Tuwasikilize hawa wanataaluma wawili Dr. Charles Enock Msonde naibu katibu mkuu TAMISEMI sekta ya elimu na kamishna wa elimu wa wizara ya Elimu Dr. Lyabwene Mtahabwa kusisitiza umuhimu wa kiingereza katika kupata elimu yenye maarifa mapana
Hii ni dhana potofu na ya kipuuzi kabisa toka Kwa watu wanaojiita "wasomi"...
Kiingereza ni lugha sawasawa tu kama kilivyo kiswahili..
Ujinga ni watu
wawili wajinga kuamua kulazimisha kuwasiliana kwa lugha wasiojua. Matokeo yake ni kuwa watu hawa hawataelewana. Hii ndiyo hali ya mwanafunzi na mwalimu wa Tanzania. Wanatumia lugha ya Kiingereza wasioijua vyema kufundisha a...!
Huo kama siyo ujinga ni Nini eti??
maana kiswahili kina maneno machache yanayobeba dhama maalum ya sayansi, sheria, utabibu, fizikia ndiyo maana lugha kubwa duniani zimekopa maneno ya maeneo ya kitaaluma, sayansi n.k toka lugha za Kigiriki, kilatini..
Mawazo potofu na ya kipuuzi tena toka kwa wanaojiita "wasomi".
JIBU LA HOJA YAKO: Si kweli...!!!
Kiswahili ni lugha iliyo sawa tu na lugha nyingine yoyote kikiwemo Kiingereza. Kiswahili Kwa wanaokijua kiswahili na Kiingereza Kwa wanaojua Kiingereza.
Kiswahili kina misamiati yote utakayo katika nyanja zote za maisha iwe ni siasa, uchumi, sayansi, utsbibu, elimu viumbe hai, ubaharia, sheria nk nk
Tujiulize je kiSwahili mbali ya kuwa lugha iliyonikita zaidi ktk maeneo machache tu kama kuwezesha Mawasiliano mepesi na kutumika katika mashairi na tenzi.
Unaandika kwa hisia tu kwa kuwa ndivyo ulivyofundishwa kwa kukaririshwa na walimu wako waliokufundisha kwenye shule zenu hizi wakikudanganya kuwa Kiswahili hakina misamiati mingi kwa kuwa eti;
✓
Hutumika kwa mawasiliano mepesi..!!!!???
====Sijui hata unamaanisha Nini hapa===!
====mawasiliano magumu (ambayo ni kinyume cha mepesi) ni yepi hayo eti===?
✓
Hutumika kwenye tenzi na mashairi..!!!????
====Na hapa sijui umefyatua nini tu===!!
====Je, una maana kichina, kijapan, kiarabu, kurusi nk ni lugha isiyotumika kwenye mashairi na tenzi??
Je lugha ya kiswahili na mapungufu yake haya inaweza kutumika kama lugha za Mandarini, Kijapani, Kingussie kufundisha utabibu, bailojia, fizikia, molekula, uhandisi, uwakili, internal medicine, Nishati ya Nuklia n.k
bagamoyo, lugha ya kiswahili Haina shida wala upungufu wowote. Mwenye shida na mapungufu ni wewe mwenye fikra potofu za namna hiyo..
Kila lugha inajitosheleza yenyewe ili mradi inaeleweka na jamii yote ya watu hao wazungumzao lugha hiyo...
Na pale inapoonekana imepungugua, basi inaweza kukopa au kuazima maneno toka lugha nyingine. Na kiuhalisia kiswahili chetu kipo hivyo...
Hata Kiingereza, kimekopa au kimetohoa maneno mengi toka lugha zingine mfano Kifaransa, kiarabu, kigiriki, kiyunani, Kiyahudi nk nk
Mfano masuala haya kweli yanaweza yanafundishika ktk kiswahili kwa sasa upande wa utabibu / uganga na ukapikika kitaaluma ?
- Medical cell biology and genetics.
- Pathological processes.
- Health behaviours, musculoskeletal, respiratory and digestive systems.
- Evidence based medicine and research methods.
- Clinical procedural skills.
- Ethics and law in clinical practice.
- Mechanisms of drug action.
- Biology of disease
Absolutely, Yes...!
Yanaweza kufundishwa Kwa lugha yoyote na mtu anayeelewa lugha hiyo akapokea maarifa kwa kiwango stahili na ukamilifu wake....
Ni kazi moja tu inahitajika. Nayo ni kuyatafsiri maneno hayo kwenda ktk lugha ya
waliokusudiwa na kuweka wazi maana/mantiki iliyo ktk terms hizo...
That's all. Hakuna kingine hapo...
Otherwise, wewe
bagamoyo ndiye utuambie kwanini unadhani hayawezekani?
Mfano, unaifahamu
Biblia Takatifu wewe? Kwa taarifa yako tu ni kuwa, hicho kitabu hicho kimetafsiriwa kwa lugha zote za dunia hii..!!
Kwanini kimetafsiriwa kwa Kila lugha za hapa duniani?
Jibu ni rahisi tu. Kwamba, ni ili ujumbe na maarifa yaliyomo kwenye kitabu hicho yasomwe na kueleweka na watu wote duniani kwa Kila mtu na lugha yake...!
Kama Hilo limewezekana, kwanini isiwe kwenye VITABU vya elimu dunia Kwa ajili ya jamii???
Ukipata jibu la SWALI hilo☝️☝️☝️☝️, njoo tuzungumze