4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Hili likitekelezwa litaimarisha Muungano.
 
Yaani! ndugu zetu wa damu! the 4% tunayogaiwa wazanzibari na ambayo ni haki yetu imewatowa roho kiasi hiki? tuwaeleweje ndugu zetu nyie?
 
Asante mkuu kwa huu ufafanuzi. Hata hivo kama mzanzibari nimejisikia vibaya sana na masimango ya ndugu zetu hawa kwa kitu kidogo sana kama 4%. Ambapo kiukweli Zanzibar kama ingeachwa vitu hivi viingie ndani yake bila ya kupitia kwenye muungano, Zanzibar ingefaidika mno. Leo hii watanganyika wanaona kama vile hii 4% ni fadhila na upendeleo na kwamba Zanzibar haistahiki nayo! Na ndio maana ni vyema Zanzibar ikawa na mamlaka yake kamili.
 
Kama vipi iwachieni Zanzibar ijitawale.
 
Acha uongo, tra ukusanye mapato znz alaf yote yaachwe znz basi itakua tra yenu ya kikundi cha majambazi
 
Kama mzanzibari, na kwa masimango haya, how I wish lisitekelezwe ili iendelee kuwa chachu kwa wazanzibari kudai Zanzibar yao!
Nimekuelewa, tatizo waliotaka Muungano walifikiria tu kujilinda ili Sultan asirudi kutawala maana alishataarishiwa msaada wa kijeshi kutoka Oman.
 
Ukitathimi kwa kina utagundua iyo 4% inatoka Tanganyika kwenda Zanzibar.

Ni kama vile Tanganyika inalipia gharama za muungano.
Huku ni kuchoshana tu na sisi tutaanza kudai mirabaa ya Ubuyu wa Tangawizi, viladu na mashelisheli.
 
kuna kipindi nilisikia wanalalamika kuwa ukiagiza bidhaa toka zenji, inakuwa imelipiwa ushuru zenji lakini ikifika dsm inalipiwa tena. ina maana kule wana ushuru wa kikwao na wana makusanyo ya pesa ya kikwao.
 
Usichokifahamu ni kwamba TRA wanakusanya kodi hadi Zanzibar. Ndio maana sheria inataka 4% ya mapato yote Tanzania iende Zanzibar. Tena hio 4% kwa maoni yangu ni ndongo ingepaswa walau 15%.
Mi naona kuweka vitu simple Zanzibar iwe na ZRA, iwe inakusanya mapato yenyewe ila shida sasa kwenye kugaramia shughuli za muungano itabidi Zanzibar ichangie. Au shughuli za muungano zipunguzwe zaidi ibaki moja tu ya Ulinzi.
 
1. pesa ya visa: hivi kweli itakuwa nyingi kiasi hicho? manake hata bara kuna watalii wengi wanakuja.

2. makampuni ya simu:- naona zanzibar hapo wanafaidika kwa kupata huduma zao, kwasababu kama isingekuwa bara sidhani kama kungekuwa na kampuni la simu lingeenda kwao kugombania wateja chini ya milioni moja. kwahiyo wanapata huduma za simu kwa mgongo wa population ya bara, hapo washukuru wasilaumu. kama vipi wapige marufuku yasitoe huduma kule kama wataweza.

3. zaidi ya yote, wazanzibar bara wengi sana sana na binafsi huwa nawaona ni watz wala si wazazibar, pamoja na kwamba wao huwa wanapenda kujionyesha ni wa kisiwani sio wa uku. wanafaidika na chochote kinachofanywa na serikali ya muungano. sasa kama raia wao wanakula matunda ya muungano, utasemaje wanatudai? wanatudai chakula ambacho tulipokitenga hadi watoto wao wamekula? na kwanini sisi hatumiliki ardhi kisiwani wakati wao wanamiliki ardhi hadi migodi bara?
 
