4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

Unapoambiwa watanzania tupo milion 60+.
unaelewa nini?.
au wanzibar sio watanzania?
 
Hakuna pesa mtalipwa..tumewasamehe madeni mengi achlilia mbali umeme...mnakula bure bado mnataka kutupangia aina ya chakula ch akuwalisha?.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huwa nawaza, huu Muungano wa nchi mbili kuwa nchi mbili badala ya kuwa nchi moja sijui tumeutoa wapi. Wanajificha kwenye kero za Muungano,hakuna cha kero wala nini ni watu waoga kuamua kama tuwe nchi moja au kila mtu kivyake.
 
Kama vipi iwachieni Zanzibar ijitawale.
Zanzibar ilikuwa nchi huru kabla ya Muungano, lakini ni mali halali ya Sultan wa Oman. Muungano ni ukuta tu uliojengwa kumzuia mwenye chake asidai haki yake aliyodhurumiwa na mapinduzi MATUKUFU. Zanzibar mkiona vema kujitenga mjue Sultani anaweza kuja kudai chake kama hajasamehe.
 
Bara tunapenda dhuluma kama mwenda zake na Gang wake
 
Mafuta na gesi yapo vizuri tu Zanzibar, katika jambo moja ambalo limesababisha yasichimbwe, ni uroho wa JMT kutaka yawe ya Muungano. Tangu lini rasilimali za sehemu moja zikawa za Muungano ila za upande mwengine zisiwe za Muungano? Lengo ni nini?

Mimi nasema Mafuta yasichimbwe, yaachwe huko huko yalipo mpaka Zanzibar ipate kiongozi anaetaka maendeleo sio hawa wa mfano waliotoka serikali kina Balozi Sua Mbaya Idi, kazi yao ilikuwa kufanya ufisadi tu!
 
kwahiyo, kama zanzibar kuna mafuta, unaamini bara hakuan mafuta? yaani mafuta yawepo tu pale zanzibar na kwenye bahari yetu kuanzia mtwara kwenye gas hadi Tanga kusiwe na mafuta? au unaamini umiliki wa bahari zanzibar wanamiliki ukanda wote? kama zanzibar kuna mafuta na bara nako kuna mafuta tena na gas pia. ila kwa haki, bila kumung'unya maneno, mafuta ya Zanzibar yanatakiwa yakiendeleze kisiwa kile,na gas na mafuta na madini ya bara hayatakiwi kugawiwa hata sent kwa wazenji, hiyo ni haki. nakubaliana nao.

kitu kizuri ni kwamba, zanzibar pakiendelea, bara patafaidia pia, hivyo kama kuna vitu vinavyoweza kuwasaidia kuendelea, tunatakiwa kuwaunga mkono.
 
Kwani Chato ilikuwa inachangia nini kwenye pato la Taifa mpaka ikapelekewa mbuga ya wanyama,uwanja wa ndege na ikulu??
 
1. hivi Zanzibar inachangia kitu gani kwenye kwa Tz bara kinachowastahilisha tuwagawie hiyo asilimia? Bara inafaidika nini toka Zanzibar?
ilichangia BOT 12% kama sikosei, hadi dakika hii haijawahi kupata faida kutoa hio 12% iliowekeza hapo kwenye BOT.

2. Mgao unaoongelewa ni wa misaada toka nje, au ni mapato ya nchi (pato la madini bara, TRA, navitu vyote vya bara)?
Misaada/Mikopo kutoka nje

3. kama ni mapato ya nchi, kwani TRA haipo Zanzibar ya kikwaokwao?
Hi ni bodi ya mapato ya Tanzania na sio Zanzibar, nafikiri unajua sasa pesa yake inaungia akaunti ya nani.

4. proportion ya wingi wa watu + ukubwa wa eneo vinazingatiwaje wakati wa kugawa pato ya muungano?
Zimeungana nchi, sio ukubwa wa eneo au wingi wa watu.

