Umeenda kabila gani vile?
Umeenda kabila gani vile?
Siku ile mimi nilikuwa kimataifa zaidi, muda huo mnawanyanyasa Mtibwa nilikuwa nimepumzika kusubiri mtanange mkali kati ya Ivory Coast na Ghana ambao nilijua ungechukua muda mrefu na kweli ikatokea.Yalaaaaaaah!!! kumbe upo hai mkuu Masuke!!!!, Nikajua umedondoka pale taifa baada ya kuona timu ya wananchi ilivyokuwa inawanyanyasa wale wakulima wa miwa wa kutoka kule Manungu!! Habar za kuadimika!!!
Kubadilisha kabila kunaendana na kujua tamaduni, mila na miiko ya kabila husika, endapo utaniambia baadhi ya miiko, baadhi ya tamaduni, baadhi ya mila za kisukuma na kuniambia umechagua jina gani na ukoo gani wa kisukuma then i will have to think about the offer of becoming Yanga supporter for at most one match.Nakuwa Msukuma Masuke, sasa tumemaliza wewe Yanga, mimi Msukuma powa kabisa.
Hatubadilishi ndio tayari imepitishwa hii, mimi kubadili kabila si mchezo. Karibu sana Yanga.
Kubadilisha kabila kunaendana na kujua tamaduni, mila na miiko ya kabila husika, endapo utaniambia baadhi ya miiko, baadhi ya tamaduni, baadhi ya mila za kisukuma na kuniambia umechagua jina gani na ukoo gani wa kisukuma then i will have to think about the offer of becoming Yanga supporter for at most one match.
Uwiii hayo mambo mengi sana, Masuke kama ni la ukoo nachukua hilohilo lako lol...
Mila najua hiyo ya chagulaga. Kuchunga ng'ombe, miiko hapo ndio nisaidie eeh.
Yanga tunapokea shabiki mpya leo, karibu tena...
Umeshindwa mtihani huu inaonekana huna nguvu ya ushawishi, ngoja nikuitie hawa ndugu zangu wanaweza kukusaidia. Makoye Matale, sembo na Crashwise hebu njoni huku mjaribu kumpa tuition huyu mtu maana tunataka kumuasili ili ajiunge na wananzengo. Mpeni darasa kuhusu utamaduni, mila na miiko yetu.
Mkuu Masuke wewe ni ndugu katika kabila letu na Bantu lady ni dada katika Yanga yetu. Na-declare conflict of interests katika mjadala huu, hence no comment.
Lengo ni kumpa machache yanayohusiana na kabila letu ili ikionekana anaelewa nitaamini kweli amedhamiria kubadili kabila hivyo nitaona inawezekana hivyo na mimi nitaweza kuwasupport vijana wa jangwani siku mtakapokutana na wale wa Botswana.
Kumbe unakuwa Yanga kwa mechi moja tu? Mkuu Masuke hapo nami nakuwa Msukuma kwa siku hiyo tu hahahahahahaaaa.
Uwe Yanga jumla ndio nami nitakuwa Msukuma jumla. Ila hiyo janja yako, nabaki na ukurya wangu mmmh
nashukuru nimerudi salama, hongereni kwa ushindi mnono sana...............mimesoma Gazeti nimemkubali sana Ngassa ingawa inaonekana bado mashabiki wa simba na Yanga washamba sana
nilienda kwa palizi la ufuta.......uache unazi sasa, Rage alipata alichotaka kwenye michezo kama anavyitaka sasa Malinzi na Tenga................Yanga walimozmea Okwi.................Mkuu ulikuwa wapi? Sisi mashabiki wa Yanga siyo washamba bali mashabiki wa Simba kwa mujibu wa Rage ni 'mbumbumbu'.
nilienda kwa palizi la ufuta.......uache unazi sasa, Rage alipata alichotaka kwenye michezo kama anavyitaka sasa Malinzi na Tenga................Yanga walimozmea Okwi.................
Hayo majina kiboko, jina la Nshoma ni common sana ila hayo mawili ni balaa.Sasa mkuu Masuke nimekuwekea full nondo, jina langu nitaitwa Nshoma.
Upande wa baba itakuwa Jongh'eka na upande wa mama ni Ngh'ungulu hata kutamka siwezi hahahahahaaaa!!!
Haya mila sasa huwa wanapiga magoti wakati wa kusalimia eeh, mdogo kumuanza kumsalimia mkubwa, mnatambika na kulima kwa ng'ombe.
Pia huwa mnao mke zaidi ya mmoja sijui hii inakuaje aah.
Halafu sijui naanza jisikiaje, miye kuwa msukuma aaah kama sitaki vile. Hivi naanzaje kuhama kabila kwanza hahahaaaa.
Ila karibu Yanga na ndio tayari kuanzia leo Masuke ni Yanga, nimeshakamilisha usajili hapo juu!!!