Mi naona kuweka vitu simple Zanzibar iwe na ZRA, iwe inakusanya mapato yenyewe ila shida sasa kwenye kugaramia shughuli za muungano itabidi Zanzibar ichangie. Au shughuli za muungano zipunguzwe zaidi ibaki moja tu ya Ulinzi.
yaani, kila mmoja akusanye mapato kwenye nafasi yake. kama ni watalii wanaenda zanzibar, wakatoe visa pale zanzibar kwasababu si nchi ile? kama ni kukusanya mapato basi kuwe na ZRA ya kwao, nchi mbili zikusanye mapato kila mmoja kwa nafasi yake halafu kila mmoja sasa achangie kwenye muungano.

litakalotokea hapo, zanzibar hawatakuwa na cha kukusanya zaidi ya visa za watalii kimuungano. mitandao ya simu watabaki na zantel yao tu ambao haitakuwa na faida kwasababu ya pupulation ya kisiwani, ni ndogo kufanya biashara hizo, the same applies kwa mabenki. tuishie kusema muungano unawafaidisha pande zote mbili na zanzibar inafaidika nao indirectly na wanakula kwa mgongo wetu sana.
 
Binafsi sina shida kama hiyo 4% itahusisha mapato na madeni. Kama ni mapato tu, hapo kuna tatizo.
Kwahiyo na hili deni letu la taifa la 71tr wao pia wanachangia asilimia ngapi?..au tunagawana nusu kwa nusu.[emoji28][emoji28]

Kimsingi huu muungano ni pasua kichwa..vizenji tegemezi zaidi ya chawa..bado vinataka pasu huu ni upuuzi.

Leo hii vi zenji vikija huku ni free kwa kila jambo..ila mbara aakienda huko ubaguzi kuanzia akishuka bandarini..mara kitambulisho cha ukaazi..ni ushezi tu...harafu tunajiita watanzania etu tuna muungano.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni zamu ya watanganyika kulalamika!!

Zanzibar wamelalama Hadi vichwa vinauma, lakini yote Kwa yote, huo mgao usiwe tu wa mapato ya ndani, upole wote wa watanganyika Mbona utaisha hivi karibuni!!!
 
unataka tugawane deni? hahaaha, kwahiyo kama kuna mikopo tulichukua na hatukuwapatia, ile mikopo hadi leo tunadaiwa trillion 70 kwa mfano, itabidi kama wao wakitaka tuwapatie mgao wa mkopo huo wakubali kuchukua na mgao wa kulipa deni lake. asilimia 4% ya deni la taifa inakuwa ngapi i li wenzetu pia waje wadaiwe.
 
Mnapoungana kuna vitu unapata na vingine unapoteza, hizi kero za muungano ni ubinafsi wa kufikiri kwanini mimi napoteza hiki.
Muungano pamoja na kwamba uko kikatiba pia ni sera ya Chama tawala bahati mbaya viongozi na wanachama wengi wa chama tawala hawajui kwanini chama chao kina sera ya muundo wa serikali mbili wa muungano matokeo yake kila kiongozi anaamua kwa utashi wake.
Mara zote kero za muungano huwa zinahusu Zanzibar ukiondoa swala la kwenda visiwani kwa passport.
Ni vema tukawa na muundo ama wa serikali tatu au moja kuliko muundo wa sasa kwani tukiwa na serikali hizo mambo ya mgawo wa asilimia 4 yataondoka na kero kama mafuta lisiwe swala la muungano pia litaondoka na hata migawo ya asilimia au kwanini huchangii pia vitaondoka.
 
Abstract

One hundred and nineteen states signed the Law of the Sea Convention in Jamaica in December 1982. This Convention will enable coastal states inter alia to extend their jurisdiction over living and nonliving resources to 200 miles from their coastlines. Tanzania has consistently supported the concept of the Exclusive Economic Zone but has not yet claimed its own. This paper examines considerations of law and policy relevant to the requirements of a developing country in preparation of an EEZ claim. It shows that the notion of “grabbing jurisdiction”; with its implication of unilateralism in disregard of the law is certainly mistaken so far as Tanzania is concerned. It seems clear that many ratifications of the Convention will be delayed, and for a period of time at least careful attention will have to be paid to state practice grounded in national legislation extending jurisdiction to 200 miles as well as to bilateral and regional agreements. It is on the basis of scrutiny and evaluation of ongoing and unfolding state practice that a state is able to determine its obligations based on international law and to define its policies.​
 
To upompoma wako..mbara ni mgeni huko hatambuliki..ndio mana kuna kitambulisho cha ukaazi..kukipata mpka ukae miaka mitatu..sasa hii ni Tanzania au malawi..kwani NIDA haitoshi?

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…