23% tu ya wanafunzi ndiyo wanamudu lugha ya kiingereza kidato cha kwanza sekondari

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Mwanza, Tanzania

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Elimu - wizara ya TAMISEMI Dr. Charles Enock Msonde na Dr. Lyabwene Mtahabwa - kamnishna wa elimu kutoka wizara ya elimu wahimiza waalimu wa darasa la kwanza na darasa la tatu shule ya msingi wawe mahiri ktk masomo yao huku vigezo vya lazima kwa waalimu viwe digrii yenye matokeo ya daraja la ufaulu wa juu vya elimu ya juu ya Chuo Kikuu
video : source : millard ayo

Habari hiyo muhimu juu ya yanayojiri katika hatua za kujaribu kuleta Mapinduzi ya elimu yalifahamika katika mkutano wa maafisa elimu wa mikoa na halmashauri kuhusu njia gani zitumike kubadili hali hiyo ya sasa hasa ktk kuwajengea msingi imara wa uwezo wa masomo ya kuhesabu, kuandika, hisabati, lugha ya taifa kiswahili na lugha ya kigeni kwani katika umri huo mdogo wa darasa la kwanza na la tatu katika elimu ya msingi ndiyo itawajengea msingi mzuri wa kielimu kwenda mbele.

N.B
Waalimu wengi wa chekechea na shule za msingi nchi za Scandinavia na Ulaya huwa na elimu za Ph.D na masters ili kuwajenga watoto wadogo vizuri kuelimu
 
Hivi mlishawahi kukaa na kujadiri maslahi ya hawa waalimu?

Mwalimu analipwa 300k per month jumlisha mfumuko wa bei na hali mbaya hii ya maisha mnafikiri huo umahili atautoa wapi?

Mbunge ambaye elimu yake ni darasa la saba analipwa mil 12 na posho za vikao juu, lakini mwalimu mwenye diploma analipwa 400k na mnamuandama huyu mwalimu aongeze ufanisi autoe wapi?
 
Hiyo 23% labda ni kwa shule za Mijini tu, Vijijini hawafiki hata 0.1%, kimsingi hakuna Form One anayetoka shule za serikali vijijini, na kufika sekondari anajua kingereza, Hayupo.

Wameng'ang'ania Lugha ya watu, Tunaua Elimu.
 
Hata waalimu watanzania 10% hamudu kugha ya kiingerza itakua je kwa wanafunzi iwe 23% wewe pitia mashuleni usikilize kiingereza cha hao waalimu.
Umahiri wa kiingereza ni tatizo la kitaifa hata kwenye ualimu kuna nafuu sana bcoz kiingereza chao ni chakufundishia but in fluent speaking specifically kwenye maongezi ya kawaida nakubali hawako mahiri but ulishawahi kuwasikia mawaziri wetu wakiongea kiingereza tena wengine wana mpaka PhD
 
Hiyo 23% labda ni kwa shule za Mijini tu, Vijijini hawafiki hata 0.1%, kimsingi hakuna Form One anayetoka shule za serikali vijijini, na kufika sekondari anajua kingereza, Hayupo.

Wameng'ang'ania Lugha ya watu, Tunaua Elimu.
Usikariri bos sku english medium zipo mpaka vijijini
 
Unategemea mtoto kwenye foundation level (shule za msingi) umfundishe kwa kiswahili halafu aje ajue kiingereza kimiujiza ghafla tu.

Mfumo wetu wa elimu ni mbovu haujawahi kuwepo pengine duniani.
Ni nani atakaye kubaliana na ukweli huu nje ya moyo wake kati ya walio na dhamana?
 
Anayo point ya msingi sana, wataalamu wanasema kuna umri fulani wa mtoto ambapo ni rahisi zaidi kujifunza lugha. Kiingereza kifundishwe na wabobezi kwenye kipindi hicho (chekechea mpaka darasa la tatu)
Ni kweli kabisa,nikiwa bado sijaanza darasa la Kindergarten/vidudu,mimi na dada yangu tulikuwa kipindii tunakaa kwa wazee Dar,then tunaenda kwa Babu Munkinyaa,tunakaa hata miezi mitatu hadi minne..sasa kipindi tukienda kwa babu ile miezi 3 hadi minne (4) tulikuwa tunasahau Kiswahili lakini tunamasta kilugha,kinyaturu..tukirudi Dar hivyo hivyo,baada ya muda kidogo tumesahau Kilugha,tumemasta Kiswahili

Hivyo naunga mkono hoja LUGHA ya Kiingereza watoto wafundishwe ingali wadogo,na waalimu wabobezi bila kusahau uwepo wa nyenzo na miundombinu ya kutosha
 
hapo kwenye “NB”, tutume kamati iende huko, walipiwe VIP class tiketi za ndege waje na mapendekezo namna ya kulitekeleza suala hilo. Elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa. 😃😃
 
Hiyo 23% labda ni kwa shule za Mijini tu, Vijijini hawafiki hata 0.1%, kimsingi hakuna Form One anayetoka shule za serikali vijijini, na kufika sekondari anajua kingereza, Hayupo.

Wameng'ang'ania Lugha ya watu, Tunaua Elimu.
Hakika ndivyo ilivyo...

Tatizo ni mfumo mzima wa elimu yetu unaobebwa na msingi wa lugha..

Nenda shule zetu za sekondari iwe za mjini au vijijini, ambako tunaambiwa lugha ya kufundishia ni Kiingereza, lakini cha ajabu ni kuwa language competence ya walimu hawa kwa zaidi ya 90% iko below average.

Yaani kwa lugha rahisi na ya moja kwa moja ni kuwa, walimu hawa hawamudu kabisa lugha ya kiingereza kiasi cha kupewa nafasi ya kufundisha wengine na wengi wa walimu hawa eti ni university graduates..

Na maana yake ni kuwa tatizo hili lipo kuanzia huku chini kwenye grassroots (kindergarten & primary school levels) mpaka huko University level...

Na huko kindergarten & primary school level, hakuna walimu competent wa lugha ya lugha ya kiingereza...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…