5. kwanini marais waliopita walikuwa hawashughulikii hilo jambo, kulikuwa na kitu gani walichokiona? including one of them who was Zanzibari.
Hakukuwa na lengo la kuisaidia wala kutaka kuona Zanzibar ikipiga maendeleo, kuendelea kwa Zanzibar ilikuwa mwiba kwao. Lengo ni kujimilikisha na kujifaidisha kile walichokuwa nacho wazanziba, BAHARI.
 
Nilichogundua humu kuna watu hawawezi hata kupewa uongozi wa family, yaani watu wengi wanaongea kiunafiki na inaonyeshea wamezoea maisha ya wizi na uongouongo, kama wao wamekubaliana hivyo tokea enzi sasa kinachowauma ni nini? Kwann hio 4% inawauma na still hamjawapa? Kwanza mnatakiwa mpiganie hayo matrillioni wanayoyachukua kina kingwala na wenzake yarudishwe, mnatakiwa mpiganie ufisadi mkubwa unaofanywa na ccm kwa mfano miradi ya ndege nk, mkishakupapatua huo ufisadi mtapata zaidi ya 4%, yaani znz wanahaki ya kupata zaidi ya 4% sio mnataka kuwadhulumu
 
Hatuna tatizo ikiwa mna mafuta kila chochoro hapo tanganyika. Tatizo tulokuwa nalo na nyinyi ni kuyataka Mafuta ya Zanzibar kuwa ya Muungano, ilhali ya kwenu hamutaki yawe ya Muungano. Kwanini Almasi, Dhahabu na madini mengine yasiwe ya Muungano?

Hio 4% hatupewi na mafuta pia JMT inataka kuyachukua?!!!
 
Nimegundua humu jamvini huwa tunachangia amma kwa ushabiki au kwa kutokujua baadhi ya mambo. Afadhali umetoa mwanga. Chanzo cha mgao huu ni wakati EAC liyovunjika 1977 ilipokuwa inagawa mali zake kwa washirika. utakumbuka mgao wa Zanzibar uliingizwa Tanzania. Akatafutwa mshauri elekezi ambaye alishauri Zanzibar ipewe 4.5%. Bahati mbaya Serikali ikaamua 4% kwa kila jambo. Wakati tunadai hiyo 4% ni kubwa, pamoja na ufafunuzi huu, kuna jambo halisemwi na huwa hatutaki lisemwe; kwamba wakati wa kuanzisha BOT mwaka 1967 Zanzibar ilichangia 11.5% ya mtaji wa benki hiyo. Tokea wakati huo hakuna mgao wowote uliotolewa kwa Zanzibar kama mwanahisa mshirika mkubwa wa benki hiyo. Nadhani wakati tukijifaragua kwa dharau na kejeli tufike mahala tuukubali ukweli kwamba katika hili Zanzibar imedhulumiwa, inadhulumwa na itaendelea kudhulumiwa kwa jina kulinda muungano ikiwa hatutachukua hatua kurekebisha uendeshaji wa mambo yetu. Tuseme basi
 
Jeshi lipi walilonalo? Vile ni vikosi tu havina hadhi yakuitwa jeshi maana majeshi ni suala la muungano.
Hiyo asilimia 4 huenda ni mapato yatokanayo na biashara za nje ama mambo ya nje kama misaada nakadhalika kwakuwa masuala ya kimataifa ni ya muungano.
 
Yaani! ndugu zetu wa damu! the 4% tunayogaiwa wazanzibari na ambayo ni haki yetu imewatowa roho kiasi hiki? tuwaeleweje ndugu zetu nyie?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Wakati kingwala na wenzake wanakula zaidi ya hizo %4 but wanawacha wadunde kitaa ila znz ambayo inachangia pato wasipewe, hawa jamaa waajabu sijapata kuona na hawasarifiki
Mm siko znz ila napenda kuongea ukweli kama anavyoongea TL
 
Acha roho mbaya wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…