23% tu ya wanafunzi ndiyo wanamudu lugha ya kiingereza kidato cha kwanza sekondari

Hata waalimu watanzania 10% hawamudu lugha ya kiingereza itakua je kwa wanafunzi iwe 23% wewe pitia mashuleni usikilize kiingereza cha hao waalimu.
Tema mate chini, sio 10%, ni 7% ndio wanamudu kiingereza tena sio kile fasaha bali ni kile cha kigugumizi chenye the the the. Mbaya zaidi hata Udsm kuna lecturer wengi tu viingereza vyao vimepindapinda sana, imagine PhD hamfikii kijana wangu wa Form 3.

Tukitaka tuwe wazuri ktk lugha basi tukubali kiingereza kifundishwe kuanzia std 1 . Shida hao walimu watatoka wapi!!? Labda tuagize Kenya na Uganda .

Dr......wa Udsm usiwe na wasiwasi siwezi kukutaja humu kuwa kiingereza chako ni cha kuungaunga, japo ulinisumbua sana nusu ni rudie mwaka
 
. Shida hao walimu watatoka wapi!!? Labda tuagize Kenya na Uganda .

Naunga mkono wakati huu wa mpito kukazania lugha ya kigeni Tanzania ipande basi serikali iajiri waalimu toka nchi jirani ulizotaja pamoja na za Malawi, Zambia, Zimbabwe kwa wingi kisha baada ya miaka 20 ya mkakati huu nchi itakuwa na watanzania mahiri ktk lugha hiyo ya kigeni ktk nyanja / kada zote za jamii ikiwemo waalimu wa shule zote za kata / serikali na private za chekechea msingi, sekondari na wahadhiri wa vyuo vikuu.


Hili linawezekana maana mfano nchi ya Rwanda imefanikiwa kubadili kutoka lugha ya kiFaransa tu na kuongeza umahiri wa matumizi ya lugha ya Kiingereza katika shule na vyuo vya elimu ya Juu.

Rwanda kuwa na lugha nne zinazofundishwa shuleni

"Haina maana lugha hii haikuwepo na wala haina uhusiano wa kuchaguliwa kwa Waziri Mushikiwabo hapana huo ni uzushi mtupu na ndiyo maana tunasema tunaimarisha. Kuimarisha maana yake ni unaimarisha kitu ambacho kilikuwepo. Jjitihada hizi ni mojawapo ya mchakato mzima wa kutathmini jinsi lugha zinavyofundishwa kuanzia kule chini."

Lakini wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lycee de Kigali jijini Kigali wametoa maoni tofautitofauti. Mmoja amesema "Masaa ya kujifunza kifaransa yalikuwa machache ikiliganishwa na yale ya kiingereza." mwenzake mwengine naye ameongeza akisema:

"Ilikuwa haitoshi kwa muda tuliokuwa tunajifunza lakini kwa vyovyote tulijitahidi kuzingatia hayo tulokuwa tunafundishwa."

Kwa uamuzi huu sasa ni dhahiri kwamba lugha nne za Kiswahili, Kingereza, Kifaransa na Kinyarwanda zitakuwa zinafundishwa kwa kiwango sawa nchini Rwanda hali inayowapa wanafunzi fursa kwenye lugha hizi muhimu ulimwenguni ..... Soma zaidi Azma ya Rwana : Rwanda kuimarisha lugha ya Kifaransa – DW – 25.10.2018

 
Bado wapo pale pale tuuu ! Wabadilishe kwanza namna zinavyo patikana degree huko vyuoni ili kuwe na degree zenye tija

Lakini pia ambacho hawakijui ni kwamba ufahuru mkubwa sio kigezo kikubwa sana katika kumfanya mtoto aelewe, cha msingi mwalimu anauwezo wa kufundisha na watoto wakafundishika? Pili jee? Watoto wenyewe katika makuzi na malezi yao wana lelewa katika misingi ya kufundishika kirahisi ,

Ni upumbavu na ujinga msomi kabisa wa daraja lake kuchukua nchi za scandinavia kama case study na kutaka ya scandinavia yawe aplied huku ambako hadi sasa watoto wanatoka katika familia ambazo hata uhakika wa kula mlo wa siku moja hawana , anatembea over 7kms kwenda shule tena na kandambili rangi tofauti,

Hebu tuache .huu ujinga kulinganisha nchi zilizo endelea zilizo weza kukabiliana na over population ili kumudu provision of social services na kinchi kama tanzania ambacho tunazaliana kama panya wakati ni maakini

hawa ma professor hawa hebu watupishe kwanza maana kwanza unaweza kukuta tangu azaliwe hajawahi hata kunya porini au hata choo cha shimo hivyo wanadhani watanzania wote wana enjoy maisha kama wapi upanga na oysterbay
 
Mawaziri wenyewe stress tupu hahahaa nakumbuka kile kingereza cha joyce ndalichako 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tuwasikilize hawa wanataaluma wawili Dr. Charles Enock Msonde naibu katibu mkuu TAMISEMI sekta ya elimu na kamishna wa elimu wa wizara ya Elimu Dr. Lyabwene Mtahabwa kusisitiza umuhimu wa kiingereza katika kupata elimu yenye maarifa mapana
Hii ni dhana potofu na ya kipuuzi kabisa toka Kwa watu wanaojiita "wasomi"...

