50 People Who Are Screwing Up Tanzania

Status
Not open for further replies.
Huyo no. 15 mbona haonekani? Nashauri ubadilishe rangi yake ifanane na wengine au kama ni kinara basi weka nyekundu

No. 15 ni invisible but inasomeka mkuu...! Huyo ndie kamanda mkuu a.k.a Mh. Dr. Col. Mr P.
 
Mkuu Sonara,

Serikali ipi hiyo unayoizungumzia!!! Ya Kikwete?????? Ni kichekesho unless umetoka usingizini na hujui kinachoendelea Tanzania la sivyo, nina wasiwasi majibu yako yanalengo lililofichika!!!!

Tiba
 

Usitudanganye umakini na ukimya wa Kikwete ni upi unaotuambia nao?EL ni makini sana kuliko Kikwete,Amini usiamini anachokizungumza Mmaroroi ni sahihi sana.Kwa gharama yoyote Lowasa yuko tayari kutaka madaraka ya kuongoza nchi.Na nikuambie hujui aliko Lowasa na kambi yake wakati huu ,na wanachokifanya wala hujui.Pia ukumbuke mtu huyo huyo Lowasa ndiye alikuwa behind Wanamtandao na kumweka Kikwete madarakani.Sasa hoja siyo nani makini au mkiya bali NCHI ISIINGIZWE MATATANI KWA UFISADI WA MAFISADI!!!Lowasa yuko na atakuwa tayari kumwaga damu ili aingie madarakani kwa udhaifu wa aliyeko madarakani.Kwa hiyo ni vyema tukachukua tahadhari kabla ya shari.
 

Waua nchi na wauza nchi muna sura nyingi
Asante kwa kujitambulisha, unaturahisishia kazi wazalendo
 
Na ukiangalia ni watanzania wenzetu waliopata kusoma kwa fedha za watanzania na kisha kupewa madaraka na kuyatumia vibaya madaraka yao.

ongeza na wajumbe wa shina wa CCM, wanauza viwanja mara mbilimbili huko serikali za mitaani na wanasumbuaa kweli watanzania wenzao
 
Mfumwa hatukuelewi. We nani katika hao unaona hastahili au una mjomba wako katika hao?
 

Jamani tuache wivu, mtu akiwa na hela kidogo kwetu tayari huyo ni fisadi! Ndiyo maana Tanzania tunazidi kurudi nyuma. Hao tunaowaita mafisadi ndo wajasilimali kwani bila wao tusingekuwa na Mbezi Beach, Masite ya Tegeta, masaki, Makongo Juu na kadhalika.

Tujifunze kutoka kwa wenzetu Wakenya. Kibaki, Odinga, Kenyatta nk ni matajiri wakubwa wanaomiliki mali nyingi na wanasaidia katika kukuza ajira.

Huku kwetu, hao mafisadi mnaowasema hata nyumba ya kupangisha hawana!! Umasikini ndo unatusumbua.

Nakubaliana na wale wanaosema kuwa mafisadi wa nchi hii ni wewe na mimi, period!
 
Napendekeza shortlist zaidi ya 50 halafu tukipiga kura ndio wabaki hao 50 ili kuondoa walioonewa! Ongezea James E. Sinclair,Chairman & CEO,Tanzanian Royalty Exploration Corporation swahiba mkubwa wa mkulu!
 
Apson Mwang'onda
Rostam Azizi
Ben Mkapa
Rajab Maranda
Johnson wa EPA
Abdallah Kinana
Peter Serukamba
Subhash Patel
Manji
Chavda
Vithlan

.....hawa wote kuna sifa moja wana share mnaijua hiyo?
 
Maximo ....kwa kushindwa kuchukua kombe la Challenge,na kwa kushindwa kuipeleka Stars 2010.. ha ha ha ha aaaa
 
Pius Msekwa
Tuendeleze list
Wakuu, nimemwongezea Spika wa zamani mzee Msekwa. Nimekumbushwa na mdau pembeni kuwa anastahili kuwepo kwenye list.

Kama kuna niliyemwonea kwenye hii list naomba mnifahamishe tumwondoe.

6 screwers missing 🙁
 
Kuchafuana maana yake nini mfumwa au yupi wewe kati ya hao unaona hawastahili. Au nawe unakuwa kama wale waandishi wa NeW Habari(2006) wanaomtetea RA na kumuona msafi wakati nasikia anawafanyia ufisadi hata wao kuwapa titles za consultants ili akwepe kodi yav TRA. Muulize Muhingo kama halijui hilo.

Mungu ibariki Africa
 
Maximo ....kwa kushindwa kuchukua kombe la Challenge,na kwa kushindwa kuipeleka Stars 2010.. ha ha ha ha aaaa

ha,ha kwani yeye ndio alikuwa akicheza. Ndio maaana nakubaliana kabisa na mwana Jf aliyesema namba one katika list ni sisi wenyewe wananchi
 
Hi,

Hiyo list imetumia vigezo gani, mbona watu wengine hawamo, au just if have ever appeared in newspaper then you are part of MAFISADI.

Mh!!!!
 
Mimi nafikiri tuanze na wananchi wenyewe.

We are actually screwing ourselves for allowing CCM to rule our country!!!!!!!!!!!!!!!
 
Duh Kazi kweli kweli...

Ingependeza kama ungekuja na list ya watu kama 100 ili tuwa-shortlist wabaki 50....hivi kuna watakaodai wameonewa...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…