FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Tanzania watu wote 95% ni omba omba, wasioomba ni5% tu.Wasalaam wana JF
Naomba niwasilishe utafiti wangu uchwara kuhusu hawa watu. Ni reflection ya ukweli.
Katika jitihada za serikali kupunguza umasikini na kuondoa omba omba hili kundi haliangaliwi, yaani wanawake na akina dada.
Wana njaa kali na wanajitoa muhanga kwenye front zote. Wako wanaofanya ukahaba wa wazi mabarabarani, maofisini, na mitandaoni. Na wapo wengine wanafanya hivyo indirect kwenye mahusiano na mpaka kwenye ndoa zao pia. Yaani, exchange ya viungo vya uzazi na pesa. Na sehemu kubwa ni wale wanaopenda slope, yaani kimjini kitonga au udangaji.
Kimsingi, siyo rahisi kuwa na meaningful relationship hapa Tanzania. Ukimtongoza binti au mdada leo, kesho yake wewe umekua sponsor, utaambiwa gesi na umeme vimeisha, anataka hela ya saloon, mafuta ya gari na service kama hilo gari analo,na wakati mwingine ata vitu vidogo vidogo kama vouchers, yaani invoices ni nyingi mpaka unashangaa alikua anaishije kabla haujakutana nae.
Wanawake wengi wanachukulia mahusiano kama chanzo cha mapato au relief from their financial responsibilities na mbaya zaidi kama wameshnda bingo (bahati nasibu)
Pengine, sisi kwa sisi, kibongo bongo tunaweza kuhimiliana, je wenzentu wa maitaifa mengine wataweza? Sasa bssi, ni aibu gani hawa dada zetu wanalipa hili taifa kwa wageni kutoka nje ya nchi? watawachukulia kama Gold digqģers.
Tunaomba serikali iwe na mkakati wa makusudi, pengine kuanzia shule za msingi kuwapa ujasiri wanawake. Ujasiri wa kujitegemea, kuwafundisha kuona aibu kuomba na kuwa wategemezi. Kuwa mwanamke siyo kuwa handicapped na siyo justification au leseni ya kuwa omba omba. Tusiruhusu kuwa na taifa lililojaa wanawake wadangaji na omba omba.
katika muktadha huu, kama nchi za wenzetu wameweza sisi kwanini tushindwe? Nchi za wenzetu katika mabara ya ulaya na america wanawake omba omba wapo kwa idadi ndogo sana.
Ikumbukwe, hakuna omba omba anaye heshimika, hizo ndizo harsh realitiies of capitalism.
Mwenye akili na aelewe.
Hata lugha yetu umejijenga kwenye uomba uomba, kila "naomba, naomba". Kuanzia chini mpaka juu, wote ni omba omba. Cheyo (Bwana mapesa) aliwahi kusema Tanzania ni taifa omba omba.