Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
YANGA SC VS MTIBWA NI MECHI YA KISASI AMBAYO TUSITEGEMEE UFUNDI MWINGI ZAIDI KUKAMIANA
Mzunguko wa kwanza Yanga SC ikiwa chini ya Mbrazil Maximo ilikubali kichapo cha magoli 2-0 , ilikuwa ni mchezo wa kwanza katika ligi lakini matokeo hayo mabovu yalifunikwa na historia ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC kwenye ngao ya jamii.
leo kazi itakuwa pevu sana kwa timu zote. Wakati Yanga mpaka sasa wamecheza mechi 12 na kushinda mechi 6 huku wakitoka droo mara 4 na kuruhusu kutikiswa mara 2 wao Mtibwa Sugar wamecheza mechi 11 huku wakitoka sare mara 6 kushinda mechi 4 na kufungwa mechi 1. Tazama vizuri hapo timu zote zinaonekana kuwa defence nzuri lakini bado kuwa na forward line kali zenye uhakika wa kushinda mechi tatu mfululizo. YANGA katoa droo 4 katika mechi 12 hapo hapo kafungwa mechi 2 sasa kiufundi kapoteza takribani pointi 14 katika mechi 12 na kuambulia pointi 22. Mtibwa yeye katika mechi 11 katoa droo 6 na kufungwa mechi 1 hapo kapoteza pointi 15 huku akiambulia pointi 18.
Sasa hapo utaona timu zote zinakosa forwad makini kuhakikisha ushindi kwa wastani wa mechi tatu mfululizo.
Yanga wataingia na tension ya kulipiza kisasi huku wakicheza mchezo wa kufunguka zaidi wakikataa man to man ili kupunguza idadi ya majeruhi kutokana na ujio wa mechi ya kimataifa tarehe 14 hivyo basi mchezo wa yanga leo utakuwa wa pasi ndefu na zonal marking katika ukabaji.
Mtibwa Sugar wanao mtegemea sana Ame Ali katika ushambuliaji na Salumu Mbonde katika ulinzi watataka kulinda heshima yao mbele ya Yanga hali hiyo itawafanya kukamia sana.
Ni mechi ngumu sana ila dakika 25 za mwanzo zitatoa Mwanga nani mshindi ingawa naona 60% game itaamuliwa kwa matokeo ya kushangaza
===========
===========
Matokeo ya mwisho: Yanga 2 - 0 Mtibwa