23% tu ya wanafunzi ndiyo wanamudu lugha ya kiingereza kidato cha kwanza sekondari

SASA TUKIWAAMBIA WALIMU KUWA WAJIONGEZA WANATUPIGA MAJUNGU


WALIMU WA KIIINGEREZA NI KICHEKESHO
 
Hakuna mwalimu anayelipwa kiasi hicho.
Una lengo la kupotosha umma kwa maslahi yako.
 
Unategemea mtoto kwenye foundation level (shule za msingi)

Na mbaya zaidi waalimu lugha ya taifa ya Kiswahili pia hawaimudu vilivyo, hivyo kufundisha kuhesabu, hisabati, kuandika maneno sanifu ya kiswahili n.k pia ni mtihani mkubwa maana lugha ya kiswahili wanayoitumia waalimu inashindwa kuleta mantiki kirahisi ktk bongo za watoto.
 
Ndio iko hivyo mwisho wa siku wanalaumiwa watoto kuwa wanafeli. Hatari sana.
 
Tatizo la kiingereza ni lakitaifa ,watanzania hata baadhi ya malecturers hawapo vizuri kwenye ngeli
 
Huwezi ukasoma shule za Tz Hadi chuo kikuu ukaelewa kingereza kwa ufasaha , sisi baadhi yetu tulisoma Uganda ndo tumeweza kidogo kuongea kimalkia
Uongo

Tanzania watoto kibao English medium.za Tanzania wa chekechea ns Primary wanaongea kingereza kilichonyooka kibao
 
lugha ya kiswahili ibaki kama somo katika ngazi zote za elimu
 
Hata waalimu watanzania 10% hawamudu lugha ya kiingereza itakua je kwa wanafunzi iwe 23% wewe pitia mashuleni usikilize kiingereza cha hao waalimu.
... mwalimu mmoja anafundisha utitiri wa watoto. By the way, hiyo 23% ya wanaomudu kiingereza booster ni English medium schools otherwise ingekuwa 3%!
 
Huwezi ukasoma shule za Tz Hadi chuo kikuu ukaelewa kingereza kwa ufasaha , sisi baadhi yetu tulisoma Uganda ndo tumeweza kidogo kuongea kimalkia
Waliosoma Tz miaka ya 50, 60 na robo 70 walikimudu vizuri kiingereza kabla siasa za kijinga za ujamaa hazijaingia nchini.
 
Kujua kuzungumza lugha na ku Imaster vizuri ni mchakato unaoanzia nyumbani unaenda shuleni nk,

Mfumo wetu tulio wengi si rahisi kuimaster lugha hii ya 3 vizuri,

Mfano watoto wa vijijini huko huwa wanaanza na lugha mama,alafu kiswahili kwa taabu,tena wengi wao kiswahili kinaanza ukiwa darasa la 4 huko,na kumbuka kuwa kiswahili kinazungumzwa na jamii kubwa,

Sasa unakuja kumsuprize na lugha ya watu ambayo inampasa aikariri kwa muda wa dk 80 za ufundishaji,Then kwingine huko aendelee na lugha yake kunakuelewa hapo0?

Na sio wanafunzi wa sekondari tu,nenda mpaka wanafunzi wa vyuo vikuu wengi tu,kizungu ni tatizo

Sln, Kama tunahitaji watoto waongee au wapate idea ya kizungu Tuanze na awali huko na sio darasa la 3 kama sasa,iwekwe mikakati ya kiushindani na ki motisha kuhakikisha juhudi binafsi za kusoma lugha zinafikiwa

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimewahi kusikia wakiongea, kina Joyce Ndalichako, Jpm etc. Mbona kiingereza kizuri tuu? 🤣🤣🤣
 
Serikali ibadilishe mitaala iwe ya Kiingeleza na Kiswahili....

Lugha ya kufundishia iwe kingereza toka chekechea hadi chuo kikuu.

Kiswahili kifundishwe kama somo toka chekechea hadi form six.

Tatizo kuna walimu kiduchu sana wa kiingereza.

Kung’ang’ania kiswahili kwa sababu za kizalendo ishapitwa na wakati.
Hata hivyo uzalendo wa kweli hakuna, ni mtindo wa unafiki, uongo na ufisadi umejaa.
 
Anayo point ya msingi sana, wataalamu wanasema kuna umri fulani wa mtoto ambapo ni rahisi zaidi kujifunza lugha. Kiingereza kifundishwe na wabobezi kwenye kipindi hicho (chekechea mpaka darasa la tatu)
Hili mimi nililiona mapema nikapeleka mtoto shule ambayo hataongea kiswahili mpaka likizo. Leo hii anashuka ngeli kama maji tu shwaaaa. Wakati baba yake the the the kibao. Uko sahihi
 
Tatizo la kiingereza ni lakitaifa ,watanzania hata baadhi ya malecturers hawapo vizuri kwenye ngeli
Kimsingi hili ni Tatizo la Kujitakia. Ni upumbavu na utumwa kuendelea kung'ang'ania kutumia Kigeni kutolea maarifa.

Ni utumwa!
 
Nakubaliana na wewe kuwa Walimu wanalipwa mshahara kidogo sana.
Lakini kwa mfano mwalimu ambaye si mahiri wa kingereza, hata ukimlipa milioni moja atamudu hiyo lugha?!

Tatizo limetengenezwa na utaratibu wa kuchukua wanafunzi waliofeli au ambao hawakufanya vizuri sana kusomea kozi ya ualimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…