40% ya Wagonjwa wanaotibiwa Saratani Hospitali ya Bugando ni Wanawake wenye Saratani ya Shingo ya Kizazi

40% ya Wagonjwa wanaotibiwa Saratani Hospitali ya Bugando ni Wanawake wenye Saratani ya Shingo ya Kizazi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkuu wa Idara ya Saratani wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. #NestoryMasalu amesema 40% ya Wagonjwa wote wanaotibiwa tangu mwaka 2009 ni Wanawake wenye #Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Dkt. Masalu amesema #Bugando inahudumia Wagonjwa wapya 1,500 wenye tatizo la Saratani kwa mwaka huku zaidi ya nusu yao wakiwa na Saratani iliyofika hatua ya 3 na 4 ambayo ina ugumu katika kutibika.

Saratani nyingine zilizotajwa kuoongoza kwa Wagonjwa ni #SarataniyaMatiti na Saratani ya #TeziDume kwa Wanaume. Dkt. Masalu amewataka Wananchi kuwa na kawaida kupima Afya mara kwa mara na kuanza matibabu mapema.

===============

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imesema wagonjwa 22,000 kati ya 55,000 sawa na asilimia 40 ya wagonjwa wote ambao wanatibiwa saratani katika hospitali hiyo tangu mwaka 2009 ni wanawake wenye saratani ya shingo ya kizazi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 4, 2023 na Mkuu wa Idara ya Saratani Bugando, Dk Nestory Masalu kwenye maadhimisho ya siku ya saratani duniani yaliyofanyika kikanda katika hospitali hiyo ambapo watu zaidi ya 370 wamepimwa saratani bila malipo.

Dk Masalu amesema Bugando inahudumia wagonjwa wapya 1,500 kwa mwaka wenye tatizo la saratani huku zaidi ya nusu wakibaini saratani ikiwa katika hatua ya tatu na nne ambayo ni ngumu kutibika.

Amesema saratani nyingine zinazoongoza kuwa ni saratani ya matiti na saratani ya tezi dume kwa wanaume huku akiwataka wakazi wa mikoa ya Kanda hiyo kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara ili kuanza matibabu mapema wanapobainika kuwa saratani.

"Tunaendelea kutoa elimu ya uchunguzi wa saratani kwa watoa huduma ya afya na jamii ili kuongeza utambuzi wa visa vipya ambavyo havijabainika. Pia huduma ya mkoba inatusaidia kuwafikia walioko vijijini na kuwabaini wakiwa katika hatua za awali," amesema Dk Masalu

Shujaa wa Saratani, Jeredina Nzongela (31) ameiomba jamii kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kubaini hali ya afya yao na kuepuka kuchelewa matibabu ya magonjwa waliyonayo ikiwemo saratani na magonjwa yasiyoambukiza.

"Mimi nilikuwa na saratani ya titi ambayo niliibaini kwa kuchelewa matokeo yake watalaam walinifanyia upasuaji wa kuondoa titi la kulia na sasa naendelea vyema na matibabu. Saratani imeisha nakamilisha dawa

Naye, Mkazi wa Bugarika, Makoye Mashine amesema pamoja na kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa korodani ya kulia kutokana na saratani, afya yake imeimarika huku akiwataka wanaume kujitokeza kupimwa saratani ya tezi dume kabla haijafika hatua ya tatu na nne.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom