Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Mimi nasema HAPANA..Lugha ya kufundishia iwe kingereza toka chekechea hadi chuo kikuu.
Kiswahili kifundishwe kama somo toka chekechea hadi form six.
Tatizo kuna walimu kiduchu sana wa kiingereza.
Kung’ang’ania kiswahili kwa sababu za kizalendo ishapitwa na wakati.
Hata hivyo uzalendo wa kweli hakuna, ni mtindo wa unafiki, uongo na ufisadi umejaa.
Lugha ya kufundishia iwe hii tunayoita "LUGHA YA TAIFA" yaani KISWAHILI...
Honestly, Mimi nilishashindwaga kuelewa kwanini hasa tunaogopa kutumia lugha yetu ya Kiswahili tunayoielewa kutolea ElLIMU (yaani UJUZI na MAARIFA) kwa watoto wetu...
Lugha ya Kiingereza iwe ni somo la kawaida na mtu akitaka kuimudu, atumie bidii yake kujifunza....
Lakini MAARIFA na UJUZI yahamishwe toka kizazi hata kizazi kwa lugha inayoeleweka na pande zote mbili, yaani atoaye na apokeaye hayo maarifa na ujuzi...
Taifa lolote lililopuuza na kudharau component muhimu ya "lugha" kama sehemu ya utamaduni wake na kuuenzi utamaduni huo, lisahau milele kukua kisayansi na kiteknolojia na kisha kimaendeleo...!!
Tujifunze kwa nchi kama China, Japan, Ubelgiji, Korea, Urusi na zingine nyingi huko duniani wanaotumia lugha zao kutolea elimu. Mengi yamezagaa dunia nzima yakijenga mabarabara, madaraja, yaki - operate viwanda vya kila aina nk lakini mengi ya haya mamtu hata Kiingereza hayakijui...!!!
Tuwe tunapenda au hatupendi, sisi kama Taifa la bado tuko kwenye "ukoloni mamboleo wa lugha ya Kiingereza" na kwa maana hiyo, lugha ni kikwazo kikubwa cha kushindwa kwetu kupiga hatua za haraka za maendeleo ya sayansi na teknolojia hapa nchini kwetu...!!
Kosa lilifanyikaga toka mwanzo wa kuwekwa kwa misingi ya Taifa hili. Hayati Mwl Julius K. Nyerere na waasisi wenzake wa Taifa hili walikosea sana kutuwekea lugha mbili za kutolea elimu. Wangeamuaga tu toka mwanzo kuwa aidha iwe KIINGEREZA a KISWAHILI kuanzia chini mpaka juu. Lakini kwa mbili, it was a big mistake...
Hata hivyo, tunaweza kurekebisha sasa makosa hayo...!!