80% ya Wanawake Tanzania ni 'omba omba'

Wanawake wanawaomba wanaume sababu na wanaume wanawaomba wanawake. Ingekua sivyo wanaume wangeacha kutoa wanachoombwa ili kukomesha tabia ya kuomba

Siku hizi wote wanawake na wanaume wanadai haki sawa
Jua haliwezi kuchoza Magharibi likazama Mashariki, haiwezekani ku control nature mkuu, unadhani wale ombaomba walemavu wanaopewa mimba mitaani chanzo ni nini kama siyo wanaume wenye ndoa zilizoyumba nyumbani
 
Mwanamke kuwa omba omba haifai na siyo sawa hata kidogo.

Tubadilishe namna yetu ya kufikiri na mitazamo juu ya hilo.


Imeandikwa katika Biblia

Mithali 31:10 nakuendelea

Mwanamke mwema hufanya yafuatayo;

- Anafanana na Merikebu ya Biashara

Yani anaposafiri na kurudi nyumbani hurudi na bidhaa za biashara mbalimbali [emoji108]

Containers kwa containers za bidhaa mbalimbali zitakazouzwa na kuleta faida.

- Hutafuta shamba akalinunua kwa pesa itokanayo na mapato ya mikono yake na sio kudanga au kutegemea hela ya Mwanaume [emoji108]

- Huamka kabla usiku haujaisha na kuanza shughuli za uzalishaji wenye tija.

- huleta chakula chake toka mbali

- huwapa watu wa nyumbani mwake chakula na wajakazi sehemu yao.

- hali chakula cha uvivu

Huangalia njia za watu wa nyumbani mwake.

- Huitwa Kheri Na wanaume.

N.k.

Someni hadi mwisho
 

Mithali 31:10-31
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;

Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.

Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.

Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.

Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Asante sana naomba niiweke mwazo kabisa wa uzi
 
Mithali 31:10-31
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.

Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.

Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.

Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Hilo ni jambo jema sana,serikali iimpe support huyo mzee aendelee kuwasitiri akina mama wenye mahitaji maalum
Ni kweli kabisa, anapokea kila mtu pale kwake, vijana na wazee, wake kwa waume, anaowafindosha kazi mbali, anaowafundisha ufundi mbali, anaowafundisha ujasiriamali na kutafutia mitaji mbali, anaowapatia ukulima mbao. Ilimradi kwa Mzee Abdul ushindwe mwenyewe tu.

Nilivypasikia nilikuwa siamini ikabidi nimtumie whatsapp kwa namab ya mtu nijifanye kama mimi ni single mother mwenye mahitaji maalum. Alinijibi kwa ufupi tu, njoo huku kwetu tuone tutanyanyuana vipi, unaishi wapi sasa hivi? Nikamwambia nipo Manzese kwa rafiki yangu, akaniuliza "utaweza maisha ya kwetu huku nje ya mji"? Kama utaona taabu siku ya Jumamosi tutampa mtu namba zako atakutafuta anakuja huko mjini, aone jinsi ya kufanya. Mie mwenyewe nikaonaa enheeeee, nimebeep amepiga. Nikamtumia message nikamwambia, asihangaike kumtuma mtu nimeongea na mdogo wangu kaniambia nikaishi kwake. Yalkaishia hapo.

Siku nyingine nikamtafuta kama ni mtu atakae kusaidia sadaka zake, akanambia "hatupokei sadaka za samaki" njoo huku uone sadaka zako zinavyoweza kurudi tena kwako, njoo uwekeze kwenye mambo ya waja wema. Hatutaki sadaka bila kuifanya kuwa endelevu. Haapo nikamshangaa sana na bado naendelea kumdadisi, nimeanza kuipata picha, ana very simple but highly effective ideas za empowerment. Tena akanifahamisha kuwa hata wao hawatoi sadaka ya samaki, wanakupa nyavu ukavue ili nawe uendeleze wengine. Siwezi kuyaeleza mengi aliyonifahamisha, atakae kuyafahamu amwandikie whatsapp, kanoiruhusu niitangaze namba yake, Hana neno.

Allah amzidishie kila la kheri, yaani kwanza utapoongea nae tu, unatambua kuwa huyu mtu yupo serious na anachokifanya.

Abdul Ghafur, hongera sana kwa juhudi zako. Allah akupe umri mrefu uwe mfano mwema wa kuigwa hata na serikali.
 

Ni kweli kabisa utoto unasumbua....

Ni kweli kiasilia mwanaume ni mtoaji sababu sisi kiasilia ndio tunabeba mimba na kulea,hivyo most times hatuko kwenye shughuli za kimaendeleo...na tunategemea 'resources' kutoka kwa mwanaume..ni trait tunayo share na wanayama wengi kasoro simba.
 
Mithali 31:10-31 SRUV
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.

Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.

Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.

Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Natamani sana kutoa sadaka yangu kwake ili asaidie hao watu wenye mahitaji maalum. Nitamtafuta nione nini cha kufanya.
 
joseph1989 Hii comment inastahili kufanyiwa lamination na kuwekwa kwenye hifadhi ya kumbukumbu ya Taifa
 

sasa ndio nini....
 
Kubalance the story ungeleta na mume mwema yukoje....
Ni balance story kivipi, hayo siyo mandishi yangu ni mitume na manabii, yameongelewa hayo mambo toka zamani katika jitihada za kuzuia uomba omba na udangaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…