Kiingereza ni lugha sawasawa tu kama kilivyo kiswahili..

Ujinga ni watu wawili wajinga kuamua kulazimisha kuwasiliana kwa lugha wasiojua. Matokeo yake ni kuwa watu hawa hawataelewana. Hii ndiyo hali ya mwanafunzi na mwalimu wa Tanzania. Wanatumia lugha ya Kiingereza wasioijua vyema kufundisha a...!

Huo kama siyo ujinga ni Nini eti??
maana kiswahili kina maneno machache yanayobeba dhama maalum ya sayansi, sheria, utabibu, fizikia ndiyo maana lugha kubwa duniani zimekopa maneno ya maeneo ya kitaaluma, sayansi n.k toka lugha za Kigiriki, kilatini..
Mawazo potofu na ya kipuuzi tena toka kwa wanaojiita "wasomi".

JIBU LA HOJA YAKO: Si kweli...!!!

Kiswahili ni lugha iliyo sawa tu na lugha nyingine yoyote kikiwemo Kiingereza. Kiswahili Kwa wanaokijua kiswahili na Kiingereza Kwa wanaojua Kiingereza.

Kiswahili kina misamiati yote utakayo katika nyanja zote za maisha iwe ni siasa, uchumi, sayansi, utsbibu, elimu viumbe hai, ubaharia, sheria nk nk
Tujiulize je kiSwahili mbali ya kuwa lugha iliyonikita zaidi ktk maeneo machache tu kama kuwezesha Mawasiliano mepesi na kutumika katika mashairi na tenzi.
Unaandika kwa hisia tu kwa kuwa ndivyo ulivyofundishwa kwa kukaririshwa na walimu wako waliokufundisha kwenye shule zenu hizi wakikudanganya kuwa Kiswahili hakina misamiati mingi kwa kuwa eti;

Hutumika kwa mawasiliano mepesi..!!!!???
====Sijui hata unamaanisha Nini hapa===!
====mawasiliano magumu (ambayo ni kinyume cha mepesi) ni yepi hayo eti===?
Hutumika kwenye tenzi na mashairi..!!!????
====Na hapa sijui umefyatua nini tu===!!
====Je, una maana kichina, kijapan, kiarabu, kurusi nk ni lugha isiyotumika kwenye mashairi na tenzi??
Je lugha ya kiswahili na mapungufu yake haya inaweza kutumika kama lugha za Mandarini, Kijapani, Kingussie kufundisha utabibu, bailojia, fizikia, molekula, uhandisi, uwakili, internal medicine, Nishati ya Nuklia n.k
bagamoyo, lugha ya kiswahili Haina shida wala upungufu wowote. Mwenye shida na mapungufu ni wewe mwenye fikra potofu za namna hiyo..

Kila lugha inajitosheleza yenyewe ili mradi inaeleweka na jamii yote ya watu hao wazungumzao lugha hiyo...

Na pale inapoonekana imepungugua, basi inaweza kukopa au kuazima maneno toka lugha nyingine. Na kiuhalisia kiswahili chetu kipo hivyo...

Hata Kiingereza, kimekopa au kimetohoa maneno mengi toka lugha zingine mfano Kifaransa, kiarabu, kigiriki, kiyunani, Kiyahudi nk nk
Absolutely, Yes...!

Yanaweza kufundishwa Kwa lugha yoyote na mtu anayeelewa lugha hiyo akapokea maarifa kwa kiwango stahili na ukamilifu wake....

Ni kazi moja tu inahitajika. Nayo ni kuyatafsiri maneno hayo kwenda ktk lugha ya waliokusudiwa na kuweka wazi maana/mantiki iliyo ktk terms hizo...

That's all. Hakuna kingine hapo...

Otherwise, wewe bagamoyo ndiye utuambie kwanini unadhani hayawezekani?

Mfano, unaifahamu Biblia Takatifu wewe? Kwa taarifa yako tu ni kuwa, hicho kitabu hicho kimetafsiriwa kwa lugha zote za dunia hii..!!

Kwanini kimetafsiriwa kwa Kila lugha za hapa duniani?

Jibu ni rahisi tu. Kwamba, ni ili ujumbe na maarifa yaliyomo kwenye kitabu hicho yasomwe na kueleweka na watu wote duniani kwa Kila mtu na lugha yake...!

Kama Hilo limewezekana, kwanini isiwe kwenye VITABU vya elimu dunia Kwa ajili ya jamii???

Ukipata jibu la SWALI hilo☝️☝️☝️☝️, njoo tuzungumze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…