27 June 2015: Yanga SC vs SC Villa [Mechi ya kimataifa ya kirafiki]

Grader

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Posts
445
Reaction score
64
Kwa sasa nipo Taifa ili nione mechi ya kimataifa kati ya Yanga vs sc villa ya Uganda, mpaka sasa timu ya villa haijawarm up na haijulijani kama kuna mechi leo. Villa wanataka wapewe kiasi cha dolla 10000 cash kabla ya kuanza mchezo kama contract inavyoeleza. Yanga pamoja na muuandaaji kwanza promotion hawana
 
Hivi kwa nini Yanga hamfanyi uchaguzi? Manji magumashi sana
 
Mbona Kichwa kina ujumbe mzito halafu content zake zipo very weak!!.
 
Mpaka sasa taifa hakuna Umeme. Hakuna refa anayefanya warm up wala wachezaji wa villa.
 
Villa wakikubali kucheza ila fweza wapewe mwisho wa mchezo itakula kwao...
 

Yanga naipenda sana..shida rangi tu ya jezi zao!
 
wabongo bana yaani hawa villa safi sana hakuna kwenda uwanjani bila hela kwanza.
 
Wanajukwaa tujiunge hapa kupeana mawili matatu baina ya mpambano wa kirafiki wa kimataifa baina ya Yanga SC ya Tanzania dhidi ya SC Villa ya Uganda.

Yanga wamevalia jezi za manjano kuanzia bukta hadi fulana wakati SC Villa wamevalia jezi za bluu huku soksi zao zikiwa na michirizi ya rangi ya bluu na nyeupe.

Mpambano ndio unaanza muda si mrefu na ni mpambano wa hisani katika kuchangia fedha kwa watu wenye mahitaji muhimu.

[Size =5]Yanga SC 0 - 0 SC Villa
Dk 90 FT
[/size]

Livestream: AZAM Media Flash Page

 
Naangali hapa Mechi Live Azam Tv.
Mechi imeanza muda huu saa kumi na moja na dakika ishirini badala ya muda wake wa kawaida.
Na muda huu ndio umeme umerejeshwa.

Kwa ufupi ni kwamba wachenzaji na makocha hawakufanya warm up,wameingia moja kwa moja uwanjani.
Na pia inasemekana Waandaaji ni vimeo,usanii unaendelea kwenye Timu zetu.
Inasemekana pia Club Villa walichelewa kufika uwanjani suala jingine ilikuwa ni nauli.Yaani kuna aibu kubwa ipo chini ya Carpet.

Usanii kila sehem,we Club to hivi unategemea team ya Taifa itakuwaje?

Hizi Team nyingine ni NGOs tu
 
Jambo la kushangaza mchezaji aliyekuwa akifanya majaribio Yanga...

Kamara leo anachezea SC Villa na sababu ni Yanga kutoridhishwa na kiwango chake...

Sasa hatma yake Yanga sijui ipo vipi...
 
Halafu Club Villa kuna mashabiki wachache najua Simba wamechomekea.
Yaaani wanashangilia ile mbaya kuliko wenyeji.
Mpira umeanza bado bila bila
 

hapana wamefanya warmimg up. wameingia uwanjani saa 11.47 kwa warming up halafu wakarudi vyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…