweka downpipes lakini bado haikutakiwa kuwa hapo, tena isinge kua moja.
4. Kwenye living room kuna mansory closet, huoni kama itaongeza gharama sizizo za msingi?
It's better kutumia flexible carpentry cabinet na sio la kujengea tofali
Sisemi unipe kazi ya kukutaftia Ramani nzuri nipate hela hapo🖐️
Nataka upate Ramani nzuri kwanza then tuiandalie gharama