Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo no. 15 mbona haonekani? Nashauri ubadilishe rangi yake ifanane na wengine au kama ni kinara basi weka nyekundu
Nami ndani ya list mkuu? Duh!No. 15 ni invisible but inasomeka mkuu...! Huyo ndie kamanda mkuu a.k.a Mh. Dr. Col. Mr P.
Hao hawamuwezi Kikwete hata dakika moja ,Kikwete ni mtu mkimya sana sana ,na hatari ya mtu mkimya ni kubwa kuliko yule anaepiga makelele,maana mtu mkimya anakuwa alert kwa kila step anayochukua,japo ataonekana hajui au mtamuona zezeta lakini hesabu zake haziendi upande,anapanga ,anayajua,na kuelewa ni wakati gani anahitaji kuchukua hatua ili kuidhibiti hali. Hivyo hao akina Rostam na wengine inakuwa kama wadudu waliokuwemo ndani ya sufuria kubwa ,hivyo Kikwete aliepo juu anawaona na kuwatazama movement zao na nani anataka kutoka kwenye sufuria atamuona tena kwa urahisi zaidi ,natumai umepata picha halisi ,hivyo Kikwete anayatazama haya yanayofanywa kwa upole kabisa akiamini watu watajirekebisha intime kabla hajaamua kuwarudisha ndani ya sufuria kwa yule anaekuja juu akiamua kutaka kutoka ndani ya sufuria ,kwa ufupi hawa watu wamewekwa ndani ya kona au uangalizi na kila hatua wanayofanya inadhibitiwa na kupimwa kwa kina na malengo yake,kiasi kwa walipo wanaonekana wamo katika kugombea ukubwa wao kwa wao,hivyo Kikwete analielewa hilo ,na wao kama ndugu lazima mkubwa amuheshimu mdogo ,sasa wanapotokea ndugu kupigana inabidi uwawache ili mmoja aweze kumuheshimu mwenziwe.
Kikwete ni Raisi ambae amekuwa mvumilivu sana kiasi kuwa uvumilivu wake unaonekana kuwa umepita mipaka ,lakini anaamini kuwa kila mtu atauona ukweli wa anayoyafanya na atajirekebisha hivyo tunaweza kumuweka katika kundi la watu wenye subira.Na ndivyo nimuonavyo mimi kwa upande wangu ,ni mtu ambae anaweza kukasirika mpaka akabadilika rangi lakini mwisho wake hurudisha hasira zake na kuwa katika uvumilivu na ndio tunavyokwenda nae he is a man of GOD & we can do nothing to force him to take action by our makelele.
Hata Mtume wetu Muhammad alikuwa mpole sana kuna sehemu alipigwa mawe na yakamtoa ngeu na damu,malaika alimshukia na kumwambia sema tuwafanye nini wale watu ,Mtume akawaombea dua tu na hakuwatakia waadhibiwe. Hivyo wavumilivu ni watu wa aina hawawezi kabisa kufuata matakwa ya mtu mwengine katika kuchukua hatua.
Usiwe na jazba unaushahidi wowote wa kubainisha hilo au ni chuki tu hao watu sioni kama wanamakosa hadi sasa. hivi tuseme iwe ni wewe ndio umeona hilo vyombo vya dola halioni hicho kitu na kama ingekuwa hali ipo hivyo ulivyo isema basi sidhani kama serekali ingewachia watu hao wa 3 wafanye hayo wakati serekali inauwezo wa kuwashuhulikia na sifikiri serekali ingekubali nchi kuchafuliwa lakini kwa hali inavyokwenda nahisi hata serekali inajuwa kuwa hao watu wanazuliwa tu
Nami ndani ya list mkuu? Duh!
Na ukiangalia ni watanzania wenzetu waliopata kusoma kwa fedha za watanzania na kisha kupewa madaraka na kuyatumia vibaya madaraka yao.
ongeza na wajumbe wa shina wa CCM, wanauza viwanja mara mbilimbili huko serikali za mitaani na wanasumbuaa kweli watanzania wenzao
Wakuu, nimemwongezea Spika wa zamani mzee Msekwa. Nimekumbushwa na mdau pembeni kuwa anastahili kuwepo kwenye list.Pius Msekwa
Tuendeleze list
Maximo ....kwa kushindwa kuchukua kombe la Challenge,na kwa kushindwa kuipeleka Stars 2010.. ha ha ha ha aaaa